Showing posts with label ujumbe. Show all posts
Showing posts with label ujumbe. Show all posts

Monday, May 20, 2019

HUU NI UJUMBE WA JUMATATU YA LEO.......

Wakati mwingine unaweza kupata msaada kwa mtu ambaye hukuwahi ku/mtegemea au ulimdharau, hivyo ni kheri kuishi vizuri na kila mtu kwa kuwa hujui kesho yako.....

Wednesday, February 13, 2019

UJUMBE WA LEO- TOFAUTI BAINA YA SHULE NA MAISHA.....

Shuleni unajifunza somo/masomo na baadaye unapata mtihani. LAKINI- Katika maisha , kuna mitihani ambayo tunajifunza masomo.
PANAPO MAJALIWA , Kapulya wenu!

Sunday, April 15, 2018

UJUMBE WA JUMAPILI YA LEO..MSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KILA JAMBO

Usiwe na hofu kwa kuwa binadamu kukuacha katika udhaifu ulio nao kwa sababu yeye sio Mungu, na pesa sio kila kitu katika maisha, maisha hayajakamilika kwa mtu yeyote.

Kuna  mwenye nyumba lakini hana gari, kuna mwenye gari na hana watoto, kuna mwenye pesa hana afya, na kuna mwenye vyote lakini hana AMANI wala FURAHA. MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO

Sunday, March 11, 2018

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMAPILI NJEMA SANA

UJUMBE WA LEO:- Katika maisha ni muhimu kuuliza pale unapokuwa na dukuduku  Udadisi  una maana yake.

Monday, October 30, 2017

TUANZE JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU NA UJUMBE HUU....PUNGUZA MZIGO, PUNGUZA MARAFIKI WANAFIKI,PUNGUZA KABISA TENA WAPUNGUZE SANA TU, WAPUNGUZE ILI UWE MWEPESI



*Punguza marafiki ambao ukiwaambia unataka kufanya kitu wanakujibu "utawezaaa?" Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao kutwa wanataka mchafue meza bar. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao umeongea nao kitu mkiwa wawili mwisho wa siku unakikuta kimeenea sehemu nyingine. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao wako sahihi kila siku wenyewe hawataki kuambiwa wamekosea. Punguzaaaa!* 

*Punguza marafiki ambao wakija kwako wao urafiki unahamia kwa mumeo au mkeo aliyekaa sebuleni wakati wewe kakuacha nje. Punguzaaaa!* 

*Punguza marafiki ambao wanakuwa na urafiki na maadui zako kwa ukaribu zaidi. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki wa kwenye raha tu ukiwa na shida unajikuta peke yako. Punguzaaaa!* 

*Punguza marafiki wanaokusifu huku wakijua umekosea. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao kila ukiwapigia simu na wao utawasikia yaani nilitaka kukupigia sasa hivi. Punguzaaaa!*

*PUNGUZA MIZIGO ISIYOKUWA NA UMUHIMU*
JUMATATU NJEMA  MAANA WIKI IJAYO ITAKUWA JUMATATU YA MWEZI MPYA WA KUMI NA MOJA:-)

Saturday, September 2, 2017

UJUMBE WA LEO:- KILA AITAZAMAYE KESHO YAMPASA KWANZA AIMALIZE LEO:- ACHA NIKUDOKEZE JUU YA MAISHA YA LEO...

1.Ishi kwa UPENDO usio na Unafiki.
2.Ishi na FURAHA isiyo na mipaka.
3.Ishi kwa AMANI na kila Mtu.  
4.Usiweke MAMBO yako wazi kwa kila mtu kwani binadam hatufanani.
5.Jiheshimu kwani HESHIMA yako inatokana na jinsi ulivyo.
6.Kuwa MVUMILIVU katika kila jambo ili kufikia mafanikio.
7.Weka MSAMAHA mbele kwa kila anaekukosea na unaemkosea.
8.MISUKOSUKO ni sehemu ya maisha na ndio hatua ya kuvuka ili kufanikiwa katika MAISHA hivyo usikate tamaa.
9.Omba na kumshkuru MWENYEZI MUNGU kwa kila jambo kwani yeye ndiye anayekupa UHAI.
TUMALIZIE NA WIMBO HUU ....

