Wednesday, December 31, 2008

NIMEFIKA SALAMA

Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kunilinda mimi na familia yangu katika safari hii ndefu. Tumefika salama mpaka hapa Dar, safari bado inaendelea. Yaani mpaka Songea kama mnavyojua natoka Songea mngoni. Raha sana kuwa nyumbani joto, watu wachangamfu halafu nyumbani ni nyumbani. Leo sisemi kazi kweli kweli ila nasema raha kwelikweli.

Kwa hiyo napenda kuchukua nafasi hii kwa kuwatakieni wootee HERI SANA KWA MWAKA MPYA 2009. Ila mimi nafaidi zaidi kwa wale wote waliokuwa kwenye nchi za baridi. Ha, ha, haaaaa.

Monday, December 29, 2008

TANGAZO AU NISEME MSAADA WA GARI LA KUKODISHA TAFADHALINI JAMANI

Mwenzenu nimekwama nahitaji msaada wa gari kwa bei nafuu PLEASE nitumie mail kama unajua kuna mtu au wewe mwenyewe una gari ambalo mimi na familia yangu tunaweza kukodi Tafadhalini nisaidieni. Tunahitaji gari toka Dar kwenda songea na tutakaa Songea kwa muda wa miezi miwili na baada ya hapa kuliacha dar tena.

Saturday, December 27, 2008

BLOG MAISHA SAFARINI = YASINTA


Blog Maisha, nimeona ni vema niage sitakuwa hewani kwa muda kidogo NASAFIRI. Nakwenda Peramiho, nakwenda ungonini. Nakwenda kula likolo la nanyungu na malombi (mahindi ya kuchoma) Wangoni wote myumwike?
Walongo Vangu!!!!
Tutaonana karibuni tena. KWA HERINI KWA MUDA. NAWATAKIENI WOOOOTEEE MWAKA MPYA 2009.

Friday, December 26, 2008

SALA YA FAMILIA PAMOJA

Napenda kuwashukuru wana-blog wote kwa ushirikiano mzuri mlionao. Kwa hiyo leo nimeamua kuweka sala hii kwani pia kumshukuru mungu kwa yote nawaombeni kila mmoja kwa nafasi yake na wakati wake aiombee familia yake kabla mwaka huu 2008 haujaisha kwa sala hii asanteani sana:

Milango imefungwa, Ee Bwana.
Yule mtoto mchanga amelala.
Tunajisikia salama., tuna raha ya ndani, kwani tumeshiba.
Chakula kilikuwa kizuri, kinatuletea faraja.

Huu ndio wakati wa kukugeukia.
Mwisho mwa siku hii ya leo, kama familia – familia yako,
Ambapo Kristu anaishi.

Kwa ajili yetu, kila mmoja wetu; Bwana tunakushukuru.
Kwa ajili ya siku hii ya leo, iliyojaa mambo mengi,
Mema na yasiyo mema sana, Kwa yote tunakushukuru.

Tunapoangalia nyuma, mara ngingine, ni rahisi kuona,
Kwamba ingeliwazekana kuwa vizuri zaidi.
Hapa na pale, tumeshindwa kukupendeza. Kwa neno la hasira,
Na lile ambalo hatukulitimiza.

Tunasikitika, Bwana tusamehe. Kwani tunahitaji upendo wako.
Tunakuhitaji wewe, ukae nasi usiku huu wa leo,
Ili kutulinda, kutubariki. Kwani wewe ndiwe kuta za kweli na paa za nyumba hii.

Utubariki tulalapo. Utujalie ndoto zetu ziwe za furaha.
Na utujalie tuamke kesho. Tukiwa na uzima mpya tele.
Nguvu mpya na starehe mpya, ili tuweze kuishi tena siku nyingine.

Thursday, December 25, 2008

WATU TUNATOKA MBALI +KUMBUKUMBU = MAISHA

Nimetoke kuipenda tu hii picha. Swali Je? kuna mtu anajua huyo mtoto ni nani?

PIA NAPENDA KUWATAKIENI WOTE (Chrismas) NOEL NJEMA.

Wednesday, December 24, 2008

MFANO WA WAWILI WALIOOANA: ”STEFANO NA MARGARET”

Soma hapa na utoe maoni yake;-

Margaret na Stefano walikuwa wameadhimisha harusi yao miezi miwili iliyopita. Ilikuwa sikukuu kubwa. Marafiki wote wa Margaret, wanaofanya kazi ya uganga, na wafanyakazi wa idara ya kilimo ammbako Stefano anafanya kazi, wote walikuwepo. Miezi miwili imepita tangu sikukuu ile. Tangu zamani Stefano na Margaret walikuwa wanafikiri kwamba wanafahamiana. Wakati wa miezi sita ya uchumba walikuwa wamewahi kuzungumza mara chache kwa dhat juu ya mambo fulani. Lakini mara chache tu. Sasa matatizo yalianza kutokea, kwa kweli matatizo mengi.

Siku moja, Margaret alimwuliza Stefano, Ni aina gani ya chakula unataka ninunue kwa majuma mawwili yajayo? Bila kujali Stefano alijinu; Nunua chochote kile upendacho. Margaret alimtazama na mara Stefano alikwisha toka nje. Siku iliyofuata alimwuuliza tena, Stefano, unaonaje ikiwa tutanunua cherehan, naweza kujishonea nguo zangu? Bila saburi Stefano alijibu, Unafikiri nitapata wapi fedha zote hizo? Hakuwahi kuchukua muda kidogo na kukaa na Margaret ili waone pamoja kama kwa miezi ijayo wangeweza kufanya mpango wa kuweka akiba ya kiasi fulani cha fedha na baada ya muda Margaret angeweza kujipatia cherehani.

Mwezi mmoja ulipita. Usiku mmoja Stefano aliporudi nyumbani alisema, wiki ijayo nitakuwa safarini. Unatambua jinsi anavyomjulisha Margaret juu ya uamuzi wake. Hakuongea juu ya msafara wake wala hakumshirikisha kwa nini alitaka kwenda.

Unafikiri Margaret alikuwa anawaza nini kichwani mwake? Usiku huo alikwenda kitandani na kuanza kufikiri. Stefano hanipendi wala hanijali. Nikimwuuliza juu ya kitu fulani haonyeshi kuwa kinamhusu hata kidogo. Nikisema nahitaji kitu fulani ananiambia hatuna fedha. Lakini sasa yeye atafanya safari na hiyo safari inahitaji fedha aliendelea kuwaza je kwanini anasafiri? Atakwenda na nani? Kwa muda gani atakuwa safarin? Ananiache peke yangu bila kujali jinsi ninavyojisikia. Sawa, nami nitafanya vivyo hivyo. Nitatunza mshahara wangu wa mwezi huu ninaopata toka hospitalini na nitakwenda nyumbani kwangu. Nitakaa huko kwa muda wote nitaopenda:- Swali:- je? Hapa kunakosekana nini?

Tuesday, December 23, 2008

KARIBUNI TULE NA TUNYWE


Matunda ni muhimu sana. vinywaji pia, ila hapa mwenzenu naumia kweli yaani haya matunda mmh basi tu.

SALAMU ZA MWAKA ZA MWISHO


Hii nimetumiwa, nimeona tuwa pamoja katika salamu hizi za mwisho wa mwaka. Asante sana kwa salam hizi:


Ni wakati mwingine wa mwisho wa mwaka.
Ni wakati wa kupumzika na kutafakari ya mwaka 2008.
Kabla ya Mwaka Mpya, tunalazimika kusherekea
kuzaliwa kwa mkombozi wetu Bwana Yesu Kristo.
Kwa mantiki hiyo basi, mimi na famili yangu
tunakutakieni Heri ya Noël na
Furaha ya Mwaka Mpya 2009!
Tunakutakieni kila aina ya furaha na fanaka
kwa Mwaka Mpya 2009.
Tusisahau kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwani
kwa mapenzi yake tumeufikia msimu huu wa
sikukuu za mwisho wa mwaka.
Joyeux Noël et Bonne Année

Remigius & Regina Gama

Monday, December 22, 2008

MAISHA,MAISHA MAISHA, MAISHA


Kila mtu anahitaji maisha mazuri. Angalia hapa hawa watoto wanaonekana wana njaa na pia ukame wanahitaji msaada.

Sunday, December 21, 2008

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA

Mungu nakuomba unisaidie niwakumbuke wenye njaa ninapokuwa na chakula, wagonjwa nianpokuwa na afya nzuri, wote wanaoteseka kwa sababu ya vita ninapokuwa na amani, wasio na nyumba ninapokuwa nimelala na pia kuwa ndani ya nyumba yenye joto, pia nakuomba unisaidia niwakumbuke yatima kila ninapokuwa na wazazi wangu.

Na pia nakuomba:

Bikira Maria mama wa msaada na uibariki familia yangu, kaka zangu, dada zangu, wazazi wangu na watu wote dunia hii katika dhambi: AMINA

Saturday, December 20, 2008

INAENDELEA TOKA JINSI YA KUPEANA HABARI KATIKA MAISHA YA NDOA:- NI LINI TUPEANE HABARI?

Kuna mambo yawezayo kuongelewa kila wakati, kuna taarifa na habari tunazoweza kutaja wakati wowote. Kuna mambo mengine – yaliyo magumu zaidi kuongelea – nayo yanahitaji wakati wa pakee. Mume amwambiaye mkewe kuwa si mpishi hodari, hapo akijua kwamba mke wake amechoka sana siku hiyo, hatumii busara katika kupeana habari. Hali kadhalika, mwanamke atafutaye nauli ya kwenda nyumbani kwao akijua kwamba mumewe amekula hasara katika biashara yake juzijuzi tu, bibi huyu hatumii busara pia.

