Sunday, February 28, 2010

TUMALIZE DOMINIKA HII YA MWISHO YA MWEZI HUU FEBRUARI KWA WIMBO HUU!!Napenda kuwatakieni wote jumapili/dominika hii kwa wimbo huu. Na pia ni Dominika/Jumapili ya mwisho ya mwezi huu Februari. Duh! Jamani siku zinakimbia kweli. Ok, JUMAPILI/DOMINIKA NJEMA KWA WOTE JAMANI

Friday, February 26, 2010

HII NDOA AU NDOANA: KAMA UNATAKA KUJUA CHANZO, BASI SOMA HAPA.

Wadau,

Nimepata maelezo ya ziada toka kwa kaka Mlachaombwani baada ya kuona kuwa wengi wenu mmekuwa na maswali mengi sana kutaka kujua ni nini chanzo cha mtafaruku huo. Majibu yake ni haya kwa ufupi:

Mwaka 2001 wakati wakiwa na mtoto wao wa kwanza (akiwa na umri wa chini ya miezi 3) mume alimuomba mke akakae kijijini kwa mume ili wazee wamwone mtoto na pia kumpa jina. Mke alikwenda huko ukweni na alikaa kwa muda wa miezi mitatu.

Kwa mujibu wa maelezo ya mke mara baada ya kurudi kutoka ukweni, alidai kuwa alipokuwa huko kwa huo muda wa miezi 3 aliteswa sana na mama mkwe wake kwa sababu si wa kabila la mume kwa kuwa mume hakuoa mke toka kwa kabila lao.

Awali wazazi wa mume walimtafutia mume mke wa kabila lao lakini huyo mchumba alimtosa kaka wa watu kwa kigezo kuwa ‘hawezi kuolewa na mtu ambaye kwao hakuna hata kuku’ na ‘mtu ambaye jogoo hawiki’ (stori ya ‘jogoo hawiki’ ilikuwa kwamba kaka Mlachaombwani, kutokana na malezi aliyopata hakuamini katika kuonjana kabla ya ndoa hivyo kila mchumba alipotoka naye alitegemea kumegwa na kwa kuwa alikuwa hamegwi basi akadhani jogoo hawiki kumbe jamaa anaitunza kwa ajili ya ule wakati mzuri wa –Bwana na Bibi arusi sasa wanakwenda kujipumzisha)

Hivyo alipompata huyu mke aliye naye, hakufanya ajizi akaingia kichwa kichwa na kumtundika mimba iliyopelekea binti kuondoka kwao na kwenda kuishi na kaka Mlachaombwani ili kuepusha vurumai na rabsha zaidi kutoka kwa wazazi.
Na inavyoonekana wazazi wa kijana hawakupendezwa na hilo.

Kwa hiyo kutokana na makosa hayo ya mama mkwe ya kumtesa (mke anadai kuwa wakati mwingine alikuwa analazwa njaa ilhali ananyonyesha na pia kufuata maji na kuni umbali mrefu-zaidi ya km 5- wakati mgongo ulikuwa haujakomaa).

Hapo mnamo mwaka 2003 kama alivyosema ndipo jinamizi la kunyimwa unyumba lilipoanza kwa kile kilichoelezwa kuwa ‘mke hajisikii’ na kumuuliza mume kuwa ‘kwani huwezi kuishi bila kuonja’. Kaazi kwelikweli!

Katika kutafuta faraja, nadipo akajikuta akiwa na watoto nje ya ndoa kitu ambacho haikuwa ni dhamira yake. Saswa hivi chuki imekuja kuwa kubwa baada ya wazazi kumpokea mmoja wa watoto wa kaka Mlachaombwani na pia kuuliza kwa nini hakai na watoto wake (waliozaliwa nje ya ndoa) nyumbani kwake.
Mbali na hayo, haelewani na shemeji zake kwa sababu zisizoeleweka.

Kaka Mlachaombwani anakiri kuwa yeye ndiyo chanzo kwa kuwa, kama asingempeleka mkewe kijijini pengine kusingetokea hayo yote. Lakini anashangaa kuwa pamoja na kutumia wasimamizi wa ndoa na viongozi wa dini MKE hataki kuwasamehe wazazi na ndugu zake kwa kile alichosema mwenyewe kuwa AMEWA-DELETE kwa hiyo, hakuna msamaha kwa yeyote yule.

Kaka Mlachaombwani anabainisha kuwa mkewe huyo hataki apeleke matumizi kwa wazazi wake na hata wakiwatembelea nyumbani kwao, kama mume hayupo basi hawatakarimiwa.

Kwa maelezo ya kaka Mlachaombwani, ndiyo anataka kuachana na huyo mkewe lakini watoto wao ndiyo kikwazo kwa sasa. Na anakiri kuwa anampenda sana mkewe lakini cha kushangaza mkewe anamchukia saaaaaana! Na kutokana na hilo anajikuta wakati mwingine anachuki na kila mwanamke anayekutana naye njiani kwa kuwa anadhani wanawake wote wako hivyo.

Hataki kuoa tena na anasema mipango yake ikifanikiwa ataondoka na kumuachia huyo mkewe kila kitu na kuanza upya kwa kuwa anajua alipoanzia huku akiishi na wanawe wote.

Vipi hapo? Je kuna msaada wa ushauri kwa kila mmoja wa hao wanandoa? Mnadhani kuondoka na kumuachia kila kitu ni suluhisho au ushauri wa Dada Koero kuwa amfukuzie mbali ndio mzuri zaidi?

Thursday, February 25, 2010

JAMANI HII NI NDOA AU NDOANO?


Je? kuna upendo hapa?

Ndugu wasomaji na wanablog wenzangu, leo nina jambo moja ambalo ningependa tulijadili kwa pamoja.

Kuna msomaji mmoja wa blog hii ambaye ningependa kumuita Mlachaombwani (Sio jina lake halisi) amenitumia email akinitaka ushauri kutokana na kile alichoita jinamizi linaloitafuna furaha ktk ndoa yake.

Kusema kweli, hata mie nimejikuta nikishikwa na kizunguzungu maana mambo ya maunyumba haya yanahitaji umakini pale unapotakiwa ushauri.

Kaka Mlachaombwani anasema kuwa ameishi na mkewe kwa takribani muongo mmoja sasa na wamejaaliwa kupata watoto wawili katika ndoa yao hiyo. Maisha yao kwa ujumla ni mazuri kiasi, kwani ni familia iliyojitosheleza kwa kiasi cha mboga. Awali ndoa yao iloanza kwa bashasha zote ilikuwa na amani na utulivu na kila mmoja alimpenda mwenzake.

Lakini mwaka 2003 mkewe huyo alimbadilikia sana na akawa hawapendi kabisa ndugu zake, yaani ndugu wa mume. Hataki kuwaona wazee wa mumewe wala ndugu zake. Pamoja na ushauri toka kwa viongozi wa dini yao mkewe huyo alishasema kuwa ‘hata kama akija MALAIKA kumshauri hataweza kubadili msimamo wake kwa kuwa akishamchukia mtu basi ni mpaka kiyama’! Kibaya zaidi kafikia hatua anamnyima mumewe huyo unyumba au labda niseme chakula cha usiku, na sasa maisha yao ya ndoa yamekuwa kama vile sio wanandoa, yaani hakuna kupeana lile tendo la ndoa kama ilivyokuwa zamani wakati wanaoana.

Anasema hata kama akiamua kumpa tendo ni pale anapoamua yeye (mwanamke) yaani akipenda yeye na hii inaweza kuwa ni baada ya mwezi au baada ya miezi. Nilipomuuliza kama anapopewa, je wanafanya kwa ile hali ya mapenzi kufurahia tendo la ndoa au vipi? Akasema ni mradi kutimiza tu wajibu lakini hakuna raha yoyote ile. Ni kama vile anabakwa ama anabaka vile.

Nikukumbushe msomaji wangu kuwa ndani ya miaka hiyo kuanzia 2003 ilisababisha huyo kaka Machaombwani kuingia katika ‘mahusiano yasiyofaa’ nje ya ndoa ambayo yalisababisha kupatikana watoto wengine wawili. Nadhani ni baada ya kuona hapati haki yake hapo nyumbani.

Hata hivyo amebainisha kuwa tatizo jingine kubwa linaloitafuna ndoa yake ni wivu usiofaa aliokuwa nao mkewe huyo. Anasema mke wake amekuwa akimlinda sana akijaribu kumpeleleza kama ana wanawake wengine nje ya ndoa (nyumba ndogo?) hata baada ya mume kukiri kilichokwisha kutokea. Kwamba pamoja na kumnyima tendo la ndoa lakini bado anamuonea wivu, na kumlinda. Na cha ajabu pia pamoja na mume kusema kuwa kwa muda wa miaka 2 sasa hamjui mwanamke mwingine nje ya ndoa hataki kusikia chochote ikiwa ni pamoja na kumzuia mumewe kutoa matunzo kwa watoto hao waliozaliwa nje ya ndoa kutokana na ‘ujinga’ wa wanandoa hao.

Tatizo lingine ni matusi, yaani anamtukana hadharani mbele ya watoto bila hata ya aibu. Kuhusu malezi ya watoto, watoto wanalelewa kana kwamba wako ktk kambi ya mateso kwani ni matusi (kama vile mbwa wee, kunguni, mjinga, taahira n.k) na mangumi kwa kwenda mbele. Heshima ndani ya nyumba imepungua na hakuna amani kabisa. Kwamba unaweza kuwakuta wanacheka lakini ni vicheko vya kebehi na ukiwaona leo baada ya saa moja ukiwakuta utadhani ni maadui wa siku nyingi.

Kaka Mlachaombwani anadai kuwa amani yake yeye ni pale anapokuwa kazini, safarini au kwa marafiki zake tu, lakini nyumbani kila siku moto unawaka. Amekiri kuwa sasa wakati wake mwingi anaupotezea katika kompyuta kwa kuwa hapo ndio hupata farijiko huku akijifunza mambo mengi kadha wa kadha ili kupoteza mawazo.

Nimemuuliza kwa nini asimuache huyo mwanamke na kumfukuza kama hali yenyewe ndiyo hiyo naye amenijibu kuwa yupo kwa SABABU ya WANAWE na si vinginevyo. Anasema kuwa muda ukifika ataondoka yeye tu na kumwachia kila kitu huyo mkewe! Yaani pamoja na mahusiano haya mabaya bado yupo tu? Na atakaa kwa muda gani akiyavumilia hayo? Kuna haja ya kuondoka? Kuna haja ya kuoa mke mwingine? Afanye nini?

