Friday, August 31, 2012

TUMALIZE MWEZI HUU WA UJUMBE HUU: MWAISHA WAKUMBUKE WAZAZI!!


Nachukukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kunilinda/kutulinda katika mwezi huu bila ya magonjwa makali sana. Pia kwa kuweza kunipa/kuwapa nguvu wale wote waliopoteka na kuweza kurudisha mioyo yao na kuomba msamaha. NAWATAKIENI WOTE MWISHO MWEMA WA JUMA/WIKI NA PIA MWEZI.  IJUMAA NJEMA!!!

Thursday, August 30, 2012

KUHESHIMU BENDERA YA TAIFA!!!!!!

Nimekaa hapa nikajikuta naimba huu wimbo je wewe unaukumbuka? Ungana nami katika kumbukumbu hii haya moja,mbili, tatu..............

1. Bendera ta Tanzania, ndiyo ya kujivunia,
Ilianza kupepea, mwaka sitini na moja,
Hapo inashuhudia, tunavyojitegemea,
       Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.

2. Siku ya tarehe tisa, saa sita kamili,
                         Mwezi wa kumi na mbili, yalikuwa mambo sasa,
                    Mlima Kilimanjaro, bendera yetu hutwekwa,
                Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.

3. Rangi kijanikiwiti, yaonyesha mbuga zetu,
     Manjano ndiyo madini, yaliyo uchumi wetu,
    Buluu huonyrsha maji, yaliyo nchini mwetu,
Nyeusi ni yetu sisi, Waafrika asilia
Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.

4. Bendera yetu mwanana, yajulikana bayana,
Duniani twatukuka, katu hatuwi mateka,
   Bendera yapeperuka, Uchina na Amerika,
Wala haitatatuka, na juani kuchujuka,
  Muumba wetu Rabuka, ijaze yako fanaka.
.......................................................................................................................
Kama sikosei ilikuwa darasa la sita au la saba

Wednesday, August 29, 2012

MTOTO/KIJANA AFUNGA NDOA NA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI -SONGEA!!!



Mke na Mume, Bi Condorada Ngonyani (70) na Bw. Joseph Mapunda, ambao ni Mama na Mwanawe, wakiwa nje ya nyumba ya Mganga, wakati walipofikishwa kwa suala hilo la Mama Mzazi na Mwanawe kufunga ndoa.
*********************************************************************************

Na Mwandishi Wetu, Namtumbo Ruvuma
MARA kadhaa kumekuwa kukijitokeza matukio mbalimbali ya kustaajabisha, kusikitisha na kutisha na mengine yakihisiwa kuwa ni imani za kishirikina, ambapo mengi ya matukio hayo ambayo hutokea si kwingine ni hapa hapa nchini kwetu, huwaacha watu hoi na maswali mengi yasiyokuwa na majibu.
Kwa mara nyingine tena tukio la kushangaza na kutoaminika kama ni kweli ambalo huwezi hisi kuwa ni la imani za kishirikina, kwani wahusika wote wamefanya hivyo kwa malengo na kuweka wazi sababu za kufanya hivyo japo si sahihi kwa itikadi za kidini, mila na destuli za mtanzania.
Tukio hili ni Mama Condorada Ngonyani (70) mkazi wa mkoani Ruvuma, ambaye aliamua kufunga ndoa na mtoto wake wa tatu wa kiume wa kimzaa na kuishi naye kinyumba kama mke na mume, ambapo wameonekana wao kama wao kuwa wapo sahihi na kuwashangaa wanadam, majirani zao na Jamii kwa ujumla kuingilia mapenzi yao.

Wananchi wapatao 400, wa mkoa wa Ruvuma walijitokeza kushuhudia kimbwanga hii wakati uongozi wa Serikali ya Mtaa walipoamua kuwafuatilia na kuwahoji na kuitisha mkutano wa wanakijiji na kuwaweka hadharani, ambapo Wananchi wa Mkoa wa huo wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na watoto, kufuatilia kwa karibu suala hilo na kuwaondoa hofu wananchi kama kuna sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa.

Alipohojiwa Mama huyo, Condorada Ngonyani, anasealisema kuwa mara tu baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda, yeye aliamua kumchagua mtoto wake huyo Joseph Mapunda, ili amrithi baba yake katika kuumiliki mwili wake kama ambavyo alikuwa akifanya Baba yake mzazi, ili kuondokana na tamaa na vishawishi wa kiulimwengu.
Alisema kuwa baada ya uteuzi huo walifunga ndoa ya kimila japo kuna baadhi ya wanafamilia hawakufurahishwa na tukio ama jambo hilo, lakini yeye aliamua kufunga masikio na kuamua kuvunja amri ya sita na mtoto wake huyo wa kumzaa.
Tukio kama hili ni mara ya kwanza kutokea kwa mkoa wa Ruvuma na hata kwa Tanzania nzima, ambapo wakaazi wa Ruvuma wamekuwa wakibaki na maswali mengi juu ya tukio hilo na kuhoji Jamii sasa inaelekea wapi kwa baadhi ya Watanzania kuibomoa wenyewe mila na desturi zetu.
Kwa upande wake, Joseph Mapunda, yeye anasema kuwa upendo na mahaba anayoyapata kutoka kwa mkewe huyo ambaye ni mama yake mzazi, hajawahi kuyapata kokote na kusema kuwa wanapendana sana na wanaheshimiana kama mke na mume.
Josepha amehiji kulikoni wanadam kuwafuatilia katika mapenzi yao na kusema kuwa ''hawa watu wanaotufuatilia hadi leo hii kutuweka hadharani namna hii, wanataka nini kwetu?''.
Wananchi hao waliofurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo, wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma, wameiomba Serikali kuingilia kati suala hilo na kuchukua hatua kisheria ili iwe fundisho kwa wanatanzani wengine wenye akili kama hizo za kuharibu mila na desturi za kitanzania kirahisi kama hivyo. Picha na Songea Habari

Bi. Condorada Ngonyani. ''Nawashangaa wanadam kuingilia mapenzi yangu, mtuache''.
Bwana, Joseph Mapunda, ''Wananchi mtatutakia nini na mapenzi yetu''?
CHANZO:HAPA  NA PIA UNAWEZA KUSOMA HAPA. ..
.................................................................................................................................................................
Habari hii imenigusa sana, jamani kumwoa mama yako mzazi /kuolewa na mtoto wako uliyemzaa  kweli? kwanini wasingeishi tu kama mama na mtoto ? huko tunakoenda sasa ni balaa tu. Dunia imekwisha jamani au nini hii sasa...mama ana miaka sabini ...nimeishiwa maneno ya kusema nimebaki natafakari bila kupata jibu....Maisha haya jamani .....