Kuna nyakati nzuri za kusema kitu na kuna nyakati mbaya za kufanya hivyo, yaani wakati unaofaa na usiofaa kusema jambo fulani. Mara nyingi mazoea ya maisha ndiyo yanayotufundisha. Maisha ni mwalimu wa waalimu. Mambo ambayo ni magumu kuyasema, kwa sababu yaweza kumshangaza ama kumwumiza mtu, yasemwe wakati ambapo yule mtu yuko katika hali ya kuweza kuyapokea. Jaribu kupata mzuri zaidi wenye hali ya utulivu mwingi ndipo mzungumze naye pamoja juu ya matatizo yaliyopo. Kwa mfano, wakati ambapo yupo tayari kukusikiliza, akiwa hana wasiwasi juu ya mambo mengine, wakati ambapo anajisikia vizuri

Kuna njia moja ya kufanikiwa katika kupeana habari, njia ya kufaulu kujenga uhusianao wa mapendo, nayo ni kusikiliza kwa upendo na kusema kwa upendo. Maana yake, kuwa na usikivu na pia kumjali mwenzangu. Ninamsikiliza si kwa masikio tu bali hata kwa moyo, tujitahidi kukisia maana iliyofichika ndani ya maneno anayosema.

Kuna wimbo unaojulikana sana usemao, “Watu wanaosikiliza bila kusikia, watu wanaoongea bila kusema kitu....” Mara nyingi tunakuwa hivi, watu wenye kusikiliza bila kusikia na kuongea bila kusema kitu. Maana yake ni kwamba tunasikiliza maneno lakini hatusikilizi kwa makini ya kutosha ili maneno hayo ytoe maana halisi kwetu.
Na mara nyingi tunaongea tu bila ya kufikiri tunalosema na bila kumfikiria huyu ambaye tunasema naye. Tumezoea kuongea lakini hatukuzoea kupeana habari itakiwavyo. Kuna tofauti kubwa hapa.

Mara nyingi pia hatujui jinsi ya kusikiliza. Ni ya maana sana kwangu ikiwa naongea na mtu mwingine, kujua kwamba ananisikiliza kwa uangalifu kweli au nusunusu tu. Nusu ya mafanikio katika kupeana habari kwa namna bora yatokana na kusikiliza vizuri. Ninaweza kushirikiana kimawzao kweli kama ninaweza kujiingiza mwenyewe akilini na moyoni mwa mtu, kama ningelikuwa moyoni mwake kabisa na kuona mambo jinsi ayaonavyo yeye.

Kupeana habari ni kitu kisichokoma, lazima kiendelee. Huwezi kamwe kusema, “Najua mambo yote juu yake.” Au, “Namjua kabisa kwani si tulifunga ndoa miaka 10 iliyopita.” Hapana. Siku kwa siku mabadiliko hutokea kwako na kadhalika kwa mwenzako hubadilika pia. Hili ni mojawapo la mambo ya ajabu sana katika ndoa yako, kwamba kila mara yapo mambo mapya ya kuvumbuliwa, mambo ya kuongea pamoja.

Kupeana habari kusipofanyika siku kwa siku utashangaa siku moja na kushtuka kuona kuwa mwezi wako ni mgeni kabisa na mgeni huyu si mwingine bali ni mume wako au mke wako. Kwa sababu tu, wakati fulani mliacha kupeana habari, mliacha kuongea pamoja juu ya namna mnavyofikiri, jinsi mnavyojisikia, mambo mnayotumaini.

Ni jambo la kusikitisha kweli kuona kwamba wapo watu wengi wa ndoa wanaishi pamoja, hula,hufanya kazi na kulala pamoja lakini kwa kweli hawaongei pamoja. Wanaongea, ndiyo, lakini siyo juu ya mambo yanayowapenya mioyoni mwao. Hawathubutu kungea waziwazi juu ya mambo yanayowafanya wasisikie wenye upweke, kutoeleweka na wenye huzuni. Na maisha yao ya ndoa hayana maana tena. Hatuwezi kupeana habari baada ya mwezi au juma. Kupeana habari ni chakula cha kila siku cha ndoa yako.

Thursday, December 18, 2008

JE? BINADAMU NA NYANI NI JAMII MOJA?

.............................Mrs. Ngonyani................Mr. Nyani

Aina hii ya nyani ipo zaidi katika nchi ya Gaboni tu. Angalia jinsi alivyo ni maalumu kidogo.Wanaitwa Mandrill.

JINSI YA KUPEANA HABARI KATIKA MAISHA YA NDOA

Leo nimeona kichwa kinataka kuongelea mambo mengine na pia vidole vyangu vilikuwa vinawasha sana yaani kutaka kuandika kidogo:- Hivi nimeona tuangalie kidogo jinsi ya kupeana habari katika maisha ya ndoa:-


Je?, umewahi kuamka usingizini asubuhi moja, na kubaki umejinyosha kitandani, ukisikiliza sauti mbalimbali kutoka nje? Huenda bila shaka ulisikia ndege wakiimba. Ikiwa ulisikiliza kwa makini, huenda ulingámua kuwa kila ndege anao mlio wake ambao huitikiwa na ndege mwi ngine wa aina hiyo kwa namna ya pekee. Ikiwa unaishi mjini, bila shaka unapoamka uachukizw na makelele ya magari na makelele mengine mitaani ambapo shughuli nyingi hutendeka. Lakini uendepo shambani au kijijini waweza kusikia tena sauti zote za machweo. Hali kadhalika wawez kusikia wadudu wakiitana katika hali tulivu ya jioni. Kwa hiyo tujue hata ulimwengu wa wanyama kuna kupeana habari.

Kati ya binadamu, kupeana habari ni jambo kubwa na muhimu zaidi. Ni kitu tunachokihitaji mno. Kwa mfano watoto wanaosoma mbali na kwao hufanyaje? Hukumbuka nyumbani kwa wazazi wao na hupenda kupata habari kutoka nyumbani. Hivyo huandika barua, kwani barua ndiyo njia ya kupeana habari ni nusu ya kuonana.

Je? Wewe huwa unafanyaje upatapo habari njema? Huwezi kunyamaza. Mara unatamani kumwambia mtu fulani ili mfurahi pamoja, unataka kumshirikisha furaha uliyopata.

Katika mada iliyopita kuhusu mapendo nilisema kwamba mapendo hukua na kuendelea. Njia ya kwanza ya kukua kwa mapendo, namna ya kwanza ya kusitawisha upendo ndiyo kupeana habari. Upendo unahitaji kule kupeana habari, na bila kufanya hivi, unakufa. Upendo ukiacha kuongea, basi hauwezi tena kutiririka, hufa.

Tukiangalia neno lenyewe lilivyo katika lugha mbalimbali, twaweza kuelewa kidogo maana yake. Katika nyingi neno la “kupeana habari” ama kuongea pamoja, ama kushirikiana kimawazo, linatafsiriwa ka kusema. KUFANYA UMOJA NA MTU.

Kufanya umoja na mtu


Kupeana habari na mwingine hufanya mtu kuwa na umoja na mtu yule. Kupeana habari ni tofauti na taarifa. Taarifa ni kujulisha kitu au kutoa ujumbe. Kupeana habari kuna mikondo miwili:- kutoa na kupokea mara. Katika kpeana habari uhusiano huzaliwa kati ya watu wawili, kifungo hutengenezw. Kifungo kile kinazidi kuimarika kwa njia ya kuendelea kupeana habari. Kwani ndiyo maana halisi ya kupeana habari. Natoa kitu fulani, napokea kitu kingine. Na ndio msingi wa mapendo.

Kupeana habari ni muhimu sana hivyo hata twaweza kusema kuwa kunalingana na umuhimu wa damu katika mwili. Sote twajua jinsi damu ilivyo ya lazima kwa uhai wa mwili wetu. Kama damu itapata ugonjwa au kudhoofika ni nafsi yetu yote inapata taabu. Vivyo hivyo kama hakuna kupeana habari, hakuna uhusiano na ushirikiano, basi upendo kati ya watu wawili huzidi kuzorota na kudhoofika.

Itaendelea.....!!!

Wednesday, December 17, 2008

MAISHA YA ENZI ZA KIKOLONI (UTUMWA)

Wazungu walitutesa sana. Huyo kijana alichukuliwa toka Afrika na kupelekwa Marekani kuwa mtumwa. Je? hii ni haki kweli?

Tuesday, December 16, 2008

KAPULYA MDADISI+(YASINTA MDADISI) =MAISHA

Mwenzenu nimekuwa nimeitafuta hadithi hii muda mrefu sana kwani nakumbuka niliisoma shule ya msingi . Sababu kubwa ya kuitafuta ni kwamba watu wengi wamekuwa wakinipachika majini kutokana na udadisi wangu , wengine wananiita mdadisi, maswali magumu, dada mwenye nguvu, na wengine Kapulya ndio maana naiandika leo. Nadhani wengi tunaikumbuka sana hadithi hii:-

Mzee Mwembe alikuwa mwenye nguvu nyingi na hodari sana wa kufanya kazi za mikono. Aliishi katika kijiji cha mdulo, Wilaya ya Rungwe.

