Saturday, December 31, 2011

KHERI KWA MWAKA MPYA 2012!!

Marafiki wapendwa!

Wacha mwaka mpya huu ulete mafanikio, amani, mwanga na furaha ndani ya maisha.....

Nakuombea wewe na familia yako furaha na mafanikio. KATIKA MWAKA MPYA 2012.

KHERI SANA KWA MWAKA MPYA 2012. KAPULYA!!!

Friday, December 30, 2011

Wanawake hukubali kufa huku wakiona......!

Tunajua wote kwamba, hutokea wanawake wakateswa sana kwenye uhusiano wao wa kindoa au kimapenzi na bado wakaendelea kukaa tu kwenye uhusiano huo. Inafikia hadi mtu anakufa huku akiona kabisa. Watu wengine huiita hali hii kuwa ni ujinga na wengine huita kulogwa au huelezea hali hii kwa njia ambayo haiwapi haki wanawake hao. Zipo sababu nyingi ambazo zinawafanya wanawake kuendelea kukaa kwenye ndoa ngumu, bila hata kufikiria kuondoka. Sababu nyingine zinaweza kuonekana kama kituko, lakini ndizo zinazowafanya wafie kwenye ndoa.Kuna ile sababu kwamba, hawajui ukubwa wa kiwango cha mateso. Hii hutokana na kwamba, baada ya kuzoea mateso, mwanamke hufikia kuamini kwamba, hayo siyo mateso, bali ndivyo ndoa inavyotakiwa iwe. Kuna sababu ya kukosa marafiki, ndugu au jamaa wa karibu. Na kwa sababu hana watu wa aina hiyo, inakuwa vigumu kwake kuwa na mahali pa kukimbilia ili aweze kupata nafasi ya kujiandaa kuanza upya maisha.Kuna wanaoendelea kukaa kwa sababu dini zao zinawaambia, hawana budi kukaa, kwani wameshakuwa mwili mmoja na waume zao na hivyo hawawezi kuondoka. Wanafikiria iwapo wataamua kutoroka, viongozi wao wa dini watawaona vipi na waumini wenzao watachukuliaje jambo hilo. Kwa hiyo, wanaishi kwenye ndoa hizo kwa sababu ya dini, siyo kwa sababu yao binafsi. Halafu kuna suala la kupenda. Utegemezi wa kihisia huwa unaitwa kupenda. Kwa hiyo mwanamke anasema anampenda fulani kiasi kwamba, hawezi kumwacha, wakati ukweli ni kwamba, anamtegemea mwanaume huyo kihisia.Wanawake wanaoteswa kwenye ndoa, huwa wanajidanganya kwamba, watamudu siku moja kubadili tabia hiyo a waume zao kuwafuja. Wanajiambia kwamba, kutukanwa, kupigwa, kudhalilishwa, na matendo mengine, siyo hiari ya hao waume wao. Hivyo wanaamini kwamba, kuna siku watamudu kuwasaidia watoke kwenye tabia hizo. Lakini wakati mwingine wanaume hawa watesaji, huwa wanajidai kusema kwamba, wanafanya mambo hayo bila kujua sababu na kuna wakati wanasema wamelogwa.Hujawahi kuwaona wanawake wanaokwenda kwa waganga kutafuta dawa ili waume zao wasiwapige, ati kwa sababu vipigo vyao vinatokana na kuchananywa na uchawi wanaofanyiwa na wanawake zao wa nje? Mwanamke anaamini kabisa kwamba, mumewe hamjali na anamdhalilisha kwa sababu ya kulogwa!Mwanamke anaweza kujiambia kwamba, kwa sababu mume wake kuna wakati anamtendea wema, hata kama ni moja, basi anampenda na hayo mengine mabaya, yatakwisha au ni bahati mbaya. Mwanamke pia anaweza kufikiri kwamba, akijitahidi sana kumfurahisha mumewe, mume huyo atabadilka na kuwa na tabia nzuri. Hivyo hujipendekeza na mwanaume habadiliki na mateso yanaongezeka. Kuna wanaomudu kuishi kwenye uhusiano huu wa sababu, wamemudu kukandamiza, kupunguza ukubwa wa maumivu. Wanajiambia kwamba, wanavyotendewa siyo vibaya sana. Mwanamke anaweza kujiambia, ‘alinipiga kidogo tu, tena mara mbili kwa mwezi, kuna wanaopigwa kila siku.’ Huyu amehalalisha kipigo na mateso, hawezi kuondoka.Kuna wanawake wanaoamini kwamba, ndoa inajengwa na kuimarishwa na mwanamke au kuvunjwa na mwanamke pia. Kuna andiko moja katika Biblia hutumiwa sana kuwatisha, linalosema, ‘Mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.’ Kwa hiyo wanapofikiria kuondoka, hufikiria kwamba, watu watajua na kumzonga au kumdharau kwa sababu ameshindwa kulinda ndoa. Wengine ni woga tu, kwamba, wakiondoka waume zao watawalipizia visasi au watawasumbua. kuna wakati waume wenyewe ndiyo wanaokuwa wamewatisha kwa kiwango hicho.

**********Nimekutana na hii jamii forum na nimeona si vibaya kama nikiweka hapa...............

IJUMAA NJEMA:- HII ITAKUWA PICHA YA KUFUNGIA MWAKA 2012!!!

Kabla mwaka 2011 haujaisha/haujafikia tamati nimeona picha hii iwe ya kufungia mwaka kwa blog ya MAISHA NA MAFANIKIO. Pia nachukua nafasi hii kusema mawili matatu kuwa mwaka huu umekuwa na matukio mengi mazuri na mabaya lakini hata hivyo sina budi kusema NAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU kwa yote. IJUMAA NJEMA!!!

Thursday, December 29, 2011

YOU CAN HIRE THIS CAR IN DAR ES SALAAM!!!






The car with a driver, will only cost you 500SEK + petrol for one day in the city of Dar-es-Salaam.
About 60 Euro, 48 pounds, or 75 USD.For trips outside Dar contact us.
Torbjörn Klaesson +46 70 2217044mail: matetereks@gmail.com OR....
Yasinta Ngonyani +46 70 2569176 mail: ruhuwiko@gmail.com






Wednesday, December 28, 2011

Tuesday, December 27, 2011

"UJUMBE ULIOVUNJA REKODI KATIKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO MWAKA 2011

Ndugu wasomaji wa blog hii ya MAISHA NA MAFANIKIO, katika kupitia mada mbalimbali nilizowahi kuweka humu ili kupata ile ambayo ilivuta hisia za wasomaji wengi na kuleta changamoto, nimevutiwa na ujumbe huu ambao ulileta vuta ni kuvute miongoni mwa wadau wa blog hii. Kwa hiyo basi nimeichagua ujumbe huu kuwa ndio ujumbe uliovunja rekodi kwa mwaka 2011. Natoa shukrani kwa wadau wote mlioshiriki katika kuchangia ujumbe huu. Naomba muungane nami katika kujikumbusha kile kilichotokea katika ujumbe huu.