TANZANIA NI NCHI AMBAYO INA VIVUTIO VINGI AMBAVYO HUWEZI KUVIONA KATIKA SEHEMU YOYOT DUNIANI...!!!

Kama  Olduvai  Gorge Ngorongoro......
 ....au katika mbuga hii ya Serengeti.....
.....na bila kuusahau mlima wetu mtukufu Kilimanjaro
Tumalizia na wimbo huu ....
MUWE NA SIKU NJEMA WOTE MTAKAOPITA HAPA.....

Tuesday, August 28, 2012

HAPA WENGI TUNAKUMBUKA MALEZI YA WATOTO!!


Katika malezi/makuzi watu tumetoka mbali, huyu binti hapa ananikumbusha mbali sana.Wazazi wanaondoka asubuhi huku wakitegeme binti mimi/huyu afanye kazi ya kuchota maji. Na hapo labda sio ndoo moja tu pipa zima. Na hapo hapo amtunze mdogo wake. Na labda kuchochea maharage pia. Hali hii kwa sasa hakuna kabisa maisha yamebadilika kabisa ndiyo kwanza utakuta mtoto anamtuma mzazi wake. Maisha siku hizi yamekuwa  watoto na TV, Komputa, simu nk. Hata kumwona mtoto siku hizi anasoma kitabu ni mara chache sana. Ndiyo maana  sisi tuliolelewa  katika malezi ya aina hii kama huyu binti inatupasa tuendeleza kwa kuwahimiza  watoto wetu waweze kufanya hivyo hata kama ni kidogo. Polepole ni mwendo...Hata hivyo najua hali hii ya watoto kusaidia kazi za nyumbani vijijini bado inaendelea. Binafsi niitazamapo picha hii najiona ni kama mimi...na naweza nikasema natamani niwe tena kama huyu binti...Je? umewahi kuifanya kazi hii? au labda kuchunga mbuzi na ngómbe kama watoto hawa hapa....


....na hapa ndipo watu wanapojifunza maisha  ni nini/ hawa ndiyo  wataweza kuyamudu maisha yoyote yale na pia kujua ugumu na uzuri wa maisha ....JUMANNE NJEMA!!!!

Monday, August 27, 2012

TUENDELEZE JUMATATU HII KINAMNA HII:- MFANANISHO!!!



Nimeamka asubuhi hii kama kawaida nikafungua email yangu . Nikakutana na ujumbe/ picha hii ya kwamba nimefanana sana na huyu dada Angela Chibalonza...nimeiangalia hii picha yake na kufananisha na yangu, kwangu imekuwa ngumu kuona na nimeona afadhali nipata msaada hapa kibarazani je ni kweli tumefanana? angalia picha hizi hapa chini...

Marehemu dada Angela Chibalonza
Yasinta Ngonyani
Nawatakieni wote JUMATATU njema maana mwanzo wa juma huwa na mikikimikiki sana !!!!!!

BARANI AFRIKA:- UTAMADUNI WA KUSIMULIA HADITHI BADO NI MUHIMU!!!

Hadithi kama tujuavyo ni njia ya maridhiano isiyo na gharama na ya kudumisha utamaduni.

Wengi wetu tunakumbuka nyakati ambazo wazazi au mababu na mabibi zetu walipokuwa wakitusimulia hadithi za kufurahisha zilizotokea zamani. Nilipoiona picha hii nimekumbumbuka sana zamani nilipokuwa mdogo wakati wa jioni wote mnakusanyika na kusikiliza hadithi na hapo hapo mnamenya karanga au kupukuchua mahindi na hapohapo mnaota moto.....

Sunday, August 26, 2012

JUMAPILI YA LEO : NA WIMBO HUU AIYELELE KWAYA YA MT. CECILIA PAROKIA YA MAVURUNZA DAR ES SALAAM!!


Nimejikuta nipo kanisa langu nililobatizwa MAKWAI/Lundo au sijui Kingole mmhh labda Litumbadyosi au pengine Matogoro Songea mmmhh labda Ruhuwiko...Haya jamani ndugu zangu katika kristu tuwe na JUMAPILI NJEMA NA AMANI NA UPENDO  VITAWALE MAJUMBANI MWETU. AMINA

Saturday, August 25, 2012

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KUOMBA RADHI/SAMAHANI!!

Nachukua nafasi/fursa hii na kuwaomba wote radhi kwa picha niliweka hapo jumatano 22/8 katika KIPENGELE CHA MARUDIO. ILE PICHA IMETOLEWA. Nia yangu haikuwa /sikulenga kuwaumiza au kuwa/kumdhalilisha/aibisha mtu. Bali ni kutoa elimu kwa jamii nasema tena KWA TAARIFA HII NAOMBA SAMAHANI KWA WOTE WALIOATHIRIWA kwa namna moja au nyingine. Nami nimejifunza kitu kupitia maoni yenu.Naomba tuendelee na safari pamoja.Yasinta/kapulya.

Friday, August 24, 2012

Thursday, August 23, 2012

ALIYE TELEKEZA MTOTO SONGEA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI!!!!