Siku moja baada ya shughuli nyingi za mchana kutwa, Mzee Mwembe alijipumzisha kivulini huku akibugia bwimbwi la mahindi. Karibu naye alikuwepo Kapulya, mtoto wake wa kiume wa kwanza. Kapulya alikuwa mdadisi sana alipenda sana kuuliza maswali. Baba yake alimpenda kwa kuwa maswali yake yalikuwa na busara. Alipomwona baba yake awtulia, kamwuliza, “Baba, babu zetu waliwezaje kuishi na kupata chakula chao bila majembe, mikuki, mapanga na miundu?” Tatizo hili lilikuwa likimsumbua sana kichwani mwake kwa sababu alikwisha sikia kwamba vifaa hivi havikuwepo siku za kale. Mzee Mwembe akachukua bilauri ya maji akayanywa na huku akimsikiliza sana mwanawe. Baada ya kukohoa mara mbili hivi akamweleza, akisema, “siku hizi tunasikia katika mikutano ya siasa maneno mengi sana. Kwa mfano, mawazo ya kujitegemea yanatufundisha tusiwe wanyonyaji au makupe. Katika kujitegemea yatupasa kufikiri na kuvumbua vitu vyetu wenyewe ili kuyafanya maisha yetu yawe rahisi. Hivi ndivyo wazee wetu wa zamani walivyoishi. Pengine utasema kuwa maisha yao yalikuwa magumu lakini wao waliyafurahia. Kila kitu walikipata kwa kukifanyia kazi. Mtu goigoi na mnyonge aliishi kwa taabu na dhiki. Hii yote ilisababishwa na uhaba wa vifaa bora vya kufanyia kazi. Hapakuwepo na majembe, miundu, wala mikuki iliyotengenezwa kwa chuma kama ilivyo sasa. Hata hivyo kila mtu mwanaume aliweza kujitegemea kwa kutumia vifaa vyake vya kumsaidia kuendeshea maisha yake. Ilibidi kutengeneza vifaa hivi kwa kutumia miti. Miti yenyewe ilikuwa ni ile iliyochaguliwa maalum kwa kazi hii. Miti iliyokuwa inafaa ilikuwa ni ile iliyoweza kudumu muda mrefu bila kuharibika.

Matumizi ya vifaa hivi yalikuwa ya aina nyingi. Watu walitumia mikuki kwa kuwindia na kama kinga yao wakati wa safari. Majembe yalitumika kwa kazi ya kulimia na mashoka yalitumika kwa kupasulia kuni”

Kapulya alivutwa sana na maelezo hayo. Akabaki akimsikilza baba yake kwa makini sana. Mzee Mwembe hakukomea hapo, bali aliendelea kusimulia kwamba watu wa zamani walikuwa na tabia nzuri sana. Baadhi ya vitu vingi walivyogundua walivitoa vitumike kwa faida ya wote. Kwa njia hii maarifa ya uvumbuzi yaliendelezwa vizazi hadi vizazi. Kwa kutumia maarifa ya vizazi vilivyotangulia nasi pia tunaweza kuvumbua vitu vipya. Hivyo maisha ya binadamu huendelea kuwa bora na yenye manufaa.

Kapulya alipenda kujua pia jinsi watu wa kale walivyopata moto kwa kupikia vyakula vyao. Alikwisha sikia kuwa hawakuwa na mitambo ya kutengeneza vibiriti kama tuliyo nayo sasa. Hapo Mzee Mwembe hakutaka kmweleza kwa maneno tu. Akamwambia, “Chukua hicho kijiti kilicho hapo nyumba yako. Kichonge kidogo kwa kisu mpaka kipate uso uliosawazika.” Kapulya akafanya kama alivyoagizwa.

Kisha Mzee Mwembe aliendelea kusema. “Sasa tafuta kijiti kingine chenye unene wa kidole chako cha mkono. Halafu kikate kiwe na urefu wa kutosha. Baada ya Kapulya kukusanya vitu hivi Mzee Mwembe akamwelekeza atengeneze kijishimo karibu na ncha ya kile kijiti cha kwanza. Akafanya hivyo. Kisha baba yake akamwambia, “Sasa chukua kijiti chenye kishimo na kiweke juu ya majani makavu yaliyo laini.” Halafu baba yake alimwambia apekeche kile kijiti katika kile kishimo. Akafanya hivyo kwa nguvu sana. Basi akaona vumbi lenye moto sana likianguka juu ya yale majani makavu. Hapo aliona moshi ukitoka. Akazidi kupekecha kwa nguvu zaidi. Baba yake akamwambia, “Sasa chukua hayo majani yanayotoka moshi. Yapulize taratibu.” Akafanya hivyo na mara akaona moto ukiwaka Kapulya akawa amagundua njia ya kupatia moto. Uso wake uliwaka kwa furaha. Akaongeza majani. Halafu alichochea kuni ndogo ndogo na mwishowe akaongeza kuni kubwa. Akakata mahindi akayachoma.

Kwa njia hii ya kuuliza maswali na kwa tabia yake ya kujaribu kugundua vitu vipya Kapulya amejifunza mambo mbalimbali. Haoni haya kuuliza maswali kwa sababu anajua ya kuwa “kuuliza si ujinga.”

SWALI langu kwa ninyi mlionipachika hayo majina:- Je kweli nastahahili kuitwa hayo na kweli nipo sawa na Kapulya? Ni hilo tu.

Monday, December 15, 2008

HAPA NI JIMBONI MBINGA


Leo nitakuwa kimya nasubiri wenzangu mseme !!!

PADRE RAPHAEL M.K. NDUNGURU TULISOMA SHULE YA MSINGI LUNDO PAMOJA=KUMBUKUMBU


Dunia hii ni kubwa kwa kweli Padre Raphael Ndunguru tumesoma shule ya msingi pamoja. Ni muda mrefu sana sijamwona kwa hiyo nimefurahi sana kuoma picha yake na kujua amekuwa padrea. Nami nasema Imani, Matumaini na Mapendo.

Saturday, December 13, 2008

FARAJA YA MALAIKA(MAISHA)

Wakati unahitaji faraja ni ndipo uhakika wa maisha yako yanakuwa na muda,
Tafuta uhusianao kwa malaika wa faraja yako,
Mpe jibu hata kama mefumba macho.

Malaika mlinzi anakulinda,
Kila kitu kitaenda safi kwako.
Hakuna mwingine zaidi ya yeye,
Yupo kila mahali bila kusemas kwa heri.

Anatusikia wote na kutuona.
Unatakiwa kusema kwa sauti yako,
Usiwe na wasiwasi na ukawa mzigo kwako,
Uwe na imani kuwa kuna mtu atakufariji.

WIKI END NJEMA PIA JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!!

Thursday, December 11, 2008

VIAZI VITAMU (MBATATA) = UTAMU


Chips ya mihogo, chips ya viazi vitamu kwa kachumbali hicho ndio kilikuwa chakula changu. Yaani basi tu. Asante Fadhy Mtanga kwa kunikumbusha kuhusu vyakula hivi.:)

JINSI YA KUANDAA MIHOGO(KUMENYA)


Hapa nimekumbuka wakati nilikuwa mdogo hapo ni mama, mimi na kakangu kama sikosei. Ha ha ha ha. Halafu nimekumbuka sana wakati nasoma Songea pale Majengo chakula changu kilikuwa chips mihogo.Miaka ya 1990, kazi kwelikweli.

HIVI NDIYO MWISHO?

Leo nimeamua kuandika hivi kwani kila asubuhi nikiamka ni giza na niandapo kulala ni giza na hata nitembeapo ni giza:-

Pake yangu barabarani natembea,
Kuna mtu anakuja nyuma yangu,
Je? naweza kugeuka na kumwangalia nyuma?
Peke yangu katika njia hii na gizani
Peke yangu - hakuna aliye nami.

Kwa nini lazima nitembee peke yangu?
Wakati nataka tuwe wengi?
Nipo peke yangu gizani, bila penzi,
Na mtu wa kunituliza. Kwa nini?

Wednesday, December 10, 2008

BAISKELI+TENGA LA SAMAKI+KUUZA SAMAKI


Halafu pia inabidi niwahi sokoni kuuza samaki. Nimerudi jana tu kutoka Mbamba bay kununua
hawa samaki (mbelele) kwa hiyo hapo safari ya kwenda kuwauza.

MKOKOTENI+USAFIRI+UMOJA+MBOLEA =MAISHA

Ngoja tuache mambo ya kukaa chini na kusoma vitabu vya hadithi. Sasa ni wakati wa kilimo kwa, mbolea zinahitajika. Na huu ndio usafiri wetu hapa Ruhuwiko. Kuna majembe mengi tu kwa hiyo msiona aibu. KARIBUNI

Tuesday, December 9, 2008

MJI MKUU WA NCHI YETU

Kumbukumbu kutoka kitabu cha TUJIFUNZE LUGHA YETU! Kitabu cha darasa la nne. Wengi natumaini mnakumbuka, binafsi nimekumbuka na nimefurahi sana. Binafsi nimekumbuka na nimefurahi sana soma ufaidi au ukumbuke pia:-)


Kusala ni mtoto wa Songea. Anasoma shule ya Lilambo. Ana mjomba wake, anafanya kazi jiji la Dar es Salaam, ambao ni mji mkuu wa Tanzania. Ni karani wa bandari.

Wakati wa likizo, Kusala alikwenda Dar es Salaam kumsalimu mjomba wake. Alichukua sanduku lake la mbao na kifurushi cha chakula, akaenda mpaka mjini Songea. Kesho yake akaondoka kwa basi kwenda Dar es Salaam.

Basi hili lilipitia njia ya nNjombe. Jioni likafika Iringa. Hapa wakalala. Asubuhi yake wakaanza safari kwenda Morogoro kupitia Mikumi. Mikumi ni mbuga ya wanyama.

KUsala aliona wanyama wengi. Kutoka hapo walikwenda moja kwa moja mpaka Morogoro ambako walifika kama saa kumi jioni. Baada ya kupumzika kidogo waliondoka kuelekea Dar es Salaam.

