Sunday, April 29, 2012

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE WATAKAOPITA HAPA!!

Upendo na Amani Ametujalia Mungu!!
Hili ndilo neno la Jumapili ya leo!!

Friday, April 27, 2012

NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA KWA WIMBO HUU NAJUTA!!


WAKATI MWINGINE INAKUWA KAMA USIVYOTARAJIA...NA MWISHO NI MAUMIVU ILA KAMA MKIONGEA MNAWEZA KUELENA!!!!NAWATAKIENI MWISHO WA WIKI UWE SALAMA KWA WOTE!!!

Thursday, April 26, 2012

TUKUMBUKE METHALI ZETU!!!

1. Shida ingekuwa sumu tungekufa wengi.
2. Mwisho wa biashara yoyote ni faida au hasara.
3. Mpe akupaye, ukimpa asiyekupa ni sawa na kutupa.
4. Nyumba ya udongo haipingwi deki.
5. Hata mbuyu ulianza kama mchicha.
6. Kucheke sio dalili ya wema kwa mwenzio.
7. Usilie kwa kupigwa lia kwanini umepigwa
8. Akupendaye katika shida ndiye rafiki wa kweli.
9. Raha ya pilau ni kula kwa mkono
10. Usimchokoze kichaa ukiwa unakaa kwenye nyumba yenye vioo.
KILA LA KHERI.

Wednesday, April 25, 2012

MWANAFUNZI AKUTWA AKIFANYA NGONO NA NGÓMBE WA JIRANI!!

Kwa vile ni siku ya KIPENGELE CHA MARUDIO YA MADA BASI TUENDELEE KUSOMA NA HII. Binafsi imenisikitisha sana.... na nimestaajabika mno.

Habari na Ezekiel Kamanga, Kyela

Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Ikolo, Wilaya ya Kyela Bakiro Hance (18), amekutwa akifanya mapenzi na ng’ombe wa jirani yake.

Tukio hilo limetokea Machi 28 mwaka huu majira ya saa sita mchana katika Kijiji cha Ikolo ambapo mtuhumiwa alimchukua ng’ombe mmoja kati ya wawili wanaomilikiwa na Bwana Dickson Mwakimi, waliokuwa wamefungwa karibu na nyumba anayoishi mmiliki huyo.

Bwana Mwakimi alisikia ng’ombe wake akitoa sauti isiyo ya kawaida, kisha akatoka nje na kumkuta mwanafunzi huyo akifanya mapenzi na ng’ombe, ambapo alimkamata mwanafunzi huyo alimpeleka kwa mzazi wake aitwaye Bwana Hance, na mwanafunzi huyo alikiri kutenda kosa hilo ingawa hakuweza kueleza sababu zilizompelekea kufanya kitendo hicho cha aina yake.

Ameongeza kuwa mara kadhaa amekuwa akitenda tendo hilo na kwamba alijaribu kumkamata ng’ombe wa kwanza lakini alikuwa mkali hali iliyopelekea kushindwa kutimiza azma yake mwingine wa Bwana Mwakimi, ndipo alipoamua kumkamata ng’ombe wa pili na kumfunga kamba kwenye mti uliokaribu na kisha kuanza kufanya naye mapenzi.

Hata hivyo familia zote mbili za mmiliki wang’ombe na mwanafunzi zinaendelea kufanya mazungumzo ili kuondoa tofauti zilizojitokeza za tukio hilo la ajabu lililofanywa na mwanafunzi huyo.
via blogu ya ChimbukoLetu
-----------------------------------------------------------------
Najiuliza:- Ama kweli sijui sijui huyu kijana aliwaza nini?


MAPAPAI :- UTAMU ,FAIDA NA MATUMIZI YAKE!!

Kama kawaida ni kile KIPENGELE CHETU CHA MARUDIO MBALIMBALI YA MADA, PICHA NA VITU VINGINE MBALIMBALI. NA LEO TUANGALIE KUHUSU MAPAPAI. Hiii niliiweka hapa kibarazana lakini kama mnijuavyo huwa napenda kurudia kusoma kitu ili nielewe zaidi. kusoma maoni mazuri ya wasomaji gonga KAPULYA. Karibuni sana.


Hapa ni mti wa papai, leo nimekumbuka faida mbili za majani ya mipapai moja ni dawa ya tumbo hasa kama una tatizo la choo kubwa . Unachukua hayo majanai na unachemsha na halafu unakunywa yale maji yake. Pili ni sabuni unaweza au niseme mimi nimewahi kufulia nguo ila usifulie nguo nyeupe basi itakuwa kijana. Nguo nyingine zote sawa kabisa.


Na hapa ni tunda lenyewe nalo lina faida zake kwanza ni kwa ajili ya kula ni tamu sana na pia nalo kama una tatizo la choo kubwa ni nzuri. Halafu jambo jinginge papai ni kilainisho kizuri sana cha chama hasa nyama ya ngómbe. Toa hizo mbege weka kwenye chombo, pondaponda papai na uchanganya na hizo mbegu koroga taratibu katakata nyama vipande vidogovodogo weka humu kwenye mpondo na subiri masaa kadhaa. Hakika utaifaidi nyama yako mno itakuwa lainiiii. Ila kusema kweli nimetamani kweli papai ni muda sasa sijala:-). PANAPO MAJALIWA BASI TUONANE TENA KATIKA KIPENGELE HIKI JUMATANO IJAYO!!!!!!