Wenzangu kwangu mimi huu ni mtihani maana hata sijui nimshauri nini kaka Mlachaombwani.

Swali langu kwa ndugu zangu wasomaji:- Je ndoa ni kupendana kati ya wanandoa au ni tendo la ndoa? Je ni kipi kinachowaunganisha wanandoa, ni upendo au ni tendo la ndoa?
Je kweli kuna upendo kati ya wanandoa hawa na ni namna gani tunaweza kuwasaidia wanandoa hawa?

Wednesday, February 24, 2010

Swali la leo :- Lahusu uumbaji+Meno kwa viumbe hai!!!

Mwenzenu nimeulizwa hili swali na watoto wangu niimeona ni vema kama nikipata msaada wenu kwani kwangu lilikuwa swali gumu kidogo. Swali lasema hivi:- Hivi kwa nini viumbe hai vyote vizaliwapo havina meno na baada ye huota meno? Na kwa mfano binadamu, baada ya kukua na kufikia miaka 4 mpaka labda 13 meno ya utatoni hutoka na kuota mapya. Na halafu jinsi wazeekavyo hupoteza meno yote. hivi ni kwanini?

Tuesday, February 23, 2010

KAMA MASIHARA: BLOG YA MAISHA YATIMIZA MIAKA MIWILI LEO!

Sijui hapa nipo wapi au kweli ni mimi?

Ni kama vile mtoto azaliwapo na kukua katika hatua tofauti tofauti, na mara nyingi hatua hizo huenda sambamba na mabadiliko ya kimwili na kiakili. Nakumbuka ilikuwa ni kama mzaha hivi, siku moja nikiwa kazini, tena nikiwa nimechoka , nikaanza kuwaza na kujiuliza, hivi kuna akina Yasinta wangapi hapa duniani. Sikujua kwa nini nilijiuliza Swali hilo, kwani sisi binaadamu huwa tunapitiwa na mawazo mengi sana, kama sikosei niliwahi kusoma pale kwa kaka Shabani kwenye kijiwe chake cha Utambuzi na Kujitambua kuwa kwa kawaida sisi wanaadamu huwa tunapitiwa na mawazo 5000 mpaka 6000 kwa siku…..ajabu eee!!!

Basi swali hilo lilinifanya nijaribu kufanya utafiti kupitia Google, na pale nikaandika neno Yasinta, nililetewa habari nyingi sana zinazowahusu akina Yasinta, lakini nilivutiwa na habari iliyoandikwa Kiswahili na nilipofungua nikakutana na Blog ya kaka Markus Mpangala ya KARIBU NYASA.

Nilikutana na habari nyingi sana za nyumbani na nilivutiwa na sana baadhi ya makala zake na maoni ya wasomaji mbalimbali, niliisoma habari ile ya Yasinta kwa kirefu sana, ilikuwa ni simulizi nzuri mno iliyoniondolea uchovu kwa siku ile na si hiyo tu bali nilijikuta nikipitia blog mbalimbali za wanablog wengine ambao Markus aliwaunganisha na blog yake.

Nilishikwa na hamasa na nikaona ni vyema niwasiliane na kaka Markus ili niweze kumfahamu zaidi, nakumbuka nilipomtumia email hakukawia kunijibu na ikawa ndio tumefungua ukurasa mpy wa mawasiliano kati yetu.

Ni katika kipindi hicho ndipo nilipopata wazo la kutaka kublog na kwa msaada wa kaka yangu huyu Markus Mpangala ndio hapo mnao tarehe 23/02/2008 blog hii ya maisha ikazaliwa.

Leo hii Blog hii ya Maisha inatimiza miaka miwili kamili huku nikijivunia mafanikio niliyoyafikia tangu nilipoianzisha blog hii. Kama nilivyosema hapo awali kuwa mtoto anapozaliwa hukua katika hatua tofauti tofauti na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa blog hii ya Maisha, kwani nilianza kama masihara kuandika habari mbalimbali za kijamii, za kufurahisha, za kuhuzunisha na za kuburudisha pia, na kupitia michango ya wasomaji na wanablog wenzangu nimeweza kujifunza mambo mengi sana, kiasi kwamba siwezi kusahau mafanikio niliyoyafikia, na ndio maana, hivi karibuni nikaboresha jina la blog hii na kuiita MAISHA NA MAFANIKIO, kwani mafanikio niliyoyafikia ni kutokana na maoni na ushauri kutoka kwa wasomaji na wana blog wenzangu.

Sitaweza kuyataja mafanikio ya blog hii kama sitawashukuru wale wasomaji ambao kwa kuvutiwa na blog hii ya MAISHA NA MAFANIKIO wamekuwa wakinitumia habari zao na kunitaka niziweke hapa kwangu nan hivyo kuleta changamoto kutoka kwa wasomaji wengine.

Kusema kweli siwezi kumtaja mtu mmoja mmoja, wale wote waliofanikisha uwepo wa blog hii kwani ni wengi sana na ninaamini nitawachosha kwa kusoma, ila ningependa kuwashukuru wooote mliofanikisha uwepo wa blog hii, bila ninyi naamini nisingiweza kujivunia mafanikio haya niliyoyafikia.
Naomba msichoke kutembelea Blog yenu hii na bila kusahau kuwa michango na maoni yenu ni muhimu sana katika kuiboresha blog hii.
Pia napenda kumshukuru dadangu Mariam Yazawa kwa kunitumia hiyo picha hapo juu. kwa kumsoma zaidi gonga hapa
Nawashukuru sana na ninawatakia kila la kheri katika shughuli zenu za kila siku Mungu awabariki wote.

Monday, February 22, 2010

Siri ya mafanikio Ruhuwiko Sekondari

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Ruhuwiko
wakisikiliza hoja kwa umakini

KILA anapotembea shuleni na maeneo mengine mkoani Ruvuma, Mkuu wa shule ya sekondari ya Ruhuwiko, Meja Paul Rugwabuza kifua chake kiko mbele. Kwanza ni kwa vile yeye ni mwanajeshi hivyo lazima awe mkakamavu, lakini pili ni kutokana na matokeo mazuri ya shule anayoiongoza.
Anaonekana mwenye furaha kwa sababu jukumu alilopewa la kusimamia elimu ya watoto katika shule hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limefanikiwa kwa asilimia kubwa.
"Kitaaluma shule hii imekuwa ikipiga hatua mwaka hadi mwaka hususani kwa kuzingatia matokeo ya kidato cha cha nne na sita viwango vizuri zaidi vya ufaulu ambavyo shule inaweza kujivunia sana ni vya kidato cha sita kwani tangu shule ianze," alisema Meja Rugwabuza katika mahafali ya tano ya kidato cha sita yaliyofanyika hivi karibuni.
"Mfano mzuri wa matokeo ya mock wa kidato cha sita mwaka 2009 katika Mkoa wa Ruvuma kulikuwa na daraja la kwanza 17, daraja la pili 108, daraja la tatu 84 na daraja la nne walikuwa wanne. Hakukuwa na mwanafunzi aliyefeli hivyo tunatarajia kupeleka wanafunzi wengi zaidi kujiunga na elimu ya juu (vyuo vikuu)."
Mbali ya mock, matokeo ya kidato cha sita mwaka 2006 yanaonyesha mmoja alipata daraja la I, daraja la II walikuwa 15, daraja la III walikuwa saba na mmoja daraja la IV.
Mwaka 2007 wanne walipata daraja la I, daraja la II walikuwa 20, daraja la III walikuwa 18, daraja la IV walikuwa sita; na mwaka 2008 mmoja amepata daraja la I, daraja la II walikuwa 30, daraja la III walikuwa 36 na daraja la IV walikuwa 13.
Hata nafasi kitaifa, Ruhuwiko huwa inashika nafasi nzuri. Mathalani mwaka 2006 shule ilishika nafasi ya 16 kati ya shule 57, mwaka 2007 ilishika nafasi ya 38 kati ya shule 230 hivyo iko ndani ya malengo kusudiwa ya maendeleo ya shule.
Takwimu hizo za kitaifa ndizo anajivunia Meja Rugwabuza aliyerithi mikoba ya mtangulizi wake Meja Celestin Mwangasi (amehamia Makongo Sekondari) kuiongoza shule hiyo iliyoko kilomita nne kutoka Songea mjini.
Mbali ya uwezo wa darasani, imeelezwa wana nidhamu nzuri na mitihani yao ya ndani wamekuwa wakifanya vizuri kwa viwango vinavyokubalika.
Matarajio ya baadaye ya Ruhuwiko, Meja Rugwabuza anasema yamo katika mpango wa maendeleo ya shule wa miaka tisa (2006-2015) unaotilia mkazo mambo mengi ambayo ni pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa afya za wanafunzi, walimu na wafanyakazi.
Katika kukabiliana na tatizo la utoro wa wanafunzi na kuondoa visingizio vya hapa na pale shule imeendelea mazingira ya shule kwa kuongeza bidhaa kwenye duka la shule, kujenga kibanda cha kutengeneza nywele, kuweka uzio kwenye bweni la wasichana na kumalizia pia bwalo la chakula kwa wanafunzi wa bweni.
Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1995 inatoa elimu ya sekondari kwa vijana wote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita na kwa kuzingatia umuhimu wa maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano wameajiri walimu wawili wenye diploma hivyo kuwa na walimu watatu. Matarajio yao ya hivi karibuni ni kuanza kufundisha hata watu wazima muda wa jioni.
"Vijana wengi wanaomaliza kidato cha sita katika shule hii wanajiunga na vyuo vikuu na taasisi nyingine za elimu ya juu.
Pamoja na kujivunia mafanikio hayo shule pia inawawezesha vijana kukabiliana na umasikini kwa kutoa elimu ya ujasiriamali na kompyuta ili mwanafunzi anayehitimu katika shule hii aweze kukabiliana na mazingira yanayomzunguka," anasema Meja Rugwabuza.
Pamoja na mafanikio hayo shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika uendeshaji na utekelezaji wa mipango yake ya maendeleo ikiwemo tatizo la kukatika mara kwa mara umeme hivyo kusababisha shule kutumia jenereta. Kutokana na gharama za mafuta kupanda imeongeza gharama za uendeshaji.
Changamoto nyingine ni ujenzi wa ukumbi wa mikutano na mitihani ambao huo uko katika hatua za awali. Nguvu kubwa ya vifaa na fedha inahitajika kwani shule peke yake haiwezi kumudu kwa muda mfupi.
"Tatizo jingine ni kupanda kwa gharama za uendeshaji kutokana na kupanda sana kwa bei ya chakula na vifaa. Hata hivyo, shule imejitahidi kuepuka kupandisha sana gharama za malipo ya ada ili lengo la kuwapatia elimu watoto wengi zaidi liweze kufanikiwa," anaeleza Meja Rugwabuza.
Japo shule hiyo inakabiliwa na changamoto hizo na nyingine kadhaa zinaoendana na uboreshaji wa elimu, Ruhuwiko haijatetereka katika utendaji wake na mfano mzuri ni matokeo yake ya mitihani ya taifa ya kidato cha sita kwa miaka mitatu mfululizo. Matokeo hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya watu wengi kuvutiwa na elimu ambayo inatolewa na shule hiyo.
Meja Rugwabuza anasema mafanikio ya shule hiyo kwa kiasi kikubwa yanatokana na ushirikiano mkubwa uliopo baina ya walimu, wafanyakazi, wanafunzi pamoja na wanajumuiya wa shule hiyo akiwemo Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Dk Emmanuel Nchimbi.
Dk Nchimbi amekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya shule hiyo hususan kwa misaada yake ya mabati na saruji. Aliipatia shule hiyo mabati 240 na saruji mifuko 1000 msaada ambao umefanikisha kukamilika kwa ujenzi wa bweni la wasichana.
"Napenda kukushukuru Mbunge na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa misaada mbalimbali ambayo umekuwa ukitupatia na mara zote umekuwa mstari wa mbele kwa kutusaidia kila unapopata nafasi ya kufanya hivyo ,"anasema mkuu wa shule mbele ya Dk Nchimbi.
Dk Nchimbi, kwa upande wake aliipongeza shule hiyo kwa kufanikiwa kuongeza ufaulu mwaka hadi mwaka na kuwataka waendelee kuweka mkazo zaidi katika masomo ili kuongeza ufaulu zaidi.
"Nawashauri wanafunzi wa kujenga tabia ya kujiendeleza na kusoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari ili wasiambukizwe virusi vya ukimwi,"anasema.
Amewataka wanafunzi hao wachukue tahadhari mapema na wawe makini na wenye nidhamu kwa kuacha kujiingiza katika vitendo viovu kama uvutaji bangi, uzinzi pamoja na kufanya ngono ili wasiambukizwe ukimwi.
"Nawapongeza kwa mafanikio makubwa mliyopata kwa kuweza kuongeza ufaulu mwaka hadi mwaka, ila nawashauri wanafunzi kuwa makini na msijiingize katika vitendo vitakavyowaingiza katika mtego wa kuambukizwa virusi vya ukimwi kwani taifa na jamii linawahitaji,"anasema.
Naye mwanafunziwa kidato cha sita shuleni hapo Frank Milinga, anasema kutokana na uongozi bora wa shule hiyo wameweza kuonyesha juhudi kubwa katika taaluma, nidhamu, michezo na utawala kwa jumla hivyo kuiwezesha shule hiyo kufanya vizuri katika mitihani ya ndani na nje.
"Bado shule yetu inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya ukosefu wa vitabu vya kutosha vya kiada na ziada, upungufu wa mabweni, vifaa vya maabara, ukumbi wa mikutano pamoja na gari la shule," anasema mwanafunzi huyo anayetarajiwa kuhitimu mwezi huu.
Wanafunzi hao wamewaomba wadau mbalimbali kuongeza jitihada za kuwasaidia ili kupata ufumbuzi wa tatizo hilo ikiwa ni pamoja na wazazi kuwasilisha michango ya ada kwa wakati
Habari hii imeandikwa na Joyce Joliga katika gazeti la mwanancchi. Nimeona si vibaya kama wasomaji wa blog hii pia wakisoma. Kwani wote tuna nia moja

