Wednesday, February 18, 2015

Kitabu Kipya cha NYUMA YA PAZIA KIMETOKA!

Nyuma Ya Pazia
Thursday 12 February 2015, author(s)-editor(s) Nkwazi Nkuzi Mhango
Nyuma Ya Pazia inazungumzia ubadhirifu unaomhusisha rais na mawaziri wake katika nchi ya Mafuriko au Abracadabra. Rais akishirikiana na waziri mkuu walileta kampuni ya kigeni ya kuua wadudu ya Richmen kuwekeza kwenye kuzalisha umeme nchini Mafurikony; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Kupitia rushwa na ushawishi wa wakubwa hawa Richmen ilipata tenda na kutumika kama mrija wa kuibia mabilioni ya fedha za umma toka Benki Kuu. Wananchi walipogundua jinai hii waliiangusha serikali na kuwaaadhibu watawala wao kwa kuwafunga maisha na wengine kuhukumiwa vifo. Kitabu kinaupiga kijembe tawala fisadi barani Afrika.
Nyuma Ya Pazia or Behind the Curtain is about corruption involving the president, and his ministers who rob the country of Mafuriko or Abracadabra. President in conjunction with his Premier brought fake foreign insecticide company; Richmen to invest in power generation in Mafuriko. Through logrolling Richmen lands a very lucrative tender used as a conduit of stealing millions from the Central Bank. Richmen is used to syphon billions of dollars from the treasury. When people get wind of this theft, force the government to crumble thereby rulers are punished by being jailed or other being sentenced to death. The book satirizes African kleptocratic regimes.
Purchase on African Books Collective
Purchase AMAZON
ISBN 9789956792184 | 254 pages | 203 x 127mm | 2015 | Langaa RPCIG, Cameroon | Paperback

15 comments:

Anonymous said...

Hii inafanana na kisa cha Escrow/Richmond. By Salumu.

NN Mhango said...

Da Yasinta asante kwa kunitoa kimasomaso. Ni bahati mbaya kuwa "wapenzi" wa vitabu wenye blog "wamekishit" kiasi cha kutokitoa kama ulivyofanya kana kwamba si habari. Hata hivyo, hakuna tatizo.Kupanga ni kuchagua. Habari njema ni kwamba kingine cha Souls On Sale kipo jikoni. Habari mbaya ni kwamba kile cha watoto cha Safari Mbugani tulichotunga na mke wangu Nesaa, kilichokuwa kimeishapata ISBN number tumekiondoa kwa mchapishaji baada ya kuona anataka kukikalia kama Nyuma ya Pazia. Kiko kinatafsiriwa ili tukichapishe nje kwa ajili ya soko la nje pia.Nakushukuru sana dada yangu japo wabongo wengi si wapenzi wa vitabu. Hiki ni kitabu cha pili baada ya SAA YA UKOMBOZI iliyotoka miaka mitano nyuma. Kimechapishwa Cameroon baada ya wachapishaji wangu wa Saa ya Ukombozi kukilia kwa muda mrefu. Maana kilipaswa kutoka mwaka 2005 lakini kikatoka 2009 mwishoni. Unaweza kuamini kuwa niliandika Nyuma ya Pazia mwaka 2006? Unaweza kuona kilivyocheleweshwa. Ninacho kingine cha Kwetu ni Wapi nilichokitunga mwaka 1988 na hadi sasa hakijawahi kupata mchapishaji. Hata hivyo, ya Mungu mengi lisilowezekana kwa binadamu kwake lawezekana.

Mbele said...

Ndugu Mhango, hongera kwa kuchapisha kitabu kingine.

Dada Yasinta, shukrani kwa taarifa. Binafsi, sikujua, hasa kutokana na matatizo ya afya, ambayo yamefanya ufuatiliaji wangu wa hizi blogu kulegalega.

Ndugu Mhango, kuhusu hizi blogu, ni chache sana ambazo zinaandika habari za vitabu. Ni suala pana, lenye vipengele vingi.

NN Mhango said...

Kaka Mbele nashukuru kwa hongera zako. Kumbe bado unaumwa? Huwa napita kwako na kusoma machache unayojaliwa kuyaweka. Tangu tuwasiliane wakati ule nilidhani ulipona kumbe bado. Inshallah Mungu atakuafu upone urejee ulingoni kama zamani. Ndugu yetu Matondo alitoweka kiasi cha wengine kumkatia tama. Kaka mbele ungekuwa si mgonjwa huenda kuna siku ningekutumia sura chache toka kwenye kitabu cha kiada ninachoandaa dhidi ya grand au tuseme metanarrative.
Najua kuwa blog ni chache zinazoweza kushabikia vitabu. Ndiyo maana ukiangalia kwenye kijembe changu nimeweka alama za funga na fungua semi nikilenga ujumbe uwafikie. Ni kweli. Sikutegemea blog za mapicha bila uchambuzi wa mwenye blog mwenyewe kushabikia vitabu. Nilijua fika kuwa blog nyingi za kibongo si zote ni za wapiga picha ambao sijui kama wanafahamu maana ya kuandika ni nini. Na wachache wanaojaribu utaona wanavyoandika mdomdo.
Nimshukuru tena da Yasinta kwa kunitoa kimasomaso.

