Saturday, February 28, 2015

TANZIA: MBUNGE WA MBINGA MAGHARIBI KAP. JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA...

Mbunge wa Mbinga na mjumbe wa Halmashauri kuu ta Taifa ya CCM Kapteni John Damian  Komba afariki dunia leo saa 10 jioni katika hospital ya TMJ Dar es salaam kwa tatizo la kisukari. Marehemu asterehe kwa amani Bwana ametoa  bwana ametwaa  jina lake lihidimiwe. Amina

Thursday, February 26, 2015

MWONEKANO MPYA WA DADA MKUU AKA KAPULYA

Jinsi uzee unavyokaribia na ndivyo macho nayo yanazidi kufifia :-) SIKU NJEMA KWA WOTE.

Wednesday, February 25, 2015

MTWA MPYA WA WAHEHE NA HISTORIA YA MAREHEMU ABDUL MKWAWA

 


Adam Abdul Sapi (13) ametawazwa kuwa Chifu mpya wa Wahehe, akirithi nafasi ya baba yake, Abdul Sapi Mkwawa (66) aliyefariki Februari 14, 2015 na kuzikwa katika kijiji cha Kalenga, nje kidogo ya mji wa Iringa ndani ya makumbusho yaliyowekwa fuvu la babu yake, Chifu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga Mkwawa.
Kabla ya kifo chake kilichosababishwa na maradhi ya sukari na figo, Abdul Sapi Mkwawa aliyekuwa mtoto wa tatu wa Spika wa kwanza mweusi nchini, Adam Sapi Mkwawa, alikuwa akifanyakazi katika kiwanda cha maji Afrika cha Kidamali, Iringa.
Amewahi pia kufanyakazi katika Chama cha Wazalishaji Tumbaku Iringa na Shirika la Elimu Supplies.
Alizaliwa Mei 4, 1949 katika kijiji cha Kalenga na kupata elimu ya msingi katika shule za Kalenga na Tosamaganga kati ya mwaka 1956 na 1963.
Mwaka 1964 hadi 1970 alijiunga na shule ya sekondari Iyunga na Mkwawa, ambako alipata elimu ya kawaida na ya juu ya sekondari kabla ya kujiunga na elimu ya juu ya biashara na utawala 1971 hadi 1973.
Mmoja wa ndugu wa marehemu, Hussein Sapi alisema mpaka umauti unamkuta, Abdul Sapi Mkwawa alikuwa Mtwa (Chifu); alisimikwa mwaka 1999 baada ya kifo cha baba yake, Adam Sapi Mkwawa aliyefariki Juni 25, 1999.
Kabla ya maziko ya Chifu huyo, wazee wa kabila la Wahehe walimsimika Adam ambaye ni mtoto wake wa tano, kuwa Chifu mpya wa kabila hilo.
Hata hivyo, mtoto huyo aliyeko darasa la Saba katika shule ya msingi ya Highlands ya mjini Iringa, atalazimika kusubiri kufanya shughuli za kichifu mpaka atakapotimiza umri wa miaka 20. Badala yake, mdogo wa marehemu, Saleh ndiye atakayeshikilia wadhifa huo mpaka Adam atakapofikisha umri huo.
TUONANE TENA PANAPO MAJALIWA:- Kapulya/dada mkuu.
 

TUANZE JUMATANO HII NA UJUMBE HUU KUTOKA KWA MJOMBA WETU MRISHO MPOTO!!!

JUMATANO IWE NJEMA SANA KWA WOTE.

Monday, February 23, 2015

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO YATIMIZA MIAKA SABA /7 LEO :-Mmmmhh! Miaka saba leo imefika kama mchezo!!!!