Sunday, February 21, 2010

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KWAKO CAMILLA !!Miaka 12 imepita leo tangu binti yetu Camilla azaliwe. Ni binti ambaye anapenda sana kusoma, kuandika, kucheza mpira wa mikono (handball) pia anapenda aina ya mziki wa kupuliza au (trombone. ) Twakuomba Mwenywezi Mungu uwe /uzidi kumbari binti yetu Camilla azidi kuwa kama alivyo. Na pia twakoomba uzidi kutupa sisi wazazi/walezi nguvu ya kumlea ili azidi kuwa binti mwema na mwenye busara. CAMILLA HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA.
mama mdogo Koero anasema

Hata hivyo ningependa kufanya sala fupi kwa ajili yako.

‘Nakutakia sherehe njema ya siku yako ya kuzaliwa na natumaini kila jema lililosemwa na wote waliokutakia sherehe njema ya siku yako ya kuzaliwa litatimia. Mungu atakubariki uwe na afya njema na ukue kwa umri na kimo na pia mungu akujaze na Hekma na Busara na uwe na uzingativu katika masomo yako’

Aaamen..............

Pia maneno haya ya mjomba Mzee wa Changamoto ni mazuri sana na ndio nimemwomba mama ayaweke hapa mbele Ahsante "mjomba"

Dah!!!
Sijui nianze na lipi hapa?
Ok.... Kwanza POLE na HONGERA kwa wazazi.
Kwa wale waliopitia uzazi na ulezi wanajua kuwa HONGERA ya kulea ni vema ikaambatana na POLE yake. Ni kwa kuwa kulea ni zaidi ya kazi. Ni zaidi ya wajibu.
Lakini HONGERA kwa mara ya tena kwa baadhi ya yale niyajuayo kwa "Mjomba" Camilla. Kwa kuendelea kupenda asili za atokako, kupenda kujua na kuongea lugha ya asili ya Mama. Kupeda na kufanya kazi kama kilimo, usafi, kuchota maji na nyingine nilizoona ukifanya wakati wa likizo ndeeefu ya Ruhuwiko.
Hongera kwa wazazi kwa kuanzisha haya yote.
Kwa "Mjomba" Camilla. Uko ulivyo na unavyotakiwa kuwa. Unayotenda ndiyo yenye uzuri kuliko mtazamo wa wengi kuhusu watu. Ninalomaanisha hapa ni kuwa UNA MATENNDO MAZURI AMBAYO NDIO TAFSIRI YA UZURI.
Tatizo pekee la umri unaokabiliana nao sasa (na pengine miaka 8 ijayo) ni kuwa watoto wenye umri huu "hujiona wenye akili zaidi ya yeyote huamini marafiki kuliko wazazi" na huamini kuwa wako mbele na sahihi kimawazo kuliko wazazi.
Najua umekuwa msikivu na mtii kwa wazazi, basi hilo ndilo nikuombealo na kukusihi uliendele.
U-mrembo kwa Taswira tuonazo na TABIA tujuazo.
Baraka kwako katika miaka teleee ijayo.
HERI YA SIKU YA KUZALIWA "Mjomba"

Friday, February 19, 2010

Hongera Kwa Siku Ya Kuzaliwa Kaka SAVIO!!!!

2007 Ruhuwiko!!

Wote tunakutakia kheri sana kwa siku hii maalum kwako kwa kutimiza miaka. Twakutakia mafanikio mema katika maisha na kila jambo ufanyalo pia familia yako . Kumbuka kwamba sisi ndugu, marafiki, wajombo, watoto, shemeji twakupenda sana. HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA SAVIO.!!!!

Kwa vile leo pia ni Ijumaa basi ngoja tusherehekee siku yako kwa kipande hiki cha muziki:-)

Thursday, February 18, 2010

HADITHI YA MWANA MPOTEVU

Hiii hadithi inanikumbusha mambo mengi sana sijui wenzangu mnasemaje?

Kulikuwa na baba mmoja aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. Siku moja yule wa mwisho akamwambia baba yake : baba mimi sasa ni mkubwa naomba haki yangu nataka kuondoka kwenda mbali kutafuta maisha. Baba yake akampa pesa nyingi tu. Akaondoka akaenda zake na pesa zote.

Muda si mrefu akapata marafiki wengi tu. akawa anakula na kunywa nao pamoja na yeye ndiye aliyekuwa analipa kila kitu.

Lakini muda si mrefu pesa zote zikamwishia. Akawa hana kitu cha kula. Marafiki zake wote hawakumpa wala kumsaidia chochote isipokuwa walimtupa barabarani.

Siku moja akaondoka akaenda kwa mkulima mmoja na kusema ya kwamba anaomba chakula, aina yoyote ile, na halafu atafanya kazi kwake. Mkulima akamhurumia akampa chakula na akamwambia kazi yake ni kuchunga nguruwe wake.

Hata hiyo kijana bado alikuwa ana njaa. Akaanza kuwaza: kwa nini napata taabu hapa wakati baba yangu ana chakula kingi tu. Narudi nyumbani kwa baba tena. Nataka kufanya kazi kwa baba kuliko hapa.

Mara akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Na kusema baba, naomba radhi nimekosa. Ilibidi nisirudi na wala usinipokee tena hapa nyumbani kwako. Lakini baba kwa uchungu wa furaha akamkumbatia na kumpokea. Kwa furaha kubwa baba akamfanyia kijana wake sherehe kubwa kwa kufurahia kwa sababu kijana wake alikuwa amerudi tena kwake.

Kaka mtu akawa anarudi toka kazini(shambani) akakutana na babake asemaye. Mdogo wako amerudi tena nyumbani njoo tumsherehekee. Alipotea sasa amerudi tena.

Swali: Je? Hadithihii wewe inakufundisha nini?
Na je? ungekuwa wewe ni yule kaka mkubwa ungefanyaje?

Hebu sikiliza hapa lugha ya mwenzetu wasukuma mimi nimeipenda kwani nimeelewa neno moja moja hata hivyo najivunia lugha zetu za asili zinasikika.


Au kama hujaelewa hapo basi sikiliza hapa lugha yetu ya kiswahili

Wednesday, February 17, 2010

Then Good Created............

God created the donkey


and said to him.
"You will be a donkey. You will work un-tiringly from sunrise to sunset
carrying burdens on your back. You will eat grass,
you will have no intelligence and you will live 50 years."
The donkey answered:
"I will be a donkey, but to live 50years is much. Give me only 20 years"
God granted his wish.
............ ......... ......... ......... ......... ......... ......... ...


God created the dog


and said to him:
"You will guard the house of man. You will be his best Friend.
You will eat the scraps that he gives you and
you will live 30years.
You will be a dog. "
The dog answered:
"Sir, to live 30years is too much,give me only 15 years.
" God granted his wish.>
............ ......... ......... ......... ......... ......... ......... ......

