Sunday, October 31, 2010

HUU NI UJUMBE WA JUMAPILI HII YA LEO!!!

Wapo watu ambao nyoyo zao ni kama lulu au almasi inayongáa kwa usafi, hazibebi chuki, choyo wala kejeli, bali hubeba mapenzi, imani na ukarimu. Hakika hata wewe unayesoma hapa ni mmojawapo. NAWAPENDA NYOTE. . NA NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI HUU WA KUMI IWE NJEMA. NA PIA, NI JUMAPILI MUHIMU SANA KWA NCHI YETU YA TANZANIA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA PIA WATU WAKE ILI UCHAGUZI UWE SALAMA!!!!

Saturday, October 30, 2010

Uchaguzi wa amani

Wakati umeshafika, uchaguzi Tanzania,
Kura zetu kutumika, viongozi kuchagua,
Umakini na hakika, ni wakati kuamua,
Naombea Tanzania, uchaguzi wa amani.

Vurugu hatuzitaki, tunapaswa kutulia,
Chaguzi iwe ya haki, uhuru wa kuamua,
Matokeo yale feki, amani itapotea,
Naombea Tanzania, uchaguzi wa amani.

Tuutimize wajibu, kuijenga Tanzania,
Kura zikawe majibu, nani kututumikia,
Hatuhitaji ghilibu, mabaya kutufanyia,
Naombea Tanzania, uchaguzi wa amani.

Kila aloandikisha, aende kupiga kura,
Tushiriki sababisha, ndoto ya maisha bora,
Ubovu kuuondosha, utufanyao dorora,
Naombea Tanzania, uchaguzi wa amani.

Kumekucha Tanzania, la mgambo lishalia,
Chaguzi imewadia, tuijenge Tanzania,
Makosa kutorudia, Mola atutangulia,
Naombea Tanzania, uchaguzi wa amani.
Shairi hili limeandikwa na Fadhy Mtanga

Friday, October 29, 2010

Haya wandugu niambieni hapa ni Kanyigo au Mbinga???

NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJEMA SANA NA MWISHO WA JUMA MWEMA NA PIA LABDA MWISHO WA IJUMAA YA MWEZI HUU WA KUMI.!!!

Thursday, October 28, 2010

WANABLOGGERS KUKUTANA JANA MJI WA TAMPERE


Malkiory Matiya na Mtakatifu Simon Kitururu
wakutana uso kwa uso!!!

Wanablogger hawa walikutana jana katika mji wa Tampare. kujua nini kilitokea huko bonyeza
Mtakatifu Simon na pia Malkiory Matiya. Ila jamani ugimbi huo mmmmhhh!!!

TANZANIA NAIPENDA SANA NA NADUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO!

Tanzania; Utulivu na Amani ni siraha yetu, tudumishe Amani yetu tunu yetu njema. Tunu hii tumepewa kwa upendeleo...hatukuinunua kwa fedha tunu hii, bali Amani imetawala...Amani ni namba moja Tanzania.
Madaraka yasituchanganye, utajili usituchanganye, bali amani ni mhimu na ni namba moja kwa Tanzania. Tunapo kosoana wapendwa, tunapo elezana ukweli...Amani itawale daima! kwenye shida na kwenye furaha, kwenye njaa na kwenye huzuni...Amani itawale daima!
Tukumbuke ametupa bure, tukimwuzi ataiondoa Amani hii...tuitunze kama yai tunu hii njema ya Amani, tuilee na tuipambe vizuri tunu hii njema, tuitunze ili nayo itutunze, tuilishe na tuinyweshe daima kwa Utulivu na Amani sisi Watanzania hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
IDUMU DAIMA AMANI TANZANIA.

-Mimi kila ninapopata wakati mgumu wa kutafakari, wanapotupeleka viongozi wetu, huwa natafuta solitude kwenye Amani waliotuachia Wazee wetu wa enzi za Mwalimu, Baba wa Taifa letu. Unajua Amani ni kila kitu, hata kama umezingirwa na mafisadi...lakini walau unapata wasaa wa kuburudisha roho yako ukiwa kwenye Amani yako.
Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa letu, alicheza sana aliposema; Ukabila uishie utani, dini iwe ni mapenzi ya mtu na nafsi yake. Maneno haya yametuweka hapa tulipo leo. Nasikitika tu generation ya watoto wetu, maana sisi Baba zao tunadhani Amani hii tuliyo nayo Mungu anaona aibu kutuondolea na kuwapa wenye akili na mapenzi nae.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE!

Makala hii nimeipenda na nimeona si mbaya nikiibadika hapa. Ni kutoka kwa kaka Baraka CHibiriti. Duh! naa sasa ni siku tatu tu zimebaki kwa kweli naiombea nchi yetu Tanzania uchaguzi uwe wa amani. Mwenyezi Mungu atutangulie.

Wednesday, October 27, 2010

Chai inapunguza mshtuko wa moyo!!!

Unajua kuwa kunywa chai vikombe vitatu kwa siku au zaidi kunapunguza mshtuko wa moyo kwa asilimia 21. Haya jamani tunywa chai!!!!

Tuesday, October 26, 2010

Hawa ni ndio wacheza mpira watarajiwa!!