Hapa nipo nyumbani Songea/Ruhuwiko katika shughuli za kuandaa madikodiko nikiwa na wifi yangu tukisaidiana  na pembeni ni kakangu mdogo. Ilikuwa inakaribia mwaka mpya 2015.
Blog ya Maisha na Mafanikio kama mchezo leo yatimiza miaka saba (7) kamili. Napenda kuchukua nafasi hii na kusema:- Hii yote ni kutokana na uwepo wenu ulioambatana na upendo pia ushirikiano mzuri mlio nao. Na kubwa zaidi ni kwa familia yangu kwa kuwa bega kwa bega nami. Pia napenda kusema kwa kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kijifunza mambo mengi sana. Na ndiyo kwa sababa hii napenda kusema:- AHSANTENI SANA KWA USHIRIKIANO WENU NASEMA TENA KWANI NAAMINI BILA NINYI, NISINGEFIKA HAPA NILIPO LEO. KWA KWELI NAAMINI KUWA SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. UPENDO NA UMOJA WETU UDUMU DAIMA NA PIA MILELE!!!!!.......... HAYA JUMATATU IWE NJEMA SANA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA NA WENGINE WOTE.

NIMEONA SI MBAYA TUKIMALIZIA NA BURUDANI KIDOGO YA KIODA/CHIYODA KUTOKA KWA NDUGU ZETU HUKO KIJIJINI MANDA.... KARIBUNI

TUPO PAMOJA DAIMA...KAPULYA/DADAMKUU.

Sunday, February 22, 2015

NI JUMAPILI YA KWANZA YA KWARESMA:-JUMAPILI NJEMA! UJUMBE WANGU.....

Usimfanyia mwenzio jambo ambalo ukifanyiwa wewe litakuumiza!
JUMAPILI NJEMA!!

Friday, February 20, 2015

KARIBU CHAKULA CHA MCHANA ILA MJE NA MBOGA!!!

Maana mie mwenzenu nakula bila mboga wangono wanasema ("ugali wa kisuma")  au umewahi kula ugali na maji yaliyowekwa chumvi tu...
BASI NIWATAKIENI SIKU NJEMA NA TUONANE TENA PANOAPO MAJALIWA!!

Thursday, February 19, 2015

TASWIRA:- SEHEMU FULANI AFRIKA

Alhamis njema kwa wote...pabapo majaliwa tutaobana kesho ijumaa!!

Wednesday, February 18, 2015

Kitabu Kipya cha NYUMA YA PAZIA KIMETOKA!

Nyuma Ya Pazia
Thursday 12 February 2015, author(s)-editor(s) Nkwazi Nkuzi Mhango
Nyuma Ya Pazia inazungumzia ubadhirifu unaomhusisha rais na mawaziri wake katika nchi ya Mafuriko au Abracadabra. Rais akishirikiana na waziri mkuu walileta kampuni ya kigeni ya kuua wadudu ya Richmen kuwekeza kwenye kuzalisha umeme nchini Mafurikony; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Kupitia rushwa na ushawishi wa wakubwa hawa Richmen ilipata tenda na kutumika kama mrija wa kuibia mabilioni ya fedha za umma toka Benki Kuu. Wananchi walipogundua jinai hii waliiangusha serikali na kuwaaadhibu watawala wao kwa kuwafunga maisha na wengine kuhukumiwa vifo. Kitabu kinaupiga kijembe tawala fisadi barani Afrika.
Nyuma Ya Pazia or Behind the Curtain is about corruption involving the president, and his ministers who rob the country of Mafuriko or Abracadabra. President in conjunction with his Premier brought fake foreign insecticide company; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Through logrolling Richmen lands a very lucrative tender used as a conduit of stealing millions from the Central Bank. Richmen is used to syphon billions of dollars from the treasury. When people get wind of this theft, force the government to crumble thereby rulers are punished by being jailed or other being sentenced to death. The book satirizes African kleptocratic regimes.
Purchase on African Books Collective
Purchase AMAZON
ISBN 9789956792184 | 254 pages | 203 x 127mm | 2015 | Langaa RPCIG, Cameroon | Paperback

Tuesday, February 17, 2015

HILI NI CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KUWA HII NI PICHA YA WIKI!!!

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE SIKU HII YA JUMANNE IWE NJEMA NA PIA TUWE WAANGALIFU JINSI YA KUTUMIA MANENO KWA WATOTO WETU!!