God created the monkey


and said to him:
"You will be a monkey. You will swing from branch to branch doing tricks.
You will be amusing and you will live
20 years. "
The monkey
answered:
"To live 20 years is too much, give me only 10years."
God granted his wish.
............ ......... ......... ......... ......... ......... ......... ...

Finally God created man...

and said to him:
"You will be man, the only rational creature on the face of the earth.
You will use your intelligence to become master over all the animals.
You will dominate the world and you will live 20years."

Man responded:
"Sir, I will be a man but to live only
20 years is very little,
give me the 30years that the donkey refused,
the 15years that the dog did not want and
the 10years the monkey refused.
" God granted man's wish
............ ......... ......... ......... ......... ......... .......

And since then, man lives
20years as a man ,

marries and spends
30 years like a donkey,
working and carrying all the burdens on his back.

Then when his children are grown,
he lives 15years like a dog taking care of the house
and eating whatever is given to him,

so that when he is old,
he can retire and live 10 years like a monkey,
going from house to house and from one son or
daughter to another doing tricks to amuse his grandchildren.

That's Life.

Monday, February 15, 2010

Da Mija na kaka Chacha O`Wambura a.k.a Ngáwanambiti nimesubiri kushonewa zile nguo nimechoka!!

Kazi ya umodo ya siku moja Habari zenu ingawa mkono umepotea:-)

Naupenda utamaduni wangu (wetu)

soma zaidi hapa Ila bahati mbaya sijapata ile rangi ya bendera yetu nadhani hizi picha au hili vazi Limekaa/zimekaa vizuri:-)

Salaam za makabila yetu

kijijini kwetu
Wasomaji wapendwa wa blog hii, najaribu kufanya utafiti wa lugha za makabila yetu hapa nchini. Kwa mujibu wa tafiti inasemekana kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini.Niliamua kuangalia zaidi salaam, hususan za asubuhi, Kutokana na utafiti wangu nimepitia makabila kadhaa na kukutana na maneno yanayotumiaka katika salaam za asubuhi ambayo yanafanana kidogo, hebu tuone maneno hayo ni yapi:
KINGONI: Uyimwiki = Habari za asubuhi


KIZIGUA: Kugona vihi = Habari za asubuhi


KINYAKYUSA: Ughonile = Habari za asubuhi


KIYAO: kwimukaga = Habari za asubuhi


KIPARE: Murevuka = Habari za asubuhi


KIUNGUJA: wambaje = Habari za asubuhi


KISAMBAA: Onga makeo = Habari za asubuhi


KIANGAZA: Mwalamtse = Habari za asubuhi


KINYAMWEZI: Mwangaluka = Habari za asubuhi


KICHAGA: Shimbonyi = Habari za asubuhi


KIMERU: Konumbware = Habari za asubuhi


KIMASAI: Sopai = Habari za asubuhi


KISUKUMA: Mwadila = Habari za asubuhi


KIHEHE: Kamwene = Habari za asubuhi


KIBENA: Kamwene = Habari za asubuhi


KIKINGA: Ulamwihe = Habari za asubuhi


KINYIRAMBA: Ulalaliani = Habari za asubuhi


KIHAYA: Wabonaki = Habari za asubuhi
Kwa leo naishia hapa mwenye nyongeza anaweza kuongeza ili tujifunze pamoja.
Tukutane wakati ujao


Mada hii nimeichukua kutoka kwenye kibaraza cha VUKANI cha dada Koero, nami nimevutiwa nayo nikaona sio vibaya kuirejea ili kujikumbusha.

Sunday, February 14, 2010

Happy Valentines Day/Upendo Daima /Alla Hjärtans Dag Pia ni Dominika/Jumapili ya Saba ya Mwaka C!!!

Leo ni Valentineday/siku ya kupendana/alla hjärtans dag. Sio kama siku zote watu hawapwndani HAPANA baki ni kuhamasisha wtu wazidi kupendana . Kwangu mimi ina maana kubwa kwani nimekuwa mwanaharakati bora wa Upendo kwa jamii haijalishi nimefika kiwango gani . Nashukuru hata kama sijafika robo. Nakuomba nawe shiriki kutangaza Upendo Duniani. HAPPY VALENTINES DAY.!!!! NA PIA DOMINIKA NJEMA

Friday, February 12, 2010

Ulanzi ukiwa mwingi ngono huwa nje nje!!

Unywaji wa pombe ya ulanzi unadaiwa kuwa chanzo cha kuongezeka kwa maambukizi ya Ukimwi Iringa!!

"KARIBU mchumba, karibu unywe ulanzi, unataka mtogwa (uliogemwa leo) au mkangafu (wa siku nyingi)? Njoo ukae nami hapa usiogope! Mama Anita, lete lita moja fanya haraka mrembo asije akaondoka," hivyo ndivyo nilivyopokewa katika klabu cha pombe cha Ndiuka, Iringa.
Nilikwenda kufanyia kazi utafiti wa wataalamu unaosema kuwa moja ya sababu zinazochangia kasi ya maambukizi ya Ukimwi katika Mkoa wa Iringa ni ulevi hasa wa pombe za kienyeji.
Mmoja wa wauzaji wa pombe hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe anasema wakati wa msimu wa pombe ya ulanzi, wanywaji wengi hushindwa kuzuia tamaa zao za ngono na kujikuta wakijiingiza katika vitendo hivyo bila kinga.
"Ulanzi ukiwa mwingi ngono pia huwa nje nje! Ndiyo maana msimu wa ulanzi ukiisha tu wanawake wengi huwa na mimba zisizotarajiwa. Ulanzi ni hatari, unasababisha watu washindwe kujizuia na hatuwezi kuuacha kwani ni asili yetu," anasema.
Pombe hiyo iligunduliwa wakati wa utawala wa machifu wa kabila la Wabena katika Wilaya ya Njombe baada ya mti mchanga wa mwanzi kukatika na kuanza kutoa maji matamu.
Tangu wakati huo, pombe hiyo imekuwa ikithaminiwa na wakazi wa Mkoa wa Iringa na tayari imeshambaa na kufika katika maeneo mengine mengi hasa kusini mwa Tanzania.
Wanywaji wengi wa ulanzi wanasema bila shaka kwamba pombe hiyo inachangia kasi ya Ukimwi.
"Msimu wa ulanzi huwa unauzwa bei rahisi ambayo hakuna inayemshinda ndo maana watu wengi hulewa hivyo kuwa rahisi kwao kufanya ngono bila kujiandaa kwani wanawake wengi wakishanunuliwa kinywaji hicho huwa wepesi kukubali," anasema Richard Mwenda.
Mtaalamu wa magonjwa ya ngono mkoani Iringa, Dk Paul Luvanda anasema pombe hiyo ndiyo kichocheo kikubwa cha ngono zembe hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Ukimwi.
"Ulevi hasa wa pombe ya ulanzi unachangia kuongeza hamu ya kufanya ngono zembe, wengi wamejikuta wakipata maambukizi kutoka na pombe hii ambayo inaheshimiwa na wenyeji," anasema Dk Luvanda.
Ulanzi siyo kichocheo pekee, Luvanda anataja mila na desturi potofu ambazo jamii nyingi mkoani humo bado inaziendeleza. Miongoni mwazo ni kurithi wajane, kukosekana kwa usawa kijinsia, kutakasa wajane na wasichana, kuoa wake wengi, imani za kishirikina na kutotahiri.
Nyingine ni umaskini wa kipato. Maisha ya wananchi wengi ni duni.
Anasema kutobadili tabia licha ya elimu ya ukimwi kuwafikia wananchi na wengine kuathiriwa kwa njia moja au nyingine na Ukimwi ni miongoni mwa sababu za kuenea kwa ugonjwa huo.
Anataja sababu nyingine kuwa ni muingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli nyingi za biashara na ongezeko la taasisi mbalimbali mkoani humo.
Hali ya maambukizi ikoje?
Dk Luvanda anasema watu 17,555 kati ya 71,628 waliojitokeza kupima kwa hiari kati ya Julai 2008 hadi Juni 2009, walikutwa na maambukizi ya VVU. Hali inayoonyesha kwamba maambukizi yameongezeka na kufikia asilimia 24.5 hali ambayo ni hatari.
Anasema kwa mujibu wa matokeo ya utafiti wa hali ya ukimwi kitaifa mwaka 2003/2004, maambukizi yalikuwa asilimia 13.4 na mwaka 2007/2008 yakapanda na kufikia asilimia 15.7.
"Utafiti unaonyesha Iringa tupo asilimia 24.5, hii siyo hali ya kawaida hata kidogo." Anasema Wilaya ya Makete inaongoza kwa kuwa na asilimia 35.9, Njombe 31.9, Iringa 30.5, Mufindi 24.0, Manispaa 23.5, Ludewa 18.6, Njombe mjini 21.1 na Kilolo 12.2.
Hadi Juni 2009, wananchi walioandikishwa kweny mpango wa dawa za kupunguza makali ni 51,137 na walioanza kutumia dawa hizo ni 25,703.
Wakati maambukizi ya Ukimwi mkoani Iringa yakiongezeka kwa kasi, takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa yamepungua kutoka asilimia saba mwaka 2003 hadi asilimia 5.8 mwaka 2007.
Hiyo ina maana kwamba Mkoa wa Iringa ndiyo wa kwanza nchini kwa kuwa na kiwango cha juu kabisa cha maambukizi, ukifuatiwa na Dar es Salaam yenye asilimia 8.9 na wa tatu ni Mbeya yenye asilimia 7.9.
Kutokana na kiwango hicho cha maambukizi mkoa unakisiwa kuwa na watu 246,935 wanaoishi na VVU/Ukimwi kati ya wakazi wake wote zaidi ya milioni 1.5 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.
Idadi ya watoto yatima nayo imekuwa ikiongezeka siku hadi siku kutokana na wazazi wengi kupoteza maisha. Watoto 67,915 wameshatambuliwa na 30,303 wanapatiwa misaada ya chakula, mavazi, malazi na elimu.
Mkoa unafanya nini?
Kupaa kwa takwimu za maambukizi ya Ukimwi kunaonyesha kuwa jitihada mbalimbali zinazofanywa na mkoa huo kupambana na janga hilo zimegonga mwamba.
Hata hivyo, Dk Luvanda anasema umeandaa mkakati wa kupambana na kasi hiyo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2008 utakaomilika Septemba 2012 ukilenga kupunguza kasi hiyo kwa asilimia 50.
Anasema tayari Sh1.8 bilioni zimeshatumika kuanzia Juni 2008 hadi June 2009. Kati ya fedha zilizotumika, Sh953.9milioni ni kutoka serikali kuu wakati Sh870.1milioni ni michango wa wadau mbalimbali wanaoshiriki katika mapambano ya Ukimwi Iringa.
Dk Luvanda anasema Wilaya ya Makete ilitumia Sh 942.5milioni, Ludewa 150.7milioni, Manispaa 22.2 milioni, Iringa Vijijini 116.2 milioni, Kilolo 54.6 milioni, Mufindi 442.6 milioni na Wilaya ya Njombe ilitumia Sh114.8 milioni.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Ezekiel Mpuya anasema mkakati huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mapambano dhidi ya Ukimwi katika halmashauri za wilaya na kuwa umeandaliwa kwa kuzingatia vipengele vilivyomo katika Mkakati wa Pili wa Taifa wa Mapambano ya Ukimwi (NMSF) wa mwaka 2008 hadi 2012.
Mpuya anasema mpango huo umezingatia pia ushirikishwaji wa wadau mbalimbali walio katika mapambano ya Ukimwi mkoani Iringa, pamoja na maelekezo ya wataalamu wa ndani ya mkoa na taifa.
Anasema mipango iliyoibuliwa inatekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja mmoja na kutathminiwa kila mwaka kisha kuendelezwa na mipya kuibuliwa kulingana na matokeo ya tathmini.
Anasema huduma za tiba zinatolewa katika hospitali 16 zilizopo mkoani Iringa na vituo vya afya 14 kati ya 26. Lengo ni kufikia vituo vya vyote.
Ili kufikia lengo hilo, mkoa unatekeleza mikakati minne ambayo ni pamoja na kutoa huduma za majumbani kwa wagonjwa wa Ukimwi, tiba na huduma muhimu kwa wagonjwa wa Ukimwi na watu wanaoishi na VVU, kuanzisha mapambano dhidi ya Ukimwi sehemu za kazi katika sekta ya afya na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mohamed Abdulaziz anatilia shaka takwimu hizo. Anawataka wataalamu kukaa upya na kuzitafiti ili kujua kama kweli ni hali halisi.
“Pamoja na mikakati yetu, wataalamu kaeni mfanye utafiti upya tujue kama kweli hizi ndizo takwimu au siyo na kama ni kweli, kuna kila sababu ya kutangaza hali ya hatari kwa mkoa huu,†anasema
Wananchi wanasemaje?
Wakazi wengi wa Mkoa wa Iringa wanataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kutoa elimu ya ukimwi na kuhakikisha kuwa misaada na fedha zinazotolewa kwa ajili ya janga hilo zinawafikia walengwa.
Lakini wanashangazwa na kitu kimoja. Ikiwa wengi wanalalamikiwa kwa kufanya ngono zembe baadhi ya maeneo hayana kondom na mengine watalaamu hawajawaeleza kinagaubaga juu ya matumuzi na umuhimu wake
IMEANDIKWA NA TUMAINI MSOWOYA WA GAZETI LA MWANANCHI LA TAREHE 15/1/2010
Ijumaa njema wapendwa na kumbukeni kupunguza ugimbi(ulanzi= ulasi)

