Tuesday, November 11, 2008

KATIKA MAISHA NI VIZURI KUWAFARIJI MWENYE MATATIZO

Huu ni ushauri wangu mimi kwa wewe iliye na rafiki aliye na matatizo:-

1) Kama rafiki yako ana matatizo usiogope kumwuuliza hali yake kwa ujumla hata kama hali yake inaonekana si nzuri. Kama una matatizo halafu watu/marafiki wanakuuliza U HALI GANI utajisikia amani yaani kuna watu ambao wanakujali haupo peke yako.

Wakati mwingine kunatokea mambo ambayo si kweli na watu wanafikiri kuwa tayari yule mwenye matatizo amepata msaada mtu wa kuongea naye, wakati kumbe wewe upo peke yako kwa hiyo kuuliza ni muhimu sana.

2) Piga simu au nenda ili kujua mpatwa matatizo ana hali gani. Pia pika chakula, nenda kwake na mle pamoja. Wakati matatizo yanapotokea, inakuwa ngumu kuelezea vitu ulivyozoea kufanya kila siku. Kama una watoto inakuwa ngumu zaidi kuwatunza wakati upo kwenye matatizo/majonzi.

3) Onyesha upendo wako, bila kuonekana ni usumbufu kwa mpatwa matatizo, uwe nusu nusu. Usizidishe au usipunguze. HAPO NDIPO UTAWEZA.

9 comments:

Unknown said...

Kweli dada kupeana moyo ni jambo la muhmu sana ktk maisha,unapompa mtu moyo kunamfanya ajisikie vizuri,na anahsi kama umempunguzia mzigo,kwahyo tutiane moyo tushirikiane na kumshirikishe Mungu kwenye mambo yetu.

Unknown said...

Sasa wapo wale wakiwa hawana matatizo hawana mpango kabisa na wenzao wenye matatizo na wenyewe wakipata matatizo kulalamika hakuishi eti watu hawanitaki na wala hawaji kunitia moyo.

Ukweli unabaki ukiwa mwema kwa wengine na wewe siku ukiwa na matatizo basi watu watakukumbuka.

Ni vizuri kutiana moyo na kusaidiana wa upendo.

Yasinta Ngonyani said...

Pia labda sio lazima mtu awe na matatizo unaweza kuwa mwema tu na kushirikiana. Kwana kushirikiana ni vizuri wakati wote wa matitizo/shida na raha

MARKUS MPANGALA said...

mm nimekumbuka swali la Mwalimu wangu Ndesanjo lakini acha lifie moyoni. jamani kuna watu ukiwapatia sehemu ya upendo wako wala hawajali, kwahakika inauma. nakumbuka wakati simu hazijavumbuliwa, enzi za sanduku la barua yaani unaandika barua inakaa majuma kadhaa. watu wanatembea kilometa nyingi kkwa miguu kwenda kuwasambahi wenzao inapendeza kweli. ndiyo ni nzuri nakumbuka nilitembea kwa miguu saa 9 toka asubuhi saa kumi na mbili hadi alasiri ili kwenda kuwasalimia wenzangu. Lakini unapotoa upendo wako halafu wenzako hawakumbuki lolote unafanyaje? unanuna? utafanyaje? hapana fanya mambo yawe rahisi{take it easy} halafu unasonga kwa mwendo wa karatasi ama kinyonga. usiwasahau kwani iwe kawaida kwako. nimeeleweka vizuri au

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana kwani siku hizi hakuna kule kutakana hali kama zamani. Misimu kila mahali kwa hiyo watu ni sms. mail hakuna kutembeleana Zamani ilikuwa safi bwana

Mzee wa Changamoto said...

"GIVE AN HELPING HAND TO YOUR BROTHER WHEN YOU SEE HIM CRYING, GIVE AN HELPING HAND TO YOUR SISTER AND GOOD WILL COME AROUND...YOU SHOULD NEVER SEE YOUR BROTHER CRYING AND IGNORE HIS PAIN, YOU SHOULD NEVER LET YOUR SISTER WALK DOWN THE WRONG LANE" Ni maneno yao Morgan Heritage hayo wakiimba juu ya Helping Hand. Unayosema ni kweli Dada. Tunatakiwa kuwa Real na sio Simple friends. Ninaposema rafiki najumuisha na ndugu na nilipo-quote Brother na Sisters ni wake kwa waume. Ina maana haina haja ya kutaka kuonekana unajali ilhali unaona watu wakiteseka na kuwaacha. Mtazamo wangu katika makusudi ya Mungu kwetu unabaki kuwa ni kutimiza Amri kumi alizoweka na ukizisoma na kuzitafakari, utagundua kuwa 7 kati ya kumi (amri ya 3-10) zinahusu maisha yetu na jamii yetu. Ina maana 70% ya amri za Mungu ni za hapa Duniani na hawa tuishio nao na 30% ndizo zihusuzo maisha yetu na Mungu wetu moja kwa moja.
Ni mtazamo wangu na na-reserve haki ya kukosea na kukosolewa.

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza napenda kukukaribisha karibu sana.Nakubaliana nawe.kwa sababu kuna watu wengine ni wabinafsi sana hawajali wala kuona watu wengine wanateseka. Wana huu ubinafsi yaani kila mtu na lwake. Kwa mtu uliyezoea kushirikiana unaona ajabu sana. Kwani mara nyingine unaweza kupata kiwewe kwa kuona jinsi watu walivyo na ubinafsi.

Simon Kitururu said...

bomba la shule hii!Ingebidi binadamu walijue swala hili tokea utotoni.

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli Simon, lakini nafikiri wengi wanajua ila wanapuuzi tu. Natumaini kizazi kinachokuja kitakuwa afadhali. Matumaini yangu