Mara baada ya kukamatwa na Police alipewa mtoto amnyonyeshe huku akijutia baada ya kudanganywa na Mwanaume

Habari hii imenisikitisha sana kuona Songea yangu imegeuka na kuwa hivi. Huyu mama/binti ni bado hajakomaa kuwa mama halafu wanakuja wanaume na wamemdanganya na pengine wazazi pia wamemfukuza kwa kupata mimba haruhusiwi kuishi nyumbani halafu anapata mimba na baadaye kujifungua. Hapohapo wanakuja  mwanaume na kumdanganya tena maskini afanye nini? Nyumbani kumezuka mbogo.Najaribu kujiuliza binti wa miaka kumi na nane na halafu una mtoto peke yako aliyekupa mimba amepotea je utafanya nini peke yako?. Mwanzoni kuna kuwa na mapenzi, maneno mazuri, zawadi nzuri na msichana anazuzuka na mwisho ndio unakuwa huu..hakika ni safari ndefu sana tunayo...hebu soma hapa chini habari ya huyo dada Zawadi yalimsibu. Habari hii nimeipata hapa
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Adamu Nindi, Songea.

Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limefanikiwa kumtia mbaroni Mama aliyemtupa Mtoto katika Guba ya kutupia takataka eneo la Mitumbani Majengo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma Ana Tembo ameyasema hayo wakati akiwa katika Ofisi ya Polisi wanawake Mkoani Ruvuma amesema Mama huyo ambaye alimtupa Mtoto wa kiume mwenye ummri wa miezi 5 wiki iliyopita amepatikana baada ya msako mkali ulioendeshwa na Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Ruvuma Anna Tembo amesema Mama huyo alipatikana katika nyumba ya kulala wageni eneo la Majengo akiwa amejificha chini ya uvungu wa kitanda akikimbia mkono wa Dola.
Jeshi la police lilipo mhoji Zawadi Komba 18 alidai siku hiyo alikuwa akifukuzwa na kichaa ndipo alipo mtupa mtot lakini baada ya kubana na mkono wa sheria ndipo alipo eleza ukweli kuwa alitumbukia katika dimbi la mapenzi
Mama aliyekayekamatwa na Jeshi la Polisi Zawadi Komba18 kwa tuhuma za kumtupa mototo wake na kutaka kuhatarisha maisha ya motto kwa kuliwa na Mbwa, amesema yeye alidanganywa na Mwanaume kuwa angeweza kumuoa endapo angemtupa mototo halafu wangekwenda kuishi Mkoani Mbeya.
Wadau mbalimbali wa Mtandao wa Polisi Wanawake, wakiwakilishwa na Fadhili Chacha wameshauri Wanawake wajishughulishena katika Biashara mbalimbali badala ya kutegemea Wanaume pia wajitahidi kuingia katika mpango wa uzazi wa mpngo ili kuepukana na kubeba mimba bila kutarajia.
Kwa Mkoa wa Ruvuma kuhusu ukatili dhidi ya Watoto hii ni mara ya tano katika mwezi mmoja, tukio la kwanza Baba na Mama walidiriki kumuua Mtoto kwa kumvunja shingo na kumtupa katika daraja la Bombambili, Tukio la Pili Mama mwenyewe na Baba walimuua Mtoto na kumtumbukiza katika sinki la maji taka, tukio la tatu Mtoto alitupwa eneo la Majengo na kuliwa na Mbwa na kubakizwa kichwa, watoto wengine wawili waliweza kuokolewa akiwemo na Mtoto mmoja ambaye alitupwa eneo la Msikitin

Wednesday, August 22, 2012

WANAWAKE KUTEMBEA NUSU UCHI, KUMBE WANA LAO JAMBO.....!

Leo katika KIPENGELE CHETU CHA JUMATAN YA MARUDIO YA MADA AU MATUKIO MBALIMBALI.  KATIKA PITA PITA ZANGU LEO NIMEPAMBANA NA HII  KWA MZEE WA UTAMBUZI.

 Kuna wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.


Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.

Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya. Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao, bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.
Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao.
PANAPO MAJALIWA TUONANE TENA JUMATANO IJAYO KATIKA KIPENGELE HIKI CHA MARUDIO.!!!



Tuesday, August 21, 2012

NA MCHANA HUU NINGEPENDAA KUANDAA CHAKULA CHA AINA HII:- UGALI/WALI WA NAZI NA MBAAZI!!! LAKINI SASA MBAAZI NITAPATA WAPI?


WALI WA NAZI


 UGALI WA MAHINDI....
NA HAPA NI MBAAZI, Nimezikumbuka sana mbaazi.Kwa mimi ningependa wali kwa mbaazi lakini nimeona niweke na ugali maana kuna wengine wanapenda ugali...karibuni...

CHAKULA CHA ASUBUHI YA LEO..DADA PENINA UPOOOO??? KARIBU PIA NA WENGINE WOTE...!!!

Haya ni maoni ya Dada Penila Simon kutoka katika picha hii hapa."Hongera, jitihada zako nimeziona, nakupenda ulivyo na pia, the way ulivyo busy na pia husahau asili. i real loe u baby.
Napenda na naomba unionjeshe kidogo picha baada ya kulipika lilisindikizwa na nini na lilikaaje mezani plz..." Nami nimeona si vibaya kama nikifanya kama dada P alivyoniomba hivi ndivyo mambo yalivyokuwa dada P, pamoja na wengine wote..fuatana nami.....

 Nimeamka asubuhi. Nimeingia katika shambani/bustani yangu na  kuchuma boga..kama nilivyowaambia hapo juzi na ....hivi ndivyo ilivyokuwa....boga
Nimechemsha na halafu tayari kwa Chakula cha asubuhi. Yaani boga kwa chai ya rangi. Kwa mimi chai yangu kama kawaida bila sukari hapo nimelifaidi na kulamba mikono si mchezo..je wewe unapenda kula boga lako vipi? au unalitemshia na nani?....mmmhhh sijui mchana huu nipike/nile nini? Natamani.. naacha sisemi mtaona baadaye kidogo tu...:-)

Monday, August 20, 2012

TUIANZE WIKI/JUMATATU HII NA:- CHEMSHA BONGO KIDOGO!!!