Thursday, February 11, 2010

Karibu katika Ulimwengu wa kublog:- Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti!Karibu katika ulimwengu wa kublog kaka Chacha unaweza kumtembelea kwa kubonyeza hapa. http://mataranyirato.blogspot.com/

Wednesday, February 10, 2010

Karibuni Wote Kikombe Hiki Cha Chai!!!!!

You´re Just my Cup of Tea,
Our Love Warms my Heart.
Najua wote mnajua mie ni mpenzi sana wa chai tena ile isiyo na sukari(Chingambu) :-).

Tuesday, February 9, 2010

Kibanga Ampiga MkoloniNasoma kitabu cha Tujifunze Lugha Yetu
Wapendwa

Jana niliposti hapa kijiweni http://ruhuwiko.blogspot.com/2010/02/kibanga-ampiga-mkoloni.html juu ya kisanga cha Kibanga kumbonda mkoloni. Awali nilitaka tu kuwakumbusha wanakijiwe juu ya stori hii lakini cha kushangaza Mt. Simon http://simon-kitururu.blogspot.com/na Chacha Ng’wanambiti! wamekuja na hoja nyingine ambazo haziwezi kupita bila kujadiliwa.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
kwa kung'ang'ania bakora mkoloni ana nguvu na jeuri!Je si kuna wakati tunag'ang'ania mambo hata yasofaa huku tukijiona tuna maguvu na jeuri ya kufanya tutakavo hata kama tunaumiza wengine? :-(
February 9, 2010 12:04 AM

SIMON KITURURU said...
Nimeipenda sana staili ya ngwala a.k.a kubwengana ya Mheshimiwa mpole Kibanga.Lakini bado :``Siku hizi kijiji cha Kwachaga kina maendele mazuri ya kilimo na mifugo. Maendeleo yote yamepatikana kwa sababu ya uongozi bora wa Serikali ya wananchi.´´- inanitamanisha nitamani kwenda huko KWACHANGA kwa kuwa BADO najiuliza zaidi kuwa;- hivi huko KWACHANGA ni Tanzania? Kwa maana nahisi viongozi wao wangeifaa kweli SERIKALI ya Tanzania baada ya Watanzania kumuondoa TANZANIA Mkoloni.:-(Ngojea niwashangilie washindi,Kibanga OYEEE! Ukoloni mamboleo OYEE!Nawaza tu!:-(
February 9, 2010 12:55 AM

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
na kwa mtindo wa ushangiliaji wa mt. simon akiwa na glass ya komoni a.k.a ze bia mkoni, nina wasiwasi kama viongozi wetu watazinduka na kuuona ukweli wa kuwa twaweza kujiletea maendeleo wenyewe bila wakoloni:-(katika dunia ya sasa Kibanga angeweza kuonekana kichaa! je unadhani twahitaji vichaa wengi wa kuwazindua viongozi wetu kama alivozinduliwa waziri mkuu wa Italia?Samahani jamani, labda naanza kurukwa na akili :-( Lakini kama ndivo msinambie miye ndo niende kuwazindua hao walolala :-(
February 9, 2010 6:52 AM

SIMON KITURURU said...
@Kadinali Chacha Ng'wanambiti: Unauhakika Kibanga alivyompiga Mkoloni ni kweli Mkoloni aliondoka na Ukoloni wake?Si wajua kuwa jambo kubwa litofautishalo ukoloni na kwenda haja msalani a.k.a CHOONI ni kwamba UKOLONI hauhitaji Mkoloni awepo katika KOLONI kama Haja ihitajivyo ajisaidiaye chooni awe CHOONI?
February 9, 2010 10:49 AM

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...
@Mt. Simon: ni kweli kabisa mkoloni hakuondoka na ukoloni wake kwa kuwa kuna bado vijeba ambavyo ukiviangalia saaaaaana utastukia kuwa ni vikolini katika nguo za rangi ya kijani/njano :-(na kuhusu choo nadhani silazima mtu aende chooni kwani katika baadhi ya makabila kama la kwangu wawezakuta msitu wa jirani umesheheni uyoga kwa kuwa kuna mbolea-kinyesi cha mtu :-( na waweza ukakuta karibu na palipo na mzigo wa kinyesi aidha kuna kuna aidha jiwe ama nyasi badala ya ukoloni wa toilet paper :-(lakini, ni wangapi kati yetu tumefikiria kuhusu ujenzi wa choo au kujisitiri vichakani katika staili ya kumfukuza mkoloni mawazoni?Una hakika wewe si mkoloni ndani ya Utakatifu? :-(


Je WADAU, ni mafunzo gani tunayoweza kutohoa katika hadithi hii? Je ni kweli viongozi wa kijiji cha kibanga wanaweza kuwa suluhisho la ombwe la uongozi katika Tanzania yetu ya leo?

Msaada:- Tangazo la gari kuuzwa

Hi Yasinta
Vehicle Details

Make:Nissan

Model: MARCH

Model Type: AK12

Color: Pearl White

Year of Manufacture: 2002

Engine Capacity: 1240
Bei: 9.5m
Kwa mawasiliano na kuiona piga 0754082034 (Lulu)

Monday, February 8, 2010

Kibanga Ampiga Mkoloni

elimu ni ufungu wa maisha

Katika upekuzi wangu jana nikawa nimekifuma kitabu hiki na mwisho nikakutana na hadithi hii ungana nami kuisoma ina toka katika kitabu cha 6 Tujifunnze Lugha Yetu!

Zamani za ukoloni, palitokea Mzungu mmoja. Mzungu huyo hakuwa mtu mwema. Alikuwa mkali na mkatili sana. Kwa ajili ya ukatili wake watu walimwita mkoloni. Wanancgi wote walimchukia sana popote pale alipokwenda.

Mzungu huyo alikuwa Bwana Shamba. Alikuwa na bakora iliyokuwa imetengenezwa kwa mkwaju. Kila alipokwenda kukagua mashamba, alikuwa na bakora hiyo mkononi. Alipendelea sana kuitwa "Bwana Mkubwa". Mkolono huyo alifurahia sana kupiga watu. Aliwapiga watu waliposhindwa kupalilia mashamba. Aliwapiga pamba yao ilipokuwa chafu. Aliwapa taabu sana.

Katika kijiji cha Kwachaga, Wilaya ya Handeni, alikuwapo mzee mmoja aliyeitwa Kibanga. Mzee huyu alikuwa mwenye nguvu, hodari na shujuaa. alikuwa fundi wa mieleka. Ingawa alikuwa mwenye nguvu, alikuwa mpole. Hivyo watu wa Kwachaga walimpenda na kumtegemea kuwaongoza vitani.

Siku moja yule Mzungu alifika Kwachaga kukagua mashamba ya mihogo. Jumbe pamoja naye wakatembelea mashamba. Kwa bahati mbaya mwaka ule haukuwa na mvua ya kutosha. Kwa hiyo mihogo haikustawi. Kila wakati yule Mzungu alipotazama mashamba alitikisa kichwa na kufoka. Mwisho akamwagiza Jumbe kuitisha mkutano wa watu wote wa kijij. Waliporudi kijijini Jumbe akapiga mbiu. Watu wote wakakusanyika. Walipofika tu, yule Mkoloni akaanza kuwatukana, akawaambia, "Ninyi watu weusi ni wavivu sana. Hamfanyi kazi sawa sawa. Mashamba yenu ni mabaya sana". Jumbe akataka kumjibu ili kumweleza kwa nini mihogo haikustawi. Kabla hajamweleza yule Mzungu alimrukia na kumpiga kofi. Kisha akasema, "Sitaki kijibiwa na wewe, mvivu wa wavivu". Watu wote wakakaa kimya. Hakuna aliyeweza kufanya kitu.

