Friday, December 9, 2011

SALAMU ZA KUSHUREKEA MIAKA 50 YA UHURU TANZANIA KUTOKA SWEDEN...

Familia hii haiko nyumba katika siku hii ya kusherehekea miaka 50 ya Uhuru. Ingawa mwanafamilia mmoja hayupo katika picha. MUNGU IBARIKI TANZANIA, WABARIKI VIONGOZI WAKE, HEKIMA UMOJA NA AMANI MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE IBARIKI TANZANIA ....

10 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Amina! Nanyi ni familia yenye mfano wa kuigwa na Waafrika wote. Na mtu bila nchi yake si kitu kabisa. Kama wanavyosema:


[Ask not what Tanzania has done for you; rather ask yourself what YOU have done for Tanzania]

isaackin said...

amina,muwe na siku njema pia huko,mmependeza sana na hizo nguo za taifa

EDNA said...

Hongera,mmependeza na hizo nguo.

Rachel Siwa said...

Ahsanteni sana nayi muwe na baraka,yaani mmependeza sana lakini Shemeji yangu kama angepata na KAMSULI HAPO INGEZIDI KUPENDEZA!!!!

Mija Shija Sayi said...

Jamani shemeji ana mkwara!!!!! Mmependeza sana.

Jamani ngoja nami nitafute mashati ya hivyo.

Baraka kwenu.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mkubwa Phiri. Umenena Ahsante kwa kunikumbusha hilo.

Ka´isaacikin! kwa kweli namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunijalia afya njema kiasi kwamba nimeiona siku hii ya leo.

Ahsante Edna. Nawe pia HONGERA pia kwa MTANZANIA YEYOTE YULE.

Rachel! Kaaazi kwelikweli yaani huachi vituko mdada wewe:-) Baraka kwako pia.
Mija! nakwambia hivi hapa anatafuta kaznu:-) Haya mashati uliyaficha sana nini?...LOL. Mbarikiwe wote mliopita hapa na na kuacha kitu na pia wale waliopita tu.

John Mwaipopo said...

yote tisa, kumi kibandiko cha faza hausi

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mwenzetu mbona naona kitumbo kikubwa? Ama?

ray njau said...

Asalaam aleykum baba mwenye mji huu.
Tunakupongeza sana kwa kuamua kupenda boga na ua lake.Hukupenda tu dada yetu Yasinta bali unaipenda Tanzania na watanzania.
--------------------------
Karibu sana Tanzania shemeji yetu mpendwa baba Erik.
----------------------------

Yasinta Ngonyani said...

Kaka John! ni furaha kuona upo nasi.

Kaka Chacha! duh wewe unaangalia vitambi tu...Naona nilikula mangatungu mengi au maharage si unajua yanavimbisha tumbo hayo.
Kaka Ray! umesema kweli ila ni wachache sana wanafanya hivyo..Salam zimefika.