Thursday, December 25, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE SIKU HII YA KUZALIWA KWA MWOKOZI BWANA YESU KRISTO!!!


NOELI NJEMA KWA WOTE HIZI NI SALAMU KUTOKA RUVUMA/SONGEA/RUHUWIKO:-)

Friday, December 12, 2014

KUADIMIKA KWA MUDA KWA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO/KAPULYA!!!


HAPA MIAKA MINNE ILIYOPITA.
KWA HIYO NA SASA TUTAWAHI KULIMA NA KUPANDA PIA KUTIA MBOLEA

Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwataarifu wasomaji wake kwamba haitakuwa hewani kwa muda.
Sababu kubwa ya kutokuwa hewani,  kuwa KAPULYA atakuwa SAFARINI ....Sio safari nyingine bali ya NYUMBANI-TANZANIA.
Nitajitahidi kuwataafu mawili matatu. TUKUTANE TENA WAKATI MWINGINE PAMOJA DAIMA. NAWATAKIENI WOTE CHRISTMAS JEMA NA MWAKA MPYA 2015. TUTAONANA.
SI VIBAYA KAMA TUKIMALIZIA NA KIPANDE HIKI CHA MZIKI....

KILA LA KHERI

HII ITAKUWA PICHA YA WIKI...CHAKULA NIKIPENDACHO...KARIBUNI

Huu  utakuwa ugali wa ulezi au mtama...mlenda pia upo.

Tuesday, December 9, 2014

LEO WATANZANIA TUNASHEREHEKEA MIAKA 53 YA UHURU!!

AHSANTE MUNGU
BENDERA TAIFA LA TANZANIA

Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na Umoja
Wake kwa Waume na Watoto
Mungu Ibariki Tanzania na watu wake.
Ibariki Tanzania
Ibariki Tanzania
Tubariki watoto wa Tanzania.

Monday, December 8, 2014

SOKO KUU LA SONGEA MJINI...NYUMBANI NI NYUMBANI!!

Si muda mrefu nitakuwa napata mahitaji katika soko hili:-) 

Thursday, December 4, 2014

CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA WIKI HII :-PICHA YA WIKI!!

Nimeipenda sana hii picha  jinsi mazingira yalivyo na pia hawa wanyama TWIGA nikiwaangalia jinsi wanavyo temba mwana mwendo wa kulinga inapendeza sana. ...nami nasema KARIBU TANZANIA:-)

Monday, December 1, 2014

Sunday, November 30, 2014

JUMAPILI NJEMA NA KWAYA HII YA VIJANA KKKT SONGEA MJINI WIMBO WAITWA ZAWADI


Kama usemavyo wimbo huu basi nami napenda kumshukuru Mungu kwa kutupa afya njema mwezi huu. Maana nayo ni ZAWADI.  Nimefurahi sana kuusikiliza huu wimbo nawe ukipata wasaa sikiliza. JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI IWE NJEMA KWA WOTE

Friday, November 28, 2014

ZILIPENDWA....IJUMAA NJEMA!!

NAPENDA KUWATAKIA WOTE IJUMAA NJEMA PIA MWISHO WA JUMA UWE WENYE AMANI TELE!!

Tuesday, November 25, 2014

KISA CHA KWELI!!!

Hebu turudie tena kusoma mada hii ambayo ni kicha cha kweli na halafu sikiliza huu wimbo wa dada Jennifer Mgendi. Haya karibuni sana.
http://ruhuwiko.blogspot.se/2012/09/kisa-cha-kweli.html
Na wimbo wenyewe ni huu hapa

PANAPO MAJALIWA  KUMBUKA TUPO PAMOJA.

Monday, November 24, 2014

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI...MCHANA MWEMA!!

Hapa mlo umekamilika kabisa...haya karibuni

Friday, November 21, 2014

Wednesday, November 19, 2014

LEO NAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA PRO. JOSEPH MBELE---


 NI KITABU CHA METHALI KATIKA  HADITHI ZA KINGONI  AMBACHO KIMETAFSIRIWA KWA KISWAHILI.
Ndiyo Profesa Mbele si mchoyo wa elimu ..kwa upendo wake wote kanitumia hicho kitabu. Nasema tena AHSANTE  SANA na shukrani nyingi zikufikia najua nimekushukuru.Nilikuwa sijui kuhusu hiki kitabu. Hapa ni moja ya methali zilizopo katika kitabu hiki:- YU NDUGU MACHONI...Kingoni ni Chihali chaku.....Tutaendelea siku nyingine na methali leo leongo ni kutoa shukrani.  ENDELEA NA MOYO HUO WA UKARIMU.

Tuesday, November 18, 2014

HUU ULIKUWA MLO WANGU WA JUMAPILI JIONI...

...Ni viazi mviringo, Karoti ambavyo nipika kwa kuweka kwenye oveni kwa dakika 40, halafu ni kitimoto (amahani kwa wasiotumia) na hiyo nyeupe ni mchanganya wa mtindi na tangu lilokunwa na kitunguu saumu "Tzatziki" au twaweza sema ni saladi ya kigiriki. Na cha kutemshia ilikuwa Maji....

Monday, November 17, 2014

MALEZI YANAYOFANYA MTOTO AMSIKILIZE NA KUMWAMINI MZAZI !!!