Kibanga akajitokeza, akasimama. Akamtazama yule Mkoloni kwa dharau sana. Kisha akamwuliza, "Kutuita sisi wavivu ndiyo nini? Na kumpiga Jumbe wetu mbele yetu, maana yake nini?"

Kabla ya kumaliza kusema, Mkoloni aliamka kitini kwa hasira , akataka kumpiga Kibanga. Alishika bakora yake mkononi. Akasedma, "Nitakuadhibu vibaya kima we! Unajifanya kuwa shujua? Huwezi kucheza na bwana mkubwa. Nitakupiga, kisha utakwenga jela miezi sita." Lakini Mkoloni hakuwahi kumwadhibu Kibanga. Aliadhibiwa yeye. Kabla ya kumfikia, Kibanga alimpiga chenga. Kisha akamrukia, akamnyangánya bakorta yake. Akaitupa, ikaokotwa na vijana, wakaificha.

Kibanga alimshika yule Mzungu akamwambia. "Wewe umezoea kutoa amri kila siku, lakini leo utashika adabu, mbwe wee!" Papo hapo alimnyanyua juu na kumbwaga chini, puu! Yule Mkolono akaumia sana. Kabla ya kuamka, Kibanga alimwinua tena na kumbwaga chini kama furushi la pamba. Akamkalia.

Hapo yule Mkoloni akawa hana la kufanya. Bila ya bakora alikuwa hana nguvu. Akaomba radhi akilia, "Samahani! Naumia! Nihurumie! Sitafanya tena hivyo." Kibanga alimjibu kwa dharau, "Sikuachi mbwa wee! Leo utakiona cha mtema kuni! Ulijiona una nguvu. Leo nitakutengeneza."

Wazee wakamshika Kibanga na kumwomba asimpiga tena. Akamwacha. Kwa shida yule Mkoloni akajikokota kwenda hemeni. Alikuwa amejaa vumbi huku damu zikimtoka. Wazee wengine wakamfuata nyuma. Walinyamaza kimya, wakimhurumia. lakini vijana walifurahi sana.
Baadaye waliimba wimbo wa kumsifu Kibanga.

Jioni yule Mkoloni aliomba radhi kwa wazee. Mzee mmoja akasimama na kumwambia, "Umefanya vizuri kuomba radhi, nasi tunaipokea. Lakini tangu leo usijivunie ubwana. Jivunie utu. Ninyi wakaoloni mna kiburi. Mnatudharau. Kama ungetuuliza tungekuambia kwa nini migogo haikustawi. Haya yote yamekupata kwa sababu ya kiburi chako. Katika nchi hii tuanaamini kuwa kiburi si maungwana".

Baada ya hapo wazee wakamsamehe, lakini hawakumpa bakora yake. Ikabaki nyumbani kwa Jumbe. Yule Mkoloni akaondoka. Tangu siku hiyo hakufika tena Kwachaga. Kila mara alipokutana na watu aliyakumbuka maneno ya yule mzee, "Kiburi si maungwana".

Siku hizi kijiji cha Kwachaga kina maendele mazuri ya kilimo na mifugo. Maendeleo yote yamepatikana kwa sababu ya uongozi bora wa Serikali ya wananchi.

Sunday, February 7, 2010

Jumapili hii ya sita ya mwaka tusali sala hii!!!!!!

Ee Mungu unifanya niwe chombo cha amani yako. Penye chuki nilete mapatano, penye kukata tamaa nilete matumaini, penye huzuni furaha, Amina

Friday, February 5, 2010

Nawatakieni mwisho wa juma mwema!!!Natumaini wiki hii kwa wengi imeisha vizuri. Basi kama umemaliza kazi kaa chini na upumzike na usikilize mziki hii ukiwaza kitu kama una cha kuwaza la sivyo atapata mawazo kwa kusikiliza na kumuwaza umpendae ambaye yupo mbali nawe.

IJUMAA NJEMA NA WOTE MNAPENDWA!!

Thursday, February 4, 2010

SAYANSI YAKIRI BINADAMU HAFI, HUBADILIKA.

Kwa zaidi ya miongo miwili sasa, wanasayansi wamekuwa wakijitahidi kutafuta jibu la swali la, je binadamu anaendelea kuishi baada ya kupoteza mwili wake? Kuna wanaoonesha kwamba wanakubaliana na hilo na kuna wale ambao wanasema huenda hakuna kitu kama hicho.
Kwa mfano kuna wale wanasayansi ambao wanakiri kwamba, watoto wanaofahamika kwa jina la Indigo, ni watoto ambao wana akili kubwa kuliko zile za binadamu wa kawaida. Tafiti zinaonesha kwamba, watoto hawa walianza kuzaliwa hapa duniani kuanzia mwaka 1975. Ni watoto ambao uwezo wao katika kuelewa mambo ni mkubwa kuliko tulivyozoea kuona.

Baadhi ya watoto hawa, kutokana na uwezo mkubwa, wamekuwa wakikumbuka maisha yao ya nyuma, kabla hawajafa. Watoto hao wamekuwa wakisema waliishi zamani sana na kufa au kupoteza miili yao na kuja tena kuzaliwa mahali pengine.

Hakuna idadi maalum ya watoto hawa hapa duniani, lakini inadaiwa kwamba, wako wengi kiasi cha kufikia elfu kadhaa. Wanatofautiana pia kiuelewa, wengine wakiwa na kumbukumbu kali na uwezo mkubwa sana kiakili, kuliko wengine, ingawa wote wana ufahamu wa kiajabu.
Kwa nini wameanza kuzaliwa miaka ya 1975? Kuna nadharia nyingi zenye kujibu swali hilo. Moja kubwa ni ile inayohusisha ukuaji wa dunia na ulimwengu kwa ujumla. Kwamba itafika mahali, maarifa mengi yaliyojificha yataibuliwa. Kizazi cha watoto hawa kinadaiwa kwamba, kimekuja kumwonesha binadamu kwamba, amekuwa akiuchukulia ulimwengu na maisha, ndivyo sivyo.

Hivi karibuni mwanasayansi mmoja nchini India, amekiri kwamba binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena na kupewa mwili mwingine . Hii ina maana kwamba, sisi pia tumeshawahi kuishi huko nyuma kabla hatujafa na kurejea tena tukiwa na miili mipya, tuliyo nayo hivi sasa.
Mwanasayansi huyu Vikram Raj Singh Chauhan, amesema ana uhakika ataweza kuthibitisha hilo baada ya kukutana na mtoto wa umri wa miaka sita ambaye anakumbuka maisha yake ya nyuma kwa kiwango kikubwa sana. Mtoto huyo wa kiume, Taranjijt Singh anasema aliwahi kuishi miaka michache nyuma, ambapo alifariki kwa ajali ya pikipiki akiwa bado mdogo.

Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka miwili alianza kusema kuhusu maisha yake ya nyuma na alikuwa akitoroka sana nyumbani . Alikuwa akiwaambia wazazi wake kwamba anakumbuka kijiji alichokuwa akiishi na hata jina la shule aliyokuwa akisoma.

Alikumbuka pia jina la baba yake wa zamani {kabla hajafa}. Awali ilionekana kama aina fulani ya kisirani cha mtoto, lakini ilibidi wazazi wake waanze kuwa na wasiwasi kwa kadiri alivyokuwa akiongezeka kiumri.

Mtoto huyo alikumbuka pia siku aliyokufa . Aliwaambia wazazi wake kwamba, alikufa September 10,1992. Alikufa baada ya kugongwa na pikipiki wakati akiwa kwenye baiskeli akiwa anakwenda shuleni asubuhi. Baada ya ajali hiyo alipata majeraha kichwani na alifariki siku ya pili baada ya ajali.

Baba yake wa sasa hivi, Ranjit Singh, anasema, mtoto wake alipozidi kusisitiza kuhusu maisha yake ya zamani, waliamua na mkewe kumpeleka huko kijijini anakodai kwamba, ndiko alikoishi kabla hajafa. Awali hawakuweza kumpata mtu ambaye alikuwa anafanana na maelezo ya mtoto huyu. Mkazi mmoja wa kijiji hicho aliwaomba waende kijiji cha jirani kinachofuata.

Kwenye kijiji hicho walikwenda kwenye shule ya kijiji ambapo mwalimu mkuu wa shule hiyo alithibitisha kamba, September 10, 1992 alikufa mwanafunzi wa shule hiyo kwa ajali ya pikipiki. Kupitia shuleni hapo, walibaini mahali wazazi wa mtoto yule aliyekufa kwa ajali ya pikipiki, walipokuwa wakiishi.

Ni kweli waliwakuta wazazi ambao walithibitisha kufiwa na mtoto katika tarehe na njia iliyoelezwa. Baba wa sasa wa mtoto huyu, Tanjit Singh alieleza kwamba, mtoto wao aliwaambia kwamba madaftari aliyokuwa nayo wakati wa ajali yalilowa damu baada ya ajali ile na alitaja kiwango cha fedha ambazo zilikuwa kwenye mkoba wake wa shule.

Mama wa zamani wa mtoto huyu ambaye kwa maana hiyo ni mama wa mtoto aliyefariki mwaka 1992 aliposikia hivyo aliangua kilio kikubwa , kwani maelezo hayo yalikuwa sahihi bila doa la kosa. Alisema vitabu na fedha hizo bado vipo, kwani aliviweka kwa kumbukumbu ya kifo cha mwanaye .

Baadae mtoto huyu alirudi na wazazi wake wa sasa nyumbani kukiwa na maswali yasiyo na majibu. Wazazi wake wa zamani pamoja na ndugu zake, walikwenda kumtembelea kwao baadae. Mtoto huyu aliibaini picha ya siku ya ndoa ya wazazi wake, ambayo walikuja nayo wakati walipokwenda kumtembelea kwa wazazi wake wapya.

Awali mwanasayansi, Vikram Chauhan, alikataa kukubaliana na maelezo kuhusu mtoto huyu , lakini baadae alijipa moyo wa kuanza uchunguzi. Alitembelea vijiji vyote viwili , cha zamani alikozaliwa na kufa na hiki cha sasa alipozaliwa.