Hapa ni Erik mwaka huu mwezi wa nane anavyoufurahia mpira.
Na hapa ni shangazi zangu nao hawapo nyuma. Hawa ndio wale wanawake wa shoka Picha kutoka hapa

Na hapa nadhani wote mnakumbuka huu wimbo wa dada Shakira ebu sikiliza:-)

Monday, October 25, 2010

Cheka kidogo!!!

Mmasai kakamatwa kwa kosa la kukojoa hadharani, akafikishwa mahakamani. Aliposomewa shtaka akubali, akahukumiwa miezi sita au kulipa faini ya sh. elfu hamsini,mmasai akamuuliza hakimu, muheshimiwa huko jela nalala bure na iko chakula ya bure? Hakimu akamjibu, ndio. Akauliza tena na masiwa ya bure iko? Akajibiwa, ndio, Mmasai akamwambia hakimu, basi ongesa miaka tano na iambie mama yeyo(yaani mkewe)ije na watoto yangu yote maana huko iko na raha . Hakimu na watu pale mahakamani wakavunjika mbavu kwa kucheka….. Basi nawe nadhani umeungana nao kuvunja mbavu….

Habari hii nimetumiwa na msomaji wa Maisha na Mafanikio na nikaona si Vibaya nicheke Nanyi

Sunday, October 24, 2010

Jumapili ya Leo Tusali Sala ya Nasadiki!!!

Nasadiki kwa mungu Baba mwenyezi/mwumba mbingu na nchi,/na vitu vyote vinavyoonekana,/na visivyoonekana.

Nasadiki kwa bwana mmoja yesu kristu,mwana wa pekee wa mungu.Aliyezaliwa kwa baba tangu milele yote.
Mungu aliyetoka kwa mungu,mwanga kwa mwanga,mungu kweli kwa mungu kweli.

Aliyezaliwa bila kuumbwa,mwenye umungu mmoja na Baba,ambaye vitu vyote vimeumbwa naye.Ameshuka toka mbinguni
kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu.
Akapata mwili kwa uwezo wa roho mtakatifu kwake yeye bikira maria/akawa mwanadamu
Akasulibiwa pia/kwa ajili yetu sisi/akateswa kwa mamlaka ya ponsyo pilato,akafa akazikwa.

Akafufuka siku ya tatu ilivyoandikwa.akapaa mbiguni/amekaa kuume kwa baba
atakuja tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu nao ufalme wake hautakuwa na mwisho

Nasadiki kwa roho mtakatifu/bwana mleta uzima atokaye kwa baba na mwana anayeabudiwa na kutukuzwa
pamoja na baba na mwana aliyenena kwa vinywa vya manabii.

Nasadiki kwa kanisa moja,takaifu katoliki la mitume.naungama ubatizo mmoja kwa maondoleo ya dhambi.
Nangojea na ufufuko wa wafu.Na uzima wa milele ijayo.Amina.
JUMAPILI NJEMA WAPENDWA!!!

Saturday, October 23, 2010

Sweden:- Kwanini iwe hivi?


MUUAJI ATINGISHA JIJI LA MALMÖ NCHINI SWEDEN

Kuna mlenga shabaha anae washuti wahamiaji wanaoshi nchini Sweden Katika jiji la Malmö. Mlenga shabah huyo hatari anachagua wageni tuu ndio anaowapiga risasi.

Mpaka sasa idadi ya waliolengwa imefikia 15 ndani ya siku tatu..
Hali imezikuwa kuwa tata na wasiwasi sio kwa wageni tuu hata Polisi vichwa vinawauma maana mpaka sasa hawajapata muelekeo maalum ukoje.

Katika Mkoa wa Skåne ndiko kilipo chama cha wasiopenda na wana idadi kubwa sana ya wanachama wao kuliko miji mingine ya Sweden..Kwa habari zaidi soma Aftonbladet.se
habari kutoka blog ya kaka Michuzi
Mdau wa Iceland.
Nami ngoja niongezee hapa:- Tunamwomba Mwenyezi Mungu mauaji yasizidi kutokea kwani sasa kila mtu ambaye si raia wa Sweden anaogopa hata kwenda nje, dukani hospital hata kupeleka watoto chekechea na hata kwenda kazini ni woga sana. Kwa kweli hili ni jambo la masikitiko sana na wengi wanajiuliza kwa nini? Pamoja Daima.

Ujumbe wa leo:- Napenda kuwatakieni Jumamosi njema kwa wimbo huu hapa chini haya karibuni!!JUMAMOSI NJEMA WANANDUGU NA TUKUMBUKE SISI SOTE NI NDUGU NA NI WATOTO WA BABA MMOJA. !!!!

Friday, October 22, 2010

WANYAMA NAO WANAFIKIRI NA KUFANYA MAJARIBIO KAMA SISI BINADAMU!!

Hapa vipi???
Sijui hapa niseme huyu farasi ni mjinga au? unakubaliana wanyama wapo karibu sana na sisi binadamu? Nakumbuka nilipokuwa mdogo nilikuwa nacheza na rafiki yangu Pona tulikuwa tukipangua mbula/mabuni na mchezo huo umenipa kilema kwenye kidole changu, kwa ajili ya kufanya majaribio kama huyo Farasi. Sijui atatukaje hapo?Nadhani kama huyu Chura hapa juu wengi leo ni mwisho wa juma na kazi mpaka jumatatu tena kwa hiyo itakuwa ni kupumzika tu. Haya nawatakieni IJUMAA NJEMA SANA!!!!

Swali:- Ni ubunifu au?

