Showing posts with label wadudu. Show all posts
Showing posts with label wadudu. Show all posts

Tuesday, February 10, 2015

TUWE MAKINI TUTUMIAPO VINYWAJI MAANA KUNA WENGI WANAPENDA!!!

Hii inanikumbusha siku moja  tulikuwa na sherehe na katika shamrashamra  basi kaka mmoja akawa amechukua bia yake  na kunywa kumbe mende walikuwa wamemwahi. Na pia mwingine aliingingiliwa na nyuki akamuuma mdomoni na kuvimba vibaya mno. Kwa hiyo ndugu zangu tuwe makini. Tutaonana tena panapo majaliwa...Kapulya!!

Tuesday, July 30, 2013

BUSTANI:- BUSTANI YANGU IMEINGILIWA NA VIWAVI/BUU WANAKULA FIGIRI YANGU:-)

Kutunza bustani ni kazi kidogo leo nimeamka asubuhi hii na kwenda kuangalia bustani yangu nakutana na wadudu wanakula figiri yangu nimechukia mno tena mna na nimengóa yote na sasa nataka ushauri wenu kwa yeyote anajua jinsi ya kuwaua buu/viwavi maana sijakata tamaa nataka kujaribu tena kupanda figiri nyingine. 

 
 Mboga yaa maboga inastawi sa tena vibaya mno yaani mpaka raha hapo nimechuma jana hivyo.....
 Mchicha nao inatia nanga unapendaza..nitauchuma kesho si mnajua akiba haiozi karibuni tu hapa kutakuwa na baridi kiasi kwamba hata kuchimba shima ni shughuli....
 ....Sasa hapa ndipo nilipoudhika kwa kweli angalia figiri yangu ilivyoliwa. Nimejaribu kila njia kuwatoa viwavi/buu hawa lakini nimeshindwa. Je kuna anayejua dawa ya kuwatoa hawa wadudu/buu?...kaka Bennet upo nisaidie...nimeudhika sana sana kiasi kwamba-----
Nimengoa figiri yote lakini nipo mbioni kupanda nyingine tena leo hii nitaatika...