Alizungumza na wazazi wote na kupata maelezo ambayo yalimfanya kuona kuna jambo la maana kuhusiana na kifo na ‘kufufuka’ kwa mtoto huyu. Kwenye kijiji alichozaliwa na kufa mtoto huyu, muuza duka mmoja alikiri kwamba ni kweli , mtoto kama huyo alikuwepo na yeye alimkopesha madaftari jana yake na alipogongwa alikuwa akielekea dukani kwake kumlipa madaftari hayo.

Chauhan alichukua sampuli ya mwandiko wa mtoto huyu na ule wa kwenye madaftari ya marehemu. Ilipokwenda kupimwa na wataalamu wa mwandiko, ilibainika kwamba, ilikuwa ni ya mtu mmoja.
Kumbuka kwamba mwandiko wangu hauwezi kuwa sawa na wa mtu yeyote, kama ilivyo alama za vidole. Kila mwandiko una sifa zake maalum ambazo haziwezi kupatikana kwenye mwandiko wa mtu mwingine.

Wataalamu wana uwezo wa kubaini mwandiko wa kughushi hata kama umefanywa na mtaalamu wa kiasi gani wa kughushi miandiko.
Kubwa zaidi ni kwamba mtoto huyu ambaye alishaanza kusoma kwenye maisha yake ya kabla ya kifo, hivi sasa hajapelekwa shule, kwa sababu familia yake ya sasa ni maskini. Hata hivyo katika jambo la kushangaza zaidi alipotakiwa kuandika alifabeti za kiingereza na ki-punjabi aliweza kufanya hivyo bila tatizo. Kama hajasoma ingewezekana vipi kufanya hivyo? Anatumia akili ya zamani ya kabla hajafa.

Familia yake ya zamani imeomba kukabidhiwa mtoto wao, lakini familia yake ya sasa imesema hapana, huyo ni mtoto wao. Kisheria, bila shaka, familia yake ya sasa ambayo ni maskini sana, wakati ile ya zamani ilikuwa na uwezo, ndiyo yenye uhalali wa kuishi na mtoto huyu.
Huenda baada ya sayansi kuthibitisha kwamba watu hufa na baadae kurudi wakiwa wanamiliki miilia tofauti, familia kama hii ya zamani ya mtoto huyu, ndipo itakapoweza kupata haki.

Hata hivyo, bila shaka kila familia kati ya hizo mbili, itakayoishi naye, itakuwa na mashaka ya aina fulani.

Mwanasayansi kama Chauhan na wengine wanaamni kwamba, kama roho ikihama kutoka mwili mmoja na kwenda mwili mwingine, huenda huko na akili au mawazo na hisia pia. Kinachoachwa ni mwili unaoonekana, lakini hiyo miili mingine huwa pamoja. Hii ina maana kwamba, hata mwandiko utabaki kuwa uleule kama ilivyokuwa.
Chauhan anasema, hivi sasa anao ushahidi wa kisayansi kuthibitisha kwamba, binadamu anapokufa, huja kuzaliwa tena, lakini hutumia mwili mwingine. Hata hivyo anasema anahitaji muda zaidi kuthibitisha jambo hili.

Bila shaka, ushahidi wa wazi kabisa kuhusu watoto hawa wa indigo, unaweza kutuonesha kwamba, tunapokufa, maana yake tumepoteza mwili , lakini bado hisia, akili, na roho ambavyo huja kuingia kwenye mwili mwingine ambao utatengenezwa na wazazi wengine wawili au wale wale, vinakuwepo.

Ni vigumu kupingana na maelezo ya mtoto huyu, ambaye tangu akiwa na umri wa miaka miwili, alikuwa akizungumzia kuhusu kumbukumbu alizonazo juu ya maisha yake ya nyuma. Ugumu wa kupinga unatokana na ukweli kwamba, hatimaye maelezo yake yalithibitika.
Kama ingekuwa Chauhan sio mwanasayansi, tungeweza kusema, suala hili bado, halijatazamwa kisayansi na hivyo, haliwezi kuelezewa kama jambo halisi.

Kwa mwanasayansi kuvutiwa na jambo hili na kuanza kulifanyia utafiti huku akikiri kwamba, kuna mambo yenye kutanza, ni hatua kubwa katika binadamu kuingia mahali ambapo atabaini ukweli wa kuwepo maisha baada ya kifo.

Lakini sio maisha baada ya kifo peke yake bali pia kukubali kwamba huenda binadamu ataendelea kuwepo, kwa sababu uwepo {being} haujapotea na hauwezi kupotea. Mwili wako utaharibika, lakini uwepo wa binadamu hauwezi kupotea.

Habari hii nimeipata katika gazeti la Jitambue la huko nyumbani Tanzania, ambalo siku hizi halichapishwi tena baada mmiliki wake Munga Tehenan kufariki dunia.

Wednesday, February 3, 2010

Mapotopoto: Matunda pori yenye sifa tatu

mti wa masuku/mapotopoto
matunda kwenye mti (masuku) mapotopoto


Habari hii imenikumbusha nilipokuwa mtoto magauni yalikuwa yanachanika mpaka mama alikuwa anachukia kweli. Maana ukienda porini ukirudi mapotopoto kibao kwenye gauni. Sielewi kwa nini nilikuwa sichukui kapu. Haya ungana nami tusome:-)

*Utamu wake wamithilishwa na asali
*Miti yake yadaiwa kutibu malaria
*Magamba yake ni mbolea maridhawa

RUVUMA ni mkoa uliojaliwa neema nyingi. Una aina mbalimbali za madini na inaelezwa kwamba utafiti wa kina ukifanyika unaweza kuwa na migodi mikubwa hivyo kuinua uchumi na ajira.
Katika sekta nyingine, Ruvuma ina misitu mikubwa iliyosheheni miti ya aina mbalimbali. Pia una Ziwa Nyasa lenye samaki watamu na dagaa wazuri kuliko dagaa wowote nchini.
Vile vile Mkoa wa Ruvuma una mito mingi, Mngaka, Ruhuhu na Ruvuma, kutaja michache, inavutia na inatoa samaki watamu kama mbasa, mbufu, mbelele na wengineo. Ruvuma ni moja ya mito mikubwa nchini na ambao unatenganisha Tanzania na Msumbiji.
Mkoa huo una milima ya kuvutia ambayo kama ikifanyiwa kazi inaweza kuwa moja ya vivutio vya kitalii na kuliingizia taifa na vijiji vinavyoizunguka kipato.
Milima Mara kwa mfano, uliopo Kata ya Magagura, unaweza kuwa kivutio kutokana na urefu na mandhari yake. Pia ipo Milima ya Litenga iliyotegwa na maji ambayo inalisha vijiji zaidi ya saba kwa miaka zaidi ya 30 sasa. Kuna safu ya Milima ya Livingstone, kuna Jiwe la Mungu huko Mbinga.
Pamoja na sifa hizo nilizotangulia kuzitaja, Mkoa wa Ruvuma una sifa nyingine kubwa inayotambulika zaidi hata kwa wanafunzi wa shule ya msingi, kilimo.
Mkoa huu ni moja ya mikoa minne 'the Big four' inayolisha chakula Tanzania na nchi za jirani. Pamoja na kuwa kilimo cha mahindi kinacholimwa zaidi Wilaya ya Songea, Ruvuma inazalisha kwa wingi mpunga, ulezi, ufuta, mtama, mihogo na soya.
Mbali ya mazao hayo ya chakula, kuna mazao ya biashara kama vile kahawa inayolimwa na kustawi zaidi wilayani Mbinga, na korosho inayolimwa zaidi Tunduru.
Sambamba na mazao ya chakula na biashara Ruvuma pia ina aina mbalimbali za matunda, ya kupandwa na yapo pia ya asili yanayopatikana kwa wingi misituni. Matunda pori haya yanajulikana kama mapotopoto, pia huitwa masuku.
Matunda mengine yanayostawi kwa wingi katika hasa katika Wilaya za Songea na Mbinga ni yake yanayojulikana kama Matunda Mungu.
Katika matunda yote hayo, mapotopoto yanaongoza kwa sifa. Wenyewe wanayafananisha na asali kwa utamu. Tunda lake lina mbegu nne ndani yake zinazozungukwa na utando wenye rojorojo ambao ndio hasa unaonywewa. Msimu wake wa mavuno ni kila robo ya mwisho wa mwaka.
Matunda haya yamekuwa chanzo kizuri cha ajira kwa akina mama wengi kwani wakati wa msimu, huenda porini na kwenda kuyauza katika maeneo mbalimbali kama vile kwenye vituo vya mabasi, sokoni, na wengine wakitembeza mitaani.
MMoja wa wachuuzi wa matunda hayo, Flora Mhagama anasema wakati mwingine huuza ndoo nzima kwa siku lakini kutokana na wingi wake porini, watu wengi huyafuata hivyo kufanya bei yake kuwa ndogo.

Anasema kwa ndoo hiyo moja anaweza kuingiza kati ya Sh1,000 na 1,500. Anauza kwa kupanga mafungu na kila fungu huuza kwa Sh50... “Yanatusaidia kupata fedha ya chumvi na sabuni.”
Wenyeji pia wanaamini kwamba miti inayotoa matunda hayo huweza kutoa dawa ya kutibu malaria inapokuwa michanga. Hii ni changamoto kwa watafiti wa dawa za tiba kubainisha ukweli huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Songea Vijijini Rogatus Haule anasema amewahi kusikia fununu hizo.
“Nimewahi kusikia kuwa miti michanga huweza kuwa dawa ya malaria ila siwezi kuthibitisha kama ni kweli au la. Ni ni wakati muafaka kwa taasisi za serikali na binafsi zinazojihusisha na utafiti wa dawa kutopuuzia fununu hizi na kuifanyia utafiti mimea hiyo,” anasema.
Inaelezwa pia kwamba masalia ya maganda ya matunda hayo ni rutuba nzuri kwa zao la uyoga. Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba katika misitu ambayo mapotopoto huzaliana kwa wingi, uyoga pia huota na kustawi.
Tatizo lililopo katika biashara ya matunda hayo kama ilivyo kwa mazao mengi mengine ni soko. Kwa mfano, Mkoa wa Dar es Salaam ambao hauna msimu wa matunda haujawahi kupelekewa mapotopoto.

Tatizo la kutopanua soko na kuangalia uwezakano wa kuyasindika matunda hayo ni moja ya changamoto ambazo zinawakabiliwa wadau wa kilimo wa Mkoa wa Ruvuma.