Saturday, February 14, 2015

NAPENDA KUWATAKIENI HII SIKU YA WAPENDANAO IWE NJEMA NA YENYE AMANI.

 NAPENDA KUWATAKIENI WOTE SIKU HII YA WAPENDANAO IWE YENYE AMANI.
HUU ULIKUWA MLO WANGU WA JANA JIONI PILAU, KACHUMBALI HAKUKOSA...JUMAMOSI NJEMA.

Friday, February 13, 2015

SWALI LETU LA IJUMAA YA LEO!!!

Swali letu la lau ni kama lifuatavyo:- Kwa nini wanawake wanaishi maisha mazuri, marefu na yenye amani ukilinganisha na wanauma?
NAWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA IJUMAA/MWISHO MWISHO MWEMA WA JUMA!!

Wednesday, February 11, 2015

TUDUMISHE UASILI WETU/UTAMADUNI WETU!!!

 Mdada akichunja pombe ya asili, na hivyo ndivyo walivyofanya hapo kale na pia kuna baadhi ya sehemu Afrika bado inafanyika  hivyo
Na hapa ni nyumba ya asili huko Afrika ya kusini/ hasa kwa kabila la kizulu. Ambao inasemekana ni wanaukoo na wangoni.
Na hapa ni nyumba ya asili ya wangoni iliyopo Songea  pale Makumbusho ya Mashujua 

Tuesday, February 10, 2015

TUWE MAKINI TUTUMIAPO VINYWAJI MAANA KUNA WENGI WANAPENDA!!!

Hii inanikumbusha siku moja  tulikuwa na sherehe na katika shamrashamra  basi kaka mmoja akawa amechukua bia yake  na kunywa kumbe mende walikuwa wamemwahi. Na pia mwingine aliingingiliwa na nyuki akamuuma mdomoni na kuvimba vibaya mno. Kwa hiyo ndugu zangu tuwe makini. Tutaonana tena panapo majaliwa...Kapulya!!

Friday, February 6, 2015

IJUMAA YA LEO TURUDI TENA ZANZIBAR !!!

Nilimwuuliza aliyetuongoza (guide) kama ningeweza kutumbukia humo shimoni na kupigwa picha. Lakini alisema hairuhusiwi. Hakika ndugu zetu waliteswa sana halafu mbaya zaidi hawakuwa wanaume tu hata wanawake pia watoto. Niwachekeshe kitu  huyu guide weyu alikuwa na vichekesho mno akaniambia nami nilionekamna kama mmoja wao:-)  IJUMAA NJEMA! 

