Leo nimekumbuka kitu ni kwamba babu yangu alipenda sana kuniita mchumba Wake na pia bibi yangu alikuwa akiwaita kaka zangu wachumba zake. Nilikuwa nikijiuliza sana inakuwaje hii? Nilipata maelezo kiasi na nikaridhika ingawa ilinipa sana utata. Haikuishia hapo kulikuwa na dereva mmoja ambaye alikuwa rafiki wa familia naye alipenda sana kuniita mchumba hapo ndio nikabaki nimechanganyikia kabisa, nadhani nilichanganyikiwa kama MADENGE...hebu msome yeye alivyowaza kuhusu bibi yake..... Si mnakumbuka hadithi ya Madenge darasa la .....
Je? hapa ni utata wa lugha au ndiyo mila na desturi zetu? WOTE MNAPENDWA NA TUPO PAMOJA!!