Ni hivi:- Baba mmoja alikuwa na mabinti 6/sita na kila binti alikuwa na kaka mmoja. Je? baba huyu alikuwa na watoto wangapi ?
NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA JUMA HILI!!!!

Sunday, August 19, 2012

KAPULYA LEO ANAWATAKIENI JUMAPILI HII KWA TASWIRA HII AU NISEME KWA MTINDO HUU/MWANAMTINDO WA JUMAPILI HII!!!!

 Haya hapa sijui ilikuwa ni ukaguzi wa meno....
 ...hapa kama vile alikuwa anakimbia  maratoni? 
na hapa naona alikuwa anampungia jirani mkono  au labda alikuwa anaota jua maana ndo kwanza ile miezi ya jua inaanza...kaazi kwelikweli au sijui tusea raha jipe mwenyewe...JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA PIA UPENDO NA FURAHA VITAWALE NYUMBANI MWENU....

Saturday, August 18, 2012

NA HAPA NI BAADHI YA MAVUNO YANGU NILIYOANZA KUVUNA BOGA:-)

Leo nimevuna boga kweli atafutaye na hupata...hili litakuwa mlo wa jioni ya leo...karibuni mjumuike nasi...

Neno La Leo: " Banda Wa Malawi, Katuvalia Ngozi Ya Simba, Kututishia Watanzania​....!" Na Maggid Mjengwa



..... Hatuwezi, Hatuwezi!... Mchakamchaka, Chinja, Mchaka mchaka, chinja!
Ndugu zangu,
Utotoni niliwasikia kaka na dada zangu wakiimba wimbo huu wa mchakamchaka uliojaa hisia za utaifa.  Ni kwenye mchakamchaka wa shuleni kila asubuhi.
Naam, hata wakati huo kulikuwa na utata wa masuala ya mpaka kati ya Tanzania na Malawi . Zilikuwa ni enzi za Rais Kamuzu Banda.
Na Watanzania hatukuwa na ukame wa nyimbo za  kebehi dhidi ya Banda. Mwingine uliimbwa hivi; " Kipara cha Banda kina ukoko!" Hakyamungu.  Hata wakati huo  kulikuwa na harufu ya vita baina ya  ndugu wawili; WaMalawi na WaTanzania. Maana, ukweli  sisi ni ndugu wa damu.
Kuna hata simulizi za kweli za Watanzania upande wa pili wa Ziwa Nyasa waliokesha kusheherekea Uhuru wa Malawi. Hivyo basi, tunaweza kabisa kidiplomasia kutamka, kuwa "Jambo la Malawi ni letu!" Ndio, shida yao ni yetu, furaha yao ni yetu.
Na tushukuru kuwa JK wetu ni mwanadiplomasia. Nitakuwa mtu wa mwisho kuamini kuwa JK anaweza kutuingiza katika ' Vita vya kiwendawazimu' dhidi ya  jirani na ndugu zetu wa Malawi.
Na picha hiyo hapo juu inaongea; JK na JB ( Joyce Banda),  wanazungumza kwa furaha kama ndugu. Wawili hao hawatoi nafasi kwa wachonganishi wale wa enzi za ugomvi wa utotoni. Maana,  utotoni ilikuwa hivi, kaka zetu walipotaka kufurahia wadogo zao tukipigana makonde,  walisubiri pale mmoja anapomkasirikia mwenzake. Haraka atatokea kaka na mchanga mkononi. Atatamka kwa mmoja kati ya wawili walio mbele yake;
" Haya, puta mchanga wangu  kama kweli wewe ni mwanamme!" Nani asiyetaka kuwa mwananme? Atauputa mchanga. Kisha kaka anamgeukia mwingine; " Haya sasa, nilipie ng'ombe wangu!".
Kulipa ng'ombe ilikuwa na maana ya kuanza kurusha konde. Na hapo ugomvi ulianza rasmi!
Na kuna miongoni mwetu wenye kutamani vita. Anayetamani vita ni mtu mjinga. Mwalimu alipata kutamka; " Vita si lelemama". Na katika dunia hii inasemwa; Chagua vita vyako. Vita vingine havina lazima ya kupiganwa.
Na tofauti zetu na Malawi zinaweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya kindugu kama anavyoonekana JK pichani akiongea na dada yake; JB- Joyce Banda.
Na wala hatuwahitaji tena akina Moses Nnauye kututungia nyimbo za Mchakamchaka. Eti twende tukiimba; " Banda ( Joyce) Wa Malawi, Katuvalia Kitenge Cha Ngozi Ya Mamba, Kututishia Watanzania,  Hatuwezi, Hatuwezi!".
Naama. Wakati umebadilika.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
mjengwablog.com

JUMAMOSI HII BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA WIMBO HUU:- MTOTO WA KARIOKOO NA DULLY SYKE


NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA NA MFANIKIWE KILA MNACHOTAKA KUFANYA!!!

Friday, August 17, 2012

KUMBUKUMBU:- LEO NI MIAKA NANE (8) KAMILI TANGU MAMA YETU ALANA NGONYANI ATUTOKE!!

KUZALIWA 2/10/1952-KUFA 17/8/2004
Mama ni miaka nane sasa tangu ututoke. Umetuacha na majonzi pia maumivu moyoni mwetu. Tunaukumbuka sana uwepo wako, tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miaka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda. Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulivyokupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka, mapenzi yako, wema wako. Pia kama mama kwa mwongozo wako katika nyumba yetu, ambayo sasa ni upweke mtupu bila wewe.
Tunakukumbuka sana,  sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. KIMWILI HAUPO NASI, BALI KIROHO UPO NASI DAIMA. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI. AMINA!!!