NIMEJIFUNZA KUTOKA KWA CHRISTINA




Christina akiwa amelazwa KCMC Moshi

Akiwa mjini Arusha akifanya manunuzi baada ya kuruhusiwa kutoka KCMC

Akimsimulia rafiki yaka Laila, walipokutana mjini Arusha

Huwa tunajifunza kupitia kwa wengine hususan kwa yale mambo magumu na yaliyojificha. Naomba nikiri kwamba pamoja na kusoma ushuhuda mbalimbali kupitia magazeti na blogs, lakini sikuwahi kuzipa uzito shuhuda hizo. Naomba nikiri kuwa tukio la hivi karibuni lilipompata rafiki yangu na wifi yangu Christina aishiye Dar es salaam Tanzania nimejifunza kuwa imani ikichangizwa na ibada ina nguvu sana.Christina Kaluse ni wifi yangu wa hiyari ambaye ni mke wa mwanablog mwenzangu na ambaye ni mwanautambuzi anayetuelimisha kupitia kibaraza chake cha Utambuzi na Kujitambua, huyu si mwingine bali ni mwanablog Shaban Kaluse, ukitaka kusoma habari zake waweza kubofya hapa.Nimekuwa nikiwasiliana na Christina kwa takriban miaka miwili sasa, na tangu kufahamiana na familia hii ya mwanablog mwenzangu, nimejikuta nikiwa karibu nao tukiwasiliana mara kwa mara kama ilivyo kwa baadhi ya wanablog wengine.Nisiwachoshe, niwasimulie kisa cha kuandika kile nilichojifunza kwa wifi yangu huyu Christina au mama Abraham.Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumatatu ya Januari 31, 2011, majira ya mchana, nilipata ujumbe mfupi kupitia simu yangu ya kiganjani kutoka kwa Christina, na ujumbe wenyewe ulisomeka hivi, ‘Yasinta naomba uungane nami kwenye maombi, nimepofuka jicho moja’ .Ujumbe huo ulinishtua sana, nikaamua kumpigia simu ambapo tuliongea kwa muda mrefu sana.Kwa kifupi aliniambia kuwa mnamo siku ya jumatano ya Januari 19, 2011, akiwa dukani kwake, (Christina anamiliki duka la vifaa vya ushonaji na ubunifu wa mavazi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam) aliingiwa na vumbi kidogo kwenye jicho lake la mkono wa kushoto, na alijaribu kulisafisha jicho hilo kwa maji safi lakini halikupata nafuu na liliendelea kumuuma.Alikata shauri kurudi nyumbani kwake ambapo sio mbali na mahali ilipo ofisi yake, alipofika nyumbani aliendelea kulisafisha jicho lake hilo kwa maji safi, lakini halikupata nafuu yoyote.Usiku kucha hakulala pamoja na kumeza vidonge vya kutuliza maumivu.Ilipofika asubuhi akiongozana na mumewe walikwenda hospiali maarufu hapo jijini Dar iitwayo Regency ambapo alionana na daktari bingwa wa macho na baada ya vipimo iligundulika kuwa mboni ya jicho imepata kidonda na daktari huyo alidai kuwa huenda lile vumbi liliambatana na mchanga na hivyo wakati alipokuwa analisafisha ule mchanga ukawa umejeruhi mboni ya jicho hilo.Kumbe huo ukawa ni mwanzo wa safari ya jicho hilo kupofuka, Christina alinieleza kuwa pamoja na kupatiwa matibabu katika hospiali hiyo lakini hakupata nafuu yoyote na usiku kucha alikuwa akikesha kwa maumivu makali ya jicho hata pamoja na kumeza vidonge vya usingizi lakini hakupata lepe la usingizi.Ilipofika siku ya jumamosi ya January 29, 2011,ikiwa ni siku kumi tangu aanzwe na tatizo hilo, jicho likapoteza uwezo wa kuona na mboni ya jicho ikageuka na kuwa kama ina mtoto wa jicho, kwa maelezo yake Christina alisema kuwa hata yule daktari bingwa wa macho pale Regency alionekana kuchanganyikiwa kutokana na hali ile na alionekana kukata tamaa, lakini hata hivyo alimwandikia dawa nyingine na kumtaka akazitumie kisha arudi siku ya jumanne.Aliporudi nyumbani walishauriana na mumewe na wakakata shauri kuhamia katika Hospitali ya CCBRT ambayo ndiyo hospitali maarufu hapo nyumbani ambayo inasifika kwa kutibu matatizo mbalimbali ya ulemavu yakiwemo matatizo ya macho.Siku hiyo ya jumatatu ya Januari 31, 2011 aliyonitumia ujumbe mfupi, ndiyo siku ambayo alikwenda CCBRT. Baada ya vipimo, daktari aliyempima bila kutafuna maneno alimweleza waziwazi kuwa jicho limeshapofuka, na alimlaumu eti amechelewesha jicho huko vichochoroni mpaka limepofuka ndio anakwenda kwao…..Kauli hiyo ilimshangaza sana Christina, kwani tangu alipopata tatizo hilo alikwenda kupata matibabu kwenye Hospiali ya Regency ambayo inatambulika na inasifika kwa matibabu, sasa iweje alaumiwe na kuambiwa kuwa alikuwa vichochoroni? Christina alionesha kushangazwa kwake na maadili ya Daktari yule.Yule Daktari ambaye ni Mtanzania mwenzetu (Hospitali hiyo inayo pia wataalamu wa kigeni) alimweleza kuwa tiba pekee iliyobaki ni kuweka uzingativu kwenye kutibu kidonda tu, na hata akipona hataweza kuona kabisa kwani jicho limeshambuliwa na bacteria kiasi kwamba limeharibiwa kabisa. Hata hivyo alikiri kushindwa kubaini aina ya bakeria waliomshambulia, pamoja na kukwangua kidonda hicho na kupima maabara.Aliandikiwa aende siku ya Jumanne ya Februari 1, 2011, kwa ajili ya operesheni ndogo ya kuliweka dawa na kulifunga.Wakati naongea naye kwenye simu walikuwa wamekata shauri yeye na mumewe wamgeukie Mungu wakaamua waende kwenye maombi.Nilimuuliza zaidi ya mara mbili kuwa ana imani akienda kwenye maombi atapona, na alinijibu kwa kujiamini kabisa kuwa daktari pekee aliyebaki ni mungu.Ingawa tunatofautiana kimadhehebu, Christina yeye ni Msabato na mimi ni Mkatoliki, lakini nilimuahidi kuungana naye katika maombi.Ni kweli siku iliyofuata alinijulisha kuwa aliombewa na Mwinjilisti mmoja wa kanisa la Wasabato la Chang’ombe SDA aitwae James Ramadhan Rajabu na maumivu yakatoweka na jicho likafunguka na likaanza kuona siku hiyo hiyo….ingawa hata hivyo bado lilikuwa linaonekana kama lina mtoto wa jicho.Aliniambia kuwa anasafiri kwenda Moshi KCMC kuendelea na matibabu lakini bado imani yake kwa Yesu ni kubwa na anaamini atapona, kwani Mungu ndiye atakayekuwa Daktari mkuu atakayewaongoza Madaktari watakaomtibu huko KCMC.Tuliendelea kuwasiliana hata alipokuwa huko Moshi KCMC, na alinijulisha kuwa awali madaktari wa KCMC walikanusha kuwa jicho lake limepofuka baada ya vipimo, ingawa hawakuweza kuona aina ya bacteria waliomshambulia.Walishauri alazwe halafu watajaribu kuwasiliana na daktari mwingine bingwa aliyeko Nairobi ili kuangalia kama anaweza kuja hapo KCMC kushughulikia kesi yake ambayo hata wao iliwachanganya sana, hasa baada ya kuwaeleza kuwa CCBRT wameshindwa kutibu jicho lake.Siku iliofuata yule daktari kutoka Nairobi alifika na baada ya kulipima jicho lake mara kadhaa hakupata majibu ya kueleweka, aliamua kuchuna sehemu ya kidonda na kuchukua sampuli ambayo ingepelekwa Nairobi kwa ajili ya vipimo katika maabara kasha. Aliamuandikia dawa za matone ambazo zitazuia wale bacteria wasiendelee kushambulia jicho lake wakati akisubiri majibu.Katika kipindi chote alichokuwa amelazwa hapo KCMC akisubiri majibu ya vipimo vyake kutoka Nairobi, alikuwa akiendelea na maombi kwa kushirikiana na Mwinjilisti James pamoja na Wainjilisti wengine wa dhehebu lake la Kisabato aliowataja kwa majina ya Mwinjilisti Japhet Magoti Matotiwa kanisa la Manzese, na Mwinjilisti Benson Kilango Izoka wa kanisa la Bombo SDA Tanga.Baada ya siku tatu yule Daktari alirudi na majibu, lakini cha kushangaza alikuta kidonda kimepona kwa asilimia 75. Hali ile haikumshangaza yule daktari peke yake bali pia Madaktari wenzie nao walishangazwa na kule kupona kwake kwa haraka.Kwa mujibu wa majibu aliyokuja nayo, iligundulika kuwa jicho la Christina lilishambuliwa na Fangasi.Aliandikiwa dawa na siku iluyofuata ikiwa ni siku ya tano tangu alazwe Hospitalini hapo aliruhusiwa kurudi nyumbani Dar, lakini alitakiwa kurudi klinik baada ya wiki mbili ili kuangaliwa kama anaendeleaje.Baada ya kurudi Dar, aliendelea na dawa pamoja na maombi, na ilimchukua wiki moja tu kupona kabisa, na jicho kurudi katika hali yake ya kawaida.Aliporudi Moshi KCMC, Daktari alithibitisha kuwa amepona kabisa, na hakusita kuweka bayana kuwa kupona kwake kumekuwa ni kwa miujiza kwa sababu kutokana na hali ya jicho lake walidhani ingechukua muda mrefu hadi kupona.Jana nilizungumza naye kwa muda mrefu sana akinisimulia safari hii ndefu ya ugonjwa wake huo na jinsi maombi pamoja na imani ilivyomsaidia kupona kwa haraka.Kwa kweli nimejifunza jambo moja kubwa sana kutokana na mkasa huu uliompata wifi yangu huyu wa hiyari ya kutokata tamaa pale tupatapo changamoto za kimaisha kama vile ugonjwa na hali zetu kimaisha.Kama Christina angekata tamaa na kusikiliza ushauri wa Daktari wa CCBRT, ni wazi kuwa leo hii angekuwa amepofuka jicho moja. Lakini yeye mwenyewe alidai kuwa alikataa katu katu kukubaliana na maelezo ya Daktari yule na aliiambia nafsi yake kuwa jicho lake halijapofuka na halitapofuka.Naamini hata wewe unayesoma hapa kuna jambo utakuwa umejifunza.Napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Christina kwa kuwa na ujasiri wa kukabiliana na changamoto hiyo. Namuomba Mungu aendelee kuibariki familia yao, awape ujasiri wa kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha, na asiwape moyo wa kukata tamaa.Nimejifunza kutoka kwa Christina.
Na haya yalikuwa maoni ya wadau.....