Na Jacob Malihoja kutoka gazeti la mwananchi

Tuesday, February 2, 2010

WAREMBO WA LEO:- NAJIVUNIA MAVAZI YETU YA HESHIMA NA UTAMADUNI WETU

Hili vazi nimelimeze mate kweli

Hapa ndo natamani kama nimvua na nilivae mimi.

Monday, February 1, 2010

HAKIKA ALIVUNA ALICHOPANDA!

Ndugu wasomaji leo nina kisa hiki nimetumiwa na mdau wa blog ya MAISHA, ili niiweke hapa tupate kujifunza kutokana na kisa hiki. Naomba muungane nami katika simulizi hii.


Ni binti ambaye amezaliwa katika familia inayosifika kwa uchawi pale kijijini kwetu Matombo Morogoro. Mama yake alikuwa akiogopwa sana na watu kwa kuhofiwa kuwa ni mchawi wa kutisha.

Nakumbuka nilisoma na mmoja wa wadogo wa huyo binti, na kuna siku niliwahi kumpiga mdogo wake baada ya kuniibia kalamu yangu tukiwa darasa la nne nikatishwa kwamba nitalogwa, niliogopa sana.

Niliondoka kijijini mara baada ya kumaliza darasa la saba na kuja jijini Dar Es Salaam, na huo ndio ukawa ni mwisho wangu kuonana na binti huyu. Naambiwa kuwa alikuja mjini na kuishi na dada zake maeneo ya Mwenge, na baadae akawa akijishughulisha na biashara ndogondogo.

Inasemekana alikuwa na kawaida ya kutembea na wanaume za watu kiasi cha kuhararisha ndoa kadhaa hapa jijini. Aliendelea na mchezo huo mpaka alipokuja kukutana na huyu mzee ambaye alikuwa na mkewe na watoto wakubwa tu. Huyo mzee alikuwa na familia yake maeneo ya Kinondoni na alikuwa na kazi nzuri sana, katika taasisi za Kimataifa.

Alikutana na huyo mzee maeneo ya Ubungo ambapo alikuwa na nyumba yake ameipangisha na alikuwa na kawaida ya kwenda kuitembelea nyumba yake kila mwisho wa juma.

Siku ya kukutana, ilikuwa huyu binti amemtembela rafikiye mwenye Grocery maeneo hayo ya Ubungo, na wakati wakiwa wanapiga soga ndipo yule mzee akafika pale kujipatia kinywaji wakati akiwasubiri mafundi wake ambao walikuwa waje kufanya marekebeisho kwenye nyumba yake.

Mzee akamuona mtoto wa Kiluguru ametulia akinywa soda yake baridi, mzee udenda ukamtoka na akaomba kujiunga na meza ile, alikaribishwa na binti huyo, na baada ya kufahamiana na kupata vinywaji kadhaa, na huo ndio ukawa mwanzo wa binti kuanza uhusiano na mzee huyo.

Wakati uhusiano wao ukiwa katika kilele, baada ya kumpagawisha mzee mzima na mapenzi motomoto, na mahaba ya Kiluguru, binti hakulaza damu, alihakikisha anamshika huyo mzee vilivyo, na mzee kutokana na kunogewa na penzi la binti akaamua kumpangishia nyumba na kumfungulia biashara ya Grocery maeneo ya Ubungo External.

Inasemekana mzee alishikwa vilivyo na binti wa Kiluguru na ili kuhakikisha anamshika vizuri akamwambia mzee kama anampenda auze nyumba yake ya Ubungo kisha amjengee nyumba yake mwenyewe ambayo itakuwa na jina lake, na kutokana na mzee kunogewa na penzi la binti akakubali bila kipingamizi, na nyumba ikauzwa na binti akajengewa nyumba yake huko Kinyerezi.

Binti hakuridhika, akamshawishi mzee wafunge ndoa, na ili kuweka mambo sawa akabadili dini kutoka dini yake ya kuzaliwa ya Kiislamu na kuwa mkristo, lakini je dini ya Kikristo inaruhusu ndoa za Mitala, hili likawa ni swali ambalo wapendwa hao liliwasumbua…….any way hiyo haikumsumbua binti. Akajua tu wakati utafika.

Mzee huyo ambaye ni Mhehe wa kule Iringa ambaye alioa mke wa Kimanyema kutoka kule Kigoma, akajikuta akipewa mtihani mwingine na binti wa Kiluguru. Binti akamtaka asiwe na zamu ya kulala kwa mke mkubwa, kwani mzee alishaihalalisha nyumba ndogo kwa mkewe na mkewe hakuwa na la kusema, aseme nini wakati alishaanza kuonja uchungu wa kugawana penzi na nyumba ndogo, kwani mume alikuwa akilala nje mara kwa mara na alikuwa haihudumii familia kama zamani, kwa kifupi mume alishaanza kuitelekeza ndoa yake.

Sasa safari hii binti hakutaka tena kugawana penzi na mke mkubwa,alishaonja asali na sasa alitaka kuchonga mzinga ili arine asali mwenyewe, na ili kujihakikishia kuwa anamshika mzee wa Kihehe alimtaka mzee achague, ama yeye au mkewe wa ndoa, hapo binti alikuwa na sauti maana kajengewa nyumba na mradi wa Grocery kafunguliwa. Mzee hakuwa na ubishi akamkubalia binti, na toka siku hiyo mzee akawa amekata mguu kwenda kwa mkewe Kinondoni akahamia Kinyerezi kwa binti.

Kutokana na kuitelekeza familia yake kule Kinondoni, watoto nao wakasimamishwa shule na kila wakienda kwa baba yao kumweleza kuwa wanatakiwa kulipa ada za shule walikuwa wanafukuzwa na binti kama mbwa.

Binti hakuridhika bado alitaka makuu, mara akamwambia mzee aache kazi ili wasaidiane kuendesha mradi wao wa Grocery, na mzee hakuwa na kipingamizi, akamkubalia binti na hivyo kuacha kazi. Sasa binti akaridhika akawa amemshika mzee vilivo, mzee akawa haruhusiwi kutoka kwenda popote bila ruhusa ya binti, na akawa kazi yake ni kukaa kaunta kutoa vinywaji.

Duh! Mzee alikuwa kama kondoo aliyenyeshewa na mvua, alikuwa akifokewa na binti kama mtoto, binti alikuwa ameshika hatamu. Maisha yaliendelea na binti mambo yake yalikuwa shwari kabisa.

Inasemwa kuwa, usije ukadhani unapomtendea mtu ubaya basi utapotea moja kwa moja, jua kwamba ile nguvu hasi uliyopanda ipo siku itarudi katika njia ambayo huwezi kufahamu hata siku moja na ni lazima itakuumiza na inategemea tu ulitenda nini . Leo hii wapo watu wanaishi katika madhila makubwa kutokana na nguvu hasi walizozipanda hapa duniani. Inasemwa kuwa chozi la mtu haliendi bure, na hiyo ilikuja kudhihirika hivi karibuni.Inaweza kuwa ni nasibu tu, lakini historia inaweza kutuhukumu.Siku moja wakati binti anatoka bafuni kuoga na wakati huo mzee alikwenda kufungua Grocery kama kawaida yake huku akimwacha binti akijiandaa kumpeleka mama yake mzazi hospitali kutibiwa miguu, kwani mama yake alikuwa akisumbuiwa na ugonjwa wa miguu na binti alimfuata huko kijijini ili kumleta mjini atibiwe.

Alipokuwa akitoka kuoga aliteleza kwenye sakafu ya Tiles na kuanguka ambapo alijigonga kichwa kwenya ukuta wa bafuni na kupoteza fahamu.Alikimbizwa hospitali ya Muhimbili akiwa amepoteza fahamu na kulazwa chumba maaluma kwa wagonjwa mahututi maarufu kama ICU.

Alikaa kwa siku tisa bila kupata fahamu na siku ya kumi ndipo akapata fahamu ambapo nilikwenda kumuona, nilipomuangalia sikuona dalili za binti kupona kwani alionekana dhahiri kuyakabili mauti.

Nasikitika kuwa siku ilyofuata binti alifariki majira ya saa kumi na mbili alfajiri. Msiba uliwekwa kwa dada yake mkubwa huko Mwenge, na yule mzee aliambiwa afungashe nguo zake tu na kuondoka katika nyumba ya binti huyo kwa madai eti ni nyumba ya binti aliyoijenga yeye mwenyewe kutokana na biashara zake.

Masikini yule mzee alilia kama mtoto mdogo, sio kwa kufiwa na binti, nyumba ndogo yake bali kwa kunyang’anywa nyumba yake aliyomjengea binti. Alichaoachwa nacho ni biashara ya Grocery peke yake.

Katika msiba huo kulizuka minong’ono kuwa binti kafanyiwa uchawi na mke wa mzee. Lakini hata hivyo mama wa binti pamoja na mabinti zake ambao nao wanasifika kuwa ni Magwiji wa Uchawi walidai kuwa wanamjua aliyemuua mdogo wao, na wakaahidi kuwa wakishamzika watajua cha kufanya.

Kulikuwa na maneno mengi yalisemwa katika msiba huo, kwani kila, mtu alisema lake. Hata baadhi ya marafiki zake walidai kumuonya kuwa mchezo anaoucheza utamletea maumivu, lakini binti alikuwa akijibu kwa kiburi kuwa hakuna atakayemuweza kwa kuwa ameaga kwao. Pia yuko binti mmoja alinukuliwa akisema kuwa hata yeye huchukuwa waume za watu lakini mwenzao alizidi. Kwa maneno yake mwenyewe alisema, “Hata mie nachukua wanaume za watu lakini ikifika jioni, mwenzangu namruhusu arudi kwake, lakini huyu mwenzetu alizidi, yaani alimnyang’anya mwenzie mumme wake hivihivi, hata mie ningemloga”.

Hata hivyo baadhi ya waombolezaji walionekana kupuuza madai hayo na kusimamia dini kuwa ni mapenzi ya mungu kwa binti huyo kufariki, kwani kila nafsi ni lazima itaonya mauti kama ilivyosemwa katika vitabu vya dini.

Binti alisafirishwa kupelekwa kwao Matombo Morogoro na kuzikwa. Mzee wa watu kaachiwa umasikini maana haijulikani kama aliweza kurejea kwa mkewe wa ndoa baada ya binti kufariki au alitafuta nyumba na kupanga kwani alishafukuzwa kwenye nyumba na ndugu wa binti na kazi alishaacha.

Dada Yasinta naamini wengi wanaweza kujifunza kwa kisa hiki ambacho ni kweli kimetokea hivi karibuni.