Yale yale ya kutembea na kujisikia haja kubwa au ndogo na kwenda kwenye nyumba ya mtu na kusema naazima choo. Kwa hiyo mtu huyu kaamua kufanya ubunifu wake kuwa na choo yake kwenye baiskeli yake. Lakini sasa hapa maji yakimwishia itakuwaje?


Thursday, October 21, 2010

NDOA YA MALAIKA HAIJAWAHI KUWEPO DUNIANI


Wakati mwingine misukosuko ya ndoa huwaliza wanawake,
lakini hizo zote ni changamoto !
Kuna kudanganyana kwingi kuhusu ndoa pale mtu anaposhindwa kuwa mwangalifu sana kwa kauli za wengine walio kwenye ndoa. Hii hutokana na ukweli kwamba kuna kujumuisha kwingi sana. Kuna wakati huwa tunasikia au kuambiwa kwamba ndoa ni sawa na jehenamu. Baadhi ya watu walio kwenye ndoa kuna wakati huzungumza kwa njia ambayo hutufanya tuamini kwamba kuoa au kuolewa ni jinai. Ndoa ni ujinga mtupu haina maana, mtu anaweza kusema. Wasemaji hawa wanaweza kuwa ni watu tunaowaamini sana kama wazazi wetu na wengine wa aina hiyo.
Baadhi ya watu badala ya kuponda na kubeza kuizungumzia kama kitu kizuri sana kisicho na doa wala chembe ya usumbufu. Inawezekena kabisa nasi tukawaamini wazungumzaji hao, hivyo kuamini kwamba, ndoa hazina usumbufu.
Inawezekana dhana hii ikaingizwa vichwani mwetu wakati tukiwa wadogo au hata tukiwa watu wazima. Hebu fikiria juu ya mtu ambaye anajisifu kwamba ndoa yake haina hata chembe ya mkwaruzo. Ambaye anaieleza ndoa yake kwa njia yenye kushawishi kuwa, kumbe ndoa zenye matatizo siyo ndoa bali kisirani kitupu. Kama nawe uko kwenye ndoa na ndoa hiyo ina matatizo hata madogo unaweza kudhani kwamba ulikosa kuoana na huyo mwenzako. Dhana hiyoinaweza kuchipuka kutokana na kauli kama hiyo inayoelezea ndoa kama kitu kisicho na mikwaruzo hata kidogo.
Kama usipokuwa mwangalifu unaweza kuacha kuchukua hatua za kujaribu kuondoa tofauti zilizo kwenye ndoa yenu. Utaacha kufanya hivyo kwa sababu mtu fulani atakuwa tayari ameingiza kichwani mwako uongo kwamba ndoa ni “asali” na “maziwa” matupu. Ni uongo kwa sababu hakuna ndoa isiyo na mikwaruzo.
Tunatakiwa kujua kwamba lengo la ndoa siyo kuepuka kukorofishana , hapana . Ukweli ni kwamba kukorofishana kunapotumiwa vema huweza kujenga uhusiano mzuri na imara sana. Kwa sababu kukorofishana hakuwezi kuepukika kwenye ndoa kunatakiwa kutumika kama shule na dawa ya kuimarisha ndoa.
Bila kukwaruzana kwenye ndoa zetu inaweza ikawa vigumu sana kwetu kubandua tabaka la uongo lililotufunika ambalo humfanya kila mmoja kati yetu kushindwa kuona na kumfahamu mwenzake katika tabia yake halisi.
Bila kukwaruzana, kila mmoja wetu atajidanganya kwamba anamfahamu mwenzake kama alivyo wakati siyo kweli. Tunapokwaruzana tunapata nafasi ya kufahamiana vizuri katika hali halisi.
Mwanamke mmoja maarufu aliwahi kuulizwa kama huwa anakwaruzana na mumewe. Alikiri kwamba huwa wanakwaruzana kwa kusema , “ndiyo tunakwaruzana, vinginevyo tungekuwa hatuna tofauti, na hapo bila shaka ndoa na maisha vingekuwa vimepooza sana”. Huo ndiyo ukweli wenyewe, kwamba bila kukwaruzana hatuwezi kufahamiana vema na kujua kwa undani tofauti kati yetu na wenzetu.
Inabidi tujue kwamba hakuna binadamu aliyekamili, yaani asiyekosea, kama ilivyo dunia yenyewe. Kwa hali hiyo hakuna ndoa ambayo haina makosa, kwa sababu ndoa ni binadamu hao ambao siyo kamili. Kwa hiyo, mtu anapotarajia kuwa au kuishi kwenye ndoa isiyo na kukwaruzana, ni sawa na mtu huyo kutarajia kukutana na binadamu ambaye ni kamili, yaani asiyekosea.
Kutarajia kuwa na ndoa ambayo haina kukwaruzana kunaelezwa kuwa ni chanzo kizuri sana kwa ndoa nyingi kulegelege au kuanguka kabisa. Mtu anapoingia kwenye ndoa akitarajia kwamba huko hatapambana na maudhi au kero za aina fulani, ni lazima ajue kwamba, hatadumu kwenye ndoa yake kwa sababu ndoa hiyo anayoitarajia haipo.
Mtu ambaye hakubali au angalau hataki kuelewa kwamba, ndoa ni lazima iwe na mikwaruzo anaweza kukabiliwa na tatizo lingine baya zaidi kwenye ndoa yake. Kwa kutokujua au kuepuka kukwaruzana, hawezi kuwa tayari kukubali kujadili migogoro ya kindoa ili kupata ufumbuzi. Hawezi kulikubali hilo kwa sababu haamini kwamba ndoa yenye kukwaruzana ni ndoa.
Wakati mwingine rafiki, ndugu au jamaa zetu hutusimulia jinsi ndoa zao zisivyo na kukwaruzana kama kwamba ni za malaika watupu. Bila kujua, huwa tunajikuta tumewaamini. Tunapowaamini huwa tunachukulia kukwaruzana kuliko kwenye ndoa zetu kama jambo au kitu ambacho hakikutakiwa kuwepo. Hapo hujikuta tukitamani kuondoka kwenye ndoa hizo kwa matarajio kwamba tunaweza kukutana na “malaika” ambao tutajenga nao ndoa zisizo na doa.
Hata pale ambapo tunasema wanandoa wanapendana sana, bado ndoa yao ni lazima itakuwa na kukwaruzana. Lakini wanachofanya hawa na ambacho huenda wengine hawafanyi ni kujadili tofauti hizo sawia na kuamua kuzisahau na hapo wote kukubali kujifunza kutokana na tofauti hizo.
Wale walio tayari kujadili tofauti zao sawia ndiyo ambao ndoa zao huwa na afya sana hadi wengine kushangaa kama siyo pamoja na kuona wivu. Wale wanaodhani ndoa ni mahali pa kila jambo kwenda kama mtu atakavyo, ndoa zao hupogoka vibaya na kufa kwa kishindo........

