Tuesday, September 30, 2008

KAZI+USAFIRI NA KUJITEGEMEA

Bila kuvuka hapa basi hafiki nyumbani ,ila ningekuwa mimi sijui kwani nahisi kuna mamba hapa.
Kusafirisha cementi kwa mkokoteni. Umoja ni nguvu unyonge ni uzaifu. Kwani angalia wanavyoshiriana hivi ndivyo inavyotakiwa watu wote wawe.


Hapa ni mto Ruhuhu, Kufika ktika kijiji cha Lituhi ni lazima wavuke hapa na hapo wanasafirisha cementi mifuko 216. Watu wana imani sana.


Hakuna kulala kazi na mtu, hapa wanachonga mtumbwa kwa kutumia mti wa mwembe. Kwa hiyo mti wa mwembe sio kupata embe tu hapana mitumbwi pia.




Sunday, September 28, 2008

UJUMBE WA JUMAPILI YA LEO

Furaha:- Inakuja wakati kazi zetu na maneno yetu yanapokuwa na faida(fadhila) kwa wewe binafsi na pia kwa wengine.

Amani:- Kuleta amani kwa kila mtu, inabidi kupambana ili kuweka amani yako ya maisha yake pia.

Ushujaa:- Kutokuwepo na woga au kukata tamaa, isipokua ni uwezo wa kushinda.

Utulivu:- Ni amani inayokuja wakati nguvu zipo ndani ya upatanifu wa kirafiki upo sawasawa.

Upendo/Mapenzi:- Ni msukumo ambao tumepewa, mapenzi ni pumzi ya maisha juu ya moyo na yanaleta madaha/uzuri ndani ya roho.Bila kusahau ya kwamba upendo una mamlaka , enzi, amri na nguvu hapa duniani.

Busara:- Elimu, kipaji/uwezo wa kuelewa/kuhisi kitu haraka na uzoefu wa mchanganyiko wa kuelekezana na kufikiri jambo/tendo.

Saturday, September 27, 2008

LITUHI+MANDA+KUMBUKUMBU

Leo nimmewapelekeni mpaka Lituhi wengi labda mmefika
Hili ni basi ambali linasafiri kila siku Songea -Lituhi
Hapa ni kijijini Lituhi gengeni

Ramani ya Ngelenge na hapo juu unaona ni manda halafu unaona ziwa nyasa hapo


Hii ni Sehemu ya kupack baiskeli hapa Manda



Ni kawaida tu kubeba vitu kichwani




Lakini angalia hapa kazi ipo wataweza hawa kweli?



Matatizo ya uzeeni, Mila na desturi za kubagua watoto wa kike

........................................................

Wazee mara nyingi hupoteza uwezo wa kukumbuka vitu kwa hiyo huwa wasahaulifu sana. Huwa rahisi kuvurugikiwa akili zaidi hasa pale wanapopatwa na homa kali. Mara nyingi wazee wanapata shida ya kukabiliana na mazingira mapya au yanayobadilika. Kijadi mara nyingi wazee ni watu ambao walikuwa wakiheshimiwa sana na kutunzwa vizuri. Heshima hii iliwafanya wajione kuwa ni watu wanaothaminiwa na jamii, na kuwaongezea furaha ya maisha. Siku hizi vijana wengi wanashindwa kuzingatia mila za zamani za kuwaenzi na kuwaheshimu wazee na hivyo kushindwa kuwapa nafasi yao katika jamii. Wazee wa mijini na hata vijijini wanakuwa wapweke bila watu wa kuwasaidia. Sehemu nyingine wazee wanasakwa na kupigwa hadi kufa kwa kuhofia kwamba wao ni wachawi. Hali hii ya kuwatenga wazee na kuwasingizia uchawi ni mojawapo ya matatizo ambayo yanaathiri sana afya yao ya akili.Sijui mila ipi ni nzuri kwani mimi kwa sasa nina mila "mbili" wenzetu ughaibuni wazee wao wanatunzwa kwenye nyumba maalum hii mara nyingi inasumbua akili yangu na nataka nitakapokuwa mzee sitaki kutunzwa na mtu zaidi ya familia yangu je nakosea? semeni ninyi.
. .