Katika pitaputa zangu kama kawaida nimekutana na hii mada ambayo ipo ndani ya maisha yetu ya kila siku nimeipenda sana na sikupenda kuiacha tu nimeona ni heri niiweke hapa Maisha na mafanikio pia ili wasomaji nanyi mpata faida....nimeipata hapa. Ahsante sana kaka Bwaya...Haya karibu sana........................................................................................................................................
TAFITI zinaonesha kwamba watoto wengi ni 'mayatima' wenye wazazi tunaoishi lakini hatupo kwenye maisha yao. Wazazi tupo lakini hatuna muda wa kujua hisia zao, fadhaa zao, maoni yao, hofu zao na hata matumaini yao. Aidha, tafiti hizo hizo zinasema wazazi wengi tunatumia muda mwingi na watoto wetu ama kuwaonya, kuwakosoa ama kuwapa hotuba/maagizo ya ‘fanya hivi, acha hiki’ kuliko tunavyowasaidia kujenga mahusiano ya moja kwa moja kati yetu na watoto.
 
Wazazi kwa upande wetu, tunajitetea kwamba maisha yamekuwa na pilika nyingi. Mambo yamebadilika hivyo yatupasa kutumia muda mwingi kutafuta pesa kujenga maisha ya baadae watakayoishi watoto wetu. Tunawavalisha, tunawalisha, tunawapeleka shule na kuhakikisha wanalala na kuishi kwa usalama. Katika jitihada zote hizo tunajikuta tukikosa muda wa kutulia na kujenga maisha ya sasa ya kimahusiano na watoto wetu ambayo kwa kiasi kikubwa huathiri maisha na mahusiano yetu na watoto wetu hapo baadae.
‘Elimu ya kujitegemea’inavyowaathiri watoto
Wazazi wengi tunasubiri watoto ‘wapate akili’ ili tuanze dozi rasmi ya mihadhara ya maagizo, maelekezo, makanyo, maonyo na kadhalika, tukiamini mtoto hujifunza kwa mafundisho rasmi. Wakati mwingine tunaamini fimbo ndilo jibu la tabia njema ya mtoto. Tunatumia na vifungu vya biblia, ‘Usimnyime mtoto mapigo/fimbo’. Na tunawachapa kweli tukitarajia heshima na adabu.
Athari za mtazamo huu ni kwamba katika kipindi muhimu kabisa cha mtoto kujifunza, tangu anazaliwa mpaka miaka mitano, hatuwekezi vya kutosha. Tuko bize tukisaka maisha na kuwatelekeza watoto kimahusiano. Wanapofikisha miaka mitano tunawapeleka boarding wakapate elimu bora ya kimataifa itakayowasaidia kuzungumza kiingereza na sio kuwa binadamu atakayeishi na wenzake vizuri.
Tunasahau kwamba kipindi tunachodhani mtoto hajifunzi, ukweli ni kwamba hicho ndicho kipindi sahihi na muhimu kujifunza kuliko kipindi kingine chochote cha maisha ya mtoto. Ndicho kipindi mtoto anapojenga taswira ya ilivyo dunia na wakazi wake, tabia na ubinadamu, imani na tunu nyingine za msingi katika maisha.
Ni kipindi nyeti ambacho mtoto huhitaji mahusiano ya karibu kabisa na mzazi, ambaye naye shauri ya pesa, hapatikani. Kutokupatikana katika kipindi hiki muhimu, kumsikiliza mtoto na kuingiza kile tunachopenda kukiingiza katika moyo wa mtoto, huongeza umbali wa kimahusiano baina ya mtoto na mzazi.
Na bahati mbaya, umbali huu wa kimahusiano kati ya mzazi na mtoto huongezeka kadri mtoto anavyopata akili. Hukua akiviamini na kuvitegemea vyanzo vingine vya maarifa zaidi ya mzazi. Bila hata mtoto mwenyewe kung’amua, taratibu huanza kukosa imani na wazazi ingawa hujitahidi kuwaridhisha akiogopa fimbo na kelele. Mtoto huanza kumwona mzazi kama mtu mwingine yeyote anayeweza kumpa chakula, mavazi na malazi isipokuwa faraja ya moyo.
Hapa ndipo wanetu huanza kujifunza zaidi kupitia televisheni, marafiki na watu wengine kama walimu wanaokabiliwa na msongo wa mawazo ambao wakati mwingine hupanda mambo tofauti kabisa na mtazamo na matakwa ya sisi wazazi. Yote haya hufanyika bila taarifa ya mzazi ambaye yuko bize kutafuta maisha ya mbeleni ya mwanae.
Mtoto huyu anapofikia umri wa kuanza kufanya mambo yake kwa uhuru kwa kutumia elimu hiyo aliyoipata kwa mfumo wa kujitegemea tangu amezaliwa , tena bila 'ukaguzi' wa mzazi, ndipo mzazi hukumbuka 'shuka asubuhi'. Huurejea wajibu wake na huanza jitihada za kutafuta/kulazimisha urafiki na mtoto wakati ambao mtoto hana haja na urafiki huo. Too late wanasema wazungu. Shughuli pekee inayoweza kufanyika kwa ufanisi katika kipindi hiki kizito ni kulalamika, kufoka na kuadhibu, mahusiano ambayo kwa hakika huongeza umbali wa mawasiliano baina ya mtoto na mzazi. Mzazi humwona mtoto ameasi, na mtoto humwona mzazi anajipendekeza na kumfuata fuata.
Tuyape malezi uzito unaostahili
Ili kukwepa fedheha ya kulazimisha urafiki na mtoto hapo baadae, tunashauriwa sisi kama wazazi tuyape malezi uzito unaostahili kuanzia pale tunapofikiria kupata mtoto. Na kwa kweli malezi ndiyo fursa pekee ya mtu kubadili maisha ya mtu mwingine vile apendavyo. Fursa hii huwezi kuipata hata kwa mwenzi/mpenzi wako maana katika mahusiano ya ukubwani kinachotokea zaidi ni kuchukuliana na sio kubadilishana tabia. Kwa hiyo kama kuna fursa pekee ya kubadili mtu katika dunia hii ni malezi. Tuitumie.
Kupitia malezi mzazi anaweza kuwekeza apendavyo na kuumba tajiriba itakayoongoza mwelekeo wa maisha ya mtoto. Hata biblia imelieleza suala hili vizuri sana. Kwamba kile unachomfundisha mtoto kukifuata akiwa mdogo hatakiacha maisha yake yote. Kuwekeza katika ufahamu wa mtoto katika hatua za mwanzo kabisa za maisha yake huweka alama ya kudumu itakayoathiri mitazamo, imani na hata tabia ya mtoto katika maisha yake yote ya mbeleni. Tulitambue hili tunafukuzana na mipangilio ya kutafuta pesa.
Tupatikane kwa watoto, tuwasiliane na mioyo yao mapema
Hatuwezi kuwasiliana na moyo wa mtoto pasipo kupatikana. Kuwa nao, kucheza nao, kutembelea nao, kuzungumza nao na mambo yanayofanana na hayo huhakikisha tunaweka alama njema ya kudumu katika maisha ya mtoto. Kupatikana na kuwasiliana na moyo wa mtoto ni muhimu kuanze tangu anapozaliwa au hata anapohesabu majuma tumboni mwa mama.