Tuesday, April 24, 2012

SWALI HILI LIMENIKERA SANA:- MAJINA YA SAMAKI YANATOKA WAPI???

HAPA NI SAMAKI AINA YA MAGEGE
Ni muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza kuhusu majina ya samaki. Juzijuzi nilikuwa nikiangalia habari/pragramu kuhusu ziwa Nyasa, ziwa Viktoria na Tanganyika. Nikakumbuka majina ya samaki kama vile :- Kambale, Mbofu, Mbelele/sengefu, Magege, Vitui, Vindogo, Mbasa nk. Nikawa najuiliza hivi ni maeneo ya ziwa nyasa tu tunawaita hawa samaki hivi au? Na kama ni hivi nani aliwapa samaki hawa haya majini? Sikupata jibu...nikaona niliweke hapa kibarazani  hili swali. Kama nisemavyo/nijuavyo palipo na wengi hapaharibiki kitu. Tuwe pamoja katika kamjadala haka

Monday, April 23, 2012

TUANZE JUMATATU YETU KIHIVI:- JE UNAJUA HAPA NI WAPI?

Wengi wanaotokea kusini kwetu wanajua hapa ni wapi ila hata wale wasiotoka huko nadhani mtajua hapa ni wapi...haya tuona kama tunakumbuka Geografia ya nchi:-)....Jumatatu njema

Sunday, April 22, 2012

NI JUMAPILI YA TATU TANGU PASAKA IPITE NAMI NAWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA KWA WIMBO HUU!!


Hakika ni furaha.....JUMAPILI NJEMA KWA WATAKAOPITA HAPO MWENYEZI MUNGU AWABARIKI  NA IMANI NA UPENDO VITAWALE NYUMBANI MWENU.

Saturday, April 21, 2012

JUMAMOSI NJEMA JAMANI!!! WANDUGU WANGU:)

Tazama  jinsi ilivyo veme, ndugu wakae pamoja kwa umoja Zab 133:1
Michezo huleta burudani na kujenga miili yetu. Itusaidie pia kuleta umoja na mshikamano kati yetu; badala ya sokomoko, chuki na fitina.

Friday, April 20, 2012

MZIKI NI MOJA YA BURUDANI KATIKA MAISHA....


Leo nimepumzika kubeba maboxi  na bahati mbaya huko nje kuna mvua na kaubaridi kwa hiyo nikawa niriwadhika kwa kikombe cha chai na mziki, na ndipo nikakutana na kipande hiki na nikaona ni vizuri niburudike nanyi....jioni njema kwa wengi na wengi sijui asubuhi, mchana au usiku?

UJUMBE WA IJUMAA HII:- DAIMA KUMBUKA.....

1.SALAMU
2.SHUKRANI
3.SAMAHANI
4.SUBIRA
Basi nami nachukua nafasi hii na kumshukuru dada yangu Mariam wa http://mumyhery-jp.blogspot.se/ kwa picha hii hapa juu. Pia napenda kuwashukuru wasomaji wa Maisha na Mafanikio kwani bila uwepo wenu basi nisingeblog na salamu wa wote na wale niliowakosea snaomba mnisamehe..na mwisho nasubiri majibu  kutoka kwenu. NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA!!!

Thursday, April 19, 2012

KUMRADHI JAMANI!!

NAOMBA KUWAOMBENI RADHI KWA BADILIKO LA GHAFLA LILILOJITOKEZA KATIKA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO KATIKA BLOG LIST. NALIFANYIA KAZI TATIZO HILO. TUPO PAMOJA......

TANZANIA YETU NA UZURI WAKE....NIMEZIPENDA PICHA HIZI!!!

Hapa ni mlima wetu Kilimanjaro ambao unajulikana dunia nzima.....................................


Na hapa ni sehemu fulani huko Mtwara/Ntwara......




.......Na bila kusahau kisiwa chetu Zanzibar. Hakika kuna sehemu Tanzania mtu unaweza kuwa na usiamini kama upo Tanzania.

Wednesday, April 18, 2012

NAMNA YA KUTOKA KWENYE UTUMWA WA NDOA…….

Habari za leo..Ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO YA MAMBO MBALIMBALI. Leo nimeperuzi kwa kakangu Kaluse na kukutana na hii mada. KARIBUNI TUJADILI KWA PAMOJA.
Sio lengo langu kuwafundisha wanawake namna ya kuachana na wapenzi au waume zao. Lakini hebu fikiria kwamba kila wakati wanandoa au wapenzi wako kwenye vita. Hakuna amani, hakuna masikilizano. Kutwa nzima mtu anawaza kuhusu uhusiano wake mbaya hadi anashindwa hata kufanya kazi. Je, hali kama hii ina maana kwa mtu kuendelea kuwa kwenye ndoa?