Anonymous said...
dada yasinta ..nimeguswa sana na kisa cha christina..kwa sababu hakijatofautiana sana na cha mume wangu..kweli tunatakiwa tujifunze kutokata tamaa.
March 1, 2011 9:23 AM
Anonymous said...
Unajuwa ,Yasinta mkasa hu ni ushahidi tosha,kwa sisi binadamu,tunapo kabiliwa na shida au tatizo,liwe la mardhi nk,imani nikitu muhimu sana.vile vile mungu nimkubwa, na ananiayake na makusudi yake itokeapo shida ama tatizo kama hilo.mimi huamini kilakitu kitokeacho kwa binaadamu nimapenzi ya mungu.kama ni mkono wa binadamu na hila zake basi utateseka kwa muda lakini ,kwa imani na mapenzi ya mungu utapona.Lakini kama yeye ameaamua hataufanyeje utapofuka tu.na mwisho nisawa na tunavyo amini kuhusu kifo.unakuta mtu anapata ajali mbaya sana amboyo labda katika gari lile wote wamepoteza maisha, na ni mtu mmoja tu ka pona.hapo yatasemwa mengi,ikiwemo bahati,au mungu atasifiwa kwa sana,na wakati mwingine utambiwa jamaa alisali sana kabla hajaanza safari.Hivyo imamani ,jitihada,uvumilivu na uelawa/ufahamu nimsingi katika kukuvusha katika shida au tatizo linalo kukabili . kaka s
March 1, 2011 10:46 AM
Mija Shija Sayi said...
Mungu ni mwema. Tunaambiwa kwamba wanaadamu tumepewa jina moja tu ambalo kwalo kila kitu kinawezekana ukiamini hivyo. Jina la YESU.Tunaambiwa kwamba ktk majina yooooote hapa duniani hakuna lipitalo nguvu Jina la YESU, na yote yatalitii jina hilo, sasa FUNGUS nalo si ni jina?FUNGUS imelitii jina la YESU.Mbarikiwe wote...
March 1, 2011 12:11 PM
Koero Mkundi said...
Nimeishiwa maneno..... Nakumbuka niliwahi kumtumia kaka Shaban Email ya kumjulia hali na alinijibu tu kwa kifupi kuwa yuko KCMC Moshi akimuuguza mkewe ambaye alilazwa huko kwa kuumwa na Jicho. Nasikitika kwamba sikuwahi kuwasiliana naye tena, sijui ni usahaulifu au ni kitu gani.....Ni mara nyingi katika baadhi ya makala zangu za huko nyuma nimewahi kuandika juu ya somo la imani, na nimekuwa nikieleza kwa kirefu sana jinsi imani ilivyo na nguvu, lakini naomba nikiri kuwa pamoja na kuandika sana juu ya imani lakini siamini kama ninayo imani inayomfikia Christina. Huo ndio ukweli wenyewe.Dunia hii imetawaliwa na mapepo ya kila aina na kama mtu asipokuwa na imani basi anaweza kwenda na maji. Ahsante sana dada Yasinta kwa juhudi zako za kushirikiana na Christina katika maombi, na pia kupata muda wa kufanya naye mazungumzo hadi kutuwekea ushuhuda huu ambao kwa kweli utawafunua wengi.Mwisho napenda kuwapongeza Wainjilisti James Ramadhan Rajabu, Benson Izoka ambaye namfahamu ingawa sidhani kama yeye ananifahamu, Mwinjilisti Magoti huyu nimeshawahi kukutana naye pale Manzese SDA kwenye Effort moja, na washiriki wengine ambao kwa njia moja au nyingine walishirikiana na Christina kwenye maombi katika kipindi chote cha madhila yake.Mungu ashukuriwe.nami nimejifunza kutoka kwa Christina...
March 1, 2011 12:21 PM
Mija Shija Sayi said...
Dah! dah! Yasinta nimekukubali wewe ni shapu si mchezo..siamini..Nafikiri umeelewa naongelea nini.Ubarikiwe.
March 1, 2011 2:50 PM
Anonymous said...
Samahani kwa mwandishi, naomba kuweka kumbukumbu sawa. Mwinjilisti James Ramadhan Rajabu ni wa Kanisa la Tabata Chang'ombe.Ukitaja Chang'ombe tu, mtu mwingine anaweza kudhani ni Temeke Chang'ombe.nami natoa pole na pongezi kwa dada Christina kwa ujasiri wake.Imani ina nguvu sana. nami nimejifunza pia.Liz wa Tabata
March 1, 2011 5:31 PM
Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...
Ni kisa cha kugusa moyo. Yote yawezekana ati!
March 1, 2011 6:05 PM
Lisa said...
Inafunza sana if you have faith as small as a mustard seed, you can say to this mountain, 'Move from here to there' and it will move.Yasinta topic ni ushuhuda wakutosha hakuna lisilo wezekana kwa yesu hongera sana kristina mungu awabariki wote.
March 1, 2011 7:40 PM
Swahili na Waswahili said...
Hongera sana da Christina kwa kunga'nga'nia njia ya uzima na kweli!Mungu azidi kukubariki,Kuhusu ccbrt nami nilishakwenda pale kwa vipimo, nikaonekana ninatazizo la macho na natakiwa kuvaa miwani haraka sana, wakanipatiwa yanayo nifaa na bei yake,Mungu ni mwema siku hiyo pia nikuwa na ahadi Ubalozi saa 8 mchana,hapo ilikuwa saa 6.Nikawaambia nitarudi kesho kuichukua,kwenda ubalozi nikapata visa na tukashauriana na baba watoto tukaona tuachane nayo,kuja huku nikapimwa tena nikaambiwa tatizo langu si kuivaa miwani kwa sasa labda niaka 15/20 ijayo.Wakaniuliza ulipima wapi?nikawaambia na kuwapa vyeti vyangu vya huko yaani walilaumu sana.Asante da yasinta kwa kuungana nasi na mafundisho haya!Mungu wetu hashindwi na jambo kama kweli unamuamini na kufuatanjia zake!.
March 2, 2011 12:38 AM
Celestina said...
Kweli hata mim nimejifunza kutoka kwa dada Tina kutokata tamaa.mungu ndo kila kila kitu katika maisha yetu,hata kwa bible amesema 'sitawaacha waaibike wanitengemeao.'Be blessed.
March 2, 2011 12:21 PM
Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
Nguvu ya imani hakuna awezaye kuipinga!Pole sana da Tina na hongera kwa ujasiri!
March 2, 2011 3:12 PM
NN Mhango said...
Pamoja na tukio hili kugusa nyoyo na kufunza, tuchunge kutoa hitimisho la jumla kuwa imani ni tiba. Inategemea na imani. Maana kuna imani nyingine ni potofu zinaleta maangamizi kama vile ugaidi na mauaji ya kinyama ya albino. Shukrani dada Yacinta kukubali kushiriki nasi tukio hili.
March 2, 2011 8:52 PM
Jeff Msangi said...
Kisa au mkasa wa aina yake.Nilichoambulia mimi ni kitu kinachoitwa Power of Faith au Nguvu ya Imani.Ukiamini hakuna kisichowezekana.Asante Yasinta kwa ushuhuda huu wa Christina.The Lord is alive
March 3, 2011 1:46 AM
Salehe Msanda said...
Habari za siku kadhaa,Nimerudi kutoka mapumzikoNi kweli hilo somo tosha na ni muhimu kila wakati kuwa na matumaini kuliko kukata tamaa na hasa suala lenyewe kama linahusiana na afya yako. maana afya haina mbadala.Tumshukuru muumba kwa kuweza kumuongoza wifi yako kufikia uamuzi wa kuamini kuwa mungu yuko naye na atapona.Ni somo zuri na lina mafundisho mengi kutokana na kile kilichotokea na kwa watu wataalamu wa afya tunanaowaamini na kuwakadhi dhamana ya maisha yetu.Kila la kheri.
March 3, 2011 11:02 AM
emu-three said...
Kweli imani ni tiba, hasa unapokabiliwa na magonjwa ambayo `wataalamu wetu' wanasema `haiwezekani...usikate tamaa na muombe mungu wako kwa imani yako...utafanikiwa, lakini hakikisha kuwa `imani' ipo!
March 3, 2011 12:44 PM
Upepo Mwanana said...
Nijuavyo mimi, madakatari bingwa wa macho kwa Tanzania ni wachache sana, na hata hospitali kubwa zenye majina makubwa , nyingine hazina madakatari bingwa wa macho, ukifika unapokelewa na wasaidizi ambao kwa sera za nchi yetu ati wanatambulika kama madaktari.Hata CCBRT madaktari bingwa ni wachache, na wamejaa wasaidizi.Wanchi siku hizi tunapaswa kujifunza japo huduma ya kwanza na elimu kidogo ya magonjwa tujimudu na bidhaa feki hizi zinazojiita madaktari bingwa! Namkumbuka Kaka yangu Chib, nina imani anaweza kutoa mchango zaidi katika masuala haya ya macho!
March 3, 2011 1:25 PM
Mija Shija Sayi said...
Yasinta upo?
March 5, 2011 5:45 PM
chib said...
Habari hii imenigusa sana, tena moyoni kabisa.Nasikitika iwapo mtu ataangukia kwa mtu asiye elewa sawa tatizo la mwingine na kuishia kumwaga uongo ili aonekane kama anajua.Hospitali alizopitia Christina, nazifahamu vyema tena sana.Nina mengi ya kusema kutokana na maelezo ya Christina, lakini kusema bila kuona, ni sawa na kumwaga uongo zaidi. Kwangu kila moja linawezekana, kwa upande wa kupona haraka, na pia kwa upande wa maelezo ya madaktari. Sijui nisemee upande upi. Ila bado natafakari kwa KCMC kumuita mtaalamu kutoka Nairobi kuja kuchukua sampuli tu...., bado haijaingia kichwani kabisa.Baadaye nikipata muda, nitatoa mada ndefu kuhusu vidonda katika uso wa jicho. Nashukuru Tembe kwa kunikumbuka, japo nipo nahudumia waafrika wenzangu mbali na nyumbani.Lakini tupo pamoja
March 8, 2011 5:08 PM
Anonymous said...
NAOMBA NAMBA YA CHRISTINA .IMANI YAKE IMENITIA MOYO
March 10, 2011 7:16 AM


Ebu tumaliza kwa kusikiliza wimbo huu:-

Sunday, December 25, 2011

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE NOELI NJEMA KWA WIMBO HUU...


Kristmas njema sana ndugu zanguni ...Mwenzeni nimepata ile hisia kuwa nipo kanisani Makwai/lundo au sijui Ruhuwiko na naimba nyimbo hizi....yaani basi tu ..JUMAPILI NA KRISTMAS NJEMA KWA WOTE.

Saturday, December 24, 2011

HAPA SWEDEN LEO NDIO CHRITMAS..NAS TWASEMA HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA ..GOD JUL OCH GOTT NYTT ÅR!!!!

Picha hii ilikuwa mwaka jana siku kama ya leo angalia kulivyokuwa kweupe na hapo ndipo chrstmas inakuwa kweli christmas........Nimejaribu kuuliza kwanini wanasheherekea Christmas leo na sio kesho kama wengi wanavyofanya sijapata jibu la kuniridhisha kwa kweli kwa hiyo ukienda sehemu na ukikuta wanatembea uchi nawe tembea.


Kuamka leo asubuhi sehemu ileile kama picha ya hapo juu. Lakini leo mpaka nyasi zinaonekama hakuna theruji, Jua linawaka...ila kuna kaubaridi kwa mbali...Na hii inasemekana haijawahi kutokea.....KHERI KWA CHRISTMAS/GOD JUL TILL ALLA. Oh naondoka kwenda kubeba mabox mwenzenu...Tutaonana baadae au kesho au keshokutwa au niseme tu TUTAONANA TENA.

Friday, December 23, 2011

KAMA HUJAFANYA ,HUKUFANYA NA HUKUFIKIRIA KUFANYA BASI FANYA KAMA WIMBO/UJUMBE USEMAVYO OMBEA ADUI YAKO...