Makala hii nimeitoa katika Gazeti la Jitambue la hayati Munga Tehenan.

Wednesday, October 20, 2010

Tusisahau Fanicha zetu/Nimekipenda kitanda hiki!!!

Kuna vitanda vya aina mbalimbali lakini hiki ni cha aina yake na kina mvuto wa pekee na ni kizuri ingawa sijui bei yake lakini...... Bombi sana. picha kwa hidhini ya mtani wangu Mwananchi mimi.

Tuesday, October 19, 2010

Ataka talaka kwa nguvu ili aolewe na mwenye pesa


Mwanamke mmoja alitoa kioja baada ya kudai talaka kinguvu huku jamii iliyomzunguka ikimshangaa kwa kilichosemekana kuwa amepata mwanaume mwenye fedha.

Mwanamke huyo, alipokuja kwa wifi yake,kumueleza akamwambie kaka yake ampe talaka kwa kuwa alichoshwa na tabia zake,na kumuamuru akiwa hajampa talaka hiyo ataondoka hata kama hajapewa talaka.

“Mimi namuomba talaka kaka yako hataki kunipa ana maana gani? mimi simuhitaji tena nimechoshwa na dhiki mimi, anipe karatasi langu niondoke nyumbani kwake” na asiponipa naenda bakwata lazima aitoe” alifoka dada huyo kwa sauti bila hata aibu

Wifi huyo alijaribu kumuuliza alikosewa nini na kaka yake huyo, na swali hilo hakutaka kulijibu na kumueleza kuwa yeye anachohitaji ni talaka hahitaji maswali,

Hata hivyo mwanamke huyo ilifahamika na ndugu zake kuwa,alikuwa akitaka kuolewa na mwanaume mwingine ambaye alimuona atambadilisha kimaisha kwa kuwa ndugu zake hao alidai mwanaume huyo alikuwa na fedha zaidi ya mume wake wa sasa. Habari hii nimeipata Simon wa samvande

Swali:- Ni heshima/Adabu au ni Utamaduni/mila:- Yaani jinsi ya kuitika twiitwapo?

Nimekuwa nikijiuliza muda sasa umepita. Na sijapata jibu. Tangu nilipokuwa mtoto mdogo nimekuwa nikisikia watoto,vijana na wazee wakiitika kwa mtindo tofauti nikiwa na maana Wanaume/wavulana wakiitwa wanaitika NAAM. Na wanawake/wasichana wakiitwa wanaitka ABEE/BEE!.
Nimefanya utafiti hasa hapa Sweden kwa kweli MmmmH. hiyo haipo kabisa utakuta unamwita mtoto anatitika NINI? au EEEHH! Hapo ndio niliposema ama kweli TEMBEA UONE. Sijui wenzangu mnasemaje naomba tujadili kwa pamoja . UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU. Karibuni!!!!

Monday, October 18, 2010

Hivi Kwa Nini tunacheka?

kicheko ni njia ya mawasiliano, ambayo yanaonyesha ni ukaribu gani tunao na watu wengine. Hata kama mtu anacheka peka yake, kuna tafiti zinaonyesha kwamba hata ukiangua kicheko mara 30, kama tupo pamoja na watu wengine, kuliko tunapokuwa peke yetu.

Kwa kawaida kicheko kinaonyesha ni upamoja gani gani tunao na wale tunaocheka nao. Ni kinyume na nyani ambao wanacheka tu kwa furaha, kicheko cha binadamu kinaweza pia kumchokoza mtu , kicheko kinaweza kuwa cha dhihaka au hisia nyingine. Kicheko wakati mwingine kinaweza kuwa ni njia ya kupata huruma au huzuni pia.

