Friday, November 7, 2008

KWA NINI JINA WAZUNGU,WAAFRIKA NA CHOTARA?

Baada ya uchaguzi huu wa USA, Nimejifunza mambo mengi kweli watu tuna mawazo tofauti labda naweza kusema UBAGUZI.

Wazungu akizaa na wazungu kinachotokea ni mzungu
mwafrika akizaa na mwafrika kinachotokea ni mwafrika
mzungu akizaa na mwafrika ni mzungu, chotara au mwafrika?
Na nusu mzungu/mwafrika akizaa na mwafrika je tutaita nini?
au akizaa na mzungu mtoto ataitwa nini? Mzungu, chotara au mwafrika. Au kama asilimia 99 mzungu na asilimia 1 mwafrika huyu ataitwa mzungu, mwafrika au chotara?
Swali.- Kweli Obama ni mzungu au mwafrika? na je? watoto wao tutawaitaje? kwa sababu wote mke wa Obama na Obama ni Chotara au nimekosea?

Kwa nini majina yote haya tuache ubaguzi ndugu zangu kwani wote ni binadamu na wote ni mungu ndiye aliyetuumba na damu zetu wote ni nyekundu.

4 comments:

Anonymous said...

Au wote ni binadamu?

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana nawe ni kweli kabisa wote ni binadamu ya nini haya majina

MARKUS MPANGALA said...

najua unatetea sera zako dadangu lakini sioni tatizo kwani kutaja chotara au mzungu ni jamii tu wala haiondoi uhalisia wa mambo kwamba siyo binadamu. ni sawa na wewe kuitwa Yasinta haina maana kwamba wewe siyo binadamu bali ni utambulisho tu kwamba huyu anatoka jamii za wazungu,waafrika,wahindi,wachina n.k pia huyu anatoka mchanganyiko wa jamii fulani. swali langu linakuwa kwamba tunapombagua mtu hivi akitokea mtu ambaye asili yake ni waafrika, wazungu,wahindi,wachina n.k itakuwaje kwani Bobama tu katubabaisha mchanganyiko wake toka afrika,uzunguni, hadi kwa baba wa kambo indonesia ingawa hakumzaa. itakuwaje? jawabu ni JAMII na utambulisho labda tujaribu kusoma maandiko ya AFRICA IN SEARCH OF IDENTINTY ya Cheikh Anta Diop{kama sijakosea}, hapo utagundua kwamba jawabu ni UTAMBULISHO hakuna la zaidi

Yasinta Ngonyani said...

lakini kwa ni ni wasisema jina la yule mhusika ni lazima waseme mwafrika, mzungu au chotara?