Hapa nazungumzia wale ambao wanashindwa kutoka kwenye uhusiano, ambao wanajua kabisa kwamba, unawatesa na kuwaumiza. Kuna sababu nyingi kwa nini watu hawa wanashindwa, lakini nyingine zinatokana tu na kutojua namna ya kutoka, sio utegemezi wa aina yoyote.
Moja ya sababu, ambazo ninaziona sana hasa kwa wanawake ni kujali jamii itasemaje. Mtu anaona kabisa uhusiano haufai na anatamani kutoka . lakini anajiuliza, hivi watasemaje? Kuna wakati ndugu wanamwambia, yeye ndiye mkorofi. Kama hii ndio sababu anachotakiwa kufanya mwanandoa ni kuhakikisha kwamba anajifunza kuishi kama yeye. Nijuavyo mimi, hata wanandugu au jamii hata ikisema vipi, anayeumia au kuepuka kuumia au kuuawa ni yule aliye kwenye mateso ya ndoa
Jambo la kujiliza hapa ni kama, jamii ndiyo inayopigwa, kutukanwa, kutelekezwa au kudhalilishwa? Lakini jambo kubwa zaidi la kufahamu ni kwamba mtu alishaolewa maana yake ni mtu mzima mwenye haki ya kuamua juu ya maisha yake. Akisubiri ndugu wamwamulie, basi huyo bado ni mtoto..
Jambo lingine ni lile la, je nikimwacha nitapata mwingine? kwani wanaume siku hizi ni shida sana? Ni ujinga unaowafanya wengi kuuliza swali hilo. Unahitaji mwingine wa nini? Unahitaji mwingine ili maisha yako yawe ya maana zaidi au? Kama hakuna mwingine ni vyema kwa sababu maana yake ni kwamba hakuna mwingine wa kukutesa. Lakini wanasaikolojia wanaamini kwamba, ‘kila bidhaa ina mnunuzi.’ Kama unataka mwingine, hata ukiwa na miaka sitini utampata. Huwezi kumpata wakati ukiwa ndani ya tanuru la mateso. Ni lazima utoke kwanza.
Kuna wale wanaoshindwa kutoka kwa sababu wanaamini kwamba mwanamke haruhusiwi kutoa talaka. Hi siyo kweli. Kuna wanaoshindwa kutoka kwa sababu dini zao zinakataza kuachana, hii pia siyo kweli. Mwanamke au mwanaume, yeyote anaweza kuomba talaka na ikatolewa, kama kuna sababu zenye kukidhi haja hiyo. Chombo pekee kinachoweza kutoa talaka au kuidhinisha wanandoa kuachana ni Mahakama, siyo dini au taasisi nyingine. Kinachoitwa ‘talaka tatu’ kwa mfano, ni ushahidi tu, na sio talaka.
Kuna wale ambao hawako tayari kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu ya mali. Wanaogopa watagawana mali na wenzao, jambo ambalo hawako tayari kulifanya na mara nyingi hawa ni wanaume. Wapo pia wanawake ambao wao ndio waliokuwa watafutaji wakuu. Swali la kujiuliza ni hili. ‘Ni kipi bora, ni mali au ni amani na utulivu na uhai wako?’ kama ni mali, basi hakuna anayeweza kukuingilia kwenye uamuzi wako.
Lakini, kwa ufahamu tu, ni kwamba, pasipo na amani, mali haina maana na pasipo na amani uhai ni wa kubahatisha pia.
Wengine wanashindwa kutoka kwenye husiano kwa sababu wazazi wa mume na ndugu wanampenda sana. Anaogopa kuwaudhi kwa kuondoka kwenye ndoa ya mateso ya mtoto wao na ndugu yao. Anataka wafurahi, hivyo hawezi kuondoka. Huu nao ni upungufu.
Hivi unakuwa umeolewa na ndugu na wazazi au na mume? Lakini, kwani ukiondoka utashindwa kuwa karibu na watu hawa? Hutashindwa na pengine urafiki wenu utakuwa wa kudumu. Ukiendelea kukaa kwenye ndoa ya mateso kuna siku utakosana hata na hawa, maana unaweza ukalipukwa ukamuuwa mtoto au ndugu yao.
Kuna wale wanaoshindwa kutoka kwenye uhusiano mgumu kwa sababu wana watoto na wanaogopa kwamba, watoto wao watateseka. Hivi ni kuteseka kupi kubaya, kule kwa utotoni au ukubwani? Mtoto anayeishi kwenye ndoa yenye vurugu, anaharibikiwa kuanzia utotoni hadi ukubwani. Lakini, hata hivyo kuachana kwa wazazi, sio lazima kuwe na maana ya watoto kuteseka.
Kuna wakati hata watoto wanamwambia mama atoke kwenye ndoa, halafu mama huyo huyo anadai anakaa kwenye ndoa hiyo kwa sababu ya watoto! Kuna haja ya kujiuliza maswali kwa upana zaidi.
Ukitaka kutoka kwenye ndoa ngumu jiulize maswali haya. Je, ndoa hii ni kwa faida ya nani? Je, niliolewa au kuoa ili kupata shida au amani na upendo? Je, bila ndoa,nisingeweza kuishi mwenyewe? Tafuta mifano ya wasio na ndoa ambao wanafurahia maisha.
Jiulize ni kwa kiasi gani wengine wanasaidia kukusukuma zaidi kwenye ndoa hiyo? Jiulize ukamilifu wako. Je, wewe ni nusu mtu au mtu kamili? Kama ni mtu kamili , basi ishi kama mtu kamili. TUONANE TENA PANAPO MAJALIWA JUMATANO IJAYO. UPENDO DAIMA!!

Tuesday, April 17, 2012

NDIZI:- NI KATI YA VYAKULA NILIVYOKUWA NA UDHAIFU/NIVIPENDAVYO!!!

Mmmmhhh! sijui ni mara ngapi nimekodolea macho mlo huu wa ndizi leo. Ningependa kweli kula jioni hii hizi ndizi Bukoba..ila basi nakula kwa macho tu...Picha kutoka kwa Da´Lady Jay Dee .