Walipokaribia Dar es Salaam, Kusala aliona majengo makubwa upande wa kushoto. Alimwuuliza mwenzake aliyekuwa karibu naye, ”Yale ni majumba gani?” Mwenzake akamjibu, ”Yale ni majengo ya Chuo Kikuu. Ni mahali maarufu sana hapa nchini.” Kusala akauliza tena, ”Je? Wapo watoto ?” Akajibiwa, “La, wasommao pale si watoto. Ni watu wazima.” Akaendelea kuuliza, “Wanasomea mpaka madarasa gani?” Akajibiwa tena, “Hawana madarasa. Wanasomea shahada za elimu mbalimbali.”

Walipofika katikati ya mji, Kusala alishangaa sana kuona taa zenye rangi mbalimbali. Taa hizo zilitundikwa juu ya milingoti mirefu ya chuma. Aliona magari makubwa, mabasi mengi na motokaa ndogo nyingi. Alishangaa sana kuona magari mengi hivi. Wakati wote huu alikuwa na wasiwasi. Hakujua atakalofanya ikiwa hatamkuta mjomba wake kituoni. Basi lilipofika kituoni alifurahi sana kumwona mjomba wake amekuja kumpokea. Usiku ule Kusala alilala sana kwa ajili ya uchovu wa safari.

Asubuhi yake Jumapili, mjomba wake aliwachukua yeye na binamu yake, Njoli, akawatembeza mjini. Kwanza walitembelea kiwanje cha ndege. Kusala alishangaa kuona jinsi kiwanja kilivyo kikubwa. Aliona ndege kubwa zikitua, akauliza, “Mbona Songea hakuna ndege kubwa kama hizi?” Mjomba wake akamjibu, “Songea ni mji mdogo. Hauna kiwanja kikubwa cha kutua ndege kubwa kama hizi.”

Kutoka kiwanjani Kusala alipelekwa kutazama Jengo la Bunge. Mjomba wake alimweleza kuwa humo Wabunge hukutana na kupanga mipango ya Serikali na maendeleo ya nchi. Baada ya hapo walikwenda kwenye kivuko cha bahari kupitia Ikulu. Hapo Ikulu, Kusala aliona askari walinzi. Pia aliona mbuni, tausi na kudu. Kusala akauliza, “Askari hawa wanafanya nini?” Njoli akamjibu, “Wanalinda zamu. Hapa ndipo Ikulu.” Kusala akauliza tena, “Ikulu ni nini?” Mjomba wake akamwambia, “Ni makao rasmi ya Mtukufu Rais wetu.

Walipofika kwenye kivuko walikata tikiti wakaingia katika pantoni na kuvuka mpaka ngámbo. Huko walitembelea mtambo wa kusafisha mafuta. Mtambo huu husafisha na kutenganisha lami, dizeli, mafuta ya taa na petroli.

Waliporudi walikwenda bandarini. Mjomba wake akawaonyesha ghala kubwa na mshine za kuinulia mizigo. Pia waliona meli nyingi kubwa kwenye magudi. Zilikuwa zikipakua na kupakia bidhaa. Pia yalikuwapo madau pamoja na mitumbwa. Wavuvi hutumia madau na mitumbwa kuvulia samaki.

Kusaka vilevile alitembezwa kuona stesheni kubwa ya gari la moshi. Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuona gari la moshi. Alishtuka aliposikia makelele na kuona moshi mwingi. Watu wengi walikuwa wakingojea gari liondoke.

Siku nyingine Kusala alipelekwa kuona viwanda. Aliona watu wengi wakifanya kazi. Kusala na Njoli waliona viwanda vya kutengeneza nguo, mablanketi, sufuria na madebe. Walipofika Ubongo, alistaajabu kuona watu wengi wamesimama msululu nje ya kiwanda cha kutengeneza nguo. Kusala akauliza, “Hawa wanafanya nini?” Mjomba wake akamjibu, “Watu hawa wanatafuta kazi. Ni wageni mjini. Wameshindwa kukaa vijijini” Kusala alihuzunika sana, akamwambia mjomba wake, “mimi napendelea kuishi kijijini kwetu. Vijijini hakuna haja ya kusimama msululu kutafuta kazi. Maana kazi za shamba ni nyingi. Nitakapomaliza masomo yangu nitaanza kulima na kufuga kuku. Mimi sipendi kukaa mjini bila kazi.”

Kutoka Ubungo walipitia Kariokoo. Hili ni soko kubwa la Dar es Salaam. Vyakula na matunda mengi huuzwa hapo. Biashara nyingi huendeshwa katika maduka makubwa karibu na soko hilo. Kusala alisikia muziki wa redio ukiwastarehesha wauzaji na wanunuzi.

Kwa kweli, Kusala aliona mambo mengi mageni. Aliona watu wakikimbilia mabasi. Wengine wakienda mbio kwa miguu. Siku ya mwisho alitembelea kiwanda cha kutengeneza nyama za makopo. Alipoondoka alimshukuru sana mjomba na ndugu zake. Alipofika Songea aliwaandikia barua ya kuwashukuru na kusema kuwa alifurahi sana kuona jiji la Dar es Salaam.

NDOTO YA KUWA MTAWA/SISTA=MAISHA


Naona wengi mnataka kujua kwa nini sijakamilisha ndoto yangu ya kuwa mtawa/sista. Nitajaribu kuwaelezea:- Ni kwamba, nilikuwa na miaka 5-6. Nilikuwa nikiwaona masista nilikuwa naona kama wao ndio malaika nacheza nao. Nilikuwa nawaona wao ni watakatifu sana kwani muda wao wote waliutumia kusali tu. Ndio maana nikawa nawaza nami nitakapo kuwa mkubwa nitakuwa sista. Lakini sikumwambia mtu, Ni nini nakiwaza. Labda nilifanya kosa, kwani leo ningekuwa sista mwenzenu. Nikimtumikia mungu.
Habari ndio hii ndugu zanguni!!! Je? nimejieleza sawasawa?

Monday, December 8, 2008

MAPENDO NI KITU GANI?:-INAENDELEA

Mifano ya upendo wa kweli

Kuna mifano mingi ya upendo wa kweli katka maisha ya kila siku. Kuna upendo wa baba unaojihakikisha kwa kumpeleka mtoto wake mgonjwa hospitalini. Baba anapaswa kutembea porini maili kumi na tano bado baada ya safari ndefu, lakini baba anasukumwa na upendo, anapata nguvu na ananuia kufika hospitalini. Wala hawezi kusema, “Inatosha sifanya zaidi ya hapa.”

Kuna pia upendo wa mama ambaye kila siku huleta faraja, nguvu na kitulizo kwa watoto wake.

Upendo wataka kukua

Upendo ni kama uzima. Wote tunajua ya kwamba mungu ndiyo chanzo cha uzima wote. Uzima, unaishi, unakua na kubadilika. Hivi ndivyo upendo ulivyo. Ni lazima utiririke na kukua. Ni budi uenee, utafute maeneo na mahali papya pa kusitawisha na kutajirisha. Upendo upo kwenye matengenezo wakati wote. Tunajua upo, lakini kila mara unahitaji kufanywa upya na kukua. Kama sivyo upendo unakufa.

Ufanyacho upendo

Upendo kidogo ni kama jua, ambalo ni rafiki yetu wa daima. Hufukuza baridi, huimarisha mazao yetu na kuyaivisha. Hivyo ndiyo ufanyavyo upendo, kama jua. Katika kupendana, yule mwenye kupendwa hubadilika. Anabadilishwa kutoka hali ya mashaka, wasiwasi, hofu, upweke na kutoamini, anakuwa mtu mwingine kabisa. Mwanzoni alikuwa mwenye hofu na mashaka, sasa ni mwenye kujiamini na kuthubutu kutenda. Badala ya uchungu na upweke, imekuwa furaha na heri. Ni kama nyoka abadilishaye ngozi yake ya zamani kwa wakati fulani, na kubaki na ngozi mpya. Kwa upendo aliopata mtu huyu amafanywa kuwa mpya.

Mara nyingi twasikia watu wakisema, “Huyu mvulana anampendaje msichana huyu?” au , “nini cha kuvutia alichonacho Bwana huyu?” Haina maana kuuliza kwa nini twampenda mtu mwingine. Kama ni mapendo kweli,hatumpendi mtu kwa kuwa ana vitu fulani vya kuvutia wala hatumpendi ingawa ana kasoro, bali tunampenda mtu aliye ndani ya yote haya.

Upendo: fumbo la ajabu

Kama nilivyosema juu ya upendo kuwa ni kutoa nafsi yako. Hii bado haielezi kikamilifu maana ya upendo. Kwani upendo ni fumbo la ajabu. Ni fumbo kwa sababu maana yake ni nzito mno hata kika siku tunajifunza kitu zaidi juu yake.

Na kwa kweli, tunaweza kupata maana kamili ya upendo kutoka kwa Mungu peke yake ambaye Neno lake latuambia:-
Upendo huvumulia, hufadhili,
Upendo hauhususu,
Upendo hautabakari, haujivuni
Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake,
Hauoni uchungu, hauhesabu mabaya
Haufurahi udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli,
Upendo huvumulia yote, huamini yote, hutumaini yote na husatahimili yote.

KUASAIDIA KAZI ZA NYUMBANI

Hapa nimekumbuka nilipokuwa mdogo kutoka tu shuleni kwenda kuwafungulia mbuzi. je? kuna mtu ambaye hajafanya kazi hii.

NIMEANZA KUFUGA NG´OMBE


Naamini ufugani ni moja ya maisha yetu ya kila siku.

Sunday, December 7, 2008

SALA YA MUME AKIMWOMBEA MKEWE

Hapa nimejaribu kubadili maneno kutoka kwenye ila sala ya kumwombea mke au niseme ni kama mfano vipi mume anaweza kumwombea mke wake.