Watu wengi huwa wanafikiri au wanasena huyu/wewe ni adui yangu na hapo huanza vituko. Kuna wengine wanawaona hata wazazi pia ndugu zao ni maadui. Ndugu zanguni tuache chuki. Mwenzio akipata basi usimwone ni adui yako, kwa kufanya hivyo hakutakuwa na maendeleo. NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA USISAHAU KUMWOMBEA ADUI YAKO KAMA UNAYE..UKIZINGATIA PIA MWAKA NDIO UNAKATIKA HIVYO.

Wednesday, December 21, 2011

MVUA KUB WA YASABABISHA MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM TANZANIA!!

Hapa ni baadhi ya wakazi wa spenco Vingunguti wakiwa wamekusanyika kusubiri boti iwaokoe.
Picha toka kwa michuzi-

SALAMU/BARUA KUTOKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO:- SHUKRANI KWA WOTE!!!

Habari zenu jamani!!
Zimebakia siku chache tu kuumaliza mwaka huu 2011 na kuingia katika mwaka mpya 2012. Hakika miaka inayoyoma na watu tunazidi kuzeeka. Ninachotaka kusema ni kwamba, blog ya MAISHA NA MAFANIKIO inapenda kuwashukuru wanablog wenzake wote, wasomaji wote na watembeleaji wote kwa ushirikiano mzuri tunaoonyeshana. Najua katika maisha watu wote hawawezi kuwa sawa yaani kimawazo. Lakini katika hizi blog zetu kwa asilimia kubwa imekuwa ni changamoto kwetu. Tumekuwa hatupendi kupoteana, mara mmoja wetu anapokuwa kimya kwa muda basi wengine tunakuwa hatuna raha tunachukua hatua ya kumtafuta. Hii yote inaonyesha ni jinsi gani ukaribu wa wanaBLOG sisi tu/ulivyo, hakika najivuna sana kwa uwepo wenu na kwa hili napenda kusema SISI SOTE NI NDUGU. NA PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KILA DOGO NA PIA KILA KUBWA MTENDALO LIWE JEMA. NA MWAKA 2012 UWE WENYE MAFANIKIO. KAMA KUNA KITU ULIAHIDI KUFANYA MWAKA HUU BASI JITAHIDI UFANYA KABLA HAUJAISHA. KWANI KUMBUKA HAKUNA LISILOWEZEKANA/KISICHOWEZEKANA. NAONA TUTAENDELEA MWAKANI NA KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO YA MADA, MATUKIO MBALIMBALI PIA PICHA.. bila ninyi kipengele hiki hakingeweza kuwa. MBARIKIWE WOTE MTAKAOPITA KATIKA BLOG HII NA NYINGINE ZOTE. PAMOJA DAIMA. KAPULYA WENU!!!!

Tuesday, December 20, 2011

NIMEULIZWA SWALI HILI NA RAFIKI MMOJA!!!

Swali:- Hivi Yasinta kukoroma/kuforota (snoring) ni UGONJWA, URITHI au NI KWA AJILI YA UNENE? Maana mwenzio nina shida sana yaani silali kabisa mume wangu anakoroma sana. ....Nikakumbuka pia nilikuwa na rafiki mmoja akija kusalimia tulikuwa na taabu sana na ikabidi kumtenga na alale mbali kidogo nasi. JE? MNAWEZA KUNISAIDIA KUMJIBU RAFIKI YANGU HUYU? NATANGULIZA SHUKRANI....PIA NAWATAKIENI JUMANNE NJEMA...Kapulya

Monday, December 19, 2011

TOFAUTI YA AINA HIZI ZA UPUPU WA KUWASHA NA USIOWASHA MANGATUNGU (velvet beans au cowitch beans)

Wiki iliyopita niliweka hapa picha ya upupu na baadhi ya wasomaji walisema kwamba ni chakula kitamu sana ingawa unawasha. Lakini nijuavyo mimi picha hii hapa juu ndio huliwa kule kwetu tunaita MANGATUNGU. Chakula hiki inabidi upike kwa makini sana. Kwanza unachemsha kisha unamenya. Na hapo kazi inaanza unachemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi. Sababu ni kwamba inasemekana kuna sumu ndio maana maji ya mwanzo huwa meusi sana . Kwa lugha ya kiingereza huitwa "velvet beans au cowitch beans"...pia inasemekana:- Mangatungu ni dawa kama viagra, ni kahawa, na ni dawa ya kutibu magonjwa ya nerves kama vile Parkinson disease. Kwa habari zaidi soma http://en.wikipedia.org/wiki/Mucuna_pruriens#Uses
Na hapa ni ule upupu wa kuwasha ambao kaka Mfalme Mrope na kaka ISSACK CHE JIAH wanasema ni chakula kitamu sana. Inawezekana ila mimi najua ni aina mbili tofauti...kwa kujikumbusha soma maoni hapa.


Sunday, December 18, 2011

NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA !!!

Ee Yesu, ususamehe dhambi zetu.
Utuepushe na moto wa milele.
Ongoza roho zote mbinguni.
Hasa za wale wanaohitaji huruma yako. Amina
JUMAPILI NJEMA NA AMANI NA UPENDO VIWE NANYI DAIMA.

Saturday, December 17, 2011

MANENO YA BUSARA AMBAYO NIMEAMBIWA ....

Moja ya furaha si lazima kwa yule ambaye ana kila kitu, lakini anaweza kuwa mmoja ambaye anajua jinsi ya kufanya kwa ubora kila kitu kilicho karibu yake.
.............JUMAMOSI NA JIONI NJEMA KWA WOTE...

Friday, December 16, 2011

HUU NI UJUMBE WA IJUMAA YA LEO!!


NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA SANA NA MWANZO MWEMA WA MWISHO WA JUMA..PIA WOTE MNAPENDWA!!

Thursday, December 15, 2011

JE? UMEWAHI KUWASHWA NA UPUPU?

Leo nimekumbuka siku moja nilikuwa navuna mahindi halafu nikajisikia mwili wote unawasha. Kumbe niligusa UPUPU bwana, wacha nianze kurukaruka, mama akachukua majani ya mihogo/kisamvu na kunipikicha pikicha na muwasho ukatulia. Je? wewe umewahi kugusa upupu na kisha kupata muwasho kama huu? na kama ndiyo ulitumia nini ili kupunguza muwasho?

Wednesday, December 14, 2011

SAYANSI YAKIRI BINADAMU HAFI, HUBADILIKA.

NI JUMATANO NYINGINE TENA NA NI SIKU YA KILE KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO.UKITAKA KUSOMA MAONI YAKE GONGA HAPA.
Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema huenda hakuna kitu kama hicho. Kwa mfano kuna wale wanasayansi ambao wanakiri kwamba, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, ni watoto ambao wana akili kubwa kuliko zile za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha kwamba, watoto hawa walianza kuzaliwa hapa duniani kuanzia mwaka 1975. Ni watoto ambao uwezo wao katika kuelewa mambo ni mkubwa kuliko tulivyozoea kuona. Baadhi ya watoto hawa, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma, kabla hawajafa. Watoto hao wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao na kuja tena kuzaliwa mahali pengine. Hakuna idadi maalum ya watoto hawa hapa duniani, lakini inadaiwa kwamba, wako wengi kiasi cha kufikia elfu kadhaa. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wakiwa na kumbukumbu kali na uwezo mkubwa sana kiakili, kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa kiajabu. Kwa nini wameanza kuzaliwa miaka ya 1975? Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia na ulimwengu kwa ujumla. Kwamba itafika mahali, maarifa mengi yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kwamba, kimekuja kumwonesha binadamu kwamba, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha, ndivyo sivyo.Hivi karibuni mwanasayansi mmoja nchini India, amekiri kwamba binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine . Hii ina maana kwamba, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya, tuliyo nayo hivi sasa.Mwanasayansi huyu Vikram Raj Singh Chauhan, amesema ana uhakika ataweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa umri wa miaka sita ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa sana. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo. Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma. Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri. Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali. Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata. Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi. Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule. Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya. Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa. Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo. Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja. Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine. Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko. Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa. Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu. Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miili tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki. Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani. Mwanasayansi kama Chauhan na wengine wanaamni kwamba, kama roho ikihama kutoka mwili mmoja na kwenda mwili mwingine, huenda huko na akili au mawazo na hisia pia. Kinachoachwa ni mwili unaoonekana, lakini hiyo miili mingine huwa pamoja. Hii ina maana kwamba, hata mwandiko utabaki kuwa uleule kama ilivyokuwa. Chauhan anasema, hivi sasa anao ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kwamba, binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena, lakini hutumia mwili mwingine. Hata hivyo anasema anahitaji muda zaidi kuthibitisha jambo hili. Bila shaka, ushahidi wa wazi kabisa kuhusu watoto hawa wa indigo, unaweza kutuonesha kwamba, tunapokufa, maana yake tumepoteza mwili , lakini bado hisia, akili, na roho ambavyo huja kuingia kwenye mwili mwingine ambao utatengenezwa na wazazi wengine wawili au wale wale, vinakuwepo. Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibitika. Kama ingekuwa Chauhan sio mwanasayansi, tungeweza kusema, suala hili bado, halijatazamwa kisayansi na hivyo, haliwezi kuelezewa kama jambo halisi. Kwa mwanasayansi kuvutiwa na jambo hili na kuanza kulifanyia utafiti huku akikiri kwamba, kuna mambo yenye kutanza, ni hatua kubwa katika binadamu kuingia mahali ambapo atabaini ukweli wa kuwepo maisha baada ya kifo. Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.

Habari hii nimeipata katika gazeti la Jitambue la huko nyumbani Tanzania, ambalo siku hizi halichapishwi tena baada ya mmiliki wake Munga Tehenan kufariki dunia. Na nilishawahi kuiweka hapa Maisha na Mafanikio mwaka jana.

Tuesday, December 13, 2011

Hongera kaka John Mwaipopo kwa kuongeza mwaka"!!!