Nilizani ubaguzi utapungua lakini, naona hadi leo kuna baadhi ya wazazi ambao wanapuuza elimu ya watoto wa kike na kutoa kipaumbele kwa watoto wa kiume. Mfumo dume huu unachangia kuathiri afya ya akili ya kina mama. Nyumbani watoto wa kike wanatakiwa wasaidie kazi za jikoni na za ndani wakati wa kiume wanasoma au kwenda kutembelea marafiki. Hata katika maamuzi ya familia mawazo ya watoto wa kiume yanapewa uzito zaidi kuliko yale ya watoto wa kike. Waalimu nao mara nyingine wanawajengea watoto wa kike imani potofu kwamba wao hawawezi masomo ya sayansi.

Wasichana na vijana wanawake daima hujikuta wapo kati ya mila za zamani na mila za kisasa, kwa mfano, anapotaka kwenda shule hupambana na mila za zamani, zikiwa za dini au za kikabila.
Hili limekuwa ni tatizo kwani wasichana wa siku hizi hupenda kusoma ili baadaye waweze kupata kazi kabla ya kuolewa. Kwa hiyo wanapolazimishwa kufuata huo utamaduni wanapata mvurugiko wa akili.

Friday, September 26, 2008

JAMII YA WASUKUMA!

MAANA YA NENO WASUKUMA Wasukuma ni mkusnyiko wa makundi madogomadogo kutoka maeneo jirani , na kwamba kundi kubwa zaidi likiwa limetoka Kusini mwa eneo hili la mkoa wa Mwanza.Jina hili limetokana na neno SUKUMA maana yake wa lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi KASKAZINI, yaani moja wapo wa ya pande nne a dunia yetu. Wanyamwezi ambao lugha yao inafanana sana na Kisukuma hutuita sisi tulio Kaskazini mwao "Bhasukuma" yaani watu wa KASKAZINI. Nasi huwaita "Bhadakama" yaani watu wa KUSINI.
Tangu siku zote, wasukuma na wanyamwezi walijulikana kuwa wao ni "Bhantu" na kutokana na neno hilo kumekuja kujulikana kundi linaloitwa WABANTU. Kundi hili mara zote limetambulikana kwa lugha wanayozungumza ya KIBANTU. Hivyo, Wanyamwezi, Wakimbu hadi Wabemba walioko Zambia ni kundi kubwa la wabantu kufuatia lugha wanazozungumza.
Taarifa zingine kuhusu chimbuko la wasukuma kutoka kwenye mtandao wa internet…kwenye anwani hii.www.mwanzacommunity.com.org




Katika picha mwenye koti jeusi ndiye mzee mwenye miaka 114 ajulikanaye kama Mzee mtalimbo. Ni mganga wa kienyeji ana wake 7 watoto 14 na wajukuu 82. Mtoto wake wa kwanza ana mika 72.



Hii ni nyumba ya mzee mtalimbo ndani pia ni maazi ya nyuki ambao ni mali yake.




Nahisi hapa ni mke na mume katika safari ya kwenda shambani. Kuwajibika kwani bila kulima hakuna kula.

Thursday, September 25, 2008

NALIPENDA JINA LANGU YASINTA

Mwenzenu leo nimepatwa na kichaa au sijui nisemeje : Yasinta ni jina langu, nataka kuwaambia ya kwamba jina Yasinta nalipenda sana. Nalipenda jina langu halafu napenda sana watu wanaponiita Yasinta napenda sanaaaaa. Napata shida kidogo ninapokuwa Tanzania wote wanasema Mama fulani au Nangonyani kiasi kwamba nasahau naitwa nani. Ila hapa Sweden wote wananiita jina langu lakini wananiudhi wanatamka vibaya wanatamka na H. Hyasinta. oooh wananiudhi sanaaaaaaa. Ila wao waninijibu ni kwamba wanaposema Hyasinta wanawaza au moja ya ua ambalo linaitwa Hyacint huwa linapatikana sana hapa wakati wa Noel.
Ni hili ua liitwalo Hyacint