Inaonekana kwamba sehemu kadhaa katika ubongo zimetawaliwa na kicheko. Mwaka 2001 huko Uingereza katika majaribio yao ya NMR X-RAY waliweza kuona sehemu ndogo ya kulia na kushoto ya paji la uso ilionekema ni zenye vichekesho/utan zaidi, lakini hizo aina za tofauti za utan hazifanyi kazi kwenye ulande moja.

Wakati utani unaposomeka, kwa kupima walakini upande mwingine wa mbele wa paji la nyuso kama ilikuwa ya kuchekesha. Inaonyesha kuna chumba cha tatu cha ubongo juu ya paji la nyuso. Ambayo kicheko kinakuja chenyewe.

Pia inaonyesha kuwa mwaka 1998 huko USA, wakati wao wenye vifaa vya umeme vilimfanya msichana wa miaka 16 bila shida kuangua kicheko. chanzo Illustrerad Vetenskap nr 15/2010.

Saturday, October 16, 2010

Chagua CCM chagua mahitaji haya............................

TUKO HIVYO, Hatuoni,Hatusikii.
Tunadanganyika kirahisi Tunafuata mkumbo BAADAE TUNALALAMIKA Chagua CCMOFISI ZETU

MAKAZI YETU

SHULE ZETU


DARASANI WATOTO WETUHUKO VIJIJINI-DISPENSARY

WAO WAKICHAGULIWA........................

Ubalozi wa Tanzania Wasington

Ofisi zetuBunge
Kuna cha kuongeza?

Sasa tucheze na hesabu 6,900,000/= kwa mbunge mmoja,zidisha mara miezi 12 then zidisha kwa miaka 5 = 414,000,000/= jumlisha 50,000,000/= anayopewa mara baada ya kumaliza miaka 5 = 464,000,000/= kwa mbunge mmoja.

464,000,000/= siko tayari kuzidisha fedha hii mara wabunge wote kwa miaka 5,calculator yangu itachanganyikiwa alafu niingie gharama ya kununua nyingine.

BEFORE YOU PACK KNOW THAT SOME PEOPLE ALSO KNOW HOW TO PACK

You can also have a laugh I just did. This is wonderful!


A man and his wife quareled and had a fight. After the fight, the wife went into the bedroom.
A few minutes later, the husband also trooped into the bedroom and only to find the wife busy packing her suitcase.
He asked "You are packing! Where are you going??"
She answered "To my mother!"
The man paused for a while and also got his big brown pure leather suitcase and started packing his clothes.
The wife angrily stared at him and said "You are packing! Where are you going?"
He replied " Oh ya! I am going to my mother!"
The wife "To your mother! And what about the children! Who is going to look after them?"
The man "You are going to your mother! Fine. I am also going to my mother. The children also should go to their mother"
The woman failed to continue her packing. She looked steadily at the husband and was left without any other option but just to shed tears of joy. She then hugged the man and said, "You are very intelligent. No wonder I married you; hahahaaaaaaaa!

HABARI HII NIMETUMIWA NA MSOMAJI WA MAISHA NA MAFANIKIO NA NIMEONA NI VEMA NIKIWEKA HAPA KIBARAZANI ILI TUCHEKE PAMOJA KWANI SIPENDI KUWANYIMA LOLOTE ZURI NA HATA BAYA:-) JUMAMOSI NJEMA JAMANI!!!

Friday, October 15, 2010

NI MIAKA MITANO LEO TANGU BIBI NA BWANA KALUSE WAFUNGE PINGU ZA MAISHA!!

Kaka Shabani Kaluse,Mkewe na Mvulana wao Abraham
Katika ndoa inatakiwa uvumilivu, upendo, maelewano nk. Familia hii leo imefikisha miaka mitano ya ndoa yao na matunda pia tunayaona, si mengine tena bali ni mtoto Abraham. Binafsi napenda kutoa HONGERA nyingi sana kwa siku yenu hii ya ndoa na pia nawatakieni kila la kheri mzidi kupendana na kuishi mpaka vikongwe kabisa na muwe na wajukuu wengiiii. Hakika nafurahi sana kuwa KAPULYA maana unajua mangi mengi kuuliza si ujinga bali ni kujua mengiiiii. Picha nimetumiwa na familia yenyewe zaidi ingia hapa mzee wa utambuzi. HONGERENI SANA KWA KUTIMIZA MIAKA MITANO YA NDOA!!!!!!!!!!!!!!!!!!Mnyasa mimi kwa samaki hamnitoi kabisa....

Samaki jamini wana utamu wake
Wakati tunakula au labda kumwangalia tu huyu samaki ngoja tusikilize na wimbo huu hapa chini:-)
Nimeusikiliza wimbo huu na nimetafakari kwa nini pole samaki? Au ndo wanataka sisi wapenda samaki tuache kuwala samaki. Mmmmhhh! kwa mimi itakuwa kazi sana kuacha kula SAMAKI!! Haya jamani:- MWISHO WA JUMAMWEMA NA IJUMAA NJEMA NA KULENI SANA SAMAKI!!!

Thursday, October 14, 2010

Tumepatwa na ugeni kutoka Tanzania Ni vijana waliokuja kwenye Ziara ya Mafunzo hapa Sweden!!

Wanapata chai na Kahawa kidogo
Chai na kahawa inaendelea!!

Ni jambo la kufurahisha sana kufikiwa na ugeni huu. Wote tulifurahi sana ingawa ilikuwa dakika chache tu. Na watakuwa hapa Sweden kwa muda wa miezi mitatu hivi.!!!!