Watoto wanaoishi kwenye kitongoji cha Mathare, Nairobi. Picha: @bwaya
Ingawa mfumo wa maisha ya sasa unatufanya tukose muda wa kuwa na mtoto mmoja moja kibinafsi na kuhusiana kwa karibu na moyo wake, bado huu ni wajibu wa msingi wa mzazi anayejitambua. Kwa kuelewa umuhimu wa mahusiano haya ya mwanzo, na kuchukulia malezi kwa uzito, tunaweza kabisa kujenga utaratibu wa kuwa na muda maalum kwa siku wa kumsikiliza mtoto mmoja moja. Hili likifanyika tangu mtoto anapozaliwa, huongeza uwezekano wa sisi wazazi kuaminika kwa watoto na hivyo kuwa na nafasi ya kujua yaliyoujaa moyo wa mtoto na kuchukua hatua stahiki kungali ni mapema. Je, tunafanya hivi? Tunawapa watoto wetu muda wa kufurahia mahusiano na sisi wazazi 'kibinafsi'?
Fikiria jambo hili. Ukiweza kutumia saa 1 tu kwa wiki, sawa na dakika zisizofika kumi kwa siku kuzungumza kirafiki na mwanao mmoja mmoja, wakati anapofikisha umri wa miaka 12/13 anapopevuka na kuanza kujiona mtu mzima, utakuwa umekaa na mwanao kwa siku 27 tu! Fikiria. Wakati mtoto anaondoka nyumbani kwenda shule ya bweni akapate ufunguo wa maisha utakuwa umekaa nae kwa takribani mwezi mmoja tu! Miaka mingine yote ulimwacha akihusiana na televisheni na watu wengine usiowajua!
Hivi kwa jinsi maisha yalivyobana namna hii, wazazi tunapata hata dakika hizo kumi kwa siku kukaa na wanetu na kuwasikiliza na kuwasiliana nao kirafiki ukiacha kuonya na kuadhibu? Wengine tunaishi Dar es Salaam kikazi, watoto wako kwa bibi yao! Si ajabu hatufanikiwi kuwa na influence yoyote kwa watoto. Wakianza kufanya vitu vyao, tunaishia kulalamika ‘watoto wa siku hizi wameharibika.'
Tuwe vile tunavyotaka watoto wawe
Mtoto hujifunza kwa kiasi kikubwa kupitia kile kinachofanywa na watu wake muhimu wanaomzunguka. Ni muhimu kufanya kile tunachotaka mtoto akifanye. Tuwe na tabia na imani tunazotaka kuzihamisha kwa mtoto. Mathalani, kama ninatamani mtoto awe msomaji wa vitabu, ni lazima nihakikishe ninajenga mazingira ya usomaji nyumbani kwa kuonesha mfano mimi mwenyewe. Mtoto anakua akijua maisha ni kusoma. Na sihitaji kumwandalia somo la ‘umuhimu wa kusoma vitabu’ ili ajenge tabia ya kusoma. Nafanya ninachotaka afanye. Aone nikifanya ibada kama ningependa awe mwombaji na yeye. Niwe na upendo kwake na mke wangu kama ninataka awe mtu wa upendo kwa watu.
Kadhalika, nikitaka atukane wenzake na siku nyingine anitukane na mimi kimoyomoyo, niwe na tabia ya kumtukana yeye na kumwambia maneno magumu. Nikinywa pombe mbele yake maana yake ninamwandaa kunywa pombe ukubwani hata kama ‘sijamfundisha’ kwa maneno. Maana mtoto hujifunza kwa wepesi kupitia yale ninayoyafanya mimi kama mzazi. Vinginevyo, nitakuwa na bahati ikiwa mwenendo wangu utamwuudhi kiasi cha kumfanya aamue kuasi tabia zangu. Na hapo si ni mpaka ajue ninachofanya hakifai kwa binadamu wa kawaida?
Tuwapende watoto, wajisikie kukubalika
Ninapompenda mtoto vile alivyo bila kujali alichokifanya ninamfanya aelewe maana ya upendo na aniamini. Simpendi ili nimdai tabia njema. Hapana. Nampenda hata anapokosea. Nampenda kwa sababu ni mwanangu apatie au akosee. Na wala si kumdekeza. Wakati mwingine tunakosea kama wazazi. Tunawapenda watoto kama malipo ya tabia njema. Na wakati mwingine hatufichi, tunawaambia waziwazi kuwa tutawapenda kama watafanya tulichowaagiza kukifanya. Tutawapa zawadi wakifanya vizuri. Conditions.
 Wanapokosea tunaonesha kuwachukia na wakati mwingine tunawatenga kihisia. Tunawakomoa watoto, eti! Hatuadhibu tabia zao, tunawaadhibu wenyewe. Hali hii huwafanya watoto wawe wanyonge na wajione hawakubaliki kama watu na mioyo yao hujisikia kubebeshwa deni na mzigo wa kutekeleza msukumo wa nje wasioona mantiki yake. Hakuna binadamu wa kawaida hufurahia shinikizo la namna hii na kwa kweli huwa ni vigumu sana mtoto wa jinsi hii kufundishika. Adhabu zitaongeza usugu.
Ni kweli kuna nyakati watoto huwa watundu na mzazi hulazimika kumfokea na kumwadhibu badala ya kufikiria kumjengea mtoto tabia anayoitaka. Lakini ni vyema tukaelewa kwamba adhabu na mashinikizo yasiyotanguliwa na upendo na mazingira ya kujenga tabia njema hayana matokeo chanya katika maisha ya mtoto.
Kiboko cha kweli anachokihitaji mtoto kujenga tabia njema ni upendo. Na wala kumpenda mtoto si kumdekeza kama tunavyoamini wazazi wengi tulikulia mazingira yaliyotindikiwa upendo. Hatukulelewa kwa upendo, tunahamishia magonjwa yetu kwa watoto. Samahani. Nilitaka kusema upendo halisi hujenga mazingira ya kupanda tabia zinazofaa bila kusubiri kuadhibu tabia zisizofaa zilizotokana na kunyimwa upendo.
Tushughulike na msongo wa nafsi zetu kwanza
Kazi ya kulea inahitaji nafsi iliyotulia. Nafsi isiyotafuta amani kwa kuumiza wengine. Ninapokuwa mzazi mwenye nafsi iliyosongwa na matatizo siwezi kutekeleza ipasavyo jukumu nyeti la malezi yatakayomjenga mtoto anayejitambua, anayejiamini na atakayekabiliana na changamoto za maisha ya ukubwani. Nitajikuta nikimtumia mtoto kama dodoki la kufyoza ugonjwa unaoisumbua nafsi yangu. Nitakuwa mwepesi, pasipo mimi kujua, kusema maneno magumu yasiyolingana na umri wa mtoto. Nitajisikia kuridhika kumfanya mtoto alie na kukosa amani. Nitaadhibu na kukemea kuliko ninavyowajibika kujenga imani, mitazamo na tabia njema.
Ni muhimu sisi kama wazazi kushughulika na matatizo ya nafasi zetu na kuhakikisha kwamba tunahusiana vyema na nafsi zetu ili tuweze kujitoa kuwalea watoto wetu katika njia iwapasayo. Tukishashughulika na nafasi zetu, kinachofuata ni kujiuliza, tungependa watoto wetu waweje watakapoanza kujitegemea kimaamuzi? Kitu gani tungependa kichipue kwenye mioyo yao kitakachoongoza maisha yao ya sasa nay a baadae? Maana upo ukweli kwamba malezi yanachangia kwa kiasi kikubwa tabia tunazoziishi ukubwani. Kama tunapenda kutumia fursa ya kuumba tabia njema kwa watoto wetu, hatuwezi kukwepa kufanya maamuzi ya kulichukulia suala hili la malezi kwa uzito unaostahili. Malezi si kazi inayoweza kufanywa na yeyote. Tuyape uzito unaostahili.