Kila mara nawaambia Jina langu YASINTA si Hyasinta. kwa mara nyingine nalipenda sana jina langu. Asante baba na mama. Yasinta

SWEDENI/TANZANIA

Waswidi ni watu wa ajabu sana sio wote baadhi. Kwa kawaida wao ni watu wakimya sana. Hawapendi kuongea kama Wabongo(TZ) Ukiwakuta waswidi katika kituo cha basi au sehemu nyingine, kitu ambacho wataanza kuongea ni habari za hali ya hewa. Wao ni watu maalum kidogo. Mara ya kwanza nilipata shida sana, lakini huu ni utamaduni wao.

Waswidi ni wabinafsi sana kila mtu na kitu chake/mali yake, kila mtu na mama yake, kila mtu na baba yake, kila mtu na dada/kaka yake, kila mtu na mtoto wake na kila mtu na kazi, pesa, nyumba yake hakuna kabisa ushirikiano kama Afrika yetu. Kila mtu na lake/Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyeweeeeee.

WAMAKONDE NI MOJA YA MAKABILA YA TANZANIA

Kijana mmakonde amejipamba

Vinyago vya kimakonde hapa ikimaanisha msichana





Siku njema ndugu zanguni kwa kipande hiki cha sindimba ngoma ya wamakande. Haya burudika kidogo.





Wednesday, September 24, 2008

MJADALA WA LEO

Hili swali limekuwa likinikereketa sana miaka yote ambayo nimeishi hapa duniani kwa hiyo sasa naomba mwenzangu tujadiliana au mnipe jibu.

SWALI NDIO HILI:- Je? Kuna sheria Tanzania isemayo kama msichana akipata mimba asiendelee na masomo?

Tuesday, September 23, 2008

MAISHA YA KIFALME

Leo nimeona tuangalia kidogo Sweden, nadhani wengi mnajua ya kwamba Sweden sio nchi ya Kijamhuri ni nchi ya mfumo wa ufalme (monarch)
Hapa ni mfalme wa Sweden Carl Gustav
Mkewe Malkia Silvia yeye asili yake ni Mjerumani




Hapa ni binti mfalme,Victoria ambaye hapo baadaye ndiye atayeongoza nchi (atakapokufa babake mfalme).




Mwana wa mfame Carl Philip




Binti mfalme mdogo Madeleine





Na hapa ni familia nzima ya kifalme






Monday, September 22, 2008

JE? HII NI KWELI?



Yapo mateso ya aina nyingi ambayo anaweza kupata mtu utotoni ikiwa ni pamoja na kulazimishwa kufanya kazi nyingi kupita kiasi. Manyanyaso mfano njaa, kukosa mazingira ya usalama, kupigwa kikatili mara kwa mara na kubakwa utotoni kunawaathiri watu kisaikolojia. Watoto wanahitaji kulelewa katika mazingira ya usalama, wapewe nafasi ya kupata elimu nzuri, na wapate muda wa kucheza na kufurahia utoto wao. Watoto kucheza si jambo la anasa bali ni njia mojawapo muhimu ya kuboresha afya ya akili

