Saturday, September 2, 2017

UJUMBE WA LEO:- KILA AITAZAMAYE KESHO YAMPASA KWANZA AIMALIZE LEO:- ACHA NIKUDOKEZE JUU YA MAISHA YA LEO...

1.Ishi kwa UPENDO usio na Unafiki.
2.Ishi na FURAHA isiyo na mipaka.
3.Ishi kwa AMANI na kila Mtu.  
4.Usiweke MAMBO yako wazi kwa kila mtu kwani binadam hatufanani.
5.Jiheshimu kwani HESHIMA yako inatokana na jinsi ulivyo.
6.Kuwa MVUMILIVU katika kila jambo ili kufikia mafanikio.
7.Weka MSAMAHA mbele kwa kila anaekukosea na unaemkosea.
8.MISUKOSUKO ni sehemu ya maisha na ndio hatua ya kuvuka ili kufanikiwa katika MAISHA hivyo usikate tamaa.
9.Omba na kumshkuru MWENYEZI MUNGU kwa kila jambo kwani yeye ndiye anayekupa UHAI.
TUMALIZIE NA WIMBO HUU ....

2 comments:

Prince emac said...

Akhsante, saana mpendwa umenifungua moyo
Nafurahi kusoma post zako

Yasinta Ngonyani said...

Prince ahsante kuto kata mguu wako hapa kibarazani kwangu pia kuacha lako la moyoni.