Showing posts with label kuku. Show all posts
Showing posts with label kuku. Show all posts
Thursday, May 14, 2015
MAPISHI:- LEO KATIKA KUSOMA SOMA NIMEKUTANA NA MAPISHI HAYA....
Ni kuku mzima ambaye nimempaka viungo na halafu nimemweka juu ya kopo la bia na na halafu nimemchuma. Nyama yako ilikuwa tamu sana. Jaribu na wewe nakwambia utajiuma...unaweza kula na wali, viazi au ugali, mimi nilikuta na kachumbali/saladi. Siku na Jioni njema. Kapulya:-)
Friday, November 15, 2013
HAYA NI MAPISHI YA IJUMAA YA LEO KUKU.....KARIBUNI
Ijumaa ya leo itakuwa kuku ambayo ni:- kuku mzima, viazi, karoti, kitunguu, kitunguu saumu, tangawizi, nyanya kopo, binzari, mafuta, chumvi na maji..... Picha zaidi zinakuja baada ya muda tu....Kwa hiyo mnakaribishwa kujumuika nasi.
Na hapo ndivyo ilivyoonekana sahani yangu...wali, kuku, kiazi, karoti na mboga majani /figili ambayo imeliwa na mikono yangu mwenyewe......Karibuni chakula kipo kingiiiii kweli. Jioni njema sana na panapo majaliwa tutaonana tena kesho.
Na hapo ndivyo ilivyoonekana sahani yangu...wali, kuku, kiazi, karoti na mboga majani /figili ambayo imeliwa na mikono yangu mwenyewe......Karibuni chakula kipo kingiiiii kweli. Jioni njema sana na panapo majaliwa tutaonana tena kesho.
Tuesday, November 20, 2012
HAPA SIJUI PAPOJE? NAONA HII IWE PICHA YA WIKI HII!!!
Sijawahi kuona watu wakifunga kuku kamba..hapa naona dogo amesha chagua kitoweo cha sijui mchana au jioni? au labda ndo kapata kitu cha kuchezea? MUWE SALAMA WOTE !!!
Tuesday, June 26, 2012
JE HAPA NI ILE NJOO TULE BASI.....AU?
Hata wanyama na ndege nao wana tabia kama BINADAMU...unafikiri hapa JOGOO ANASEMA NINI KWA HUYU KUKU JIKE?
Saturday, May 5, 2012
HUU NDIO MLO WANGU WA JIONI HII YA LEO KARIBUNI!!!....
..NI kuku TANDORI kwa chips (viazi) pia kachumbali kwa mbaliiiii. Msiwe na wasiwasi kuna zaidi kwa hiyo anayejisikia kuja KARIBU SANA:-) JIONI NJEMA YA JUMAMOSI YA LEO!!!
Friday, September 2, 2011
CHAKULA NILICHOANDAA na KULA JIONI LEO/IJUMAA HII KARIBUNI TUJUMUIKE!!
Wednesday, November 19, 2008
MAISHA YA MAMA KUKU
Ebu angalieni hapa halafu fananisha na hapo juu. Maisha ya kuku hayaachani sana na ya binadamu. Kwani kuku ana bahati yeye anaatamia mayai wiki kama tatu hivi. Hapo tayari anatotoa vifaranga na atavitunza na kuvilinda na maadui wabaya kama vile mwewe na kadhalika. Baadaye wakiwa wakubwa anawadonoa hapo ndio kuwaambia SAMAHANI sasa muda umefika kwa ninyi kujitegemea.
Subscribe to:
Posts (Atom)