Katika pitapita zangu nimekuta kaka mwaipopo anatimiza miaka leo. Lakini sijui
ni miaka mingapi umetimiza?. Hongora kaka JOHN KWA SIKU HII MAALUMU. Na hapo naona unashereheke kwa ULANZI... tena linusu lizima wewe kaka weweee nakuamini.

GHAFLA NIMEJIKUTA NATAMANI NYUMBANI NILIPOKUWA NASIKILIZA WIMBO HUU AMBAO MANENO MACHACHE NI KWA LUGHA YA KINGONI!!



Kweli kuwa mjini bila pesa hakuna maisha ...bila maganga pabomani ulanga sana.... pia wanaimba kwamba usiwe na tamaa kama huna hela ....

HATA MIGUU NAYO HUPENDEZESHWA!!!! SWALI JE NI VIBAYA?



Vikuku ni urembo au?


KUNA mtu kanitumia hiyo picha anauliza hizo shanga za miguuni zinavaliwa kujiremba au zina maana nyingine?Kwa mujibu wa maelezo yake, amewahi kusikia kwamba, shanga hizo a.k.a vikuku zina maana yake hivyo anaomba kufahamu kama ni kweli. Anasema, kaelezwa kwamba, kikuku kikivaliwa mguu wa kulia ina maana yake, na kikivaliwa kushoto kinakuwa na maana nyingine, ni kweli?Kama kila mguu una maana yake, vikivaliwa miguu yote inamaanisha nini?


Pia nimesikia nchi kama Ivory Cost ukivaa mguu wa kulia basi inaonyesha kuwa wewe ni msagaji /shoga. Je ni kweli?

Monday, December 12, 2011

TUANZE JUMATATU HII KWA MWANAMTINDO HUYU JE UNAMFAHAMU?

Kuna siku mtu lazima ujifurahishe na huyu mwanadada aliamua kujifurahisha au kuwa modo wa kijapani kwa siku moja kama mnavyomwona. Huhitaji kwenda mpaka Japani na kuwa mwana mtindo:-)


Mmmmmhhh! kweli ninafaa kuwa mJapani? mbona mie MTZ.. Aaahh kwa siku moja nafaa....





あなたについて= habari zenu. Ni raha kweli kuwa mJapani kwa siku moja. Dada Mariamu upoo???

Sunday, December 11, 2011

NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA...


JUMAPILI NJEMA KWA WOTE AMANI NA UPENDO VITAWALE NYUMBANI MWENU

Friday, December 9, 2011

SALAMU ZA KUSHUREKEA MIAKA 50 YA UHURU TANZANIA KUTOKA SWEDEN...

Familia hii haiko nyumba katika siku hii ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru. Ingawa mwanafamilia mmoja hayupo katika picha. MUNGU IBARIKI TANZANIA, WABARIKI VIONGOZI WAKE, HEKIMA UMOJA NA AMANI MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE IBARIKI TANZANIA ....

Thursday, December 8, 2011

KUJIFUNZA/KUJITEGEMEA MAISHA/KAZI ZA NYUMBANI!! AU MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO!!

Tulipokuwa nyumbani mwezi wa sita mwishoni mpaka wa nane mwanzoni bahati nzuri ulikuwa ni msimu wa kuvuna. Tulimkuta Mzee ngonyani/babu amevuna mahindi. Na hapa mnamwona kijana Erik akimsaidia babu kupiga mahindi, kwa babu Songea Ruhuwiko.



Baada ya kazi nzito ya kupiga mahindi nguo zilikuwa zimechafuka kwa hiyo ni lazima kufua na hapa mnamwona anafua nguo zake....hapa ni Songea Ruhuwiko ....


Dada mtu naye siku yake ya dobi ikaja kama mnavyoona naye anafua nguo zake. Hii /hizi kazi ni moja ya kujifunza kuishi kwa kujitegemea.Uzuri wake maji tulikuwa nayo humu humu uani.

MAISHA NI KUJIFUNZA.

Wednesday, December 7, 2011

KWELI MAMA NI NGUZO YA FAMILIA/JAMII INATAKIWA KUBADILIKA ILIKUWASAIDIA AKINA MAMA!!


Duh! kaazi kwelikweli najiuliza mpaka sasa kesho kutwa ni miaka 50 ya UHURU lakini...MWANAMKE KWELI NI MWANAMKE..
Picha inamuonesha mama mmoja kutoka katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma akikabiliwa na majukumu mazito kama anavyoonekana katika picha hii.Ingawa mama huyu anakabiliwa na changamoto mbalimbali bado anaonekana mwenye furaha.

HIVI HUKU SIO KUBAKA KWELI?

KAMA KAWAIDA YETU NI ILE JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO NA LEO KAPULYA UMEFANYA UKAPULYA WAKE NA KUKUTANA NA MADA HII AMBAYO AMEIPATA HAPA. Haya karibuni.
Kama kubaka ni hali ya mwanaume au mwanamke kulazimisha kufanya tendo la ndoa bila hiyari ya mwingine, basi wanawake wengi sana walioko kwenye ndoa hubakwa na waume zao kila siku.
Kubakwa huku kunatokana na ukweli kwamba wanawake wengi hulazimika kukubali kufanya tendo la ndoa na waume zao kutokana na mazingira mbalimbali yaliyo nje ya upendo.
Kuna ndoa nyingi ambazo zimekufa, ingawa wanandoa wanaishi pamoja. Zimekufa kwa sababu hazina mawasiliano kabisa. Lakini cha ajabu ni kwamba, watu hawa wanakutana kimwili na pengine kuzaa watoto. Kwa sehemu kubwa kwenye ndoa za aina hii, wanawake huwa hawako kwenye ukamilifu wao kimawazo.
Mara nyingi athari huwa ni kwa wanawake kwa sababu wao kimaumbile huishi kihisia. Kutokana na kuathirika kimawazo hamu yao ya kushiriki tendo la ndoa nayo hupotea.
Kwa kuwa hawana hamu ya kushiriki tendo la ndoa, waume zao wanapowaambia, ‘geuka huku’ (hawaongei zaidi ya hapo kwa sababu hakuna mawasiliano), hufanya hivyo. Na hufanya hivyo huku wakiwa hawataki.
Sio wengi wanaoweza kukataa kwa sababu hawakulelewa katika mazingira yanayoweza kuwafanya wakatae. Wamelelewa kwenye mazingira ambayo yamewaambia, miili yao hawana haki nayo mbele ya utashi wa waume zao!
Ukiacha mawasiliano kuna ndoa ambazo wanaume ni Malaya sana, walevi, au wapigaji. Kwenye ndoa za aina hii unaweza kukuta mwanamke bado anaendelea kuwepo kwa sababu mbalimbali, ikiwemo ya utegemezi au watoto. Pamoja na kuendelea kwao kuwepo, hamu ya tendo la ndoa na waume zao nayo inakuwa haipo
Lakini mwanaume hatakiwi kunyimwa mwili wake anapouhitaji. Kwa hiyo, kinachotokea ni mwanamke kufanya mapenzi kwa kujilazimisha au kulazimishwa..
Kuna kesi nyingi ambapo tumesikia juu ya wanaume kuwauwa wake zao kutokana na kuwakatalia unyumba au wakiwa wanapigana baada ya mwanamke kukataa kushiriki tendo la ndoa.
Kwenye ndoa nyingi wanawake hubakwa, yaani hushiriki tendo la ndoa bila hiyari zao. Hulazimishwa au hujilazimisha kutokana na nafasi ambayo jamii imewapa.

Ni kwa nini basi tunapozungumzia kubaka tusiwaambie wanawake na kuwashauri wawe macho na ubakaji huu ambao una athari kubwa kwao na kwa jamii wakiwemo watoto wanaozaliwa kwenye ndoa hizi za kibabe?
MWENYEZI MUNGU AKIPENDA BASI TUONANE TENA JUMATANO IJAYO...NA WOTE MNAOPITA HAPA MBARIKIWE SANA .

TAARIFA ZA MSIBA WA BABU WA BLOGA WENZETU KAKA BARAKA CHIBIRITI HUKU NYUMBANI TANZANIA!!

Picha ya Babu Blezi Chibiriti, akiwa na mwanae wa mwisho mpendwa wake Fabiani Chibiriti


Kwa habari zaidi basi soma hapa. Babu yetu ustarehe kwa amani.

Tuesday, December 6, 2011

NAWATAKIENI JIONI NJEMA WOTE:- WATU WANAJUA KUUNGANISHA MANENO /KUAMSHA HISIA EBU SIKILIZA WIMBO/MANENO HAYA



JIONI NJEMA....ILA WIMBO HUU HAKIKA...

MIMI NAAMINI ANAYETAFUTA ATAPATA ANCHOTAFUTA/ANAYEULIZA ATAPATA JIBU!!

Nimelipenda swali hili: "Jamaa aliniuliza hivi; Bro hebu nijibu swali hili....au waulize hata wana blog wenzio wa kiume; Ni kweli supu ya pweza huchajisha?
- Mimi kwakweli sijui swali hili kulijibu." swali/maelezo kutaoka hapa.


Monday, December 5, 2011

MIMI NAISHI LEO, SIISHI KESHO, WEWE JE?

Watu wengi siku hizi wanaishi katika hofu kubwa, wanahofu kuhusu familia, majirani, kazi na matarajio ya maisha yao ya baadae. Hofu imekuwa ni kubwa katika maisha ya watu wengi hivi sasa, kwa sababu ya ushindi wa kuuridhisha mwili.

Tunaweza kuondoa hofu iwapo tunatabadili mfumo wetu wa kufikiri kwa kuanza kufikiri vizuri. Kwa kawaida hofu huwa zinatuletea matokeo hasi, kwa sababu kwa kutawaliwa kwetu na hofu, tunajenga woga kwa kuiogopa kesho, na hiyo ndio sababu watu wengi huanguka katika maisha.