Wednesday, October 13, 2010

HONGERA SHANGAZI YANGU PAULINA ARIANNA BANDIO KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA

mtoto Paulina mwaka mmoja leo
Binafsi nitakuita Shangazi/rafiki yangu. Lakini kuna wengine watakuita
binti, mtoto, binamu, mpwa n.k.
Shangazi/rafiki yangu Paulina leo ni siku kubwa sana kwako. Ni mwaka sasa
umepita tangu uyaanze maisha yako. Yaani leo unatimiza mwaka 1(mmoja) kwa
kweli miaka inakimbia sana, ni juzi tu ulikuwa kachanga leo hii umekuwa
binti wa kuweza kukutuma utuchotee maji ya kucnywa na karibuni tu utatupikia
na hata ugali.
Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kutoa pongezi nyingi sana kwa wazazi wa binti Paulina ambao ni Mubelwa na Esther Bandio kwa malezi
mazuri wampayo mtoto Paulina. Mwenyezi Mungu awazidishia nguvu ili muzidi
kumlea mtoto huyu na awe kama ninyi wenyewe.
Unaweza kuwatembela Mubelwa.

Tuesday, October 12, 2010

Hongera kwa siku ya kuzaliwa kwenu Dada Subi na Kaka Chib!!

Kaka Chib
Dada Subi
Blog ya Maisha na Mafanikio inapenda kuwatakieni siku hii ya kumbukumbu yenu ya kuzaliwa kwenu. Na pia muwe na Baraka tele na maisha mema na pia mafanikio mema. HONGERENI SANA.!!!!!


Monday, October 11, 2010

SWALI :- NANI ALIZIPA HIZI NCHI MAJINA NA LUGHA ZAKE??

Nani alitoa majina ya hizi nchi?

Siku, miezi na hadi miaka imepita huku nikijiuliza hivi KWA NINI au NI NANI alisema/amua haya majina ya hizi nchi zetu? Pia lugha za nchi? Kwa mfano nchi Tanzania lugha kiswahili. KWA NINI?

Na ndio nikaona niliweka hili swali hapa kibarazani ili tujadili kwa pamoja. Kwani Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Saturday, October 9, 2010

Usijemuahidi mwenye upere kucha. DC atolewa mkuku Maghala ya Hifadhi ya chakula Ruhuwiko

Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Savery Maketa, (Mwenye Suti) akizomewa na wakulima wanaosotea kuuza mahindi yao kwa wiki tatu sasa katika Maghala ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula Kanda ya Songea Ruhuwiko Manispaa ya Songea jana (Picha na Muhidin Amri-Ndolanga) Tatizo la soko la mahindi mkoani hapa limechukua sura mpya ambapo watu wanakesha usiku na mchana kusotea kuuza mahindi yao, Dc huyo alionekana kama bughudha na hana uwezo wa kuwasaidia hivyo kutimuliwa kama muionavyo hiyo picha. Dada Yasinta na mnaofuatilia Blog yenu hii mmeona mambo hayo?

habari hii nimeipata kutoka hapa na nimeona si vibaya kama nami nikiiweka hapa Maisha na mafanikia na ukizingatia ni nia moja.

Friday, October 8, 2010

Labda KUNA ambao HAWANA furaha mpaka wapate MTU MWINGINE au KITU KINGINE kisicho chao cha kukichukia au tu kukiona ni USHUZI!

Mt. Simon Mkodo Heriel Kitururu anasema...

Ukichunguza ,....
.... unaweza kupata MAFILINGI kuwa kuna wengi YAO huleta maana tu kama kwao YAWENGINE ni ushuzi.:-(

Ze mfano:

Labda MWENYE tabia nzuri furaha yake katika UPATAJI WAKE maana katika furaha zake ni kwa kuwa wengine anafikiri wana TABIA mbaya kwa hiyo yeye katika jamii anathamani zaidi .:-(

Labda Mkristo katika kufurahia UKRISTO wake- kunaleta maana tu pale astukiapo kuna WAISLAMU na WENGINE wenye dini za KIGAGAGIGIKOKO ambao afikiriao hawataenda mbinguni kwa kuwa si WAKRISTO kitu kimleteacho faraja katika UKRISTO wake ambao anaamini ni YESU tu ndio njia ya kwenda kwenye utamu.:-(

Kwenye Ukristo wa KISABATO labda faraja ni kustukia kuna WAKATOLIKI , Walutheri na hata wale WALOKOLE wa KIKAKOBE ambao kwa kisabato kuna kitu wanakosea katika mwendo wa maringo wa kulenga mbinguni kitu kifanyacho USABATO mtamu.:-(

Wenye akili kwa kuwa wanapasi MITIANI labda furaha ni kwakuwa kuna wajinga waliofeli naa ambao hata kushusha hoja kisomi hawawezi.:-(

Kwa KIMWANA mzuri SURA KAMA CHUNUSI -labda faraja huletwa na uwepo wa VIMWANA wenye sura kama JIPU kitu kisababishacho Kimwana mwenye sura kama chunusi kujisikia ahueni kwa kuwa anasifiwa zaidi ya mwenye sura kama jipu na katika kuchuna buzi akaunti yake hujaa kirahisi zaidi.:-(

Wayahudi labda huhitaji walimwengu wengine ili wajisikie kuwa wao ndio Taifa lililochaguliwa na Mungu kwa hiyo wao spesho.:-(

Ndio ,....
.... labda hakuna mwenye FURAHA kamili kivyake kama hakuna WENGINE na vya wengine vya kunyoshea vidole,.....