Ee Bwana, wakati mwingine namtazama mke wangu Nami nashangazwa.
Inakuwa kama ni kwa bahati tu nilikutana naye.Siku ile ya kwanza,
Tulikutana na kila mmoja alikuwa mgeni kwa mwenzake.Sasa ninamjua sana.
Lakini bado ninashangaa na kujiuliza.Bila yeye ningekuwa mtu wa namna gani?
Ningefanya nini?

Je? Ningekuwa nimefanya mambo mengi hivyo?
Je? Ningekuwa bado nikitafuta?
Nikitafuta anasa mbaya za maisha, nikiondoa upweke na uchungu,
Kwa chupa moja ya bia baridi au kwa kumtembelea rafiki.

Ninajua kwamba nimebadilika, yeye alinibadilisha.
Upendo wake, na upole wake, kunitunza kwake, na subira yake,
Vimenifundisha na kunijenga.Amenifundisha niwe zaidi,
Niwe zaidi mtu yule uliyetaka niwe.Amenisaidia niwe hivyo
Mlifanya kazi pamoja, ulifanya kazi ndani yake
Naye katika wewe

Ninyi -wawili- Bwana,
Mlinipa moyo, mlinipa nguvu,
Mlinipa amani ya kweli, raha na furaha.
Mlinisaidia, nikajiamini.

Na nikakuamini.
Kwani, Ee Yesu mpendwa, ulikuwa mgeni.
Picha kwenye kitabu, Mtu aliye angani mbali nami.
Mpaka nilipokutana naye.

Kwani alinionyesha nafsi yangu mwenyewe. Na alinionyesha wewe.
Alinipa watoto, watoto wako Ee Bwana. Sasa ni watoto wetu

Hali hii tuliyo nayo leo hii, ni dalili ya upendo wako,
Ninakushukuru kwa ajili yake,umbariki na unlinde.
Umweke salama, na unifundishe jinsi ya kumpenda zaidi.


NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAPILI NJEMA

Saturday, December 6, 2008

KUMBUKUMBU YA MAREHEMU BIBI YANGU

Leo nimemkumbuka sana mpendwa bibi yangu tangu anitoka imepita miaka mitatu. Bibi yangu ni huyo aliyejifunika kitenge, katikati nadhani mnajua au basi ni mimi na mwishoni ni mama yangu mdogo mdogo wa mama.

Friday, December 5, 2008

UNDUGU WA NAMNA TOFAUTI KWA MANUFAA YA JAMII

Nitajaribu kidogo kuelezea Ninakotoka mimi vipi tunaitana

Babu - Bibi

Upande wa mama
Mama
Mama mdogo, mdogo wa mama
Mama mkubwa, dada yake mama
Mjomba kaka ya mama

Upande wa baba
Baba
Baba mdogo, mdogo wake baba
Baba mkubwa, kaka yake baba
Shangazi, dada yake baba.

VIPI KUITANA
Watoto wa mama mkubwa na mdogo
Wa kike nitamwita dada au kama ni mdogo basi mdogo wangu
Wa kiume nitamwita kaka hata kama ni mdogo
Watoto wa mjomba ni binamu zangu

Watotot wa baba mkubwa na mdogo
Wa kiume nitamwita kaka naye ataniita dada
Wa kike nitamwita dada, naye ataniita mdogo wake inategemea nani mkubwa
Watoto wa Shangazi ni binamu zangu

Watoto wa kaka zangu wataniita mimi Shangazi na watoto wa wadogo zangu wa kike wataniita mimi mama mkubwa.
Watoto wa binamu wataniita mimi mama na kaka zangu baba.

Mama na baba yangu watawaita watoto wangu wajukuu na wao watawaita wazazi wangu babu na bibi.

Watoto wangu watawaita kaka zangu wajomba

Bibi ya mama/baba yangu mimi nitamwita mama na babu ya mama/baba nitamwita baba.

Naomba kama nimesahau kitu basi tusaidiane.

Sasa nina maswali:- Je? mke wa mjomba ni mjomba pia? na je? mume wa shangazi ni shangazi pia?

SHANGAZI ZANGU (WATOTO WA KAKA ZANGU)

Napenda kuwapa hongera shangazi zangu hawa watatu, kwa sababu huu ni mwezi wao wote watatu wanatimiza miaka mwezi huu wa kumi na mbili. HONGERENI SANA SHANGAZI ZANGU.

MAPENDO NI KITU GANI?

Tunaona hili neno "Mapendo" likiwa limeandikwa mahali pengi sana. Tunaliona katika magazeti kila siku. Tunaliona kwenye sinema, mara nyingi hata sisi tunalitumia, pengine hata bila kujua maana yake.
Kitu hiki kiitwacho "mapendo" ni nini hasa ? Ni neno dogo sana. Katika lugha yetu labda hakuna neno linalotumiwa na keleweka vibaya kama hili.

Tuangalia mfano huu:- Mvulana mdogo anamwambia mwalimu wake kwamba anapenda pipi. Msichana mdogo anasema kwamba anapenda mtoto wake wa bandia. Mtu mwingine anasema napenda viatu vyenye visigino virefu ambapo mwanamke "yule" naye anasema kuwa anapenda kutazama vitu vizuri kwenye madirisha ya maduka. Mwingine anapenda joto la kiangazi, mwingine mvua za masika. Je? wote hawa wana maana gani wasemapo kwamba wanapenda?

Kwa ujumla, twaweza kusema kuwa tunatumia neno "mapendo" juu juu tu na mara nyingi bila kuelewa maana kubwa ambayo neno hili dogo linalo. Mapendo ni mojawapo ya nguvu kubwa zilizomo ndani ya moyo wa mwanamume na mwanamke. Kupenda kwa nguvu zote za moyo wa mtu. Lakini kupenda kwa moyo wote ni kitu ambacho lazima tujifunze kidogo kidogo.

Hatua za kuelekeza kwenye upendo wa kweli
upendo, kidogo wafanana na ngazi:- una hatua mbalimbali.

Hatua ya kwanza ya upendo tunawea kusema ni kama ule wa mtoto mdogo. Upendo wa kutaka kupokea. Anakuwa na furaha kwa sababu amepewa kitu.

Hatua ya pili, upendo unaanza kuangalia kandokando; ni wakati ambapo mtoto huanza kutoa kwa wengine. Ndipo mtoto hugundua urafiki. Sasa mtoto anakuwa na furaha kwa sababu ametoa kwa mwingine kitu kilichokuwa chake mwenyewe na kumfurahisha mwingine. Mtoto amejifunza sasa sehemu muhimu sana ya upendo wa kweli.

Hatua ya tatu ni ile ambapo mtu anakuwa tayari kwa vyote viwili, yaani kutoa na kupokea. anakuwa tayari kutoa ili apate kumfurahisha mwingine; lakini pia anakuwa tayari kupokea kitu na ndiyo namna nyingine ya kumfurahisha mtu wakati mwingine. Sasa amekwisha gundua siri mojawapo kubwa ya maisha, siri iliyo katka kiini cha upendo wa kweli.

Kwa maneno rahisi tungesema kuwa, Kupenda ni kutoa. Lakini pia ni vigumu. Kupenda ni kutoa. katika kupenda ni lazima kutoa, kutoa kile kitu ambacho labda unakihitaji ama usingependa kukitoa. Upendo ulio mkubwa zaidi na wa ndani zaidi ndio ule wa kujitoa nafsi yako kwa ajili ya heri ya mtu mwingine.

Kutoa ndio kiini cha upendo. Ile hali ya kutaka kupokea tu kwa mwengine ni ubinafsi na upendo wa kibinafsi. Upendo hutazama kwa mwingine, kwa yule mpendwa, na kuuliza; Nitatoaje zaidi ili mwenzangu awe na furaha zaidi? Ambapo ubinafsi na kujipenda binafsi hujiuliza na kupanga namna ya kupata vitu. Nitafanyaje ili niweze kupata zaidi kutoka kwa mwenzangu? Mambo haya mawili , kama uyaonavyo ni tofauti sana.

Itaendelea...........

Wednesday, December 3, 2008

MAPACHA (DOTO NA KULWA)


Na baada ya kutembelea hapo Litembo nikamkuta huyu dada amepata watoto mapacha. Huku na huku. Maisha kazi.

HOSPITALI YA LITEMBO


Leo nimeamua kutembele hospitali ya Litembo Wilaya ya Mbinga pia Mkoa wa Ruvuma.Nimekumbuka kwani mwaka 1980 babu yangu aliuzwa hapa na mpaka Mu ngu alipopenda alimchukua.

KWA NINI WANAUME/AKINA BABA WENGI WANAFIKIRI WAO NDIO WAAMUZI/WAFALME WA NYUMBA?

Suala hili limekuwa likinikera sana akilini mwangu kwa miaka mingi. Ya kwamba akina baba/wanaume wao wanafikiri kazi yao kubwa katika nyumba ni kuwa MUME/BABA basi. Mara nyingi utasikia wanasema mimi ndio mkubwa wa nyumba. Na kama wanafanya kazi za ofisini basi ndo itakuwa kero mno. Kwani hapa atataka anaporudi toka kazini akute chakula mezani, maji ya kuoga bafuni tena ya moto, nguo zmepigwa pasi n.k. Na kinyume kama hana kazi basi atakuwa anashinda kilabuni(UGIMBI) na akirudi toka huko basi ni kelele tu, hakuna amani wala maelewano

Bado naendelea, kuna wengine wanaona kupika, kulea watoto, kutafuta chakula ni kazi ya wanawake. Yaani hawawezi hata kujipikia chai kwa vile wao ni wanaume au hata kumbadili mtoto nepi, Mtoto amabaye ni wake. Kikubwa wanachofanya ni kukaa kitini/sofani na kuletewa kile wanachotaka. Wanasahau kabisha jambo la USAWA.