Woga kuhusu kesho hauna maana, kwani kesho huwa haiji kwa namna tunavyotarajia. Sisi huwa hatuishi kesho bali tunaishi leo. Wakati unawaza nini kitakachokutokea kesho, mwezi ujao au mwaka ujao, unakuwa unajiwekea vikwazo katika kufikia malengo yako kwa kuvuruga mfumo wako wa kufikiri.

Kwa hiyo si vyema kutumia hata sekunde yako moja kuhofu kuhusu kesho, ishi leo. Kimsingi huwezi kufanikiwa na kufikia matarajio yako iwapo maisha yako yatakuwa yametawaliwa na hofu za kesho, na maisha yako yatakuwa yamewawaliwa na hofu za kesho basi utakuwa unapoteza muda wako bure, na matokeo yake unakufa ukiwa hujayafikia malengo yako ya kuwepo hapa duniani.

Lakini hata hivyo ni vyema ukumbuke kuwa katika kufikia malengo yako, ukubaliane na changamoto za maisha, kamwe zisikutie hofu, cha kufanya ni wewe kuyaona matarajio yako kwa taswira ya jicho lako, jiamini na lione kabisa kwamba lengo lako limefanikiwa. Ishi kila siku kwa namna inavyokuja, kwani kesho ni jina tu la siku inayofuata, kuihofia na kuiogopa ni UJINGA tu.
Kwa nini nasema ni UJINGA? Ni kwa sababu hakuna hata mmoja wetu anayejua kesho au kesho itakuwaje.

Sunday, December 4, 2011

HONGERA KWA SIKU YAKO YA KUZALIWA YASINTA MDOGO (KIBIBI)



Hongera kwa siku ya kuzaliwa Wajina wangu. Huyu binti ni binri wa kaka yangu. Kaka ambaye aliniachia ziwa na huyu ni mtoto wake wa pili na leo anatimiza miaka 8. Ila nampa pole kwa kuitwa YASINTA...najua mnajua kwanini nasema hivyo. HONGERA WAJINA:-)

Saturday, December 3, 2011

NATAMANI NINGEPATA MLO HUU MCHANA WA JUMAMOSI HII LAKINI....SINA. SIJUI NIFANYEJE?

UGALI......




......KWA DAGAA´


Nimepita mara mia kwa dada Rachel na kumezea meta au kujaribu kula kwa macho na nimeshindwa maana nina unga lakini sina dagaa...

JUMAMOSI NJEMA KWA WOTE HATA KAMA BILA UGALI NA DAGAA:-)

Friday, December 2, 2011

TUWE PAMOJA NA KAKA Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) KWA MAOMBI YA MSIBA WA MAMA MZAZI HUKO NYUMBANI TANZANIA!!

Kaka Mrope pole sana kwa msiba wa mama yetu mzazi kwani naamini mama yako ni mama yetu.Katika pita pita zangu nimekutana na habari hii ya kusikitisha.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
TAARIFA YA MZIBA
Napenda kuwataarifu ndugu zangu na marafiki popote mlipo kuwa nimepatwa na msiba wa mama yangu mzazi Shamsa binti Hassan aliyefariki huko nyumbani Tanzania leo tarehe 2/12/2012. Habari za kisomo na dua zitawajia baadae. BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA...Kwa pole napatikana 301 222 7739.... nahitaji maombi yenu.Wenu, Addson Noel Omari ( Mfalme Mrope ) http://tustaarabike.blogspot.com/

UJUMBE WANGU WA IJUMAA YA LEO UNASEMA!!!!

Ndoto zetu ndizo zinazotufanya tusonge mbele.
NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA NA MWANZO WA MWISHO WA JUMA PIA. NA WOTE MTAKAOPITA HAPA MUWE NA AMANI.

NI IJUMAA YA MAJONZI MSANII MR EBBO AFARIKI DUNIA


Nimepatwa na mstuko pia majonzi makubwa sana baada ya kusikia kifo cha msanii huyu kwani ni moja ya wasanii niliokuwa nikiwasdikiliza kila mara. NAPENDA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA MR EBBO NA NDUGU PIA MARAFIKI WOTE. MAREHEMU NA ASTAREHE KWA AMANIPEPONI AMINA. TUTAKUKUMBUKA DAIMA.

Thursday, December 1, 2011

PICHA YA WIKI:- SARE SARE MAUA ASIYEJUA KUCHAGUA!!

huyu ni Yasinta Ngonyani (Kapulya) picha imepigwa jana 30/11/2011.
Nilipoina picha hii ya chini nikatamani kama ndiyo ningekuwa mie kwani napenda sana mvao huu/vazi hili la asili ya kimasai. Nikaona ngoja nami nivae mgololi wangu..... ila naona kama naogopa kitu katika picha hii...mmmmhhh!!!

huyu ni ..Mhe. Namelo Sokoine
...ila naona mwenzangu mgolori wake una urembo, halafu ana mkoba, pia zaidi ya yote hiyo ya shingoni /hiyo nimeivizia kila mara lakini sijaipata bado.... Ila nadhani kidogo picha zinafanana.. Au?

Wednesday, November 30, 2011

SWALI LILILONIKERA KWA MIAKA MINGI!!!

Nimeshindwa kuvumilia mwenzenu, kwani hili jambo/swali limekuwa likinikera miaka sasa.

Ni hivi:- Hivi kwanini mwanamke mjane anweza kuishi peke yake mudamrefu au hata milele bila kuolewa tena na mwanamume mwingine? Maana ukiangalia asilimia kubwa ya wanaume wajane huwa hawaishi muda mrefu peke yao huwaa wanaoa tena.

Nina mfano mmoja, bibi yangu mzaa mama:- Babu alifariki mwaka 1980 na bibi amekuwa mjane mpaka Mwenyezi Mungu alipomchukua 2005. Na mafano mwingine nilionao ni baba mmoja nimfamuye mkewe alifariki 2004 na yeye 2006 tayari alipata mwanamke mwingine na kufunfa naye ndoa 2008.
Je?Hapa ndo kusema wanawake wanawapenda zaidi waume zao/wana uchungu zaidi kuliko wanaume?
NAOMBA TUJADILI KWA PAMOJA SWALA HILI JAMANI... KAPULYA WENU!!!!!

HISTORIA :-SONGEA MBANO KIONGOZI SHUJAA WA WANGONI ANAYESTAHILI KUENZIWA DAIMA.

Kama kawaida ni JUMATANO YA KILE KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO na leo nimeona tubaki SONGEA na kujikumbusha historia hii. Katika mipitopito nimekutana na mada hii hapa. Na nikaipenda na nimeona si mbaya nikiweka hapa Maisha na Mafanikio. Karibuni sana ndugu zanguni.