.... ili kuhalalisha kuwa vyangu vinaunafuu kitu ambacho husaidia baadhi ya watu ndani ya kibano KUSAIDIA ombaomba mtaani ikiwa ni MOJA YA NJIA ya kujisaidia kupata Uahueni kuwa angalau pamoja na kuwa MAISHA ni magumu lakini angalau mimi bado sijafikia kuwa ombaomba mtaani ingawa ni malaya kidooooogo.:-(

Swali:

SI kuna waonao mgonjwa nakupata unafuu kuwa angalau WAO ni wazima kama tu vile WEWE ukiona MZEE aliyefikia kujinyea ujisikiavyo vizuri kuwa angalau wewe bado kijana na BADO wewe unaweza kwenda mwenyewe chooni kushusha kilo kadhaa za kilichowahi kuwa chakula kwa MAMA N'TILIE?
SI kuna MKE WA MTU akiona MME wa mwenziye ni MZURI zaidi hupunguzwa faraja ya kuvumilia angalau vijambo a.k.a MASHUZI ya MME WAKE YA KILEVI aliyelala naye kitanda kimoja baada ya huyo MME kutoka BAA na kudai kwa nguvu chakula cha usiku cha ushindi wa haraka haraka kimagoli?
Ndio,....
....labda faraja zako hutegemea sana ufikiriavyo mapungufu ya wengine hata wasiokuhusu.:-(
Habari hii imeandikwa na Mzee wa mawazo Mt. Simon Kitururu . Nimeona si mbaya kama nikiibandika hapa kibaraza cha Maidha na Mafanikio.

Ngoja Ijumaa ya leo tuache ugimbi na tule matunda!!


Kula matunda uwe na afya bora poa kujikinga na magonjwa!! IJUMAA NJEMA SANA KWA WOTE!!

Thursday, October 7, 2010

Wanamitindo na warembo wa wiki hii ni hawa:- kumbe tupo wengi tunaopenda kutinga mgololi!!!


Yasinta Ngonyani na Salma Kikwete

Mama wa Maisha na Mafanikio na vazi lake la asili la mgololi na halafu hapo si mwingine tena ni mama Salma Kikwete akiwa naye ametinga vazi la asili aina ya mgololi. Ebu angalia ni kitu gani unaona ni tofauti au sawa katika picha hii:-) TUTAONANA WAKATI UJAO!!!

Wednesday, October 6, 2010

Nimekapenda kawimbo hakaSikiliza ujumbe huu !!!

WANANDOA NA KAULI HIZI: HATA VIKOMBE KABATINI HUGONGANA, ITAKUWA SIE?

Ndugu wasomaji, Habari hii nilishawahi kuivuka hapa MAISHA NA MAFANIKIO. Binafsi imenivutia sana na nimeona tuirudie tena kwani KURUDIA KITU ni KUJIFUNZA ZAIDI. KARIBUNI UNGANENI NAMI.
------------------------------------------------------------------------------------------------

Je unadhani au kuamini kwamba kuna ndoa ambazo wanandoa wake hawagombani kabisa? Kama unaamini hivyo, basi unajidanganya na labda unaishi katika dunia ya peke yako.

Ni jambo lenye ukweli wa kutosha kabisa kwamba wanandoa wote duniani hutokea kugombana, lakini kugombana huko hutokana na migongano au mizozo ya muda tu ambayo huweza kutatuliwa na pande mbili kama wakiamua kufanya hivyo.

Wewe unayesoma hapa, napenda kukuambia ukweli kwamba usiogope migogoro ya ndoa, kwani hicho ni kitu ambacho kamwe huwezi kukiepuka. Kuna msemo mmoja unatumika sana huko nyumbani usemao, " hata vikombe kabatini hugongana itakuwa wana ndoa?" Hii ina maana gani, ina maana kwamba haiwezekani watu kuishi pamoja halafu msiwe mnatofautiana, na kama ukiona hivyo, jua kwamba hiyo ndoa si salama kwani siku yoyote bomu litapasuka na madhara yake yatakuwa ni makubwa kuliko kawaida.

Kuna watu ambao hata kama wamekosewa na wenzi wao hunyamaza kimya na kumeza hasira zao, wengine huogopa kuwakabili wenzi wao na kuzungumzia jambo linalowakera kwa kuhofia kuonekana kama wana kasoro au ghubu. Jambo hili ni hatari sana.

Kumkabili mwenzi wako na kumwambia hisia zako kama amekukosea au amekwenda kinyume na matarajio yako ni jambao la maana sana katika kudumisha uhusiano. Lakini naomba nitahadharishe kwamba, ni vyema kufanya hivyo bila kumshusha, kubeza au kusimanga kwani hiyo sio dalili nzuri ya upendo.

Inashauriwa kwamba wanandoa au wapenzi wanapokwaruzana inabidi wajadili tofauti zao bila kusigishana, kila mmoja akitaka kuwa mshindi, hiyo haitasaidia kuimarisha ndoa bali itaongeza tatizo. Ni vyema upande unaohusika na tatizo, uwajibike na kuomba radhi kwa ustawi wa ndoa, huo ndio ukomavu.