MAISHA: NAIPENDA MIKOBA YANGU NA NAZIPENDA SKAFU/SHALI ZANGU!!!

HAPA NI BAADHI YA MIKOBA NIIPENDAYO
HAPA NI BAADHI YA MIKOBA YANGU

NA HAPA NI SKAFU ZANGU
NA HAPA NI SKAFU ZANG
Katika maisha sisi binadamu tupo tofauti kwa kila namna. Tukianzia tabia, sura, mwili, kupenda nk. Leo napenda kuzungumzia neno KUPENDA/TAMAA. Lakini si kule kupenda kwa kimapenzi hapana ni kupenda kwa kupenda vitu au kupenda kununua vitu hata kama anavyo vya kutosha:- Yaani utakuta mtu anapenda kikombe chake cha chai kweli kiasi kwamba mwingine akikigusa ni balaa. Mwingine anapenda kweli shati moja tu ambalo anaweza kulivaa kila siku utazani hana lingine. Mwingine akawa anapenda sweta kiasi kwamba hata kulifua anasahau. Halafu kuna hawa wanaonununua viatu, utakuta mtu ana pea za viatu chumba kizima huwa nashangaa sana je atavivaa lini? lakini hii yote ni basi tu yaani tamaa . Na kuna wanaokusanya/nunua vitabu. Kwa hiyo leo nataka kuwaambia mimi ni MDHAIFU SANA wa SKAFU/SHALIna MIKOBA. Hapo juu ni zaidi ya ishirini na bado natamani zaidi kwani nataka niwenazo rangi zote. NAPENDA SANA SKAFU.....NA PIA MIKOBA Swali je wewe ni mpenzi/mkusanyaji wa nini?

Monday, April 16, 2012

Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi?

Fikiri, matumizi nyumbani: chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni. Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu. Matibabu hospitalini, pesa ya walinzi kwa mwezi, sherehe za kuaga na kukaribisha mwaka mpya; Zaka ya kanisani na misikitini, Kupanda Mbegu/ Sadaka, Shukurani ya Neno, Ahadi na Collect, shukrani ya Chakula cha Bwana church, marekebisho ya kitasa cha mlango kabla mwenye nyumba hajashtuka, gharama za marejesho ya mkopo wa saccos kazini. Tozo za Flying (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzit...upa hapo hapo), Madalali wa nyumba/viwanja, Pango la nyumba, Fremu ya biashara/ofisi, Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers]; Mafuta ya gari, Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa); Tozo za kuegesha magari, Makato ya Mikopo, Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf. Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu, Harusi ya ndugu yako wa ukoo na zawadi, Sendoff ya mtoto wa mdogo wake rafiki yako na zawadi, Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi, Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara; Michango ya besdei party na zawadi; Ndugu wa kule kijijini, Mshahara wa Hausigeli na hausiboi; Bodaboda, teksi na bajaj; Duka la dawa kwa Mchaga, Tuisheni ya mtoto, Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko. Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa, Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu. Chakula cha mbwa, Machango wa Ujenzi wa Kupanua Kanisa, Kuchangia Uinjilisti Masasi, outing ya kitimoto, Ujenzi wa Nyumba Mabwepande, Kuendeleza shamba mkuranga (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa). Na kwa wale wenzetu wanaokwenda umbali wa Viti Virefu, moja moto moja baridi. Maji ya Traffik, Chai ya Nesi na Daktari, Kahawa ya Hakimu, Karani na PP. Vishoka waunganisha maji na umeme; Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa, makaribisho ya get together na dinner kwa rafiki wa kikazi ambaye hamjuani ila kweye simu tu, Mchango wa matibabu ya mtoto Nyumba ndogo kule Ngusero, mchango kidogo kwa rafiki aliyevamiwa na Vibaka na kuumizwa vibaya, gharama za malipo ya mtura Mkulima Bar Moshi, manunuzi ya maji ya Kilimanjaro Uwanjani Sheikh Amri Abeid Ukicheck mechi ya Yanga na JKT Oljoro, malipo kwa ajili ya Uji wa Shanga baada ya kazi Njiro jioni ya Alhamisi, Vipi manunuzi ya kandambili kwa ajili ya matumizi ya home.Hivi hali inakuwaje? Mia mbili ya watoto wa mtaani/ombaomba, kitu kidogo cha wale wanaolazimisha kuosha kioo cha gari kwenye foleni. umeme uliopanda bei, gesi iliyopanda bei, maji yaliyoadimika, bado contingency mana huu usafiri unaotembelea ball joint, bush, feni belt havijafa - hapo bado service. Bado msosi wa mchana kazini esp kama maofisi yetu mama ntilie wanakaribiana bei za restaurants, bado mchango wa kitchen pati na sare, baby shower. Na hapo bado hujatoa watoto outing jumapili, Upo wapi uwezekano wa kununua laptop mpya ambayo ni muhimu katika mfumo wa maisha ya kisasa, desktop nyingine kwa ajili ya watoto at home, rim mpya za gari ambazo zimeingia ku modernize gari lako kuu kuu, vipi kuhusu gharama za kujipendekeza kwa kimwana wa job ambaye amekubali kwenda nawe out leo, gaharama za matibabu ktk hospitali binafsi kwa kuwa madaktari wa serikali wapo ktk mgomo, Dogo naye “bro ninunulie basi japo kasimu ka promosheni, ile yangu imedondoka chooni” Mara “Bro/Sister Next week on sato shuleni tunavisit snake Park na sina shilingi 3000 za mahudhurio”, Wife naye “ Daddy leo Mwakasege yupo relini, vipi tutapitia? Hapo ujue kichwani gharama ya taxi baada ya semina, vipi tozo za toyo kwa kuwa nimeachwa na gari la staff. Dullah the balhead kama kawaida anakusubiri uwajibike kwa gharama zako. Mama yangu!!!!!!!!
Hapo mwajiri amekuongezea mshahara kwa 7% tu wakati inflation ni above 19%.Ukifikiri kwa makini, unajiuliza watanzania wana-survive vipi kwa style hii???Ndipo unapoimba "Mwokozi nitoe roho niepuke, hili balaaa"
HABARI HII NIMETUMIWA NA RAFIKI YANGU MUPENZI NA NIKAONA NIWAHABARISHE NA WENZANGU!!!

