Monday, December 5, 2011

MIMI NAISHI LEO, SIISHI KESHO, WEWE JE?

Watu wengi siku hizi wanaishi katika hofu kubwa, wanahofu kuhusu familia, majirani, kazi na matarajio ya maisha yao ya baadae. Hofu imekuwa ni kubwa katika maisha ya watu wengi hivi sasa, kwa sababu ya ushindi wa kuuridhisha mwili.

Tunaweza kuondoa hofu iwapo tunatabadili mfumo wetu wa kufikiri kwa kuanza kufikiri vizuri. Kwa kawaida hofu huwa zinatuletea matokeo hasi, kwa sababu kwa kutawaliwa kwetu na hofu, tunajenga woga kwa kuiogopa kesho, na hiyo ndio sababu watu wengi huanguka katika maisha.

Woga kuhusu kesho hauna maana, kwani kesho huwa haiji kwa namna tunavyotarajia. Sisi huwa hatuishi kesho bali tunaishi leo. Wakati unawaza nini kitakachokutokea kesho, mwezi ujao au mwaka ujao, unakuwa unajiwekea vikwazo katika kufikia malengo yako kwa kuvuruga mfumo wako wa kufikiri.

Kwa hiyo si vyema kutumia hata sekunde yako moja kuhofu kuhusu kesho, ishi leo. Kimsingi huwezi kufanikiwa na kufikia matarajio yako iwapo maisha yako yatakuwa yametawaliwa na hofu za kesho, na maisha yako yatakuwa yamewawaliwa na hofu za kesho basi utakuwa unapoteza muda wako bure, na matokeo yake unakufa ukiwa hujayafikia malengo yako ya kuwepo hapa duniani.

Lakini hata hivyo ni vyema ukumbuke kuwa katika kufikia malengo yako, ukubaliane na changamoto za maisha, kamwe zisikutie hofu, cha kufanya ni wewe kuyaona matarajio yako kwa taswira ya jicho lako, jiamini na lione kabisa kwamba lengo lako limefanikiwa. Ishi kila siku kwa namna inavyokuja, kwani kesho ni jina tu la siku inayofuata, kuihofia na kuiogopa ni UJINGA tu.
Kwa nini nasema ni UJINGA? Ni kwa sababu hakuna hata mmoja wetu anayejua kesho au kesho itakuwaje.

6 comments:

Baraka Chibiriti said...

Asante sana Dada Yasinta kwa maneno mazuri sana tena sana...na ya kweli kabisa, ukihofu kila kitu huwezi kuishi kabisa maisha haya, ya kesho yatajulikana tu, ya sasa ndo ya kuzingatia zaidi...maana hatujui hata kama kesho tutakuwepo au la! Ila isiwe sababu ya kutufanya tusihangaikie ya kesho...,.bali tuwe na moyo zaidi, na kutokukata tamaa ya maisha kuwa na hofu kila kukicha. Nayakumbuka maneno mazuri sana ya Mwalimu Baba wa Taifa letu Nyerere alisema; wewe meshawahi kuiona kesho? au umeshawahi kuingia kesho? Yanayowezekana leo yafanyike bila kusubiri kesho kesho. Na tusiwe na hofu kila kuicha sijui itakuwaje ksho.

chib said...

Shukrani!

Goodman Manyanya Phiri said...

Wewe Mdogo Wangu, Yasinta... OGOPA!!! OGOPA SANA HIYO KESHO! Bila hivyo, Kesho itakukurupusha weeee!!!

Utakuja kukimbia kwa kurukaruka na kutangatanga kama sungura mwenye kuwindwa na mbwa. Kwani hutakuwa umejipa muda wa kutosha kuwazia juu ya namna ya kukikwepa kifo cha sungura!


Hamna anaejuwa kesho ndio, lakini tunazo fununu za kutosha kufanya maandalizi ya kuiridhisha dhamira yetu:

"nimejitahidi kukabiliana nayo ya kesho lakini nimeshindwa lakini namshukuru Mungu sikushindwa kujitahidi!"



Mimi kama kawaida yake Kaka mtu (Kapulya) nakupinga sana hasa unaposema KWA KUKUNUKUU: “Ishi kila siku kwa namna inavyokuja, kwani kesho ni jina tu la siku inayofuata, kuihofia na kuiogopa ni UJINGA tu.” MWISHO WA KUNUKUU.


Hofu ni dalili ya ubinadamu. Hofu ni babu katika hisia zote na mwanae wa kwanza kabisa ni UCHUNGU.


Binadamu asiekuwa na hofu hatajuwa amani, upendo, raha, elimu, utamu na yote mazuri ya dunia hii kwani hatakuwa na vipimo vyovyote vya kupimia mazuri bila uwezo wa kuonja hofu mara kwa mara.


Kadiri mtu anavyohofia chochote kile na kutafuta namna ya kuuondoa hofu huo NDIVYO JUHUDI, SHUGHULI AU KAZI ZINAVYOFANYIKA.


Mtumwa anahofia kupigwa viboko ndipo anafanya kazi. Naye mwenye kufanya kazi kwa hiari yake ANAHOFIA kuyiaga siku moja dunia hii bila kuwaachia urithi waulimwengu watakaebaki baada ya kifo chake.

Hamna hata mmoja mwenye akili asiekuwa na hofu, nao wenye hofu nyingi ndiyo wao wenye akili nyingi.

ray njau said...

Nani kaiona kesho?

darstockholm said...

Kiukweli dada yangu haya maneno yko nipo pamoja na ww kwani ktk mfumo mzima wa maisha hakuna anaejua hata kama kesho anaweza kufika kwani kifo chetu Pia kipo kesho kama si Leo.Hapa nikiwa na maana kwamba ni vyema uifurahie Leo kuliko kuifikilia kesho na vp km Leo huna tatizo alafu unaifikilia kesho na hyo kesho ukapata ajali unadhani hutoikumbuka Jana yako ambayo ulikua sio kilema na hukuifurahia kwa kumshukuru mungu na badala yke kuiwaza kesho imekupa kilema?mm npo pamoja na ww dada yangu na kwa ufupi hayo ndio maisha yangu mm nafurahia siku nilionayo Leo hyo ya kesho sitaki kujiua 7bu sijui km nitaifika au itanipata katika hali gani.Na kiukweli na furahia sana maisha yngu kwa huu mfumo wa kuishi Leo na sio kesho.

darstockholm said...

Kiukweli dada yangu haya maneno yko nipo pamoja na ww kwani ktk mfumo mzima wa maisha hakuna anaejua hata kama kesho anaweza kufika kwani kifo chetu Pia kipo kesho kama si Leo.Hapa nikiwa na maana kwamba ni vyema uifurahie Leo kuliko kuifikilia kesho na vp km Leo huna tatizo alafu unaifikilia kesho na hyo kesho ukapata ajali unadhani hutoikumbuka Jana yako ambayo ulikua sio kilema na hukuifurahia kwa kumshukuru mungu na badala yke kuiwaza kesho imekupa kilema?mm npo pamoja na ww dada yangu na kwa ufupi hayo ndio maisha yangu mm nafurahia siku nilionayo Leo hyo ya kesho sitaki kujiua 7bu sijui km nitaifika au itanipata katika hali gani.Na kiukweli na furahia sana maisha yngu kwa huu mfumo wa kuishi Leo na sio kesho.