Sunday, November 16, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA KWA SALA HII!!!

Ee Mungu unifanya niwe chombo cha amani yako. Penye chuki nilete mapatano, penye kukata tamaa nilete matumaini, penye huzuni furaha, Amina
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!

Friday, November 14, 2014

TUMALIZE JUMA HILI NA WIMBO HUU UUTWAO WALEWALE NA CHAMELEONE!!!


NAMI NACHUKUA NAFASI HII NA KUSEMA MWISHO WA JUMA UWE  WA FURAHA NA AMANI PIA TUKUMBUKE KUSAIDIANA PALE INAPOTAKIWA. Haya tucheza pamoja basi:-)

Thursday, November 13, 2014

MCHEZO WA BAO!

Wakazi wa Tabora wanasifika kwa mchezo huu, kinachonifurahisha katika huu mchezo ni vile wanavyokuwa wanahesabu kete, na kujua wapi atakaposhinda na wapi atalala. picha na maelezo  kutoka hapa. Kuna siku niliuliza ili nipate kujua ni vipi kucheza hasa Mr. anapenda sana kujua alinituma nimuulizie lakini sikupata jibu.

Wednesday, November 12, 2014

SWALI LA LEO KUTOKA MAISHA NA MAFANIKIO A.K.A KAPULYA....

N imekuwa nikijiuliza kila siku na sijapata jibu, sasa leo nimeona niliweke  hapa kwani palipo na wengi hapaharibiki neno,   Ni hili hapa swali lenyewe:- Hivi kwa nini pilipili inamfanya/tufanya tupige chafya? Najua mtasema mbona kuna vingi vyatufanya kupiga chafya, lakini mimi naona pilipili ni zaidi.....naomba tujadili kwa kupamoja. JUMATANO NJEMA!!!