Bado wanaishi dunia ya mababu, mababu na mababuzi. Tuache UBINAFSI tuishi kwa kushirikiana/kusaidiana kwani wote ni SAWA. Nasema tena tuishi kwa kusaidiana hapo wote tutafurahia maisha. Tuache mambo ya UTUMWA.

Tuesday, December 2, 2008

ANGALIA UZURI HADI MSITUNI


Nikiangalia mtu huu naona kama sahani kubwa ya kupakulia ugali. Yaani mpaka raha.

JE? HII NI HAKI KUCHOMA MOTO


Watu wengi wanachoma sana moto mashamba yao hawajui kama wanapoteza rutuba. pia wengine wanachoma moto misitu na pia wanasahau kupanda miti mipya.

NI VIZURI KUTUNZA MAZINGIRA YETU



Hapa sisemi sa na labda wenzangu.

Sunday, November 30, 2008

SALA YA MKE KUMWOMBEA MUMEWE

Napenda kufunga mwezi huu wa kumi na moja kwa sala hii;-

Ee Bwana , ni ajabu,
Jinsi fikra zangu zinavyomrudia kila mara
Huyu, mume wangu,
Mwenzi anayeshiriki maisha yangu kwa namna ya pekee.
Ninapofagia nyumba na mazingira yake,
Nataka kutengeneza nyumba nzuri kwa ajili yake.
Ninapopika chakula vizuri,
Napenda kumfurahisha.
Ninaponunua nguo mpya na kujaribu kuonekana mrembo,
Ni kwa ajili yake tena, Ee Bwana.

Na ninaweza kukuambia kwamba
Ninamwonea fahari,
Anafanya kazi kwa bidii ili kupata riziki yetu;
Ni mtu mwenye haki, mwadilifu,
Naye hujitahidi kutufurahisha.
Kwangu, yeye ni mpole na mwangalifu.
Hunijali na kuonyesha kweli kwamba anajali.
Hunifanya mimi nijiamini mwenyewe,
Anajua jinsi ya kuondoa hofu zangu,
Hunipatia usalama na upendo ambao nahitaji sana.

Ee Bwana, ninakuomba,
Umbariki na umlinde.
Katika safari zake, umfikishe salama.
Kazini mwake, umpe fanaka
N hapa, nyumbani petu naomba apate amani na heri.

Bwana, unisaidie mimi pia
Niweze kuwa yule mke anayehitaji.
Unifanye niwe mtu anayeweza kumwamini daima,
Mwanamke ambaye anaweza kumfurahia,
Niweze kumsaidia asahau matatizo yake,
Niweze kuondolea mbali hofu zake na kupunguza uchungu wake.

Bwana, Wewe ndiwe uliyenipa mume huyu,
Na katika yeye,
Umenipatia sehemu ya nafsi yako mwenyewe.
Ninakusifu kwa ajili yake, Ee Bwana.


Napenda kuwatakieni wote Jumapili Njema.

Friday, November 28, 2008

SALAMU KUTOKA SEMINARY YA PERAMIHO


Karibuni sana Peramiho kuna mengi ya kuangalia

HOSPITALI YA PERAMIHO


Ukipatwa na homa njoo hapa utapata matibabu mazuri tu. Pia nipo hapa uliza tu.

BOOKSHOP PERAMIHO


Ukifika Peramiho usikose kipitia hapa kujipatia vitabu na magazeti ya aina yote. Karibu sana (Kunyumba Kuperamiho) ugali na likolo la nanyungu sasa ndo msimu wake.

Wednesday, November 26, 2008

LEO TUANGALIE:- UGONJWA WA KIDOLE TUMBO/KIBOLE (APPENDIX) HUWAPATA ZAIDI VIJANA

Ugonjwa wa kidole tumbo inasemekana huwapata zaidi vijana kati ya miaka 10-25. Lakini pia wazee na vijana zaidi ya miaka 25 wanaweza kupata. Sio kawaida watoto chini ya miaka 2 kupatwa na ugonjwa huu.

Ulaya na Amerika magharibi kwa wastani moja ya kumo hupa ugonjwa huu. Lakini hapa Sweden idadi ya wapatao ugonjwa huu imepungua.

Katika uchunguzi/utafiti inaonyesha watoto ambao wanapata maziwa ya mama zaidi ya miezi saba wanaepuka kupata ugonjwa huu kuliko watoto wasionyonya maziwa ya mama.

Dalili zake:-

Ghafla,maumivu makali ya tumbo pembeni au juu ya kitovu, pia huahamia chini ya tumbo upande wa kulia na kuwa makali zaidi.


Wengine, baada ya muda hupata joto kali sana, hupoteza hamu ya chakula na hupata kichefuchefu. Wakati mwingine kutapika na kuhara pia.

kwa watoto wadogo na watu wazima dalili huwa vigumu kuonekana.

Tuesday, November 25, 2008

TUANGALIE VYOMBO VYA MICHEZO NA USAFIRI

MICHEZO YA PIKIPIKI

Michezo mingine ni kujitafutia kifo angalia hapa akianguka je?

GARI (SPORT CAR PORSCHE)


Sisemi sana ninyi mtasema

USAFIRI WA BAISKELI NI RAHISI ZAIDI

Karibuni wateja kukodisha baiskeli ni bei rahisi tu.

NI NINI KINAFANYA MAISHA YAWE NA FURAHA?

Hakuna kitu kitakacho weza kufanya maisha ya yako/yangu kuwa na furaha kama hatutakubali kujipokea mwenyewe na kupanga mfumo mzima wa maisha yetu. Wengi tunajikuta katika mahangaiko na mafarakano katika uhusiano iwe wa ndoa, au marafiki wa kawaida. Je? ume/tumesha wahi kukaa chini na kujadili kwa nini hili litokee, na je ni kweli kwamba katika haya yote hakuna jibu kwa matatizo haya.

Mpenzi msomaji katika kuchunguza hilo nimegundua kwamba tulio wengi hatuipi nafasi mioyo yetu kuchagua kile kilicho halali kwa matakwa yetu. Bali tunafuata mwelekeo wa mapendeleo yetu na tunaacha nafasi muhimu ya moyo kuupa nafasi ya kuchagua kilicho cha thamani zaidi ya furaha ya siku moja, ambao tuluo wengi tumekuwa tukililia au kuionea fahari. Hapa nina maana kwamba kama mwanamke ameahidiwa kuolewa basi atataka haja hiyo itekelezwe wakati hana uhakika wa kweli kama mpenzi wake anampenda kwa dhati.

Kuna misemo isemayo kwamba:- mwanamke anapotoa uamuzi wa kuolewa anafanya hivi akitegemea kwamba mwanamume anayeolewa naye atabadilika baada ya wao kuwa mke na mume; poleni sana wanawake tumepotea, dadili mwelekeo olewa na mtu mwenye mapenzi ya dhati na ambaye yupo tayari kutoa dhamiri yake kwa ajili yako.

Na kwa upande mwingine, Mwanamume anamwoa mwanamke na kumleta ndani ya nyumba akitegemea kuwa hatabadilika; Mungu ndiye ajuaye kuwa mwandamu ni kigeugeu, sasa atutendee nini ndipo tulidhike? Naamini wanawake wengi wanavumilia katika mahusiano ila wapo ambao nao ni wasumbufu, kwa sababu tu ya tamaa, na wengine hujikuta wanabadilika kwa kuwa maisha ni magumu ndani ya ndoa, na wengine umaskini, wanataka kupata chochote au kuiga ufahali wa wengine.

Swali linakuja je? unafikiri kukamatana ugoni na kuonyeshana kwenye vyombo vya habari kwamba nataka kumshikisha adabu ajifunze ni njia sahihi ya kutatua matatizo katika jamii kama watu hawata tumia njia ya kuiweka wazi mioyo yao kwa kile wanacho kipenda na kukitamani?

Ni changamoto kwamba kweli tulichokiamua pamoja na kukubaliana basi kiheshimiwe na kuthaminiwa kama kweli humpendi mwenzako sema tangu mwanzo liwe wazi tusitake maisha ya mtelemko kwa kuwa unayemwoa ana nafasi nzuri na wewe unavimba kichwa kwa sifa ya kazi yake na sio mapenzi ya kweli. Wewe utakuwa msaliti.

Maisha ya ndoa ni kuwa tayari kwa ajili ya mwingine wakati wa raha na shida, kwa furaha na amani bila majuto.

Monday, November 24, 2008

KATIKA MAISHA KUNA KUPENDWA NA KUCHUKIWA NA WATU

Kupenda/upendo ni kitu cha ajabu sana mara nyingi nimekuwa nimejiuliza kwa nini sisi binadamu tuna upendo tofaoti kwa kila mtu. Nikisema hivi nina maana kuna wakati mtu inaweza kutokea unampenda mtu kiasi kwamba huwezi kujizuia. Na cha ajabu mara nyingine uanaweza kumpenda mtu ambaye hujawahi kumwona ana kwa ana(uso kwa uso) na upendo ukawa wa nguvu kali sana.

Halafu sasa inaweza kuwa kinyume kabisa. Yaani watu tunaweza kuwa na chuki. Unaonana na mtu siku moja tu na utasikia simpendi kabisa jamaa huyu. Au hata kuangalia tu picha yake unapatwa na chuki. Nashangaa sana kwa uwezo kama huu ambao MUNGU amatupa na pia SHETANI anaingilia na kuharibu.Swali:- Hivi hii inatokana na nini?

Sunday, November 23, 2008

MDUNDUWALO/PERAMIHO 2005

2005 tukiwa Peramiho-Mdunduwalo. Hapo tulitaka kuruka na ungo. Huo hapo nyumba yetu ni ungo wa kupozea ugimbi (pombe)

RUHUWIKO/SONGEA 2007

Kaka zangu watono, baba na mdogo wangu mmoja wa kike. Hapo ni mwaka jana raha sana kuwa na familia kubwa.

