Kama huwezi kujisamehe mwenyewe na uliyoyafanya, utawezaje kuwasamehe wengine?
NAWATAKIENI WOTE JUMANNE NJEMA SANA NA KUMBUKENI TUPO PAMOJA DAIMA!!!Kapulya!
Showing posts with label afrika nyumbani. Show all posts
Showing posts with label afrika nyumbani. Show all posts
Tuesday, September 17, 2013
Wednesday, October 31, 2012
TUTEREMKE KIDOGO MPAKA SONGEA MJINI SASA:- TATIZO LA MAJI NA PIA MAFUTA KUADIMIKA!!!
Tatizo la maji Songea mjini, ndoa moja ya maji shilingi 500....
Thursday, November 3, 2011
Kijiji cha Lilondo wilayani Songea mkoani Ruvuma kinaoongoza kwa kuwa na ndizi nyingi
Leo mwenzenu nimekumbuka kweli enzi zili wakati naishi Matetereka. Kijiji hiki na kijiji jirani cha Lilondo kuna ndizi za aina mbalimbali. Wakati ule bei yake ilikuwa ndizi tatu shilingi tano. Halafu watu wa Matetereka pia Lilondo ni wakarimu sana. Licha ya ndizi, kuna magimbi si mchezo, karanga, mahindi, maharagwe, kahawa bila kusahau kinywaji cha ulanzi pia. Halafu kulikuwa na watu walikuwa wakipisha nyama pori...nimeyatamani sana maisha haya... Mtani Fadhy upoooo maana najua hapa vyakula hivi umekua nanyo:-)
Thursday, October 20, 2011
KATIKA KUWAZA NIPIKE NINI JIONI HII? GHAFLA NIKAJIKUTA NATAMANI KWELI CHAKULA HIKI...
..ugali na kumbikumbi/mbulika ambacho mara ya mwisho nilikula 2009 nilipokuwa Lundo kando ya ziwa Nyasa . Mwaka huu nilipokuwa nyumbani msimu ulikuwa si mwenyewe. Pia nimetamani kweli ugali na LIKUNGU sijui wangapi mmewahi kula au tu kujua/kuona ? Likungu ni mboga, ni "wadudu/aina ya kama mbu". Huwa wanajitokeza ziwani na watu wanawakamata na kuwakanda kama vile unakanda unga wa mkateau maandazi pamoja na chumvi na pilipili na baadaye wanachoma ili kuhifadhi au unaweza kukanda na chumvi na pilipili na kuchemsha na kulamoja kwa moja. Bahati mbaya sina picha ya LIKUNGU. Ila rangi yake ni nyeusi. Kweli nyumbani kuna vyakula vingi vya asili na vitamu...Sijui sasa nipike nini? maana kupata vyakula hivi hapa itakuwa ngoma ..unga ninao ila...Ushauri jamani?Tuesday, October 11, 2011
Subscribe to:
Comments (Atom)