Monday, November 10, 2014

RUVUMA INAVUMA...HAPA NI RUHILA MBUGANI ...SONGEA

Nimeishi miaka mingi Songea nilikuwa sina habari kama kuna mbuga ya wanyama. Mbuga hii ipo nje kidogo ya Songea mjini Msamala . Kwa hiyo nasi tulipata bahati na kuingia hapa kwa msaada ya mwenyeji wetu ndugu Sunday Hebuka. Sijui hapo nafanya nini?Sunday, November 9, 2014

LEO NI SIKU YA AKINA BABA HAPA SWEDEN/FARS DAG.... NAMI NACHUKUA NAFASI HII NA .....

 Hapa ni baba watoto ...nao wameniomba nimpongeze baba yao kwa siku hii ya leo.
Nami nkaona si mbaya kama nami nikichukua nafasi hii na kumpongeza  baba yangu mzee Ngonyani ni huyo mwenye shati la rangi ya waridi. Na pia nawapongea akina baba wote hapa duniani kwa siku hii kwani bila wao tusingekuwapo na maisha hayangekuwa kama kawaida. NA MWISHO NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA SANA:-)

Friday, November 7, 2014

IJUMAA NJEMA KWA WOTE NA WIMBO HUU!! PENDO

IJUMAA NJEMA NA TUDUMISHE UPENDO

Thursday, November 6, 2014

HAPA NI SEHEMU FULANI AFRIKA/TANZANIA.....

Je wewe msomaji unajua hapa ni wapi katika Afrika yetu?
Kila la kheri panapo majaliwa tuonane tena wakati mwingine...kapulya mdadisi!

Monday, November 3, 2014

TUANZE JUMATATU HII NA MCHAKAMCHAKA...WIMBO

Unakumbuka wimbo huu....Idi Amin akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba....Au Alisema, Alisema, Alisema Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea sharti muanza mchakamchaka, chinja, au....Je wewe nawe kuna mwimbo wa mchaka mchaka uukumbukao?

Friday, October 31, 2014

IJUMAA NA JIONI NJEMA KWA WOTE...KARIBUNI NDIZI!!

Hakuna ndizi tamu kama hizi kule kwetu tunaziita "kaporota" ni tamu sana nazipenda mno. Je kuna ndizi nawe uzipendazo sana?

Tuesday, October 28, 2014

KUMBUKUMBU:- KWANZA NIMETAMANI UGALI WA MUHOGO!!!!

Hii kazi hii ilikuwa kazi ya karibu kila siku maana usipotwanga mihogo hakuna ugali...basi hapo unapomaliza kutwanga uso mzima ni kama vile umemwagiwa unga...Tulikuwa tukipaka usoni kama poda mweeeeee...kaaaazi kwelikweli. Nimekumbuka sana enzi zila na pia nimetamani ugali wa muhogo na kisamvu chake...si unajua hakitupwi kitu maganda ni chakula cha nguruwe  mmea mzuri sana huu

Sunday, October 26, 2014

Saturday, October 25, 2014

JUMAMOSI NJEMA .....NA KIBURUDISHO KIDOGO/UGIMBI!!!

Jamani wale wapenzi wa komoni/mnyakaya karibuni baba anawakaribisha hapa. ..Mimi naomba tongwa jamani haya mataputapu siyawezi. HAYA TUSISAHAU POMBE SI MAJI NA KUMBUKA UTAKUWA BARABARANI BASI USINYWE. :-)

Friday, October 24, 2014

UJUMBE WA IJUMAA HII KUTOKA KWA KAPULYA!!

Kitu kizuri huja kwa anayesubiri, lakini kitu kizuri zaidi huja kwa yule anayeomba  wakati akisubiri.
NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA SANA!!

Tuesday, October 21, 2014

TUSISAHAU MIZIKI YETU YA ASILI PIA LUGHA ZETU ZA ASILI ...


Leo tuangalie na kusikiliza ngoma hii ya asili na mwanadada  Saida Karoli kutoka kwa ndugu zetu huko Bukoba. Ebu angalia mavazi na jinsi walivyojiremba na pia vyombo vya mziki vya jadi na ngoma. Hakika inapendeza na inapaswa kujivunia utamaduni huu. PANAPO MAJALIWA TUTAANGALIA KWA UKARIBU MAKABILA MENGINE NA UTAMADUNI WAO!!

Sunday, October 19, 2014

SAMAHANI KWA TATIZO LILILOTOKEA KATIKA BLOG YETU YA MAISHA NA MAFANIKIO..ILA SASA NATUMAINI ITAKUWA SWALI...

Hodi, hodi! ndugu zanguni. Mwenzeni ipo ila tu semeni nilitekwa ...kwanza niliona tarehe 14/10 Dada Ester Ulaya /mama Alvin aliniambia dada kuna shida hapa Maisha na Mafanikio vipi? Nikashtuka halafu nikaangalia ni kweli lakini baadae tatizo likatoweka na nikaweza kublog kidogo. Sasa 16/10 nikatumiwa na ujumbe wa barua pepe na Pro. Mhango naye akawa anaiambia dada Yasinta vipi naona umeteka  maana nimejaribu kuingia nimeshindwa  fanya hima na utufungulie . Nikawa sasa najiuliza mwanadada mimi nitafanya nini hapa. Nimehangainga weeee bila mafanikio  naamaka  leo asubuhi nakutana na ujumbe mwingine toka kwa kaka yangu Salumu naye anasema vipi dada ?..Mmmhh hapa kajasho kakaanza kunitoka maana nilijua lile swala limetoka. Sasa hivyo nimerudi nyumbani na nimefungua hili kopo kwa woga ...nikamwomba msaada baba watoto naye kwa vile ni mtaalamu kidogo wa komputer inaonekana amefaulu kuutoa ule ujinga. Shukrani nyingi sana kwake. Ahsante...Tuwe makini kutoweka link ambazo hazina sababu. TUPO PAMOJA DAIMA. NAWASHUKURU SANA WOTE WALIOIONA SHIDA HII NA KUNIPA USHAURI MAPEMA.

