Thursday, September 27, 2018

LIJUI TUNDA LA PAPAI NA FAIDA ZAKE KWA AFYA......

Papai, tunda lenye ladha nzuri kama sukari, siyo tu ni tamu kulila, lakini ni chanzo kikuu cha virutubisho muhimu vinavyotoa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo yale hatari ambayo huchukua maisha ya watu kila kukicha. 

Leo soma faida za tunda hili ili ujiepushe na maradhi ambayo hutokea pale mwili unapokuwa na kinga ya mwili dhaifu kinga dhidi ya magonjwa ya moyo utaona kwamba maradhi ya moyo yana kinga karibu katika kila tunda au chakula cha asili.

Wiki mbili zilizopita tumeona vyakula kama karanga, korosho vinavyoweza kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo, wiki hii pia tunaona papai nalo limo kwenye orodha ya vyakula vinavyotoa kinga ya ugonjwa huo.

Inaelezwa kuwa papai ni kinga ya ugonjwa wa moyo unaotokana na kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis ) na ule unaotokana na kupatwa na kisukari (diabetic heart disease). Kwa kula papai mara kwa mara, unajiepusha na magonjwa hayo yanayosababisha kifo haraka.

HUIMARISHA MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonyesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.

KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.

KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho aina ya ‘beta-carotene’ kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k

NURU YA MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.



TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku.

CHANZO JAMIIFORUMS:- AHSANTE SANA KWA ELIMU NAMI NIMEONA NISIELIMIKE PEKE YANGU NIKAONA NIWEKE HAPA KINARAZANI.

Friday, September 21, 2018

NAWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA...HAYA TUFURAHI PAMOJA NA KIPANDE HIKI CHA NGOMA...



Tuwukeee tuwukeee kamwimbo katamu sana. Natamani kuungana  nao na kucheza ila nabaki kucheza peke yaangu....NAWATAKIENI MWISHO WA WIKI HII UWE WENYE FURAHA NA AMANI! KAPULYA WENU

Thursday, September 20, 2018

PALE UNAPOLIMA UNATUMAINA KUVUNA NA SASA MATOKEO TUNAYAONA

Hapo mwaona baadhi ya mazao niliyovuna nyanya, tikiti maji ambalo ndani ni njano tamu sana, zabibu  na pia mwaona kwa pembeni ni pilipili  ni raha sana  kula vyakula ulivyolima mwenyewe kwa mikono yako. KARIBUNI TULE NDUGU ZANGU.

Thursday, September 13, 2018

FAHARI YA MKULIMA NI KULIMA NA KULA ALICHOVUNA....KAZI YA MIKONO YAMGU...

kula vyakula unavyopanda mwenyewe ni kwamba ule utamu unazidi...nilipanda hili tunda aina ya tikiti maji lakini lenyewe ni la njano ndani  ha picha hapo chini yaonyesha vizuri zaidi. Nilianza kulifuatilia hili tunda  kwa ukuaji wake kama uonavyo ua
Na sasa lishakuwa kubwa yaani ni kama boga ila bado kukomaa ni kwamba ukomaaji wake ni mpaka hili ganda liwe njano njano....
Na leo siku rasmi ya kuvuna na kula. Utakula ulichopanda, hakika najisikia fahari sana ....

Tuesday, September 11, 2018

UJUMBE WA JUMANNE YA LEO KUTOKA KWANGU KUJA KWENU...

UJUMBE:- Kuna muda inabidi uanguke chini zaidi ya hapo ulipo ili uweze kusimama na kukaa juu zaidi ya hapo ulipo...
Hata siku moja usijaribu kukata TAMAA. Dharau, matusi na kebehi: havimzuii mtu kungára.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA HAPA HAPA...KAPULYA WENU.

Monday, September 3, 2018

TUANZE MWEZI HUU WA TISA NA WIKI YAKE YA KWANZA KIHIVI .....

Nikiangalia hawa watoto warukapo kamba natamani siku, miaka irudi nyumba ili nami niweze kuruka tena ...UJUMBE:- WAACHENI WATOTO WAWE WATOTO.