HUWEZI kuilezea na kuikamilisha historia ya vita ya Majimaji na ukombozi wa nchi yetu bila kumtaja shujaa wa kabila la wangoni Nduna Songea Mbano ambaye jina lake lilipewa hadhi ya kuuita mji wa Songea kutoka kwenye jina la Ndonde mwaka 1906.
Kiongozi huyo alikuwa ni miongoni mwa wasaidizi ( Nduna) 12 wa Chifu wa kabila la wangoni (Nkosi) chifu Mputa bin Gwezerapasi Gama.
Ambapo wasaidizi wake wengine walikuwa ni Mgendera Mawaso Gama, Kohongo Magagura, Mputa Mkuzo Gama, Magodi Mbamba Mbano, Mtekateka Muyamuya Tawete, Fratela Fusi Gama.
Manduna wengiwe ni Maji ya kuhanga Komba, Zimanimoto Gama, Mpambalyoto Soko Msalawani, Mtepa Hawaya Gama na Nduna Mkomanile ambaye alikuwa ni mwanamke pekee kuwa nduna.
Nduna Songea Mbano alikuwa ni maarufu kuliko manduna wenzake na hata chifu Mputa Gama alikuwa anamtegemea sana katika kuwaongoza Manduna wenzake na wapiganaji wa vita ya Majimaji kiujumla.
Mhifadhi kiongozi wa Makumbusho ya Taifa Maji maji Songea Philipo Maligissu akizungumzia maisha ya Nduna Songea Mbano katika viwanja vya Makumbusho hayo,alisema kuwa Songea Mbano akiwa miongoni mwa manduna alitokea kuwa maarufu sana ukilinganisha na wenzake 11 ambapo sifa kubwa iliyo mpa umaarufu ili kuwa ni ueledi na ushadi wake wa kuandaa mikakati ya kivita, na maamuzi mazito yasiyoteteleka na kuyasimamia maamuzi hayo kikamilifu.
Kwa umakini mkubwa Nduna Songea Mbano aliweza kufanya kile alichokuwa akikiamini na uthibitisho wa jambo hilo ulianza kujitokeza julai 12, mwaka 1897 katika viwanja vya Bomani kwa mkuu wa Wilaya wa wajerumani luteni Engelhardt.
Maligissu anasema kuwa kwa rekodi zilizopo zinaonyesha kuwa tarehe hiyo Nduna Songea Mbano alionekana kuwa ni mtu wa kipekee katika idadi ya Manduna 11 ambao walikuwa wasaidizi wa chifu Mputa Gama kwa kitendo chake cha kubisha wazi wazi tamko la utawala mpya wa wajerumani la kutaka wangoni wakomeshe biashara ya utumwa.
Siku hiyo ilikuwa ni siku rasmi ambayo utawala wa kikoloni ulikuwa unaanzishwa katika mji wa Songea wakati huo ulikuwa unaitwa Ndonde na Mkoa wa Ruvuma kiujumla chini ya Luteni Engelhardt wa Jeshi la Kijerumani ambaye alikuwa ndiye Mkuu wa Jeshi kwa kanda ya Kusini.
Wajerumani walipofika kuanzisha makoloni yao katika maeneo ya ukanda wa kusini walikutana na msuguano mkubwa kutoka kwenye tawala za kiafrika hususani tawala za wangoni.
Maligissu anasema kuwa wangoni walikuwa na tabia ya kwenda mikoa ya Lindi na Mtwara kuvamia na kuchukua mateka na kuwaleta Songea kuwafanyisha shughuli mbalimbali katika maeneo yao ya utawala.
Tabia hiyo ya wangoni iliwachukiza sana wajerumani kwani wajerumani walikuwa wanaheshimu sana makubaliano yaliyofikiwa kutoka kwenye mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 hadi 1885.
Katika mkutano huo moja ya makubaliano yaliyofikiwa ni pamoja na kila nchi yenye koloni barani Afrika ni lazima ikomeshe biashara ya utumwa na kwa kuwa wajerumani walikuwa wamejiimarisha sana katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Hivyo walipokuja Ruvuma wakatoa tamko kwa wangoni kuwa hairuhusiwi na haitaruhusiwa tena kwenda Lindi,Mtwara na maeneo mengine kuchukua mateka na kwamba mateka wote waliochukuliwa na wangoni waachiwe huru.
Baada ya wajerumani kutoa tamko hilo ndipo Nduna Songea Mbano alipojitokeza waziwazi na kusimama kujibu hoja iliyotolewa na wajerumani kuhusiana na tamko hilo.
Nduna Songea Mbano alisema kuwa utawala wa kabila la wangoni hauwezi kutekeleza tamko hilo na kwamba msimamo wao ni kutoutambua utawala mpya wa kijerumani na tamko lao.
Aliendelea kusema kuwa ujio wa utawala wa wajerumani na kutoa tamko hilo kwa wangoni una lengo la kudhoofisha utawala wa Machifu na Manduna katika maeneo yao kwa kufuata kanuni zao za kimila na kitamaduni.
Kuanzia hapo wajerumani walimuona Nduna Songea Mbano kuwa ni mtu hatari sana katika utawala wao mpya na walimuweka alama maalumu na kuanza kumfuatilia nyendo zake.
Kwa sababu alionekana kuwa kiongozi shupavu na mwenye misimamo mikali na anayezingatia heshima na utu wa kabila lake bila kuyumbishwa.
Alionekana kuwa ni mtu wa pekee mwenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira yoyote kwa kushirikiana na wananchi wake ambao walikuwa wana mheshimu sana na kumsikiliza.
Maligissu anaeleza kuwa Nduna Songea Mbano alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwaunganisha wananchi wake na kuwa na umoja, upendo na mshikamano na kwamba alikuwa akiwaelekeza jambo wanalifanya kwa umakini na kwa ukamilifu.
Anaendelea kusema kuwa kuanzia hapo Nduna Songea Mbano aliendelea kujizolea umaarufu mkubwa na wajerumani baada ya kuona hivyo na kitendo cha nduna Songea kutamka kuwa yupo tayari kwa lolote lile na hawezi kukubali kuona tawala za kiafrka zinadharauliwa na wakoloni kwa namna yeyote ile.
Waliamua kuwaalika Machifu na Manduna wote Julai 13 mwaka 1897 Bomani kwa mkuu wa Wilaya wa kwanza katika nchi ya ungoni ambaye pia mkuu wa jeshi la wajerumani katika nchi ya ungoni Luteni Engelhardt na kuwaambia kuwa mtu yoyote katika eneo lake atakaye kaidi amri yeyote kutoka kwa uongozi mpya wa wajerumani basi atapigwa risasi, kunyongwa hadi kufa au kufungwa maisha .
Siku hiyohiyo Machifu na Manduna walichukuliwa hadi juu ya mlima wa shabaha wa chandamari uliopo katikati ya mji wa Songea na kuwaonyesha nguvu ya risasi inavyoweza kufanya kazi katika mwili wa binadamu na kwamba silaha za kijadi na kimila za wangoni haziwezi kufua dafu mbele ya silaha hizo.
Licha ya wajerumani kutoa mkwara na vitisho vingi Nduna Songea Mbano aliendelea kushikilia msimamo wake wa awali wa kuchukia utawala wa wajerumani na kuutetea utawala wa kiafrika mpaka vilipo kuja kutokea vita vya Majimaji.
Nduna Songea Mbano alitoa ushindani mkubwa sana katika vita hivyo na alionyesha ustadi mkubwa kwenye mapigano na katika sehemu zote ambazo wajerumani walipigana wameandika kuwa hawakupata ushindi mkubwa kama waliopata katika Mkoa wa Ruvuma zamani nchi ya ungoni.
Ambapo viongozi wao hawa kuwa wanafiki kwani walijitoa kikwe likweli kusaka ukombozi wa kweli na hadhi ya tamaduni zao mpaka dakika ya mwisho, ndio maana idadi ya watu walionyongwa katika historia ya nchi yetu walitoka katika himaya ya Nduna Songea Mbano na ushahidi upo wazi kuwa watu 67 walihukumiwa kunyongwa hadi kufa akiwemo Nduna Songea Mbano.
Katika kuonyesha kuwa Nduna Songea Mbano alikuwa na uwezo wa kufanya mambo kwa uweledi mkubwa bila kusaliti dhamira yake kuanzia mwaka 1897 alianza kuandaa jeshi lake la kupambana na utawala wa wajerumani.
Akaanza kuchukua watu wake na kuwapeleka juu ya mlima wa chandamari, kufanya nao mkutano na kutoa mafunzo ya kivita na kuwaelekeza kwa nini wanawachukia wajerumani.
Katika mlima huo ndipo alipoeleza kwa kina madhara ya kuukubali utawala wa wajerumani na kutoa ahadi kwa wananchi wake ya kuwaondoa wajerumani kwa lazima na kwamba alisema kuwa eneo hilo ni lao na wamekuwa wakiishi siku zote chini ya utawala wao sasa inakuwaje waletewe utawala mpya wakati hawahuitaji.
Chokochoko hizo zilizaa vita vya Majimaji na wakati mapigano yakiendelea wajerumani walianza kumtafuta Nduna Songea Mbano ili wamkamate na kufanya nae mazungumzo ya maridhiano.
Kumbe Songea Mbano alikuwa amejificha kwenye pango kubwa lililopo kwenye mlima wa chandamari na usiku hukutana na askari wake nje ya pango hilo na kuwapa mafunzo zaidi ya kivita.
Maligissu anaeleza kuwa Nduna Songea Mbano alikuwa anaishi na Ndugu zake katika eneo la Mateka lililopo katika eneo la Manispaa ya Songea na wakati wa vita ndipo Songea Mbano alikuwa anajifisha katika pango hilo ili wasimkamate mpaka atakapotimiza malengo yake.
Wajerumani walipoona wanaendelea kupata madhara makubwa kutokana na vita hivyo waliamua kuwakamata ndugu na familia yake, chifu Mputa Gama na Manduna wengine na kuwafunga gerezani kwa lengo la kumdhoofisha Nduna Songea Mbano.
Baada ya wajerumani kumdhoofisha Nduna Songea Mbano alipata taarifa zote na akaamua kutoka kwenye pango hilo na kwenda kwa wajerumani na kutaka watu wake waachiwe ili mapigano yaendelee.
Ndipo naye alipokamatwa na kuwekwa gerezani na kwamba utawala wa wajerumani waliamua kuwa hukumu wafugwa hao kunyogwa hadi kufa akiwemo chifu wa kabila la Wangoni.
Wafungwa hao waliamuliwa kuchimba shimo kubwa bila kujua kuwa shimo hilo ndilo litakalotumika kuwa kaburi lao na ilipofika siku ya kunyongwa walinyongwa kwa zamu siku mbili na maiti zao kwenda kuwekwa kwenye kaburi hilo hadi walipofikia 66 ndipo walizikwa kwa pamoja kwenye kaburi hilo.
Nduna Songea Mbano walimuacha ili aweze kuwasaidia kufikisha malengo yao kwa wananchi kwani waliamini kuwa yeye ni kiongozi jasiri na anayependwa na watu wake na kusikilizwa vizuri.
Toka siku hiyo walipomuacha bila kumnyonga Nduna Songea Mbano aliwasumbua sana wajerumani na kutaka naye anyongwe kama ndugu zake kwani haoni sababu ya yeye kuishi wakati ndugu zake wamekufa na kusema kama hawataki kumnyonga basi hataki kula wala kunywa chochote mpaka afe.
Ndipo wajerumani walipoamua kumnyonga na kumzika katika kaburi la pekee yake wakiamini kuwa ni mtu wa pekee mwenye ushujaa na maamuzi mazito na misimamo isiyoyumba na walimuenzi kwa kubadilisha jina la mji wa Ndonde na kuubatiza jina la Songea ambapo mpaka sasa linatumika kuuita mji huo wenye hazina kubwa ya historia na utalii wa kitamaduni
Kila mmoja wetu hana budi kujiuliza ni mafundisho yepi anaweza kuyapata katika historia ya nchi yetu na mchango mkubwa alioutoa Nduna Songea Mbano na je kizazi kilichopo tunao ule moyo wa ushujaa , uzalendo heshima na usawa kama ilivyo kuwa kwa mababu zetu basi inatupasa tutimize wajibu wetu kikamilifu ili vizazi vijavyo viweze kunufaika na uwepo wetu duniani.
TUKUTANO TENA JUMATANO IJAYO NA NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA MWEZI HUU NA MWANZO MWEMA WA MWEZI WA KUMI NA MBILI.

Monday, November 28, 2011

ULIJUA KAMA SONGEA KUNA HIFADHI /MBUGAYA WANYAMA?


Nimeishi miaka mingi Songea nilikuwa sina habari kama kuna mbuga ya wanyama. Mbuga hii ipo nje kidogo ya Msamala . Kwa hiyo nasi tulipata bahati na kuingia hapa kwa msaada ya mwenyeji wetu ndugu Sunday Hebuka.


Hili ni jengo/au niseme ni ofisi ndipo ambapo unalipa....Na pia unaona magari kwa ajili ya watalii........


Ila sisi tuliona ni vizuri kutembea kama unavyoona tupo katika msululu hapo...kusaka wanyama....

Msafara unaendelea hapa ni kadaraja...
Na hapa ni mto Ruhila kwa ubunifu wao wameweka mawe ni kama daraja vile. Ila inabidi uwe shupavu kwani kulikuwa na utelezi. Hapa ni lazima kuvua viatu pia...Siku hii tulifurahi sana kuwa katika eneo hili ambalo hatukujua kama lipo...Ushauri ukifika Songea usikose kuchungulia hapaa.