Na ndiyo maana hii siku sitaisahau maishani mwangu..ilikuwa saa kumi jioni nimetoka kazini na nilikuwa nimepanga muda huo waandishi wa habari wa gazeti la habari mpya za kanisa "Kyrknytt" waje wanipige picha. Kwasababu nilikuwa muhusika mkuu katika gazeti hilo. Ilikuwa mada kuhusi wamisionari wa Peramiho/Songea. Walikuwa na bahati sana wanamaliza tu kupiga zile picha na simu inalia/ita na ndiyo tukapewa habari kuwa mama yetu mpenzi hatunaye tena. Ndiyo maana hili gazeti/picha hii ni kumbukumbu kubwa sana kwangu.
NITAKUKUMBUKA NA KUKUPENDA DAIMA MAMA!!

Thursday, August 16, 2012

HII KALI NAONA IWE PICHA YA MWAKA:- MWANAUME AFUNGA NDOA KANISANI NA WANAWAKE WATATU KWA SIKU MOJA!!!

Sijawahi kuona wala kusikia tukio kama hili kaaazi kwelikweli..na tena ni mpya. Mwanamke mmoja tu kazi kwelikweli je watatu na tena kwa mpigo. Nimeshindwa kuvumilia kushangaa peke yangu nimeona niwashirikishe na wenzangu.  

NYUMBANI NI NYUMBANI:- HAPA NI TASWIRA YA PERAMIHO!!!

Kwa vile jana tulikuwa tumeshafika Songea mjini. Nimeona tuendelee  leo  na kuangalia taswira ya hapa Peramiho kwetu. Hapa kuna huduma nyingi sana kama wengi mnavyojua, HOSPITALI, DUKA LA VITABU/MAGAZETI na bila kusahau  kuna bonge la KANISA pia SEMINARI pia unaweza kupata vyakula vya aina mbalimbali....ALHAMIS NJEMA!!!!

Wednesday, August 15, 2012

WALALAMIKIA UBOVU WA MIUNDOMBINU YA STENDI SONGEA!!!

Katika KIPENGELE CHETU CHA JUMATANO YA MARUDI LEO NIPO SONGEA NA NINGEPENDA MUUNGANE NAMI...HABARI HII NIMEIPATA HAPA KARIBUNI....
Stendi ya Songea ikiwa katika hali mbaya.
Na Gideon Mwakanosya, Songea
BAADHI ya wakazi wa Halmashauri ya manispaa ya songea wakiwemo abiria wameulalamikia uongozi wa manispaa hiyo kwa kushindwa kukarabati miundombinu ya kituo kikuu cha mabasi cha mjini Songea na kusababisha adha kubwa abilia na baadhi ya magari kukwama hasa wakati wa kipindi cha masika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana abiria hao wameeleza kuwa hali ya kituo cha mabasi cha Songea kwa muda mrefu kina hali mbaya ambapo kwa kipindi cha mvua kunakuwa na mashimo ambayo hujaa maji na kusababisha magari ya kubeba abiria kukwama katikati ya kituo hicho
Wameeleza zaidi kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakiulalamikia uongozi wa halmashauri hiyo kuhusu kuwepo miundombinu mibovu kwenye kituo hicho bila kuwepo mafanikio jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kubwa kwa wakazi wa songea wakiwemo abiria .
Mmoja kati ya wananchi hao John Komba mkazi wa Mbinga alisema kuwa hali ya kituo hicho ni mbaya sana hasa kwa wakati huu wa kiangazi ambapo kumekuwepo na vumbi ambalo limeonekana kuwa ni kero kwa watu wanaoingia na kutoka kwenye kituo hicho kwa miguu hivyo ameuomba uongozi wa Halmashauri kuona umuhimu wa kumwagia maji kwa lengo la kupunguza kero ya vumbi lililokithiri
Naye Sebastian Nombo mkazi wa kijiji cha Kihangimauka kilichopo wilayani Mbinga alisema kuwa ipo aja kwa uongozi wa Halmashauri ya manispaa ya Songea wakiwemo madiwani kuona umuhimu kwenda kujifunza jinsi mbinu wanazozitumia kuboresha miundombinu mbalimbali ya barabara za halmashauri ya wilaya ya mbinga pamoja na mikakati waliyonayo ya kukijenga kituo kipya cha kisasa cha mabasi cha mjini mbinga.
Nombo alieleza zaidi kuwa inasikitishwa sana kuona hali mbaya ya miundombinu ya kituo kikuu cha mabasi cha mjini songea ambacho kipo makao makuu ya mkoa wa Ruvuma hivyo ni vyema uongozi wa halmashauri hiyo ukachukua hatua za haraka kukifanyia ukarabati kituo hicho cha mabasi ambacho kinaonekana kuwa ni kero kwa wakazi wa Songea.
Mmoja wa wamiliki wa magari wa kusafirisha abiria kati ya Songea na Dar es salaam ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kuwa ushuru wa magari yakiwemo mabasi yanayoingia kwenye kituo kikuu cha mabasi cha manispaa hiyo umekuwa ukitolewa kila siku lakini Halmashauri hiyo imeshindwa kukifanyia matengenezo jambo ambalo limeonekana kuwa ni kero kwa abiria hasa wakati mvua zinaponyesha kunakuwa na madimbwi ya maji ambayo husababisha magari kupita kwa taabu katika kituo hicho.