Tuesday, October 14, 2014

HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII NI PICHA YA MWAKA!!!

Haki ya nane hii ni kibako ..nimewahi kusikia kuwa wanawake wanaweza kufanya shughuli zaidi ya moja kwa wakati mmoja....lakini hii kaaaazi kwelikweli. Sasa hapo sijui atapindaje kona?

Monday, October 13, 2014

KUADIMIKA...ILIKUWA SHIDA MTANDAONI!!

Napenda kuwaombeni radhi wasomaji wote wa Maisha na Mafanikio kwa kuadimika kwa siku hizi chache. Ni kwamba kulikuwa na shida ambayo sikujua ni nini. Haikuwezekana kuingia na kuweka kitu ila sasa naona nipo nanyi tena. SAMAHANI SANA!!

Friday, October 10, 2014

Wednesday, October 8, 2014

PALE UNAPOTAKA KUENEZA UTAMADUNI WAKO SI KAZI KUBWA...ANGALIA HAPA.....

ilikuwa kazi ndogo sana kuwasawishi ...Hawa ni ndio ninaoshida nao karibu kila siku katika mtindo wa kubeba maboxi. Nawatakieni wote JUMATANO NJEMA SANA. TUSISAHAU TULIKOTOKA:-) Kapulya.

Tuesday, October 7, 2014

WATU 325 WAPATA MAUMIVU BAADA YA KUNYWA TOGWA YENYE SUMU SONGEA VIJIJINI KATIKA KIJIJI CHA LITAPWASI!!!!

Wagonjwa wapatao 325 wakiendelea kupata tiba ya kutoa sumu waliyo kunywa kwenye Togwa katika kijiji cha Litapwasi Songea Vijijini. Kulikuwa na sherehe ya kipaimara. Hapa ni hospital Peramiho.

Monday, October 6, 2014

TUANZA WIKI NA PICHA HII:-MAPENDO!

Kuna wakati mtu ukipenda hakuna awezaye kusema kitu ..maana kupenda ni kupenda. Nawatakieni wote jumatatu njema.

Friday, October 3, 2014

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JANA JIKONI KWA KAPULYA YAANI MLO WAKE....IJUMAA NJEMA!!!

 
 Huu ulikuwa ni mlo wangu wajana  mchana supu ya mboga mboga..kama vile kabichi, karoti, nyanya, kitunguu bila mafuta.
Na hapa ni mlo wangu wa jana jioni samaki na saladi ya nyanya na spinachi  na kitunguu(kachumbali) hivyo ndivyo nilivyokula jana.TUKUTANE TANA PANAPO MAJALIWA:-)

Wednesday, October 1, 2014

CHAGU LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA WIKI HII:- SIO BWANA MATATA PEKE YAKE HAJUI KUSOMA ....

 Bwana Matata hana habari ya hatari amelala kwenye kibao kilichoandikwa hatari hajui kusoma
Sasa je? Na hawa wadada hawajui kusoma kama bwana matata au ndo kutojali tu?...Duh! yaani ....

Tuesday, September 30, 2014

KAMA MNATAKA MALI!!!!


Nadhani wengi hasa mlio na umri wangu mnakumbuka kitabu hiki au vitabu hivi ya TUJIFUNZE LUGHA YETU. Leo nimekumbuka shairi hili...haya fuatana nami......

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli, iwafae maishani.

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kweli kweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa, kifo kinanikabili,
Kama mwataka kauli, semeni niseme nini.

Yakawatoka kinywani, maneno yenye adili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani.

Baba aliye kufani, akalibi lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili yetu nyembamba, haijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa burianai, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuika kauli,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hata zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, usemi wakakubali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakawanunua ngómbe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mavazi na baiskeli,
Hawakuita pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Walikiweka kibao, wakaandika kauli,
KAMA MNATAKA MALI, MTAYAPATA SHAMBANI.
NA HAPA NI MWISHO....!!!!

Sunday, September 28, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA!!!

Hivi ndivyo nilivyoonekana jumapili ya leo baada tu ya kutoka kanisani kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kuniepusha na majaribu mengi na  mabaya. Napenda kuwaombea watu wote  wafu na wazima. UJUMBE WANGU WA LEO NI :- Kristo ni tumaini letu.

Saturday, September 27, 2014

ZILIPENDWA..NYUMBANI RUHUWIKO

Ilikuwa 2009 Ruhuwiko, tulifikiwa na wageni ambao ni watata viziwi toka shule ya watoto viziwi Ruhuwiko. Na siku hii kulikuwa na mvua kubwa sana na wote tukawa ndani . Bahati nzuri baraza ilikuwa kubwa sana... Ni viziwi lakini tulipata maswali mengi sana toka kwao...JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE

Wednesday, September 24, 2014

PICHA YA WIKI!!!

NAWATAKIENI WOTE SIKU NA MAJUKUMU MEMA ...KUMBUKA SISI SOTE NI NDUNGU!!