Sunday, July 9, 2017

UJUMBE WA JUMAPILI YA LEO...KUTOKA KWA BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO

Sisi binadamu daima tunafanya kazi kwa kutumaini siku ya kesho itakuwa  bora lakini wakati kesho inafika badala ya kufurahi, basi sisi tuanaanza kunafikiria kesho tena itakuwa bora?  Hebu tuwe na siku ya leo sio kila wakati kufikiria ubora  wa kesho. MAISHA NI MAFUPI UPATAPO WASAA FURAHIA....JUMAPILI NJEMA

Tuesday, February 21, 2017

UJUMBE KUTOKA KWANGU KUJA KWENU

Kabla hujadhani, jifunze ukweli kwanza. 
Kabla hujahukumu , elewa kwanza ni kwanini.
Kabla hujamuumiza mtu, hisi kwanza. Na 
Kabla hujazungumza/sema, fikiri kwanza
NAWATAKIENI WOTE SIKU NJEMA NA KILA MUFANYALO LIWE JEMA!

Friday, December 30, 2016

HII IWE PICHA YA MWISHO YA WIKI HII NA LABDA MWAKA HUU 2016

Mara nyingi inasemekana ni wanawake tu huweza kufanya vitu zaidi ya viwili lakini hapa katika picha twaona kinyume....
UJUMBE WA LEO:- Nachukua fursa hii kuwashukuruni wasomaji wote wa MAISHA NA MAFANIKIO kwa kuungana nami kila siku. Maana bila ninyi nisingeweza kuendelea kublog maana hizi zote ni juhudi zenu. AHSANTENI SANA NA TUZIDI KUPEANA MOYO. KAPULYA

Monday, September 12, 2016

JUMATATU YA LEO TUANZENA UJUMBE HUU...KAMWE USISAHAU HIZO AINA TATU (3) ZA WATU MAISHANI MWAKO

1. Mtu ambaye ame/alikusaidia katika /ulipokuwa na wakati mgumu.

2. Mtu aliyekuacha ukiwa na wakati mgumu.

3. Mtu aliyekuweka katika wakati mgumu.
DAIMA  PAMOJA ....KAPULYA WENU!!



Friday, August 26, 2016

TUMALIZA IJUMAA HII YA MWISHO WA MWEZI HUU NA MWISHO WA WIKI NA PICHA HII...HUYU KAANZA MAPEMA MNO...

Napenda kuwatakieni mwisho mwema wa juma pia Ijumaa hii ya mwisho wa mwezi huu wa nane. Huyo Ntoto kaanza mapema mno  jamani. Kaaazi kwelikweli....IJUMAA NJEMA. ujumbe wa leo:- Hatuvichukulie vitu kama vilivyo, isipikuwa kwa vile tulivyo.

Saturday, February 13, 2016

NAWATAKIENI JUMAMOSI NJEMA IKIFUATANA NA UJUMBE HUU...!

Muwe na JUMAMOSI njema sana na upatapo wasaa mkumbuke ambaye hujamkumbuka kwa muda. Ukizingatia kesho ni SIKU YA WAPENDANAO.  JUMAMOSI NJEMA NDUGU ZANGUNI...KAPULYA WENU!

Saturday, November 21, 2015

UJUMBE WA LEO TOKA KWA KAPULYA WENU......

Napenda kwatakieni wote Jumamosi njema. Panapo majaliwa tutaonana katika pitapia zetu au sivyo wandugu-:).