Mmoja wa wafanyakazi wa mabasi ya SAJDA yanayosafirisha abiria kutoka songea kwenda Mbinga Oddo Nchimbi alisema kuwa magari madogo yanayoingia kwenye kituo hicho (TAXI) Halmashauri hiyo imekuwa ikiwatoza shilingi 500 kila siku wakati magari yenye uzito wa tan 1 nusu hadi tani 7 kila anapoingia kwenye kituo hicho hutozwa shilingi 1000 kila siku na magari makubwa yakiwemo ya kusafirisha abiria kuanzia tani saba na kuendelea kila yanapoingia hutozwa shilingi 2000 kila siku lakini hali ya kituo hicho cha mabasi ni mbaya.
Alisema kuwa abiria wanayoijua stendi hiyo hasa wakati wa masika wamekuwa hawapandii mabasi ndani ya kituo na badala yake wamekuwa wanapandia nje ya kituo kwa kukwepa adha ya tope .
Kwa upande wake kaimu wa mkurugenzi wa manispaa hiyo Naftari Saiyori alipoulizwa kuhusiana na kero hiyo alikiri hali ya kituo cha mabasi ni mbaya lakini alieleza kuwa halmashauri yake inampango kabambe wa kujenga kituo kikuu cha mabasi cha kisasa huko katika eneo la msamala ambapo alidai kuwa mpango huo uko katika hatua ya upembuzi yakinifu na kwamba kwa hivi sasa kutakuwa na gari la maji litakuwa linapita kwa wiki mara tatu kwa lengo ya kupunguza kero ya vumbi iliypo kwenye kituo hicho.
TUKUTANE TANA KATIKA KIPENGELE HIKI CHA MARUDIO JUMATANO IJAYO PANAPO MAJALIWA!!!!!

Tuesday, August 14, 2012

NIMELIPENDA GAUNI HILI JAMANI..!!

Mdada huyu kila nguo anayoivaa inamkaa utafikiri ndo ilitengenezwa kwa ajili yake..Ingekuwa hivi na kwa sisi wengine ingekuwa bambi kweli..Nimelipenda gauni hili jinsi lilivyo hakuna makolombwezo mengi, rangi nzuri na la heshima yaani ndefu.... Ngoja nitaichukua picha hii nikashone hivyo Je? unafikiri nitapendeza kama mdada huyu?

METHALI ZETU:- METHALI ZAFAA SANA KWA MAFUNDISHO YA ADILI!!!!

1. Penye urembo ndipo penye urimbo.
2. Radhi ni bora kuliko mali.
3.Siku utakayokwenda uchi, ndiyo siku utakayokutana na mkweo.
4. Ukitaka kula nguruwe, chagua iliyenona.
5. Ulipendalo hupati, hupata ujaliwalo.
6. Ungelijua alocho nyuki, usingekula asali.
7. Vyako, vyako na mwenzio; vikikupata ni vyako peke yako.
8. Wagombanao ndio wapatanao.
9.Yote yangáayo usidhani ni dhahabu.
10. Zimwi likujualo, halikuli likakwisha.
Tusisahau methali zetu, tuwetunazitumia katika mafundisho. Pia tuwaambia na kizazi kijacho. Maana hii ndio asili yetu......

Monday, August 13, 2012

TUANZE JUMATATU HII NA PICHA HII YA WAREMBO WA KINGONI!!!

Picha:- Ni ya wanawake wa KINGONI (mzimba) hapa ni mapema miaka ya 1900.... Nimeipenda picha hii maana inaonyesha jinsi wanawake  hawa wanavyojali urembo wa asili ebu watazame...inavutia kwa kweli. JUMATATU NJEMA...

Sunday, August 12, 2012

SALA YA LEO NI KUWAOMBEA WATU WOTE DUNIANI!!!



Salam Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu. Amina. JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI NA WOTE MNAPENDWA!!!!

Saturday, August 11, 2012

TUMALIZE JUMAMOSI HII KWA MLO HUU:- UGALI KWA MLENDA/BAMIA HALAFU KUKU!!!


UGALI WA MAHINDI
MLENDA /BAMIA AMBAYO HUPIKWA KWA KUCHANGANYA NA MBOGA YA MABOGA..Msiogope,,,yaani ugali na mletu tu ....hapana
atachinjwa na huyu jogoo akijitokeza mchinjaji kwani mwenyewe naogopa...Kwa hiyo jitokezeni ...
KARIBUNI SANA..KWA WENGINE SASA NI ASUBUH, WENGINE MCHANA , WENGINE WANAENDA KULALA NA HAPA SASA NI MUDA WA KUPIKA CHAKAULA CHA JIONI KWA HIYO KARIBUNI SANAAAAA....

CHEMSHA BONGO YA JUMAMOSI YA LEO!!!!

Nani anapata mshahara bila kufanya kazi hata siku moja katika maisha yake yote?
JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE!!!

Friday, August 10, 2012

TUANZE MWISHO WA JUMA NA WIMBO HUU:- NAKUPENDA


NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA NA WOTE MNAPENDWA!!!!

Thursday, August 9, 2012

NIPENDAVYO MSIMU HUU WA JOTO NI KAMA HIVI KWENDA MSTUNI NA KUPATA VITU KAMA HIVI!!!

 Hapa ni blåbär/ blueberries kwa kiswahili sijui zinaitwaje anayejua naomba mnisaidie...Basi leo jioni yangu ndo imesiha hivi kwenda mstuni kuchuma ..bluberries unaweza kula kama zilivyo,kula na maziwa, kutengeza keki, kutengeneza kinywaji, kutengeza jam/jelly...nk. ..Halafu nikakutana na ugonjwa wangu.......
...UYOGA..Hakika nikiwa mstuni kuchuma/kutafuta uyoga hakuna mtu anaweza kunipita...nakuwa mawazo yote ni uyoga tu na leo nimepata lita 2...nadhani utakuwa mlo wa jioni hii. Kitu kimoja nipenda wakati huu wa joto hapa ni mambo haya kwenda mstuni na kupata vitu freshi kabisa ...kama NYUMBANI...KARIBUNI TUJUMUIKE....

FIKRA/WAZO LA LEO:- UTOFAUTI WA BINADAMU JINSI ULIVYO!!