Monday, September 22, 2014

JUMATATU YA LEO INATUPELEKA MPAKA SOKONI SONGEA

Yaani hapa ni aina zote za ..kuanzia dagaa, samaki wadogo mpaka mbelele chagu lako tu...Mimi nimetamani zaidi dagaa tena wala madafu na  samaki aina ya mbelele. Kwa chakula ulichokua nacho ni ngumu kukisahau..HAYA NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA JUMA !!

Friday, September 19, 2014

KWA NINI SALOMON ALIKUWA NA WAKE 700?/Why Solomon had 700 wives?

 
Katika matembezi yangu nimekutana na habari hii, nimeipata Jamii Forum. Haya karibu......

Juzi nilipokwenda dukani kununua liwa kwa ajili yakurembesha uso wangu. Muuzaji alinifungia liwa hiyo kwenye kipande cha karatasi ambacho kilikuwa na habari inayomhusu Nabii Suleiman AS.Huyu nabii anaelezwa kwamba alikuwa na utajiri mkubwa usiyo kifani, lakini pia alikuwa na busara na hekima haijapata kutokea hapa duniani. Alikuwa na nguvu sana na utajiri wake ulikuwa ni mkubwa usioweza kupimika.Lakini pamoja na kujaaliwa neema zote hizo lakini vyote hivyo havikuwa na maana yoyote kwake.
Inasemekana alikuwa ni mwanaume shababi mwenye siha nzuri. Pamoja na kuwa na wake 700 na nyumba ndogo zipatazo 300, lakini kamwe hakuna na amani moyoni mwake.
Je ni kitu gani alikosa nabii huyu?
1. Wake warembo alikuwa nao 700
2. Nyumba ndogo zilizojaaliwa neema za Allah zilikuwa
3. Hekalu kubwa lenye kila aina ya nakshi vikiwemo vito vya thamani
4. Utajiri mkubwa usio na mfano ulikuwa mikononi mwake
Alikuwa ana uwezo wa kupata starehe zote alizozitaka hapa duniani zikiwepo pombe za kila aina huku akiwa amezungukwa na wanawake warembo wa kila sampuli waliojaaliwa neema za Allah……. Mh!
Unaweza kushangaa, Je ni kitu gani amekikosa mtu huyu?

Naam, hebu angalia maisha ya vijana wa kiume wa nyakati hizi.
Wanahangaika sana kutafuta fedha, wanajenga mahekalu,wananunua magari ya kifahari, wanaoa wake warembo, wanakuwa na uwezo wa kula starehe sana tena za kila aina, watatafuta nyumba ndogo zisizo na hesabu,lakini bado hawatatosheka.

Pamoja na habari hiyo ya nabii Suleiman ambayo wengi wetu tunaifahamu vyema, lakini bado vijana wa kiume wameshindwa kung’amua kwamba hivi vitu vya nje, yaani Fedha, na fahari zote za dunia si chochote, na kamwe haviwezi kutuletea amani na ridhiko hata siku moja katika maisha yetu.


Kama Nabii Suleiman hakupata ridhiko kwa amali alizojaaliwa na Mwenyenzi Mungu seuze wao!


Ni kuhangaika tu kusiko na mashiko na kamwe fedha,mahekalu na wanawake wanene wanene wenye makalio makubwa na matiti yenye kututumka vifuani na sura za kuvutia si mali kitu, havitawafaa hata kwa miaka dahari.

Mtafuteni Mungu atawaongoza, acheni michepuko,tulieni na wake zetu.
NACHUKUA NAFASI HII NA KUWATAKIENI MWISHO MWEMA WA WIKI....KAPULYA

Wednesday, September 17, 2014

MAMA MJASILIAMALI AKIWA AMEBABA ZAMBARAU ANAKWENDA KUUZA!!!

Maisha ni kuyakubali na mwisho wa siku utaona mafanikio yake. Ila ukisema unataka mafanikio ya haraka hakika sijui kama yapo. Nimependa kuona watu/huyu mama anavyojituma. Mafanikio ni kujituma. NAWTAKIENI WOTE JUMATANO NJEMA NA KUMBUKENI TUPO PAMOJA.

Tuesday, September 16, 2014

NIMEKUMBUKA SANA KWETU LUNDO/NYASA

 
Hapa ni samaki wapo kwenye mtungo ndo wanatoka tu kuvuliwa...nadhani ni vituhi, ukipata na ugali wa muhogo hapo halafu na tembele au kisamvu eeeehhh bwana we basi tu. Haya kila la kheri kwa wote!!!

Saturday, September 13, 2014

NIMETAMANI HII...UTAMADUNI OYEEEEE!!!

Huki kiatu/sandali nimekifia kabisas yaani nimekipenda mno nitatafuta tu mpaka nikipate...JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE!!

Friday, September 12, 2014

TUMALIZA WIKI KWA UJUMBE HUU UKIWA DUNIANI USIHUZUNIKE NA USIWE MNYONGE HATA KAMA UNA UMASKINI KIASI GANI!!!!

Ukiwa DUNIANI USIHUZUNIKE  na usiwe MNYONGE hata kama una UMASKINI kiasi gani, Mungu yuko pamoja nawe, na unatakiwa kizingatia haya;.

1. Usijilaumu kwa lolote lililokutokea.
2. Usihofu kuhusu hali uliyo nayo sasa.
3. Usijilinganishe na mtu yeyote duniani.
4. Usifikirie sana yaliyopita katika maisha yako
5. Kumbuka Mungu ndiye mpangaji wa kila linalokutokea.
6. Usiwaze sana kuhusu kesho waza kuhusu leo.
7. kukikosa ulicholikusudia yote ni mipango ya Mungu.
MUWE NA SIKU  PIA IJUMAA NJEMA NA MWISHO MWEMA WA JUMA.