Sunday, September 21, 2008

VIJIJI/MITAA YA SONGEA

Nimeona labda niingia kidogo vijiji/mitaa ya Songea na umaarufu wake pia

Naanza na:-

  • Peramiho inajulikana sana kwa hospitali yake nzuri, seminari na pia kanisa nzuri.
  • Maposeni kuna sekondari
  • Lundusi anaishi babangu mkubwa
  • Mkurumo ni kijiji alichozaliwa mamangu pia amezikwa pale
  • Morogoro ni mashuhuri kwa hospitali yake ya kutibu wagonjwa wa ukoma
  • Ndirima/mdunduwalo kuna mashine moja ya kusaga
  • Likingo ni sehemu moja ambayo hutengeneza umeme wa nguvu za maji hydro-electric power station)
  • Matogoro maalufu kwa milima mizuri pia chuo cha Ualimu
  • Lizaboni hapa bwana ni maalufu kwa kitimoto mara nyingi tulinunua hapa
  • Mfaranyaki hapa tulikuwa tunatengeneza gari
  • Majengo nilijifunza kuchapa mashine yaani kuna chuo cha uchapaji
  • Mahenge niliishi wakati nasoma typist
  • Bombambili ni stendi ndogo kwenda Njombe - Dar
  • Litapwasi ni maalufu kwa uchomaji mkaa

kama nimesahau mitaa au vijji vingine basi samahani au nitaandika siku nyingine. Jumapili njema

Saturday, September 20, 2008

MKOA WA RUVUMA

Leo nmeamua kutembelea Ruvuma kijiografia na Historia fupi.

Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania. Mkoa huu umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake upande wa kusini ni Msumbiji, upande wa magharibi umepakana na ziwa Nyasa na mkoa wa Morogoro, upande wa kaskazini umepakana na mkoa wa Iringa na Lindi na upande wa mashariki umepakana na mkoa wa Mtwara.

Katika Mkoa wa Ruvuma kuna mikoa mitano:- Songea mjini na wakazi wake ni 131,336, Songea vijijini ina wakazi 147, 924, Tunduru ina wakazi 247, 976, Mbinga ina wakazi 404,799 na mwisho Namtumbo wakazi wake ni 185,131.
Songea ni makao makuu ya mkoa kwa hiyo jumla ya wakazi wa mkoa wa Ruvuma ni 1,117,166 (sensa 2002) Makabila makubwa katika mkoa wa Ruvuma ni Wayao, Wangoni, Wamatengo, Wandendeule na wandengereko.

SONGEA
Jina Songea ni kumbukumbu ya Chifu Songea wa wangoni, aliyekuwa na Ikulu pale wakati wa kuenea kwa ukoloni wa Ujerumani akauawa na Wajerumani, wakati wa vita ya majimaji.
Mji wa Songea wakati ule iliandikwa Ssongea, mji huu ulianzishwa mwaka 1897 kama kituo cha kijeshi cha kijerumani.
Mazingira ya mji yaliathiriwa vibaya na viya ya majimaji na ukandamizaji wake na Wajerumani.
Songea ikaendelea kuwa makao makuu ya mkoa wakati wa utawala wa Uingereza katika Tanganyika na baada ya uhuru katika Tanzania huria.

MAISHA MAGUMU NA MARADHI

Maradhi ya kuambukiza yanayompata mama mwenye mimba yanaweza kusababisha athari kwa mtoto anayezaliwa. Kama mama mwenye mimba atakuwa na kaswende, ataweza kuzaa mtoto kipofu, kiziwi, mwenye kifafa au taahira.
Mtoto akipokelewa vizuri katka ulimwengu huu, kama vile mama huyu anavyofanya kwa mtoto wake, inamfanya mtoto awe na matumaini na kuvumilia matatizo ya maisha katika utu uzima.

Mtoto huyu ana njaa na ametekelezwa. Hana mtu anayemsimamia haki zake za msingi (chakuli, malazi, upendo, elimu na malezi)
Mtoto kama huyu amekwishawekewa msingi mbaya wa maisha na ana hatari ya kuathirika kisaikolojia siku zote za maisha yake.

CHAKULA (Kräftor=kamba wa mtoni)


Karibuni wote huu ndiyo mlo wa leo. Ni hivi kila mwaka hapa Sweden mwezi wa nane katikati mpaka wa tisa katikati .Ni kipindi cha kula kamba wa mtoni, mila na desturi. mimi napenda sana. Kama kuna mtu hapendi asiogope kuja kuna chakula kingine tena kingi tu. KARIBUNI SANA

Friday, September 19, 2008

RUHUWIKO


Ruhuwiko ipo baina ya Songea na Peramiho. Ruhuwiko ni mtaa, mtaa huu una sifa za kuvutia. Kwanza mwaka 1990 alifika papa, baba mtakatifu pale kanisani wakati huu halikuwepo kanisa kilikuwa kiwanja tu. Alitoa misa, pia wengine walibahatika kupata kipaimara. Siku ile hata mimi nilikwenda kumwona papa, kuhudhuria misa. Kwa hiyo mwenzenu nimebarikiwa kubarikiwa na papa. mtajiju msiobarikiwa.