Saturday, August 8, 2015

UJUMBE WA LEO

Ilikuwa ni majira ya saa mbili na nusu asubuhi ambapo mzee mmoja mwenye umri wa miaka zaidi ya 60 aliingia katika
hospitali moja ili kusafisha kidonda chake cha mguuni.
Mzee akaanza kwa kuomba afanyiwe haraka kwa kuwa alikuwa na appointiment
ya muhimu sana ifikapo saa tatu kamili ya asubuhi hivyo afanyiwe msaada wa
huduma ya haraka.
Daktari mmoja akaguswa na mzee yule baada ya kuona kila mara akiingalia saa yake na kutikisa kichwa cha kukatishwa tamaa na kuamua kumhudumia kwani alijua ingechukua zaidi ya saa kabla ya
mzee kuhudumiwa kutokana na idadi
kubwa ya watu kwa kuwa yeye hakuwa na
mgonjwa wa kumhudumia wakati huo.
Baada ya uchunguzi wa kidonda chake
kikaonyesha kuwa kimepona na daktari
akaanza kukifungua akishirikiana na nesi
kukisafisha. Wakiwa wanaendelea kukisafisha
kidonda daktari na mzee wakaanza mazungumzo na daktari akamuuliza kama mzee alikuwa na apolintiment na daktari mwingine kwa jinsi alivyokuwa na haraka.
Mzee akajibu hapana, ila natakiwa kuwahi kwenda kunywa chai na mke wangu
ambaye amelazwa kwenye kituo cha kuhudumia wagonjwa wenye matatizo ya ubongo .
Mzee akaendelea kumwambia daktari
kuwa mkewe amelazwa pale kwa zaidi ya
miaka miwili akitibiwa maradhi hayo na hana kumbukumbu kabisa
 Daktari akauliza sasa kama kapoteza kumbukumbu atakumbuka kama umechelewa?

Mzee akamjibu daktari kuwa mke wangu hajawahi kukumbuka kuwa mimi ni nani au nini kinaendelea kwa zaidi ya miaka hiyo miwili.
Kwa mshangao daktari akamuuliza, "Na umekuwa ukiendelea kwenda kunywa
naye chai kwa miaka yote hiyo kila siku asubuhi hata kama amekusahau wewe ni
nani?"
Mzee alitabasamu na kuushika mkono wa
daktari na kumwambia "hanifahamu tena
mimi, ila mimi bado namfahamu ni nani
kwangu na umuhimu wake kwangu"
Daktari alifuta machozi huku akimtazama
mzee yule akiondoka kulekea kwa mkewe
kunywa chai kabla ya saa tatu kamili.
Daktari alijishika mikono yake kichwani na kusema, "Hii ndio aina ya mapenzi
ninayoyataka katika maisha yangu"
Upendo wa kweli hauko kwenye mwonekano wa mtu au mapenzi. Mapenzi
ya kweli ni kukubaliana na hali zote zilizopo, zitakazotokea na ambazo
hazitatokea pia.
Kama umeguswa na kisa hiki tafadhali
CHANZO:- NIMETUMIWA NA RAFIKI

Thursday, August 6, 2015

UJUMBE WA JIONI YA LEO TOKA KWANGU KUJA KWENU

Maisha  ni mtihani Mkubwa na tofauti. Watu wengi huwa wanafeli kwa sababu wanajaribu kuiga maisha ya wengine, bila kujua ya kwamba kila mmoja ana swali lake tofauti.

Thursday, June 18, 2015

Saturday, June 6, 2015

UJUMBE WA LEO KUTOKA KWA KAPULYA WENU!!

Usiumizwe na mtu ambaye haumizwi kwa ajili yako. Tambua maisha ni mafupi kama umeme. Kuwa na furaha na acha kuwa mnyonge.
JUMAMOSI NJEMA.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA!!!

Wednesday, April 22, 2015

UJUMBE!

KAZI YA MOYO NI KUSUKUMA DAMU, KUPENDA NI KIHEREHERE CHAKO!  HIVI NI KWELI JAMANI??...Kapulya wenu.

Friday, April 17, 2015

UJUMBE WA WIKI HII KUTOKA KWA KAPULYA

Huu ujumbe nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio:-
CHOCHOTE UTAKACHOWEKA KWENYE AKILI YAKO KITATOKEA, UKIWEKA KUCHINDWA UTASHINDWA, UKIWEKA UOGA NDIO UTAKAOTOKEA CHAGUA UNACHOWEKA KWENYE AKILI YAKO. IJUMAA IWE NJEMA KWA WOTE MPITAO HAPA......Kapulya.

Monday, March 30, 2015

TUANZE JUMATATU HIII/WIKI HII NA UJUMBE HUU!!

"Mafanikio makubwa katika maisha sio kutoa anguka bali ni kuinika kila unapoanguka"
- Nelson Mandela