Wednesday, September 10, 2014

NINA IMANI WENGI WETU TUNAKUMBUKA VIFAA HIVI....ZILIPENDWA-PICHA YA WIKI!!!

Bila redio kama hii ilikuwa hakuna kucheza disko,  bila pasi basi ni kuvaa shati la makunyanzi, bila kibatari/koroboi basi kulala kiza/giza na mwisho ni mpira huo ......

Monday, September 8, 2014

MWENZENU NIMETAMNI KWELI MLO HUU JIONI YA LEO...DUH MATE YANACHURUZIKA TU HAPA...

Sina jinsi nimebaki kutamani tu leo maana nimeishiwa unga ... halafu ebu angalia  hayo maharage mabichi ...ila inakosekana mboga majani maana mimi na mboga damudamu.....je wewe utakula nini jioni hii au sijui mchana  huu?

Saturday, September 6, 2014

UJUMBE TOKA MAISHA NA MAFANIKIO....

Nimeamka asubuhi hiii.... kama kawaida yangu huwa napitia barua pepe yangu...na leo nimekutana na ujumbe huu nimetumiwa na msomaji wa maisha na mafanikio. nikaona si mbaya nikiweka hapa ni kama ufuatavyo--------- karibu tujadili pamoja

Ni kwamba usipoteze muda  wako kuwa na watu/marafiki ambao hawana muda na wewe, yaani kila siku uwafuate wewe, kila siku ni wewe kuwapigia simu, kila siku ni wewe kuanzisha hadithi. Kama kweli wanakupenda na kukujali kama wasemavyo basi  watakutafuta, kwa vile wanajua wapi unapatikana, huna  haja ya kujipendekeza/kubembeleza, na wewe ni binadamu muhimu vilevile.
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA. TUPO PAMOJA

Thursday, September 4, 2014

VAZI LA LEO GAUNI : NAONA IWE PICHA YA WIKI!!!!

 Ukiwa mfupi kuna kila njia ya kuwa mrefu kwa mfano hapa kusimama kwenye kiti:-) ujanja eehhh . Halafu sijui madada huya anataka kuruka pia.
 Hapa afadhali mdada katulia
Tabasamu kwa mbali.
Gauni hili nimenunua:- Indiska
 

UJUMBE WA LEO kutoka kwa Rais Kikwete "TUTATOA ELIMU YA MSINGI, SEKONDARI BURE"


Katika pitapita zangu jana nikakutana na hii habari/ujumbe kama ni kweli kwa kweli ni habari nzuri sana. Nikaona si vibaya nami nikiiweka hapa Maisha na Mafanikio...Nimeipada hapa haya karibuni tujadili kwa pamoja.
 
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali inakusudia kufuta karo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za serikali, ili kutoa fursa kwa watoto kusoma bure kuanzia elimu ya msingi, ikiwa ni jitihada za kuinua elimu na kuwapunguzia mzigo wazazi.

“Zipo sababu za msingi zinazosababisha wanafunzi wengi wa shule za sekondari kukatisha masomo yao, ikiwamo wazazi wao kushindwa kulipia karo za shule kutokana na changamoto mbalimbali zikiwamo za umasikini” alisema.
Rais Kikwete alisema kufutwa kwa ada hiyo utekelezaji wake upo mbioni ili kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bure, hatua ambayo itasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini.

Tuesday, September 2, 2014

KAPULYA SI MPENZI WA SCALFU NA KULIMA BUSTANI TU HAPANA ANAPENDA MIKOBA PIA!!!

 Nimeupenda mno mkoba huu rangi yake na jinzi ulivyokaa kaaa
Huu nilinunua nilipokuwa Estonia nako kazuri....Je wewe msomaji unapenda kukusanya nini labda bangili ???au shati? au labda viatu?:-)

Monday, September 1, 2014

MLO WA JANA JIONI.....KARIBUNI!!!!

Hivi ndivyo mlo wetu wa jana ulivyokuwa:- Wali, nyama ya ngómbe na kabichi na hiyo ni sahani yangu kiteremshia ni maji

Saturday, August 30, 2014

PICHA YA WIKI...SEHEMU FULANI TANZANIA..JE? UNAJUA WAPI?

Nimeipenda hii picha na nimeiona iwe picha ya wiki hii haya sema kama unajua hapa ni wapi?:-) ni mimi Kapulya wenu:-)

Friday, August 29, 2014

NAPENDA KUWATAKIENI MWISHO MWEMA NA KIPANDE HIKI CHA MZIKI ........ASILI YA MZIKI


Hakuna mwanamziki ambaye alikuwa akimba na wengi wakimwelewa anasema nini. Katika nyumba hii Remmy anapendwa sana...kwa hiyo nimeona leo tumkumbuke/tumuenzi. MWISHO WA JUMA UWE MWEMA KWENU!!

Wednesday, August 27, 2014

MSIMU WA MAVUNO UMEFIKA /YAANI MWISHO WA BUSTANI KWA MWAKA HUU NA HAYA NDIYO BAADHI YA MATOKEO....!!!!

 viazi mviringo (sisi wangongo twasema matosani)
 Vitunguu saumu/swaumu
Na hapa ni vitunguu maji / au ni vitunguu vya kawaida
NAWATAKIENI SIKU NA KAZI NJEMA