Mbele said...

Ndugu Mhango, niko katika kupona, na nimesharuhusiwa na madaktari kuendelea na ufundishaji. Ninafundisha kozi mbili muhula huu, badala ya tatu, ila inategemewa kuwa nitafundisha tatu muhula utakaoanza Septemba.

Watu walioenda shule na hawapedi vitabu nawashangaa, na hao ni pamoja na wengi wa hao vilaza wanaoitwa viongozi. Wale ambao hawapendi vitabu sababu ya umbumbumbu huwa nawaonea huruma.

Lakini mtu anayejua thamani ya vitabu anabaki daima ngangari katika kusaka elimu na faida zinginezo zitokanazo na vitabu.

Kila la heri. Na kwa Dada Yasinta, nasema endelea kusukuma hili gurudumu.

NN Mhango said...

Kaka Mbele
Nimefurahi kusikia kuwa unaendelea vizuri. Insh'Allah upone haraka na kuendelea na shughuli zako za uelimishaji jamii. Umesema vyema. Tunatawaliwa na vilaza na vihiyo wasiofikiri sawa sawa kiasi cha taifa letu kugeuka kichekesho na shamba la bibi. Watapendaje vitabu wakati hawasomi wala kuandika. Nyerere aliandika na kutufanya tupende vitabu na kuwa kama tulivyo. Hivyo, hawa si wa kusikitia tu bali kulaaniwa kwa jinsi wanavyoharibu nchi yetu. Nakumbuka usemi wako kuwa kuandika kitabu si kuwa tajiri bali kujaribu kueleza unavyoyaona mambo ili watu wafaidike na kile unachojua. Mtunzi, kimsingi, si mchoyo wala mwoga wa kukosolewa hata kulaumiwa. Kuna watu wamekwenda shule hadi vyuo lakini hawakuelimika, na hawa ni wengi kuliko walioelimika vilivyo. Ukinunua kitabu watu wanakucheka. Ukisafirisha kontena na vitabu toka ughaibuni kwenda nyumbani badala ya magari na upuuzi mwingine wanakuona hamnazo. Ndiyo binadamu tulivyo. Wauza unga na mafisadi wanaabudiwa ukiachia mbali wabangaizaji kwa vile wanapata fedha ya haraka inayoishia kuwa mauti yao na ya wengine.
Kila la heri upone haraka kaka.

Mbele said...

Ndugu Mhango, mimi yalinipata hayo unayosema. Nilikuwa masomoni katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison kuanzia miaka ya 1980-86, nikafanya juhudi sana kujipatia elimu na pia nikanunua vitabu vingi sana ili wakati wa kurejea tena kazini kwangu pale Chuo Kikuu cha Dar, niwe na zana za kufundishia kwa kiwango cha juu.

Niliporejea nchini na shehena yangu ya vitabu, watu waliniuliza "pick up" yangu iko wapi, au gari liko wapi. Walipoona sijaleta hiyo "pick up" ay gari, waliniona nimechemsha.

Upuuzi huu wa jamii ya ki-Tanzania wa kutothamini elimu na upuuzi mwingine mwingi, niliuvumilia kwa miaka mitano na hatimaye ulichangia mimi kuja na kufundisha hapa Marekani, mwaka 1991, ambapo nimeridhika kabisa kwa sababu hapa wanathamini elimu na utaalam wa mtu, hata kama unatembelea baiskeli au unapekua kwa mguu.

Kama unavyosema, Tanzania hatuna uongozi ufaao, ambao ungeonyesha njia na mfano katika masuala haya ya elimu kama alivyofaya Mwalimu Nyerere.

Yasinta Ngonyani said...

Kusoma vitabu au kuandika vitabu nadhani ni wito kwa hiyo hapa tukubaliane tu kwamba watanzania wote hawana wito wa kusoma/kuandika. Ni bahati mbaya kwetu kwani tunakosa mambo mengi sana na nashangaaaa kwa nini huwa tunapenda kuiga mabo mengi sana lakini si kusoma au kuandika???

NN Mhango said...

Da Yasinta sina la kujibu. Kuandika vitabu ni kujali kufanya hivyo. Ni kuwa na mawazo. Ni kweli wengi wanapenda kuiga upuuzi badala ya mambo ya maana. Nangoja kusoma kitabu chako cha kingoni dada.

Yasinta Ngonyani said...

Utaweza kweli kusoma kingoni???

NN Mhango said...

Kwani kingoni kinaandikwa kwa mawe au moto. We andika tu tena nitakitafsiri kwa kiingereza na kimakonde.

Yasinta Ngonyani said...

Haya mlongo wangu yatiniyandika koto kuganda chivili mujiku!:-)

NN Mhango said...

Hii nitaitafsri kesho.
Zikomo kwa mbiri

Yasinta Ngonyani said...

Kwanini sio leo?
haya zikomo!!

NN Mhango said...

Subira yavuta heri. Kitabu chenyewe hujatunga nitatafsiri nini dada yangu?