Friday, October 31, 2014

IJUMAA NA JIONI NJEMA KWA WOTE...KARIBUNI NDIZI!!

Hakuna ndizi tamu kama hizi kule kwetu tunaziita "kaporota" ni tamu sana nazipenda mno. Je kuna ndizi nawe uzipendazo sana?

Tuesday, October 28, 2014

KUMBUKUMBU:- KWANZA NIMETAMANI UGALI WA MUHOGO!!!!

Hii kazi hii ilikuwa kazi ya karibu kila siku maana usipotwanga mihogo hakuna ugali...basi hapo unapomaliza kutwanga uso mzima ni kama vile umemwagiwa unga...Tulikuwa tukipaka usoni kama poda mweeeeee...kaaaazi kwelikweli. Nimekumbuka sana enzi zila na pia nimetamani ugali wa muhogo na kisamvu chake...si unajua hakitupwi kitu maganda ni chakula cha nguruwe  mmea mzuri sana huu

Sunday, October 26, 2014

Saturday, October 25, 2014

JUMAMOSI NJEMA .....NA KIBURUDISHO KIDOGO/UGIMBI!!!

Jamani wale wapenzi wa komoni/mnyakaya karibuni baba anawakaribisha hapa. ..Mimi naomba tongwa jamani haya mataputapu siyawezi. HAYA TUSISAHAU POMBE SI MAJI NA KUMBUKA UTAKUWA BARABARANI BASI USINYWE. :-)

Friday, October 24, 2014

UJUMBE WA IJUMAA HII KUTOKA KWA KAPULYA!!

Kitu kizuri huja kwa anayesubiri, lakini kitu kizuri zaidi huja kwa yule anayeomba  wakati akisubiri.
NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA SANA!!

Tuesday, October 21, 2014

TUSISAHAU MIZIKI YETU YA ASILI PIA LUGHA ZETU ZA ASILI ...


Leo tuangalie na kusikiliza ngoma hii ya asili na mwanadada  Saida Karoli kutoka kwa ndugu zetu huko Bukoba. Ebu angalia mavazi na jinsi walivyojiremba na pia vyombo vya mziki vya jadi na ngoma. Hakika inapendeza na inapaswa kujivunia utamaduni huu. PANAPO MAJALIWA TUTAANGALIA KWA UKARIBU MAKABILA MENGINE NA UTAMADUNI WAO!!

Sunday, October 19, 2014

SAMAHANI KWA TATIZO LILILOTOKEA KATIKA BLOG YETU YA MAISHA NA MAFANIKIO..ILA SASA NATUMAINI ITAKUWA SWALI...

Hodi, hodi! ndugu zanguni. Mwenzeni ipo ila tu semeni nilitekwa ...kwanza niliona tarehe 14/10 Dada Ester Ulaya /mama Alvin aliniambia dada kuna shida hapa Maisha na Mafanikio vipi? Nikashtuka halafu nikaangalia ni kweli lakini baadae tatizo likatoweka na nikaweza kublog kidogo. Sasa 16/10 nikatumiwa na ujumbe wa barua pepe na Pro. Mhango naye akawa anaiambia dada Yasinta vipi naona umeteka  maana nimejaribu kuingia nimeshindwa  fanya hima na utufungulie . Nikawa sasa najiuliza mwanadada mimi nitafanya nini hapa. Nimehangainga weeee bila mafanikio  naamaka  leo asubuhi nakutana na ujumbe mwingine toka kwa kaka yangu Salumu naye anasema vipi dada ?..Mmmhh hapa kajasho kakaanza kunitoka maana nilijua lile swala limetoka. Sasa hivyo nimerudi nyumbani na nimefungua hili kopo kwa woga ...nikamwomba msaada baba watoto naye kwa vile ni mtaalamu kidogo wa komputer inaonekana amefaulu kuutoa ule ujinga. Shukrani nyingi sana kwake. Ahsante...Tuwe makini kutoweka link ambazo hazina sababu. TUPO PAMOJA DAIMA. NAWASHUKURU SANA WOTE WALIOIONA SHIDA HII NA KUNIPA USHAURI MAPEMA.

Tuesday, October 14, 2014

HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII NI PICHA YA MWAKA!!!

Haki ya nane hii ni kibako ..nimewahi kusikia kuwa wanawake wanaweza kufanya shughuli zaidi ya moja kwa wakati mmoja....lakini hii kaaaazi kwelikweli. Sasa hapo sijui atapindaje kona?

Monday, October 13, 2014

KUADIMIKA...ILIKUWA SHIDA MTANDAONI!!

Napenda kuwaombeni radhi wasomaji wote wa Maisha na Mafanikio kwa kuadimika kwa siku hizi chache. Ni kwamba kulikuwa na shida ambayo sikujua ni nini. Haikuwezekana kuingia na kuweka kitu ila sasa naona nipo nanyi tena. SAMAHANI SANA!!

Friday, October 10, 2014

Wednesday, October 8, 2014

PALE UNAPOTAKA KUENEZA UTAMADUNI WAKO SI KAZI KUBWA...ANGALIA HAPA.....

ilikuwa kazi ndogo sana kuwasawishi ...Hawa ni ndio ninaoshida nao karibu kila siku katika mtindo wa kubeba maboxi. Nawatakieni wote JUMATANO NJEMA SANA. TUSISAHAU TULIKOTOKA:-) Kapulya.

Tuesday, October 7, 2014

WATU 325 WAPATA MAUMIVU BAADA YA KUNYWA TOGWA YENYE SUMU SONGEA VIJIJINI KATIKA KIJIJI CHA LITAPWASI!!!!

Wagonjwa wapatao 325 wakiendelea kupata tiba ya kutoa sumu waliyo kunywa kwenye Togwa katika kijiji cha Litapwasi Songea Vijijini. Kulikuwa na sherehe ya kipaimara. Hapa ni hospital Peramiho.

Monday, October 6, 2014

TUANZA WIKI NA PICHA HII:-MAPENDO!

Kuna wakati mtu ukipenda hakuna awezaye kusema kitu ..maana kupenda ni kupenda. Nawatakieni wote jumatatu njema.

Friday, October 3, 2014

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JANA JIKONI KWA KAPULYA YAANI MLO WAKE....IJUMAA NJEMA!!!

 
 Huu ulikuwa ni mlo wangu wajana  mchana supu ya mboga mboga..kama vile kabichi, karoti, nyanya, kitunguu bila mafuta.
Na hapa ni mlo wangu wa jana jioni samaki na saladi ya nyanya na spinachi  na kitunguu(kachumbali) hivyo ndivyo nilivyokula jana.TUKUTANE TANA PANAPO MAJALIWA:-)

Wednesday, October 1, 2014

CHAGU LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA WIKI HII:- SIO BWANA MATATA PEKE YAKE HAJUI KUSOMA ....

 Bwana Matata hana habari ya hatari amelala kwenye kibao kilichoandikwa hatari hajui kusoma
Sasa je? Na hawa wadada hawajui kusoma kama bwana matata au ndo kutojali tu?...Duh! yaani ....