Sunday, November 27, 2011

NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA KWANZA YA MAJILIO PIA YA MWISHO KWA MWEZI HUU PIA NAPENDA KUWASHUKURUNI KWA USHIRIKIANO WENU KWA SALA YA FAMILIA PAMOJA

Milango imefungwa, Ea Bwana.Yule mtoto mchanga amelala, tunajisikia salama.Tuna raha ya ndani, kwani tumeshiba, chakula kilikuwa kizuri, kinatuletea faraja.
Huu nio wakati wa kukugeukia , mwishoni mwa siku hii ya leo, kama familia-familia yako, ambapo Kristu anaishi.
Kwa ajili yetu, kila moja wetu Bwana, tunakushukuru. Kwa ajili ya siku hii ya leo, iliyojaa mambo mengi, mema na yasiyo mema sana. Kwa yote tunakushukuru.
Tunapoangalia nyuma, mara nyingine, ni rahisi kuona kwamba ingaliwezekana kuwa vizuri zaidi. Hapa na pale, tumeshindwa kukupendeza, kwa neno la hasira. Na lile ambalo hatukulitimiza.
Tunasikitika, Bwana tusamehe. Kwani tunahitaji upendo wako. Tunakuhitaji wewe, ukae nasi, ili utulinde, utubariki, kwani wewe ndiwe kuta za kweli na paa za nyumba yetu.
Utubariki tulalapo, utujalie ndoto zetu ziwe za faraha. Na utujalie tuamke kesho tukiwa na uzima mpya tele. Nguvu mpya na starehe mpya. Ili tuweze kuishi tena siku nyingine.

Baada ya hapa napenda kuwashukuruni wote kwa upendo wenu, ushirikiano wenu kwa kushirikiana nami kwa Wiki hii inayokwisha leo kwa maombolezo ya mdogo wetu Asifiwe. AHSANTENI SANA. PIA NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA KWANZA YA MAJILIO IWE NJEMA NA MBARIKIWE SANA WOTE MTAKAOPITA KATKA BLOG HII YA MAISHA NA MAFANIKIO. AMINA

Saturday, November 26, 2011

LEO NI 26/11/2011 NDIYO SIKU ALIYOZALIWA ASIFIWE NGONYANI

Tarehe 26/11/1989 ilikuwa siku ya furaha kwa familia ya Ngonyani kupata binti mwingine ambaye ni Asifiwe. Ni hisia za ajabu sana mwaka huu bila kumpigia simu na kumtakia HERI kwa siku yake ya kuzaliwa ambayo ni leo. Na hii ni sababu kubwa nikaona wiki nzima iwe yake kwa vile imekuwa wiki ya matukio matatu kwa mpigo. Kweli Mwenyezi Mungu ndiye muweza ebu jaribu kuangalia Asifiwe alizaliwa 26/11/1989 siku ya jumapili ,na leo na jumamosi 26/11/2011 ange/ametimiza miaka 22 halafu sasa siku aliyozikwa ni 26/3/2011 siku ya jumamosi tena…HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA MDOGO WETU,DADA YETU,MAMA MDOGO WETU, SHEMEJI YETU, PIA RAFIKI YETU. NA USTAREHE KWA AMANI, TUTAKUKUMBUKA DAIMA.
UA HILI NIMETUMIWA NA KAKA ISSACK CHE JIAH AMBAYE PIA NI MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO. AHSANTE SANA.

Thursday, November 24, 2011

MWAMBA ULIOPASUKA...



TUMTEGEMEE MUNGU WETU KWA KILA TUTENDALO. PAMOJA DAIMA.

Wednesday, November 23, 2011

TUTAKUKUMBUKA DAIMA ASIFIWE NGONYANI!!!

Kwa vile leo ni JUMATANO NA NI JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO YA mada/makala/matukio mbalimbali. Basi JUMATANO YA LEO imeangukia kuwa tarehe 23/11 ambayo si mara nyingi inakuwa hivi. nasema hivi kwasababu 23/3/2011 siku ya jumatano tuliondokewa na mpendwa wetu Asifiwe na leo imetimia miezi nane na imeangukia siku ya jumatano na tarehe 23/11-11 kusema kweli nimeshikwa na butwaa kidogo maana si mara nyingi inakuwa hivi. Kwa hiyo nimeona si vibaya kama tukimkumbuka Asifiwe wetu.

Hapa ndipo mahali alipopumzika Asifiwe katika safari yake ya mwisho. TUTAKUKUMBUKA DAIMA ASIFIWE.KWANI UPO NASI KIROHO ILA SI KIMWILI. PUMZIKA KWA AMANI MDOGO WANGU/WETU.

Tuesday, November 22, 2011

ASIFIWE NGONYANI (1989- 2011). Kioo kingine cha maisha yetu, kwa maisha yetu na wenzetu

Kama jana jumatatu nilivyosema ni wiki ya kumkumbuka mdogo wangu Asifiwe Kwa hiyo nimeona si mbaya kama tukimkumbuka Asifiwe kwa mada hii iliyoandikwa na Mzee wa changamoto.

"..see you in ZION, holding hands together standing by MY FATHER'S SIDE. Meet you in ZION singing songs together....." LUCIANONi mwaka mmoja na siku 24 tangu ilipobandikwa MAKALA HII YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUFANIKISHA UPAUSAJI WA Dada Mdogo Asifiwe Ngonyani. Leo hii NAMSHUKURU MUNGU kwa maisha na mapumziko ya Dada Asifiwe, ambaye aliaga dunia Machi 23 na kuzikwa Machi 26.Dada wa Asifiwe, ni Da Yasinta Ngonyani. Sio bloga mwenzangu tu, bali ndiye anayewasiliana na familia yangu kuliko bloga yeyote. Twawasiliana kwenye chat, kwenye simu na hata skype ambapo huwa tunaongea mara kwa mara.Mara nyingi tumezungumza kuhusu Asifiwe.Na kila mara alikuwa akitujulisha maendeleo yake. Na kwa kila wakati ambao afya ya Da Asifiwe ilikuwa ikihitaji msaada wa uangalizi wa watabibu, Da Yasinta alikuwa mnyonge. Na nakumbuka siku ambayo alisema hakuweza kuweka bandiko kwenye blogu yake kwa kuwa hakuwa na furaha. Baadae tukawasiliana kuwa ameweza kuongea na Asifiwe na alikuwa na furaha kusika maendeleo yake ni mema.Lakini juma hili, taarifa zimefika kuwa ASIFIWE HATUNAYE. Binafsi niliumia sana. Nilikuwa sijapata kuonana na Asifiwe, lakini mazungumzo juu yake kutoka kwa Dadake na Da Koero yalinifanya kuwa karibu naye kwa namna ya pekee.Lakini kwa wote hawa (Yasinta na Koero), nililogundua ni namna ambavyo FURAHA ZAO ZILIATHIRIWA NA HALI YA ASIFIWE. Kwa maongezi nao, niligundua juu ya maisha yake ambayo ndicho kilikuwa kivutio kikubwa kwa ndugu zangu hawa ambacho ni TABIA. Da Yasinta hakuwa tu akimzungumzia Asifiwe kama ndugu yake ambaye ni wao wawili pekee wa kike katika familia, lakini alikuwa akimzungumzia kama RAFIKI.NA HILI NDILO NILILOJIFUNZA NA NINALOJIFUNA.Ninapomuwaza ASIFIWE, nikimuwaza Dada Yasinta na dugu, jamaa na marafiki wakimlilia, naona AKISI YA MAISHA YA ASIFIWE. Naona jambo ambalo sisi sote twatakiwa kujifunza kutoka kwa Asifiwe, kisha kuona maisha yetu na ya wali walio kwetu yakibadilika.KILIO cha kumlilia Asifiwe ni ishara nyingine kuwa alipendwa, na licha ya kuwa ni KAZI YA MUNGU kumpumzisha baada ya kuyagusa maisha yetu kwa namna alivyoyagusa, bado tungependa kuendelea kuwa naye.Nakumbuka Juni mosi mwaka 2009, NILIBANDIKA MAKALA HAYA KUHUSU KILIO CHANGU KWA MJOMBA WANGU, ambaye nililia kwa kuwa nilimlilia, na katika makala hiyo, niliandika kuhusu kilio cangu kwa mjomba kuwa "nililia kwa kuwa kwa tafsiri yangu, kulia ni kutokubali kuwa wakati wa mjomba kupumzika ulikuwa umefika na hakika alistahili kupumzika baada ya kutenda mema mengi tena kwa mapambano ya hali ya juu. Mjomba alikuwa mtu mwema kwangu na kwa wengi..." Mtu wa kwanza kutoa maoni kwenye bandiko hilo (kama ilivyo kwa mabandiko mengi kwenye blogu nyingi) ni Dada yangu Yasinta ambaye alisema "Mzee wa Changamoto pole sana tena sana. Nalia pamoja nawe kwani nakuelewa kabisa. Na nakushauri lia sana kwani kulia ni moja ya kutoa uchungu wako. Natumanini Mjomba wako yupo nawe kila siku amini. Astarehe kwa amani."Leo hii nami namkumbuka Asifiwe, na licha ya kuwa NAMLILIA, bado nakumbuka kuwa ALISTAHILI KUPUMZIKA na kuwa aligusa maisha ya waliohusiana na kuishi naye na yetu tuliomfahamu kupitia ndugu na marafiki.Lililo kubwa kwetu tuliobaki, ni kuishi maisha sahihi na maisha yaliyo mema. Kama ambavyo aliishi ASIFIWE NGONYANI....Na ndio maana (kama kisemavyo kichwa cha post) namuona "ASIFIWE NGONYANI kama Kioo kingine cha maisha yetu, kwa maisha yetu na wenzetu"Chris Rice anasema....COME THOU FOUNT

AHSANTE MZEE WA CHANGAMOTO/KAKA MUBELWA BANDIO!!!