Sunday, April 15, 2012

JUMAPILI NJEMA:- UNALIA NINI?


Napenda kuwatakieni Jumapili njema wote mtakaopita hapa ....na pia mbarikiwe wote watakaopit​ia hapa.!!!

Saturday, April 14, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA IJUMAA KWA KAPULYA...KUSIKILIZA MZIKI WA SILI/UKIWAKUTA WATU WANATEMBEA UCHI NAWE FANYA HIVYO;.)

Ndo wanaanza kutumbuiza mziki /burudani



Wanaendelea kwa nyimbo, fidla, ngoma na kinanda...........................................

...............................na watu wametulia wakisikiliza ila kilichonishangaza hakuna hata mmoja alisimama na kucheza..mmmhhh kazi kwelikweli....


inaendelea na hakuna anayecheza...na mimi sijui ni vipi kucheza

........inaanza kufikia mwisho hapo amekuja muhusika na kuwapongeza kwa zawadi kwa kuwaburudisha watu kwa mziki nyororo....

Na bila kuchelewa mdada kutoka Tanzania akaona ni lazima achukua picha ya pamoja na hawa wanamziki ....

Na hivi ndivyo jana yangu/ijumaa yangu ilivyokuwa na ilivyoisha......napenda mziki wa asili kwa lugha yoyote ile. JUMAMOSI NJEMA KWENU JAMANI!!!...

Thursday, April 12, 2012

PICHA YA WIKI HIII:-NYWELE


Baada ya wiki kadha mdada huyu kufikiria afanye nini na nywele zake, leo amepata msusi na sasa anajiandaa kwenda kusuka........

....baada ya masaa tisa anaonekana hivi...bahati mbaya msusi wangu hakutaka kuwa katika picha ni mdada kutoka Kongo....Nimesuka rasta (tena) ila si za wamasai ..hahahaha...Oh! halafu nimesahau kusema bei yake ni 500 kr. Maana nimesoma maoni ya Da´Mija ameuliza ni shiling ngani kusuka hivi?

Tuesday, April 10, 2012

SALAMU NA SHUKRANI KUTOKA KWA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO!!!

Kwanza kabisa napenda kuwasalimu wote. Pia napenda kuchukua nafasi hii na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila dakika anipayo. Halafu nashukuru nimeisherekea sikuku hii ya kufufuka kwa Bwana wetu Kristo vema. Kwa hiyo namalizia na salamu hizi:-
Tuni/mafuatano ya sauti ndogo inaweza kukufanya/kutufanya uanze/tuanze kuimba, pia kukumbatiwa kunaweza kukufanya ujisikie vizuri. Vitu vidogo vinaweza kukufanya/kutufanya uwe/tuwe na furaha. Ni matumaini yangu SALAMU yangu hii, imekufanya UTABASAMU.....SIKU NJEMA....Yasinta/Kapulya

HUU NI UJUMBE WA JUMANNE HII YA LEO SHIKAMOO MWALIMU...!!!



Shikamoo mwalimu ....... pamoja Daima:-)

Sunday, April 8, 2012

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO INAPENDA KUWATAKIENI WOTE PASAKA NJEMA SANA!!

Salamu za Pasaka ziwafikieni wote popote mlipo na baraka kwa wote wataopita hapa. Muwe na pasaka njema wote....MNAPENDWA SANA.


Neno La Leo: Yesu Akasema; " Simon, Acha Kuvua Samaki, E Nenda Ukawe Mvuvi Wa Watu"

Ndugu Zangu,

Bwana Yesu alipotembelea mto Galilaya, aliwakuta wavuvi wakivua samaki, Simoni alikuwa ni miongoni mwa wavuvi hao. Yesu akasema; " Simoni, acha kuvua samaki,nifuate ukawe mvuvi wa watu. Naam. Watu wengi wanaangamia kwa kukosa uelewa. Kwa kutojitambua. Wanahitaji ukombozi wa kifikra.

Na siku zote, haki uinua taifa, vivyo hivyo, dhulma huangamiza taifa. Na mahala pasipo na haki, basi, hapo hapatukuwa na amani.Oneni, maovu yametamalaki katika dunia tunaoishi. Siku zote, kujipendelea ndilo shina la maovu.

Si tuna mifano hai. Oneni, wale wenzetu waliokaa na wakaamua kuuza nyumba za Serikali. John Magufuli ni mmoja wa watu hao. John alisimamia utekelezaji wa dhulma ile kwa Watanzania. Lililopelekea uamuzi wa hila na ghilba wa kuuza nyumba za serikali ni ubinafsi na hulka ya baadhi ya viongozi kutaka kujipendelea.