Friday, November 21, 2008

HADITHI YA MWANA MPOTEVU

Hiii hadithi inanikumbusha mambo mengi sana sijui wenzangu mnasemaje?

Kulikuwa na baba mmoja aliyekuwa na watoto wawili wa kiume. Siku moja yule wa mwisho akamwambia baba yake : baba mimi sasa ni mkubwa naomba haki yangu nataka kuondoka kwenda mbali kutafuta maisha. Baba yake akampa pesa nyingi tu. Akaondoka akaenda zake na pesa zote.

Muda si mrefu akapata marafiki wengi tu. akawa anakula na kunywa nao pamoja na yeye ndiye aliyekuwa analipa kila kitu.

Lakini muda si mrefu pesa zote zikamwishia. Akawa hana kitu cha kula. Marafiki zake wote hawakumpa wala kumsaidia chochote isipokuwa walimtupa barabarani.

Siku moja akaondoka akaenda kwa mkulima mmoja na kusema ya kwamba anaomba chakula, aina yoyote ile, na halafu atafanya kazi kwake. Mkulima akamhurumia akampa chakula na akamwambia kazi yake ni kuchunga nguruwe wake.

Hata hiyo kijana bado alikuwa ana njaa. Akaanza kuwaza: kwa nini napata taabu hapa wakati baba yangu ana chakula kingi tu. Narudi nyumbani kwa baba tena. Nataka kufanya kazi kwa baba kuliko hapa.

Mara akaanza safari ya kurudi kwa baba yake. Na kusema baba, naomba radhi nimekosa. Ilibidi nisirudi na wala usinipokee tena hapa nyumbani kwako. Lakini baba kwa uchungu wa furaha akamkumbatia na kumpokea. Kwa furaha kubwa baba akamfanyia kijana wake sherehe kubwa kwa kufurahia kwa sababu kijana wake alikuwa amerudi tena kwake.

Kaka mtu akawa anarudi toka kazini(shambani) akakutana na babake asemaye. Mdogo wako amerudi tena nyumbani njoo tumsherehekee. Alipotea sasa amerudi tena.

Swali: Je? Hadithihii wewe inakufundisha nini?
Na je? ungekuwa wewe ni yule kaka mkubwa ungefanyaje?

Wednesday, November 19, 2008

MAISHA YA BINADAMU NI SAWA NA MAISHA YA KUKU


Mama na watoto wake tangu miezi tisa tumboni mpaka wanaanza darasa la kwanza wanamaliza na siku moja anabaki mama na baba tena peke yao kama walivyoanza maisha. Angalia hapo juu kila mama aendapo nao wapo. Mmh kazi kweli kweli.

MAISHA YA MAMA KUKU


Ebu angalieni hapa halafu fananisha na hapo juu. Maisha ya kuku hayaachani sana na ya binadamu. Kwani kuku ana bahati yeye anaatamia mayai wiki kama tatu hivi. Hapo tayari anatotoa vifaranga na atavitunza na kuvilinda na maadui wabaya kama vile mwewe na kadhalika. Baadaye wakiwa wakubwa anawadonoa hapo ndio kuwaambia SAMAHANI sasa muda umefika kwa ninyi kujitegemea.

Tuesday, November 18, 2008

SWEDEN NA MISITU YAKE

Ngoja leo tutembelee Sweden kuangalia mali asili(misitu)

Nitajaribu kutafsiri kwa kifupi tu yale mambo muhimu yaliyoandikwa hapo chini kwa kiswidi

Sweden ni nchi tajiri kwa misitu kati ya nchi zote duniani kama ukiangalia uhusiana baina ya maeneo ya misiti na uwingi wa watu. Kwa wastani kila mtu ana hekta 2,5 ya msitu.

Hekta milioni 41 hapa Sweden ni ardhi. Hekta milioni 23 ni misitu. Na zaidi ya nusu la eneo la nchi ni misitu.

Katka misitu hiyo zaidi ni misonobari na spruce(jamii ya misonobari)


Sverige består av 41 miljoner hektar land. 23 miljoner hektar är täckt av skog. På mer än halva landytan växer det alltså skog.
Skogarna består mest av tall och gran. Lövskogen är vanligare ju längre söderut i landet man kommer. I nordvästra Sverige ligger fjällkedjan med kalfjäll och fjällbjörkskog.
Sverige är ett av de skogsrikaste länderna i värden om man ser till förhållandet mellan areal skog och folkmängd. Vi har ungefär 2,5 hektar skog per person.



Sjöar och vatten drag9%= maziwa na mito 9%
Jordbruksmark 8% = Mashamba8%
Berg och fjäll = Milima 10%
Våtmarker 10%= Sehemu za majimaji(adimba) 10%
Produktiv skogsmark 51%= Sehemu nzuri za mavuno 51%
Övrigt 12%= Iliyobaki 12%


TAFSIRI YA HAPA CHINI

Kama ukijumlisha pamoja mimea yote kwenye miti utaona ya kwamba misitu hapa Sweden inachukua kwa wastani milioni 100 m3 kila mwaka. Pamoja na hivyo kila mwaka huvunwa kwa wastani milioni 85m3 . Pichi hiyo hapo chini inaonyesha jinsi miti inavyo kua.

Om man slår ihop tillväxten på alla träd ser man att skogen i Sverige växer med ungefär 100 miljoner m³ varje år. Samtidigt så avverkar vi omkring 85 miljoner m³ varje år. Det innebär att vi får större och större virkesvolym i landet. Idag har vi faktiskt dubbelt så stor virkesvolym som vi hade för hundra år sedan! Figuren här nedan visar virkesförrådets utveckling.








TAFSIRI YA HAPO JUU

Övriga privata ägare6%= Wamiliki wengineo binafsi 6%

Private enskilda ägare 51%= wamilikaji binafsi (kila mmoja) 51%

Private aktieblog 24%= Kampuni binafsi 24%

Övriga allmänna agare 1%= Wamiliki wengineo kwa ujumla 1%

Staten 18% = Serikali 18%

Sveriges landareal 41,1 milj. ha
Skogsmarksareal 22,7 milj. ha
Urskog ca 85 000 ha
Ädellövskog ca 150 000 ha
Tätortsnära skogar ca 300 000 ha
Kustnära skogar ca 450 000 ha
Virkesförråd 2 666 milj. m³sk
Årlig tillväxt ca 96,2 milj. m³sk
Årlig avverkning ca 70 milj. m³sk
Genomsnittlig volym av slutavverkningsträd från 0,20 m³sk i norra Sverige till 0,40 i de södra delarna av landet
Genomsnittlig volym vid slutavverkningar 203 m³sk/ha

Monday, November 17, 2008

MISITU NA WANYAMA WAKE HAPA SWEDEN HAPA NI AINA YA KONGONI(moose)




Mnyama huyu hapa Sweden ndiye mfalme wa msitu.

DUBU (Bear)




Kama mnavyooona hapa hii picha nimepiga mwenyewe kwani hapa ilikuwa karibu na siku zangu za mwisho. Nilikuwa mstuni natafuta uyoga, uroho wa uyoga. Lakini naona siku zangu zilikuwa bado.

MISITU YA SWEDEN NA WANYAMA WAKE

Sunday, November 16, 2008

AMRI KUMI ZA MUNGU

Leo ni jumapili nimeamka na nimeona afadhali nimkumbuke mungu kwa kuzikumbuka hizi amri.

1. Usiwe na miungu mingine ila mimi.

2. Usijifanyie sanamu ya kuchongo.

3. Usilitaje bure jina la BWANA , Mungu wako.

4. Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

5. Waheshimu baba yako na mama yako upate heri na miaka mingi duniani

6. Usiue

7. Usizini

8. Usiibe

9. Usimshuhudie jirani yako uongo

10. Usitamani chochote alicho nacho jirani yako.

Je? Kwa mtazamo wako hizi amri zinatekelezwa kweli?

Saturday, November 15, 2008

TRACY CHAPMAN NA YASINTA NGONYANI



Je? mwasomaji mnakubaliana na watu wengine wanasema sisi tumefanana. Asiyewahi kusikiliza mziki wake basi sikiliza mimi nampenda huwa namsikiliza.

JE? HAPA NAPENDEZA?




Hapa mwenzenu nilikuwa Saudi Arabia, wanawake wote wanavaa hivi kazi kweli kweli

Friday, November 14, 2008

BAADHI YA METHALI NA MAFUNDISHO KUTOKA KATIKA VITABU VYA WANGONI

1) Methali:- Kweli ikidhihirika uongo hujitenga.


Fundisho:- Kesema ukweli kunatusaidia katika kuweza kuishi na watu vizuri bila
kuelemewa na soni na kujifichaficha ambayo ni madhara ya kusema
uwongo.

2) Methali:- Mkataa pema pabaya panamwita

Fundisho:- Usikubali kufunga ndoa na mtu usiyemfahamu barabara.


3) Methali:- Majuto ni mjukuu

Fundisho:- Kila tunapofanya mipango ya mambo makubwa tuchukue tahadhari yote ili
kukwepa matokeo mabaya.


4) Methali:- Anayejua joto la jiwe ni mjusi
Fundisho:- Tusilete vitu majumbani mwetu bila kujali athari zinazoweza kutupata
sisi wenyewe au jirani zetu kutokana na vitu hivyo.


5) Methali:- Kila ngoma ina wimbo wake
Fundisho:- Wazazi tusiyapuuze matatizo ya watoto wetu hata kama wamekuwa ni watu
wazima. Tuwape misaada au ushauri.


6) Methali:- Aliyekataa ukoo alikuwa mchawi.
Fundisho:- Dumisha ukoo kwani ndugu atakufaa siku ya dhiki.


