Showing posts with label Safarini. Show all posts
Showing posts with label Safarini. Show all posts

Tuesday, September 25, 2012

SINA WASIWASI NIPO SAFARINI NIKIWA NA MLINZI WANGU...!!!

Nimeipenda picha hii imenikumbusha Mgazini, huu udongo jinsi ulivyo mwekundu hapo kuvaa nguo nyeupe inabidi uwe msafi sana. Wanafunzi walikuwa/wanapata shida sana maana ukivaa shati jeupe siku moja tu  ni lazima kufua. Halafu nimeipenda hii picha jinsi mama huyo anavyosafiri huku mbwa wake katangulia kama mlinzi. Mlinzi wa asili.

Saturday, December 27, 2008

BLOG MAISHA SAFARINI = YASINTA


Blog Maisha, nimeona ni vema niage sitakuwa hewani kwa muda kidogo NASAFIRI. Nakwenda Peramiho, nakwenda ungonini. Nakwenda kula likolo la nanyungu na malombi (mahindi ya kuchoma) Wangoni wote myumwike?
Walongo Vangu!!!!
Tutaonana karibuni tena. KWA HERINI KWA MUDA. NAWATAKIENI WOOOOTEEE MWAKA MPYA 2009.