Nimekuwa nikifikiri sana jinsi binadamu tulivyo tofauti. Sio kimaumbile tu LA HASHA. Bali  ni kiMATENDO, kiMAWAZO/kiFIKRA na  kiTABIA. Kwa mfano: Kuwa na ile tabia ya UMIMI/kijionea huruma, yaani mtu anajua amefanya kosa, lakini hata hivyo anaona wewe aliyekutendea unamwonea tu.Anataka uwe upande wake.
Halafu hii ya kuwa na HASIRA ZA HARAKA ambazo watu wengi inakuwa ngumu kusamehe hata kitu kiwe kidogo kwako kinakuwa kikubwa. Sababu kubwa wanakuwa wameumizwa sana na yule aliyemuumiza mwenzake anaona si umizo/maumivu. Lakini kuna wengine ni wepesi sana kusamehe hata iweje sasa sijui wanasamehe kweli au?
SWALI LANGU ambalo nimekuwa nikijiuliza kila siku:- Je? kama wote tungekuwa hivyo dunia hii ingekuwa? Na Je? kundi lipi ni jema?

Raymond Mkandawile na Bibie Janeth Manongi tulifunga pingu za maisha!!!


Hello ndugu,mimi ni mdau na mmiliki wa mtandao wa mkandawilejr.blogspot.com
tafadhali naomba niwekee taswira hizi za siku ya harusi yangu.
Hapo juu ni taswira mbalimbali za siku hiyo ya kihistoria ya tarehe 4/08/2012ambapo mimi Raymond Mkandawile na Bibie Janeth Manongi tulifunga pingu za maisha  huko jijini mbeya katika kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa Sinai na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Teku uliyopo maeneo ya Block T.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushirikiano wenu.
Mr. Raymond Mkandawile
BA (HON) in Business Studies
University of Wales Institute of Cardiff(UK)
Mob; +255656-561-314
Email; raymonds19@yahoo.com
Website;http://www.mkandawilejr.com




Maharusi wakiteta jambo baada ya kunganishwa na kuwa mwili mmoja

Bwana na bibi Harusi wakiwa nanyuso za furaha...
Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kuwatakieni maisha mema ya NDOA na pia kuwakaribisheni katika maisha haya ya Ndoa. Ambayo yanahitaji UVIMILIVU NA USIKIVU PIA MAWASILIANO. MAISHA MEMA/HONGERENI SANA.



Wednesday, August 8, 2012

LEO TUNAADHIMISHA SIKUKUU YA WAKULIMA -NANENANE...MWAKA JANA 2011 MSAMALA/SONGEA!!!

 Mwaka jana siku kama ya leo tulikuwa  tunajumuika kwa karibu kabisa kushrehekea sikukuu hii na hapa mnaona baadhi ya picha tulizopiga....Ndizi aina: BUKOBA
 Ndizi aina: JAMAICA
 NA HAPA NI BIRINGANYA
Na hapa ni KABEJI AINA YA FI..Mambo yote haya yilifanyika katika mji wa Songea /MSAMALA......WAKULIMA OYEEEEE. NILIIFURAHIA SANA SIKU HII:-)

MISHAHARA HAITOSHI+TUACHE UZEMBE KAZINI

NI ILE JUMATANO YETU YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO NIMEMTEMBELEA JIRANI YANGU..SI MWINGINE TENA NI GONGA HAPA. PIA KWA KUJIKUMBUSHA MAONI  YALIYOPITA GONGA HAPA PIA, KWANI NILISHAWAHI KUIWEKA HAPA MAISHA NA MAFANIKIO..ILA NI NZURI MNO..HAYA KARIBUNI....
------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Makala hii nimeipenda ndiyo maana nikaamua kuiomba  Kwani najua nakamilisha lengo lake la kuifanya isomwe na wengi.
Katika nchi yetu ya Tanzania, watu wanalalamika muda wote kuwa mishahara haitoshi. Gharama ya maisha ni kubwa kuliko mishahara. Hata kwa kuzingatia mahitaji muhimu tu, watu wengi wana haki ya kusema kuwa mishahara haitoshi.
Malalamiko ya mishahara kuwa haitoshi yanasikika duniani kote. Hapa Marekani, shida kubwa inayowakabili watu ni kulipa bili na madeni mbali mbali. Marekani ni nchi ya madeni. Kutodaiwa popote ni sifa nzuri katika utamaduni wa Tanzania. Lakini Marekani, sifa inakuja kutokana na umakini wa kulipa madeni. Mishahara ya Wamarekani wengi inaishia kwenye kulipa madeni. Kwa hivi, nao wanalalamika kuwa mishahara haitoshi.
Wako Watanzania ambao wana mishahara ambayo ingeweza kutosheleza mahitaji muhimu. Tatizo ni kuwa dhana ya mahitaji muhimu ina utata.
Tunaweza kusema mahitaji hayo ni chakula, malazi, mavazi, matibabu, elimu, na usafiri. Lakini, katika utamaduni wetu, orodha ya mahitaji muhimu ni kubwa zaidi ya hiyo. Kumlipia ada mtoto wa shangazi ni wajibu. Kuchangia gharama ya msiba kwa jirani ni wajibu. Kama una gari, kumpeleka mtoto wa jirani hospitalini ni wajibu.
Kwa msingi huo, hakuna Mtanzania ambaye anaweza kusema mshahara wake unatosha. Suala haliishii hapo. Je, ukitembelewa na marafiki, utakaa nao tu nyumbani na kuongea nao, au unatakiwa kuwapeleka mahali wakapate kinywaji? Je, unaweza kuacha kuchangia gharama za arusi ya rafiki yako?Tukizingatia hayo yote, mishahara haitoshi.
Watanzania wengi wana tabia ya kutumia fedha kwa mambo mengi mengine, ambayo umuhimu wake ni wa wasi wasi, kama vile bia. Kwa Watanzania wengi, bajeti ya bia ni kubwa sana. Kwa mtu anayekunywa sana bia, mshahara hauwezi kutosha. Lakini je, bia ni kitu muhimu namna hiyo?
Kwa upande wa pili, Watanzania tunapaswa kutafakari dhana ya mshahara. Mshahara unapaswa kuwa malipo muafaka ya kazi ambayo mtu anafanya. Kazi ndio msingi. Lakini, kuna tatizo kubwa Tanzania.
Watu wengi hawafanyi kazi kwa bidii. Muda mwingi wanatumia kwenye gumzo. Lakini wanategemea kulipwa mshahara, na wanalalamika kuwa mishahara haitoshi. Je, wanastahili hizo hela wanazopewa kama mshahara? Je, wakiongezwa mishahara, wataongeza juhudi kazini au wataendelea kukaa vijiweni na kupiga soga?
Huku Marekani, watu wanachapa kazi sana. Mshahara unatokana na kazi. Mtu asipofika kazini, halipwi. Akichelewa, malipo pia yanapunguzwa. Kwetu Tanzania mambo si hivyo. Mtu akishaajiriwa, anategemea kupata mshahara wake kila mwezi, hata kama anatumia masaa mengi kijiweni. Je, ni bora kuanzisha utaratibu wa kuwalipa wafanyakazi kwa yale masaa wanayokuwa kazini tu, na kupunguza mshahara kwa masaa wanayokuwa kijiweni?
-----------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nami nataka kuongezea ni kwamba hapa Sweden ni karibu sawa na huko Marekani. Yaani hapa hata kama upo likizo hulipwi, inategemea ni likizo gani. Halafu kama unaumwa na halafu huendi kazini zile ziku mbili za kwanza hulipwi kitu kwa hiyo hapo ukiumwa basi ujue mshahara wako unapungua/unakatwa. Kwa hiyo kwa mtindo huo utakuta hata kama mtu unaumwa unajikaza na kwenda kazini. Kwani mshahara wanaokata ni mkubwa sana na ukizingatia maisha nayo yapo juu.
PANAPO MAJALIWA TUKUTANE TENA JUMATANO IJAYO NA RUDIO JINGINE...KILA LA KHERI!!!!