7) Methali:- Mwenda usiku amesifiwa kulipokucha
Fundisho:- Wewe usumdharau mtu kwa kuwa huielewi shughuli anayofanya kwa sababu
penngine shughuli yake italeta mafanikio na wenzako watamsifu.


8) Methali:- Mwanamume sio ndevu.
Fundisho:- Kila mwanamume anao uwezo. Kwa hiyo ni wajibu kwa wanaume wote kushika
moyo wa kiume.


9) Methali:- Mdomo ukila oua haitaki.
Fundisho:- Watu wengine hawafurahii mafanikio ya wenzao.



10) Methali:- Hasira ya mkizi furaha ya mvuvi.
Fundisho:- Unapokuwa na hasira usifanye jambo lenye umuhimu mkubwa ili kukwepa
kulifanya vibaya.

Wednesday, November 12, 2008

WENGI WANASEMA HIZI NI RANGI ZA WANARASTA




Je? ni kweli ni rangi za wanarasta kwani binafsi pia ni rangi zangu. Nisaidieni basi.Kazi kweli kweli.

MISS JAMAICA 2007+RASTA




Hapa ni dada Yvonne Gayle 2007 alikuwa Miss Jamaica. Swali langu: je? hizo rasta ni za kweli? au? angalieni vizuri.

Tuesday, November 11, 2008

KATIKA MAISHA NI VIZURI KUWAFARIJI MWENYE MATATIZO

Huu ni ushauri wangu mimi kwa wewe iliye na rafiki aliye na matatizo:-

1) Kama rafiki yako ana matatizo usiogope kumwuuliza hali yake kwa ujumla hata kama hali yake inaonekana si nzuri. Kama una matatizo halafu watu/marafiki wanakuuliza U HALI GANI utajisikia amani yaani kuna watu ambao wanakujali haupo peke yako.

Wakati mwingine kunatokea mambo ambayo si kweli na watu wanafikiri kuwa tayari yule mwenye matatizo amepata msaada mtu wa kuongea naye, wakati kumbe wewe upo peke yako kwa hiyo kuuliza ni muhimu sana.

2) Piga simu au nenda ili kujua mpatwa matatizo ana hali gani. Pia pika chakula, nenda kwake na mle pamoja. Wakati matatizo yanapotokea, inakuwa ngumu kuelezea vitu ulivyozoea kufanya kila siku. Kama una watoto inakuwa ngumu zaidi kuwatunza wakati upo kwenye matatizo/majonzi.

3) Onyesha upendo wako, bila kuonekana ni usumbufu kwa mpatwa matatizo, uwe nusu nusu. Usizidishe au usipunguze. HAPO NDIPO UTAWEZA.

Monday, November 10, 2008

MIRIAM MAKEBA AMETUACHA




Ni majonzi makubwa sana kwa dunia nzima lakini hasa Afrika/kusini. Kwa kuondokewa na mwanamke shujaa na Mwimbaji Miriam Makabe alikuwa Italia kusini.Jana usiku alipatwa na homa ghafla alikuwa kule kwa ajili ya kuimba. Miriam Makeba amekufa akiwa na miaka 76.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi AMINA.

Friday, November 7, 2008

KWA NINI JINA WAZUNGU,WAAFRIKA NA CHOTARA?

Baada ya uchaguzi huu wa USA, Nimejifunza mambo mengi kweli watu tuna mawazo tofauti labda naweza kusema UBAGUZI.

Wazungu akizaa na wazungu kinachotokea ni mzungu
mwafrika akizaa na mwafrika kinachotokea ni mwafrika
mzungu akizaa na mwafrika ni mzungu, chotara au mwafrika?
Na nusu mzungu/mwafrika akizaa na mwafrika je tutaita nini?
au akizaa na mzungu mtoto ataitwa nini? Mzungu, chotara au mwafrika. Au kama asilimia 99 mzungu na asilimia 1 mwafrika huyu ataitwa mzungu, mwafrika au chotara?
Swali.- Kweli Obama ni mzungu au mwafrika? na je? watoto wao tutawaitaje? kwa sababu wote mke wa Obama na Obama ni Chotara au nimekosea?

Kwa nini majina yote haya tuache ubaguzi ndugu zangu kwani wote ni binadamu na wote ni mungu ndiye aliyetuumba na damu zetu wote ni nyekundu.

Thursday, November 6, 2008

SAMAKI+MBOGA+CHAKULA



Na bila kituweo huwezi kula ugali. Haya ndugu zangu karibuni ugali na samaki wa kupaka.

KUSONGA UGALI+ CHAKULA




Sio kuandaa tu na kuacha, hapana sasa ni ile kazi ya kuandaa ugali mwenyewe.

KUTWANGA MIHOGO +CHAKULA




Hii kazi ndugu zanguni ni kazi muhimu sana. Hasa wakati ule mimi au sisi wengine tuluipokuwa wadogo. Bila hivyo huwezi kula kwani hizi mashine za kusaga hazikuwepo miaka ile ya -70, 80 na 90. Kwa hiyo picha hii imenikumbusha mbali sana wakati wa utoto wangu.Asante Lundu Nyasa kwa picha. nimechukua bila kuomba

Wednesday, November 5, 2008

TATIZO NI LIPI?

Mpaka watu wawe na roho mbaya ya:-

Usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu(Human Trafficking) ni nini?
Usafirishaji na biashara haramu ya watu (Human Trafficking) ni nini?

Usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) ni uhamisho wa mtu kutoka kwenye jumuiya yake na kwenda sehemu nyingine ndani au nje ya nchi kwa ahadi za uongo, matokeo yake ni kunyonywa kunyanyaswa, na kutumikishwa kwa kupindukia bila ya ujira kwa faida ya mtu mwengine, hii hujulikana kama utumwa mamboleo na ni moja ya matishio makubwa ya haki za binadamu. Ingawa usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) huwatokea wanaume, wanawake na watoto, lakini inaonekana wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi.


Usafirishaji na biashara haramu ya watu hutokea duniani kote na unyonyaji wa watu hutofautiana kati ya nchi na nchi (watoto kutoka Togo wanatumikishwa na kunyanyaswa katika mashamba ya kakoa Ghana, Wasichana wa Colombia wanalazimishwa ukahaba Japan n.k.)

Usafirishaji haramu wa watu/biashara ya watu katika Tanzania

Hali ya Usafirishaji na biashara haramu ya watu Tanzania.

Usafirishaji na biashara haramu ya watu (human trafficking) hutokea ndani ya Tanzania na kimataifa. Watu huletwa Tanzania kutoka Kenya, Uganda, Malawi na Burundi. Usafirishaji na biashara haramu ya watu unaoonekana kutapakaa sana ni ule wa ndani kwa ndani ya nchi unaolenga kuwanyonya watoto katika kazi za ndani.
Tanzania pia inatumiwa kama nchi ya kupitishia wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu toka nchi za pembe ya Afrika(Ethiopia, Somalia) wanaopelekwa Afrika kusini: Kuna wimbi la wahamiaji haramu wanaoingia
Tanzania ambao serikali ya Tanzania inahisi miongoni mwao wapo wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu. Kuna ushahidi wa matukio ambayo yanaonyesha kuna wahanga wa usafirishaji na biashara haramu kutoka India na Pakistan kuletwa Tanzania.

Watoto wahanga wa usafirishaji na biashara haramu ya watu waliosaidiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji/International Organization for Migration (IOM) wengi wao hutokea sana mikoa ya Iringa, Morogoro, Mbeya, Mwanza Singida na Dodoma. Zipo dalili kubwa kwamba Dar es Salaam na Zanzibar ndio vituo vikubwa wanaopelekwa wahanga hao. Watoto hao kawaida hutolewa vijijini kwa kuahidiwa maisha bora na elimu mjini na ndugu zao wa karibu au watu wanaoaminiwa na wazazi wao. Wakati mwingine watoto hawa hutolewa na wazazi wao kwa ndugu kwa mategemeo watoto wao watapata maisha bora wakiwa mjini.
Lakini wakati mwingine hali huwa sio kama walivyotegemea. Unyonyaji ni pamoja na kumlazimisha muhanga kufanya ukahaba, kazi za ndani, biashara za mitaani, kuosha magari bila kupewa nafasi ya elimu na matibabu, bila chakula au chakula kidogo sana, kunyanyaswa kijinsia, kutukanwa, kupigwa, kutishwa na kufanyishwa kazi bila ya ujira. Wengi wa watoto hawa wakifanikiwa kutoroka, huishia mitaani.

Sababu

Elimu ni moja ya sababu kubwa. Upatikanaji mkubwa wa elimu mjini huvutia vijana wa kike na kiume kutoka vijijini, wahanga wengi waliosaidiwa na IOM ni watoto walioacha shule au hawajawahi kwenda shule kabisa kijijini mwao (watoto wa kike 24 kati ya 34 waliosaidiwa mwaka 2007 hawakuwahi kwenda shule kabisa).
Kupoteza wazazi wote wawili. Hali hii husababisha watoto kulazimika kutegemea walezi.

Tuesday, November 4, 2008

MAISHA +NDOA MKE NA MUME




Kwa mawazo au akili yangu sijui ipi ni kweli au uwongo kwani labda ni kweli kila mtu duniani hapa ameumbika tofauti. Ni mungu peke yake anajua au labda ni wewe peke yako na nafsi yako ndiyo wajuzi.

MAISHA + NDOA YA WANAUME KWA WANAUME




Labda sababu ya kupenda, kazi kweli kweli ila labda kweli sababu ya kupenda semeni ninyi

MAISHA YA NDOA YA MKE KWA MKE





Semeni ninyi. mimi sina la kusema. Labda sababu ya kupenda au?