Showing posts with label ubunifu. Show all posts
Showing posts with label ubunifu. Show all posts
Monday, May 9, 2016
JUMATATU HII TUANZE NA PICHA HII ....RAMANI YA AFRIKA KWA MTINDO HUU....
Ramani ya Afrika kwa kutumia Kahawa...nimependa ubunifu huu...ndani ya ungo sisi wangoni tunasema ungo...lupalu....NAWATAKIENI WOTE JUMATATU NJEMA. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!
Monday, May 4, 2015
NI JUMATATU YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TANO ...NA MAISHA NA MAFANIKIO INAANZA HIVI....
Hakuna kisichowezekana ... si unaona hapa . Ila mmhhh sijui huu ni ubunifu au? Nawatakieni wote jumatatu hii ya kwanza ya mwezi huu iwe njema:-) Kapulya.
Tuesday, March 31, 2015
TUMALIZE MWEZI HUU WA TATU NA PICHA HII:- NIMEPENDEZA EEHH!!
Ubonifu huo..hahaaa si unaona nilivyopendeza eeehh! Watoto ni wabunifu sana ..Mwisho wa mwezi uwe mwema kwa wote na kumbuka kesho usidanganywe..
Thursday, February 20, 2014
PICHA YA WIKI...UBUNIFU MWINGINE BWANA!!!
Ndiyo ni ubunifu mzuri....ila binafsi ningetumia mkaa au kuni maana hapa...itakuwaje. Swali linakuja je? kama hakuna umeme utafanyaje?... Na je? kutaliwa nyama tu?..:-) SIKU IWE NJEMA SANA KWA WOTE NA IKIWEZEKANA JARIBU UBUNIFU HUU ILA USIMWACHE MTOTO AJARIBU:-)
Monday, November 25, 2013
TUANZA JUMATATU HII NA SWALI HILI KUTOKA KWA KAKA BWAYA ...KUHUSU MAISHA NA FURAHA!!!
Kama mnakumbuka mwezi uliopita niliweka picha hii hapa kibarazani na baadaye kulitokea na maoni. Na baadhi ya maoni aliyotoa msomaji mmoja ambaye ni kaka Bwaya ambaye alikuwa ameadimika kwa muda mrefu na sasa yupo nasi tena. Nachukua nafasi hii kumkaribisha Kaka Bwaya......Haya na maoni yenyewe yalisomeka hivi;-
Bwayasaid...
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waishio katika maisha yanayoonekana kuwa duni, ndio wenye furaha zaidi. Mfano ni hawa. Swali: kwa nini? Naomba tusaidiane kujadili swali hili kwa pamoja....JUMATATU NJEMA!!!
Bwayasaid...
Thursday, October 31, 2013
BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMEONA TUUFUNGE MWEZI HUU WA KUMI KWA UBUNIFU WA MCHEZO HUU!!!
Napenda kuwatakieni wote mwisho wa mwezi huu wa kumi. Naamini umekuwa mwezi mzuri kwa wengi na kwa wale walikuwa na majukumu kupita kiasi basi nawaombeeni mwezi uanzao kesho uwe mzuri. NAWATAKIENI WOTE MWENZI MPYA WA KUMI NA MOJA UWE MZURI NA WENYE AMANI NA FURAHA. MWAPENDWA WOTE....KAPULYA
Friday, May 4, 2012
CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA PICHA YA WIKI :- JE? HUU NI UBUNIFU AU?
Nimetumiwa picha hii na msomaji wa Maisha na Mafanikio kwanza nikashikwa na butwaa, na pili nikajiuliza ni ubunifu? Na tatu nikajiuliza kukosa mtu wa kumtunza mtoto au chekechea? Nawaachia mwenzangu tusaidiana kujadili hapa...Duh! ila sidhali kama mtoto huyo anapata raha hapo.....MCHANA MWEMA MAJEMANI!!!
Friday, January 20, 2012
Friday, January 13, 2012
JE? KUNA TOFOUTI KATIKA PICHA HIZI MBILI?
Monday, November 22, 2010
MAONI YA MTAKATIFU SIMON KITURURU KUTOKA KWENYE MADA/PICHA YENYE KICHWA CHA HABARI:- NIMEUPENDA UBUNIFU HUU!!
Nimeyapenda maoni haya ambayo yanasemaukweki wa sasa na ule wa zamani. nakumbuka wakati nilipokuwa mdodo/kabinti nilikuwa nabeba kigunzi au kile kilixhokuwa kwenye mkungu wa ndizi kama mtoto. Zamani tulikuwa hatununuliwo vitu kama sasa. Ukitaka kujikumbusha ni picha gani basi bonyeza ubunifu. Ahsante sana Mt. Simon Kituiruru- Na hivi ndivyo alivyoanza mt. Simon:-
Si utani! Ubunifu ni muhimu!
Tatizo kiitwacho maendeleo kinafunda watu wengi tu kuwa ujanja ni kununua na ununuacho ghali zaidi ndio ushahidi wewe mjanja zaidi au tu Bab KUBWA kuliko ukiwa unatatua mambo mwenyewe kiubunifu wako mwenyewe.
Kwa mfano siku hizi BONGO(mijini) unakuta hata manati watoto wanataka wanunuliwe.
Ukilinganisha na enzi zetu ukipenda kuchezea magari unajitengenezea kwa waya au hata makopo na ikibidi unaiba ndala nyumbani ukachonge matairi ikiwa ni kutatua tu tatizo la kutaka kucheza gari kibunifu ambalo unajua Mzazi anaweza asikununulie.
Tunako kwenda sijui nini kitatokea kama ubunifu ni jinsi ya kununua na wapi pa kununua wakati mengi tu unaweza kubunia na kutatua mwenyewe.
Fikiria hata chakula kwenye menu za bongo ubunifu ni hafifu sana. Ni yale yale CHIPSI mayai, ugali kwa maharage na kadhalika... wakati kibano kilitakiwa kitengeneze ubunifu kama kibano cha uhaba wa chakula kilivyowaletea ubunifu wa PIZZA kwa Waitaliano masikini.
Nawaza tu kwa sauti!

Friday, November 19, 2010
NIMEUPENDA UBINIFU HUU!!!!
Friday, October 22, 2010
Swali:- Ni ubunifu au?
Tuesday, October 6, 2009
Nimekumbuka zamani wakati nasoma+ Ubunifu wa kutengeneza vihesabio!!!

1. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kusoma huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuandika huko shuleni pamoja na mwalimu.
2. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuhesabu huko shuleni pamoja na mwalimu.
Kuchora huko shuleni pamoja na mwalimu.
3. Kwaheri baba na mama twaenda shuleni x2
Kuimba huko shuleni pamoja na mwalimu.
Twaimba sote pamoja pamoja na mwalimu.
Sunday, April 19, 2009
JE? UMEGUNDUA HAPA NI NINI KATIKA PICHA HII?
Saturday, April 11, 2009
UBUNIFU WA MICHEZO +KUWAFURAHISHA WATOTO
Monday, April 6, 2009
Subscribe to:
Posts (Atom)