Ruhuwiko kuna shule ya viziwi na bubu, pia kuna shirika la masista wa ndanina nje, Pia, Ruhuwiko kuna kiwanja cha ndege. Kwa hiyo msipate tabu. Ni sehemu nzuri imekaa katikati kwenda Songea mjini na pia kwenda Hospitali Peramiho.

Thursday, September 18, 2008

YASINTA NA WAFANYAKAZI WENZAKE

Hapo juu ni kundi la wafanyakazi wenzangu

Mimi tena, napenda sana chai bila sukari (chingambu)

Wednesday, September 17, 2008

MASHINDANO YA WALEMAVU PARALYMPIC BEIJING

Anders Olsson ni mshindi wa kuogelea kwa hapa Sweden yeye ni mlemavu hawazi kutembea .





Oscar Pistorius ni mshindi wa dunia kwa kukimbia mita 100, 200, na 400. anatoka Afrika kusini. Sio Bolt tu anaweza kukimbia wapo wengi.

Tuesday, September 16, 2008

KUFA

Kwa nini watu kwanza tunazaliwa halafu tunakufa. Wengine wanaishi dakika, saa, siku, miezi, mwaka, miaka na miaka. Mara nyingi nimekuwa nikiwaza neno KUFA lazima itakuwa ni pumziko la amani sana kulala kwenye lile sanduku giza na hali tulivu hakuna anayekusumbua peke yako.



Unajua kama una ndugu, jamaa na marafiki ambao hawakujali kwa nini kuishi peke yako hapa duniani wakati kuna uwezo wa kuwa upweke Kaburini. Afadhali kabisa kufa. Haya ni mawazo yangu.



Kama ilivyoandikwa: Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi akampulizia puani PUMZI YA UHAI na mtu yule akawa NAFSI hai.

Kufa ni kama kulala usingizi usio na ndoto. Yesu alifundisha hivyo.

Baada ya kufa ubongo unaharibika hauwezi kujua , wala kukumbuka kitu chochote. Hisia zote za moyo za kibinadamu hukoma kabisa mtu anapoishi.

"Kama mimi niishivyo, atangaza Bwana Mungu,..... kila ROHO ILIYO HAI(LIVING SOUL) ni mali yangu....... ROHO YULE ATENDAYE DHAMBI NDIYE ATAKAYEKUFA." Ezekieli 18;3-4.

Swali:- Kwa nini yesu alikufa na akafufuka na sio sisi wengine "wanadamu"?

MAISHA


Hapa ilikuwa mwishoni mwa mwezi wa nne mpaka katikati ya mwezi wa tano. Mimi na hapo ni mama mkwe wangu. Najua mtashangaa kwa nini natembelea magongo, sawa nilikuwa nimefanyiwa operesheni ya mguu. Ilikuwa kazi kweli kweli, ila sasa poa kuna wakati napata maumivu kwa mbaliiiiiiiiii.

UTUNZAJI WA MALI

Kutunza mali uliyonayo ni muhimu sana. Kila mtu anahitaji kutunza kile alichonacho hata kama ni kibaya au kidogo chako ni chako tu .
....................................... ............................................

Monday, September 15, 2008

UNGEKUWA WEWE UNGEFANYEJE?

Umekuwa kijana/msichana wa umri wa kuoa/kuolewa. Umefunga ndoa na matunda yanaonekana. Watoto hao.
Lakini katika historia/ukoo wako wewe ni mtoto pekee kwa baba na mama yako.