Tuesday, August 7, 2012

HAYA TWENDEE, TWENDE,TWENDE USICHOKE...!!!!

 Huyoooo anakuja, huyooo anakuja..anakuja anakuja....
.....na hapa ndiyo nimefika  golini...hii ilikuwa leo asubuhi...nimepanga kupata dhahabu ya olimpiki ..LOL
mazoezi tu kwa ajili ya afya ..ngoja nikapalilie bustani yangu sasa...

FILAMU YA WRONG LANE KUWA MTAANI WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA! Read more: FILAMU YA WRONG LANE KUWA MTAANI WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA!



RASTEMWI PRODUCTIONS yenye makao yake jijini Dar es Salaam itaingiza sokoni filamu yake mpya inayoenda kwa jina la wrong LANE ‘njia POTOFU’ wakati wowote kuanzia sasa.

Akiongea na WAVUTI.COM, mkurugenzi mtendaji wa RASTEMWI PRODUCTIONS, Dr. Rama Mwiru, amesema filamu hiyo imeshirikisha wacheza filamu nyota wa Tanzania kama Miriam Jolwa ‘jini kabula’, Rose Michael ‘zambarau’, Gilbert Sindani ‘mack’, Ibrahim Banane ‘mzee katembo’, na Kulwa Kikumba ‘dude aka dr lugusha’. Ma-star wengine walioshiriki kwenye wrong LANE ni pamoja na Salma Jabu ‘Nisha’, Mariam Mndeme, Kojack Chillo, Michael Philipo ‘kojack’, Alice Bagenzi ‘rayuu’, Mustafa Matambo na mwanamuziki maarufu wa zouk Rehema Tajiri.

Filamu ya wrong LANE pia inaingia sokoni ikiwa imeshirikisha wacheza filamu wapya na wenye vipaji vya hali ya juu kama Salma Tuesday ‘salma chuzi’ ambaye ni mtoto wa ma-supa stars wa bongo movie, Mr. Chuzi na Kabula. Wengine wageni lakini wenye vipaji vya hali ya juu ni Dhahabu Francis, Johnson George ‘john cena’, Salvina Stambuli, Mohamedy Ally, Fadhil, na Dr. Rama mwenyewe.

Dr. Rama amesema wrong LANE imelenga kuwaburudisha na kuwapa mafunzo mbalimbali ya kimaisha watanzania na watu wengine wanaopenda filamu.

Monday, August 6, 2012

TUIMALIZE JUMATATU HII KWA WIMBO HUU: LEKA DUTIGITE VIDEO-KIGOMA....BOMBI KWELIKWELI


Nimeipenda wimbo huu na nimeona nisicheze peke yangu JIONI N JEMA. EEEH, EEEHH KIGOMAAA LEKA DUTIGITE...Duh! nipo hoi hapa:-)

TUANZE JUMATATU HII KIHIVI:- KILIMO....UKIITUMIA MIKONO YAKO KAMA INAVYOTAKIWA :-MATOKEO YAKE NDIYO HAYA...UTAKUWA MLO WA MCHANA WA LEO MBOGA/MAJANI YA MABOGA!!!

MBOGA YA MABOGA KWENYE UNGO...
Ni furaha ilioje kuweza kula chakula ulichopande mwenyewe, hapa ni majani ya maboga na ndiyo yatakuwa mlo wa mchana wa leo:-) Napenda kuwakaribisheni wote karibuni tujumuike..Si mnajua kulima analiama mmoja lakini walaji ni wengi.... Ndiyo nimeanza  kuitengeneza....

Thursday, August 2, 2012

Wednesday, August 1, 2012

HIVI HAPA NI SARESARE AU??? VITENGE NI VIZURI JAMANI

Kapulya na sketi yake ambayo imekuwa kauka nikuvee:-) naipenda sana...
 Naye huyu sijui ni sketi au gauni? nimeipenda hii picha/vazi hili...Ila duh! huyu mwenzangu mrefu sijui kavaa mchuchumio/raizoni;.)???