Karibu wote waliouziwa au kujiuzia nyumba hizo za Serikali, nyumba za wananchi, tayari walikuwa na nyumba kabla. Siku zoe, hamu inakuwa ni jambo jema, endapo binadamu ataweza kuitawala hamu/tamaa yake.

Wanadamu tusipoitawala hamu yetu, tukaanza kujipendelea, kuwasahau wengine, basi, hilo huwa ndio chimbuko la maovu. Hupelekea kutoelewana baina ya wanandugu, na hata kwa marafiki walioshibana.

Hupelekea vurugu na machafuko katika jamii. Tunazungumzia uwepo wa upendo, haki na usawa. Dini nyingi zinazungumzia umuhimu wa upendo, haki na usawa katika jamii. Iwe ni Uislamu na Ukristo vivyo hivyo. ”

Naapa kwa zama . Hakika binadamu wote wamo katika hasara isipokuwa wale walioamini na wakafanya matendo mema. Wakahusiana na haki na wakahusiana na subira” (Koran tukufu, Surat ASWR)

Biblia nayo inasema; kuwa Kaini alikuwa mtu wa kujipendelea mno, akamwua nduguye. Mfalme Saulo alijipendelea mno, akamdhulumu Daudi. Yuda alijipendelea mno, akalikubali kumsaliti Yesu kwa Vipande thelathini vya fedha. Hatimaye, akamsaliti Yesu.

Na ufufuko wa Bwana Yesu utukumbushe jukumu letu la kupambana na maovu katika jamii. Utukumbushe jukumu la kusaidia kazi ya kuwakomboa kifikra wanadamu wenzetu. Kama Bwana Yesu alivyomkumbusha Simoni kwa kumwambia; ” Simoni, acha kuvua samaki. E nenda ukawe mvuvi wa watu. Na hilo ndilo Neno la Leo. Pasaka Njema.

Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam0788 111 765http.//mjengwablog.com

Saturday, April 7, 2012

STEVEN KANUMBA HATUNAYE TENA!!

Pole wanandugu, marafiki, majirani na pia waTanzania wote kwa kuondokewa na msanii wetu!!! Pumzika kwa amani.

Friday, April 6, 2012

IJUMAA KUU NJEMA KWENU NDUGU ZANGUNI!


MNAKUMBUKA WIMBO HUU:-
Kiongozi...mateso yake bwana yalikuwa makubwa x2
Wote: ---Na hayo yote kwa sababu ya dhambi zetu x2
Kiongozi:--- Aliteseka sana x2
Wote:....Aliteseka x2.
Usisahau na kula nyama leo...si unajua IJUMAA kuu hakuna kula nyama ....

Thursday, April 5, 2012

UJUMBE WA ALHAMISI KUU HII/MALAIKA/UPENDO

Malaika wapo, lakini wakati mwingine hawana mabawa. Nasi twawaita MARAFIKI. Wote mnampendwa.:-) NAWATAKIENI WOTE ALHAMISI KUU HII IWE NJEMA PIA MAANDALIZI MEMA YA PASAKA!!!

Wednesday, April 4, 2012

JIONI NJEMA....MNAKUMBUKA WAKATI ULE JINSI WATU WALIVYOKUWA WAKIANDIAKIANA BARUA KAMA HIZI??

NIMEONA TUENDELEE NA JUMATANO HII YA MARUDIA NA HIII...KARIBUNI

Baby Hujambo
Nimekaa hapa mbele ya computer yangu usiku huu , nafikiria leo nikuandikie kwa lugha gani , ili uelewe ninachotaka kusema , mwanzo nilitaka kuandika kwa kiingereza lakini nikasema mhh inawezekana baadhi ya maneno matamu nikakosa bora niandika kwa lugha yetu takatifu Kiswahili Baby ni jambo la furaha sana kupata nafasi hii nyingine kukaa mbele ya computer kukuandikia kitu Fulani , kuna watu saa hizi wanalia wameumizwa na wapenzi wao kwa njia moja au nyingine , kuna wengine saa hizi wanafikiria kesho itakuwaje kwa sababu wamewauzi wapenzi wao , kuna wengine wameshakata tamaa ya maisha kwa sababu walijitoa sana kwa wapenzi wao mwishowe walikosa vyote walivyokuwa wanafikiria hapo mwanzo Pole kwa kuongelea mambo hayo hapo juu lakini ni kukumbusha tu wajibu wako katika kuhakikisha mapenzi yetu kati yangu na wewe yanadumu na kuendelea kukua siku hadi siku , kila siku unaposoma ujumbe wako ujue tu kwamba nimekufikiria kuliko jana kwahiyo nakupenda zaidi natamani uwe karibu yangu ili maneno ninayoandika nikuambie moja kwa moja , ili ujisikie maalumu zaidi . Pamoja na hayo mimi hapa nilipo naendelea vizuri sana , namshukuru mungu toka asubuhi mpaka sasa hivi umefika wakati wa kupumzika hakujatokea tatizo lolote zaidi ya moyo wangu kusikitika kwanini sikuwahi kukujua toka mwanzo nilipoanza kuwa na akili timamu nimeanza kukujua tu ukubwani , kwanini haya mapenzi ya sasa hivi sikuyapata huko kwingine kote ndio nakuja kuyapata sasa hivi ukubwani natamani ingekuwa hivyo toka mtoto mpaka sasa na hata ninapoaga dunia . Ahsante sana kwa mapenzi ya dhati unayonionyesha na kunipa kwa kweli naamini mimi ndio mwanaume bora kuliko wote duniani na tukiwa na familia basi ntakuwa baba bora kuliko wote duniani nikiwa na wewe , kwa jinsi tunavyoishi sasa hivi nina ndoto na malengo mazuri sana kuhusu wewe sijawahi kuwa na wasi wasi wowote mpaka sasa hivi . Baby naomba uendelee kuwa mwaminifu mvumilivu na mwenye malengo katika maisha yetu sote wawili , mie pia naahidi kuwa mwaminifu mvumilivu na malengo katika maisha yetu sote . Napenda kukuahidi kukupenda , kukujali na kuwa na wewe wakati wote wa maisha yangu toka uliponijua sintojutia kukupenda wala kuwaza lolote baya kuhusu wewe kama yalikwepo basi yafute anza maisha na mambo mapya katika maisha yetu sote wawili Nakupenda sana , naomba niishie hapa niende kupumzika sasa hivi Ha ha ha haaaaaaaaaaa…………………………sio mimi jamani……………………Kaaaazi kweli kweliHii nimeidesa Jamii Forum……………..