Na wewe sasa una mume, watoto na kazi. Watoto wanaenda chekechea, mume ana kazi pia. Na wewe kazi yako mara nyingi mchana na usiku.
Mchana sio kitu watoto watakuwa chekechea au shuleni. Tatizo usiku, umejaribu kumwomba mama yako mzazi msaada awatunze wajukuu. Wajukuu ambao ndio hao tu ambao anao. Lakini kila mara anakataa. Je? ungekuwa wewe ungefanyeje?

Sunday, September 14, 2008

WANAWAKE UGHAIBUNI NA WANAWAKE AFRIKA

....... ...................... ............


Kama waswahili wasemavyo tembea uone, basi mimi nimeona:-


Kwani nakumbuka, pia najua ya kwamba wanawake Afrika ni wanyenyekevu mno kwa waume zao.

Lakini kwa uzoefu wangu hasa hapa Sweden baada ya kuishi miaka 14. Nimeona ni kinyume kabisa. Hapa ni wanawake ndio wanaamua/uamuzi ndani ya nyumba.


Bado sijajua nani nimwonee huruma Afrika au ughaibuni/Sweden.Nategemea sitaambukizwa na hali/tabia hii Mungu nisaidie. Na hii inachangia sana hapa Sweden kuwa na asilimia kubwa ya kupeana talaka

MAANDALIZI YA LONDONI 2012

...............

Tutaona nani ataweza huo mwaka. wote tupo katika mazoezi makali sana mtajiju. Au labda niseme karibuni kujiunga nasi.

Saturday, September 13, 2008

JUMAPILI NJEMA

Hili ni kanisa langu ambalo wakati naishi Songea (mahenge) nilikuwa kila jumapili nakwenda kumshukuru mungu hapa. Ni Kanisa la Matogoro.






Na hapa ni kanisa ambalo nilipata Kipaimara wakati naishi ubenani. Ni kanisa la Maweso. Jumapili njema tena kwa wote.

KISWAHILI

Mara nyingi huwa nakasirishwa kuona / kusikia watu wanatumia vibaya baadhi ya maneno ya kiswahili. Hapa nimechukua au nataka kutoa mfano haya maneno matatu. Karibu, Jambo na Habari

Karibu: Ni kuto kuwa mbali kwa wakati au mahali, kiasi cha kukadria. Lakini watu wengi wanaelewa zaidi karibu ni tamko litumikalo kuitikia hodi au wakati mtu anapokaribishwa au kupokewa mahali fulani.

Jambo: Watalii wengi wanafikiri wanaweza kiswahili, kusalimia wasemapo jambo hawajui kwamba Kiswahili sananifu hutamkwa hujambo/haujambo/hamjambo? kwani ukisema hivi anashindwa kuitikia sijambo. S afadhali hata wangefundishwa kusema hali yako.....

Habari: Neno habari limekuwa linanitatanisha sana. Kama kawaida maneno mengi ya kiswahili yana maana mbili azu zaidi. (1) Habari ni melezo ya jambo fulani lililotokea, taarifa, ujumbe na ripoti.
2) Habari hutumika katika kuamkiana na kuulizana hali. Lakini inaonekena wengi hatuwazi sana tunapoongea hili neno litumikeje.

Friday, September 12, 2008

HARUSI YA BONIFACE MWAITEGE


Mungu amemsikiliza sala zake za kupata mke mwema. Hapa ni Bony Mwaitege na Kipenzi chakeBi Subiraga. Naona sasa majukumu yatapungua maana sasa umepata mke mtasaidiana. Maana sasa umekamilika. Hongera sana kaka Boniface

Thursday, September 11, 2008

UREMBO, MAVAZI ,MKOBA NI MOJA YA MAISHA

mkoba wa katani Mrembo Flaviana



Mapambo ya miaka ile


Pensi nyanya

Mimi ni mpenzi wa mitindo mipya na zamani. Napenda fashion.Nafikiria labda nianze hii kazi ya kuonyesha mitindo ya nguo (fashion)