Thursday, February 5, 2015

SOMO LA ALHAMIS HII:- TUSISAHAU USAFI WA KUCHA ZETU

Kucha ni kitu cha msingi sana na kutakiwa kuwa safi wakati wote sababu mikono yetu hutumika mara nyingi mfano mapishi, kufua, kuosha vyombo n.k. Usafi wa kucha zetu ni muhimu kwetu wanawake lakini tujue tuna jukumu la kuhakikisha waume zetu, wapenzi zetu na hata watoto wetu wawe wasafi kwa kucha zao (Mikono na Miguu)
------------------------------------------------------------------------------
Wanawake na hata Wanaume wanashauriwa kuzingatia usafi wa kucha zao, kwani kucha inapokuwa safi inamfanya muhusika kuwa na mvuto na mwenye kupendeza.Wanawake wengi na hata Wanaume pia wanaume hupenda kutunza kucha zao, kwani hujikuta wakikutana na vikwazo vya kushindwa kukabiliana na matatizo ya kukatika kwa kucha zao, kutokana na kusahau masuala kadhaa muhimu wanayopaswa kuzingatia ili kuzipa kucha uimara na afya njema pia.
Kwanza kabisa ni marufuku mtu kula kucha zake kwani nasema hivyo kwa sababu wapo baadhi ya watu ambao hupenda kula kucha zao, hivyo husababisha kuzikata bila mpangilio maalumu na wakati mwingine husababisha vidonda kwani hula mpaka nyama zinazogusana na kucha.
Tumia glovsi au hata mfuko wa plastiki unaposhika vitu vyenye kemikali, kwani vinaweza kuharibu kucha zako kama dawa za nywele.
Dawa hizi za nywele ni kali sana hivyo huleta madhara makubwa endapo itashikwa bila kizuizi chochote na kusababisha rangi hiyo kushindwa kukaa vizuri.
Safisha kucha zako mara kwa mara kwa kutumia vifaa maalum wanashauri kusafisha kucha zako kwa kutumia maji ya uvuguvugu.
Usitumia kucha zako kukwangulia vitu vigumu, kuparua au kuzolea uchafu. Kwani watu wengi hupenda kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha zao, hii husababisha kucha zako kukatika vibaya na kuwa na uchafu mweusi usiopendeza.
Usitoe ovyo vinyama vinavyojitokeza pembeni mwa kucha kwani vipo vifaa maalum vya kutolea vinyama hivyo, unashauriwa kutumia vifaa hivyo ili kuziwezesha kucha zako kupumua pamoja na kukuwa vizuri.
Paka rangi kucha zako mara kwa mara kwani wakati mwingine unashauriwa kumechisha rangi ya kucha zako na baadhi ya rangi ya nguo utakazovaa.
Tumia dawa maalumu ya kutoa rangi maarufu kama remover, badala ya kutoa rangi hiyo kwa kiwembe au kitu chenye makali.

Tuesday, February 3, 2015

JUMANNE YA LEO TUANZE NA:- HADITHI YA WAPENDANAO!!!

Katika pitapita zangu nikakutana na hadithi hii na nimeona si vibaya kama nikiweka hapa ili wengi tupata faida...karibu
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Mdada mmoja alitaka kujua anapendwa kiasi gani na mumewe. Hivyo akataka kujua mumewe atafanya nini endapo ataamua kuondoka na kumuacha. Mwanamke akaamua kuandika barua inayosema"Samahani mume wangu nimeamua kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya mbali na wewe. Barua akaiweka juu ya meza iliyochumbani .Baadae jioni, muda wa mumewe kurudi akajificha chini ya uvungu wa kitanda chumbani. Mume alipoingia chumbani akakuta ile barua juu ya meza, akaisoma kisha akaandika maneno fulani kwenye ile ile barua, halafu akaanza kuimbaimba kwa furaha huku akipiga miluzi na akiwa anavua nguo. Akapiga simu na akasikika akisema"Mpenzi nina furaha sana leo ..yule mwanamke nuksi amesalenda mwenyewe kaondoka na kutuachia uwanja, jiandae nakuja "Muda huohuo akaondoka. Mwanamke alipotoka uvunguni alikuwa amenyong'onyea na ameloa mashavu kwa machozi, akasogea pale ilipo barua na kutaka kujua mumewe kaandika nini. Akakuta maneno haya. "Nimeona miguu yako uvunguni, tafadhali andaa chakula nina njaa sana mumeo, ila nimetoka kidogo nafuata maziwa nilisahau kupitia. NAKUPENDA SANA MKE WANGU".......

Monday, February 2, 2015

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO INAPENDA KUMPONGEZA KAKA SAMWEL MBOGO "SAM" KWA KUFANYA GRADUATION

Ilikuwa ijumaa tarehe 30/1/2015, Ndugu kaka yetu Samwel Mbogo wengi tunamfahamu kwa jina la kaka S au Sam. Alifanya graduation yake katika kanisa CENTERBURY CRISTIAN CHURCH CATHEDRAL university (CCCU  huko London. Amepata Master degree ya phychotherapy. Ni Arts Therapy. NAMI NAPENDA KUTANGULIA KUMPA HONGERA SANA . 

Sunday, February 1, 2015

NI JUMAPILI NYINGINE TENA YA MWEZI MPYA...DAWA YA KUSAMEHE NI UPENDO!!


JUMAPILI NJEMA!  UJUMBE TOKA KWA KAPULYA:- TUDUMISHE UPENDO NA TUWE WEPESI KUSAMEHEANA!