Neno La Leo: Ukiwa Na Roho Mbaya Na Huko Unakokwend​a Nako Ni Kubaya!

Ndugu zangu,

Msanii Remmy Ongala alipata kuimba;

" Ukiwa na roho mbaya,kweli tutakuogopa,
Ukiwa na roho mbaya, huko unakokwenda nako ni kubaya!"

Siku zote, mwanadamu usijaribu kufanikiwa maishani kwa kuwa mbaya kwa wengine. Ndio, kuna waliofanikiwa maishani kwa kuwa wabaya kwa wengine.

Siku zote, mwanadamu aliyefanikiwa kwa kuwatendea maovu wanadamu wenzake hawezi kuwa ni mtu mwenye furaha na amani maishani. Ataandamwa na jinamizi la maovu yake mpaka atakapoingia kaburini.

Je, mwanadamu huyo afanye nini?

Ajitazame mwenyewe. Aache kuendelea kuwatendea mabaya wengine katika kiu yake ya kukifikia ’ kilele cha mafanikio’- kama kweli kipo humu duniani! Hivyo basi, mwanadamu huyo atakuwa amejitambua. Na kwa vile naye ni mwanadamu, basi, hakuna mwanadamu asiyetenda makosa.

Dhambi kwa mwanadamu huyo itakuwa ni hulka yake ya kuendelea kuwakanyaga wanadamu wenzake katika juhudi za kuyafikia mafanikio yake. Misaada kwa yatima na masikini haitasaidia kuzifuta dhambi zake, maana, amezifanya na bado anaendelea kuzifanya.

Je, kwanini mwanadamu anakuwa ni mtenda maovu?
” Kwenda huko, utakufa kwa roho yako mbaya!”. Hiki kilikuwa ni kibwagizo katika moja ya matangazo ya kijamii redioni miaka ya karibuni.

Nilipata kumwuliza msanii Mrisho Mpoto swali la kifalsafa; ”Je, binadamu tunakufa kwa roho mbaya au roho chafu?”

Mpoto ananijibu: ” Kaka Maggid, naiona mantiki ya swali lako. Kama nitakunjua viganja vyangu na kuitema roho yangu kisha nikaiangalia... lakini fafanua kwanza fikra zako.”

Nikafafanua, kuwa binadamu hatukuumbwa kuwa wengine wana roho mbaya na wengine nzuri. Sote tumeumbwa na roho nzuri isipokuwa mazingira ndio yanayotufanya wengine tukawa na roho chafu na wengine roho safi. Ndio, roho nzuri tulizoumbwa nazo zinachafuka. Tunakuwa ni binadamu wenye roho chafu. Na hakika, Watanzania wengi tunakufa kutokana na roho chafu, zetu wenyewe au za wenzetu.

” Mh!” Anaguna Mrisho Mpoto. Ananiacha niendelee.

Maana, ni mtu mwenye roho chafu tu anayeweza kujaribu kuyazuia mabadiliko yatakayomsaidia mwanadamu mwenzake atoke mahali alipo na apige hatua itakayomsaidia maishani.

Ni mtu mwenye roho chafu tu atakayeweza kuhujumu mradi wa kuangamiza Malaria inayosababisha vifo vya maelfu ya watoto na watu wazima ili apate mafanikio binafsi.

Ndio, kuhujumu mradi wa kuzuia malaria ili apate fedha za kufanya mambo ya fahari au hata kununua uongozi wa kisiasa au kuendelea kubaki madarakani.

Kwa mwanadamu, ni heri ufe kwa kupambana na anayehujumu mradi wa kuangamiza malaria kuliko kufa kwa malaria inayotokana na mbu anayesababisha malaria.

Naam, You do not win by being bad. Utakwama njiani. Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa.
0788 111 765http://mjengwablog.com/
Nimetumiwa na Maggid Mjengwa.....

Je, ni muhimu wanandoa kusalimiana mnapoamka asubuhi?

Sio vinginene tena bali ni kile kipengele chetu cha JUMATANO YA MARUDIO..LEO nimetembelea Njombe kwa kutaka kusoma kazi zake zaizi unaeweza kutembelea Mbilinyi


Kwanza fahamu kwamba wanandoa wanapokaa muda mrefu baadhi ya vitu huanza kuchakaa kimapenzi. Hata hivyo upendo na wema husaidia kurudisha moto wa mapenzi na wanandoa kujiona wapya kila umri unavyozidi kuongezeka.
Matendo yanayoonesha wema kwa wanandoa ni gundi inayoshikisha wawili kujiona wapo karibu na moja ya tendo la wema ni kumsalimia mwenzako wakati mnaamka hata kama mmelala kitandani kimoja na hata mlikumbatiana usiku mzima au ulimuweka mwenzi wako kifuani usiku mzima.
Anayesalimiwa hujiona anapendwa, ana thamani na pia appreciated

+++++++++++++++++++++++++++++++++

Tupo kwenye new millennium kiasi ambacho watu tupo busy hata kuamka tunahitaji kuweka alarm ituamshe hata hivyo badala ya kukimbia bathroom kuoga ni muhimu kumpa kwanza salamu mwenzi wako ndipo uendelee na kazi zingine au na ratiba yako.
Tafiti zinaonesha wanandoa ambao husalimiana asubuhi wanajiona ndoa yao ni nzuri sana na wana mahusiano yanayoridhisha.
++++++++++++++++++++++++++++++++
Je, nini kinafanya maneno ya salaamu ya asubuhi kuwa muujiza katika ndoa na mahusiano?
Unapomsalimia mwenzi wako maana yake unamwambia na kumpa ujumbe kwamba ni asubuhi njema tumeamka pamoja katika upendo na furaha na kwamba unajisikia vizuri kuanza siku mpya na mtu wako na pia unaweza msingi mzuri wa mawasiliana kwa hiyo siku mpya.

-----------------------------------------------------------------------------------------------

Ahsanteni tukutane tena panapo majaliwa..nwatakieni maandalizi mema ya PASAKA!!

Tuesday, April 3, 2012

NIMEYAPENDA MENENO HAYA:- UBINADAMU KAZI!!!

Hapa ni mimi, nikiwa pamoja na wifi yangu na mwanae...ni mwaka jana. Hapa ni stendi KUU ya SONGEA tulikuwa tukiwasindikiza walikuwa wakirudi kwao Mbinga. Nimependezwa na maneno haya kwenye T-shirt ya Wifi. UBINADAMU KAZI.... ...KILA LA KHERI.

Monday, April 2, 2012

JIPATIA KITABU:- JINA LA KITABU MALIPO NI HAPAHAPA MTUNZI ADELA DALLY KAVISHE

Ambaye pia ni mtangazaji wa radio passion FM ambayo inarusha matangazo yake jijini Dar es salaam. Ninayo furaha kukamilisha kitabu cha simulizi cha MALIPO NI HAPAHAPA ambacho kimebeba simulizi tatu za kusisimua ikiwemo simulizi inayoitwa DADA YANGU, MAMA MDOGO pamoja na simulizi iliyobeba jina la kitabu MALIPO NI HAPAHAPA
Kitabu cha Malipo ni Hapahapa na simulizi nyingine za maisha kinaonyesha hali halisi ya maisha tunayoishi, matatizo tunayokutana nayo na namna ya kutatua matatizo tunayoyapata kwa wakati huo. Pia kwa kusoma kitabu hiki utajifunza mengi kwani kinatoa picha halisi ya maisha yetu ya kila siku.
Ndani ya kitabu hiki nimezungumzia maisha na mapenzi katika mtazamo halisi na pia kinaonyesha namna mapenzi yanavyoweza kuyageuza maisha kuwa machungu na mafupi.
Ukianza kusoma kitabu hiki hutakiacha hadi ukimalize kwani hadithi zilizomo zimesheheni matukio ya kusisimua ambayo moja kwa moja yanalenga maisha yetu ya kila siku.
Kupitia vitabu vya simulizi za maisha kama vile kitabu hiki, tunajifunza mambo mengi ambayo yanatusaidia kuishi katika mazingira tofauti ikiwa ni katika shida au raha na hata kujua namna ya kuishi na watu wanaotuzunguka.
Utapata kitabu hiki kwa bei ya sh 5000 tu.
Kwa mawasiliano kuhusu upatikanaji wa kitabu hiki.
Tafadhali tumia no zifuatazo +255652343430 au +255752817444Au kavisheadela@yahoo.com Unaweza pia kuingia humu http://www.adeladallykavishe.blogspot.com/
Nimetumiwa hii na mtunzi wa kitabu .Samahani rafiki mpendwa naomba uniwekee katika blog yako:-

NAONA TUIANZA JUMATATU HII YA KWANZA YA MWEZI HUU WA NNE NA KUTAFAKARI PICHA HII!!!

Kaazi kwelikweli, sijua nikikia itanilazimu kuoa ...au sijui itakuaje? Tutafakari pamoja naye jamani.....

Sunday, April 1, 2012

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA YA MATAWI!!

Leo ni jumapili ya matawi na pia ni jumapili ya kwanza ya mwezi huu wa nne. Pia ni sikuku ile ya WAJINGA, kwa hiyo kuwa mwangalifu unaweza kudanyanya na lolote lile. Hivi kweli kuna wajinga duniani hapa? Ebu basi dada Esther amalizie na wimbo huu Mambo yanabadilika:-)

JUMAPILI NJEMA UNGANA NA MARAFIKI AU NDUGU KWA SIKU HII NI VIZURI KUWA PAMOJA!!!