Kutojadili mgogoro kwa wanandoa na kuupatia ufumbuzi wa tatizo huwafanya wandoa kuwa mbali kihisia, na athari zake ni kuwakuta wanandoa wakiwa wageni wa kila mmoja kwa mwenzake, yaani hakuna mawasiliano, kila mtu na lwake.

Jambo la msingi kwa wanandoa ni kujadili tofauti zao pindi linapojitokeza jambo linalomkera mmoja wa wanandoa, kwani hakuna jambo linaloweza kujitatua lenyewe bila kutatuliwa na wandoa husika. Kuacha jambo lolote bila kulitafutia suluhu ni sawa na kutega bomu, ambapo siku likilipuka madhara yake ni makubwa sana.

Unaweza kukuta mwanandoa anakereka na mambo madogo madogo ya mwenzi wake lakini hasemi, ingawa yanamkera kupita kiasi akitegemea huyo mwenzi wake atajua na kuacha, thubutu…..inapotokea siku yeye amekosa jambo dogo tu na huyo mwenzi wake akamsema, basi atatumia fursa hiyo kuanza kujibu mapigo kwa kueleza yale yanayomkera kutoka kwa mwenzi wake, na hapo itakuwa kila mtu anavutia kwake kama mwamba ngoma………na aamini nawaambia kuwa kamwe hawezi kupatikana mshindi katika jambo hilo, kwani mjadala huo unaweza kutoka nje ya mada kila mmoja akijitahidi kutafuta makosa ya mwenzi wake hata yale yaliyotokea wakati wa uchumba wenu ili mradi vurugu tupu.

Inatakiwa wanandoa wajadili kila jambo linalojitokeza hadi kulipatia suluhu, vinginevyo ni kuichimbia ndoa yenu kaburi la mapema. Wakati mwingine unaweza kukuta mwanamke analalamika juu ya kutoridhishwa kwake na matumizi ya mumewe, na hapo mume naye ataanza kukumbusha juu ya matumizi yasiyo ya lazima yaliyofanywa na mke huko nyuma. Mke naye hataridhika atakumbushia jambo lingine na lingine hadi hata mada iliyokuwa ikijadiliwa inasahaulika.

Jambo lingine ni kujumuisha mambo, matumizi ya maneno kama, mara nyingi, kila wakati au mara kwa mara si mazuri sana. Unaweza kukuta mtu mwenzi wake amekosea jambo halafu mwenzie anamwambia “Kila mara huwa unafanya hivi” au mara nyingi huwa unafanya hivyo…..Hii ni hatari kwa ustawi wa wanandoa, kwani kwa kujumuisha ni sawa na kumwambia mwenzi wako kuwa kila mara yeye ndiye mkosaji.

Kwa haya niliyoyaeleza hapa sina maana kwamba huu ndio muarobaini pekee wa kuimarisha mahusiano kwa wanandoa, bali ni moja ya mambo muhimu kati ya mengi ambayo yakizingatiwa na wanandoa wote basi ndoa yao itakuwa imara Tujadili pamoja………..

Na hapa yalikuwa maoni ya baadhi ya wasomaji......

James Adolwa said...
Kweli unavyosema kuwa maranyingi mzozo ukidhihirika ni kwasababu kuna kero lililo fichika ama kufunikiwa. Swala lingine ambalo watu wanatakikana kuzingatia....wacha nitumie kiingereza kidogo....One needs to consider what one keeps steaming under the lid of the cooking pot. If you spend your time and energy focusing on the weaknesses or faults of another then all that you will see in the other person are weaknesses and faults...and you will end up cooking up a foul tasting broth that will spill over and put out the flame of your relationship.

Instead try and focus on the strengths and virtues of your partner and in the end you will find that you keep seeing more and more good things. This is not to say that all the experiences will be pleasant but rather all the bitter, sweet, sour and salty experiences work out together such that the sum total ; the big picture, the essence of the whole experience works out to be a pleasant experience for both. I am no expert but these are the thoughts that flowed from my soul.

October 12, 2009 8:34 PM
Ramson said...
Dada yangu hapo umenena, kaka James, naona imebidi kuandikwa kwa kiingereza ili kuweka msisistizo....kaaaazi kweli kweli.

Dada Yasinta hili ni darasa tosha kwa wale wanandoa ambao hawakubahatika kujifunza namna ya kutatua migogogro ya ndani katika uwanja ulio sawa. Unajua wazee wetu walipokuwa wakituambia kuwa ndoa ni kuvumiliana wengi walitafsiri vibaya, walijua kuwa ni kumeza hasira zetu pindi tunapokosewa na hii ilitumiwa vibaya zaidi na wanawake, lakini siwalaumu bali mfumo dume ndio uliowafundisha.......
Inaposemwa kuwa ndoa ni kuvumiliana maana yake ni kujadiliana kwa uwazi pale tatizo au kunapozuka kutoelewana juu ya jambo fulani na uzingativu uwekwe kwenye kutatua tatizo sio kubishana kwa ajili ya kumtafuta mkosaji. Tumelelewa katika familia tofauti, kuna baadhi ya wanume wamefundishwa kuwa hawapaswi kuwaomba wake zao radhi hata kama wamekosa,,,,,inabidi mke awe makini kama akishajua kuwa mumewe ni wa aina hiyo.....


Anonymous said...
Darsa hilo Yasinta, safi sana, umemaliza yote hata cha kuongeza sina kwa leo labda kifupi sana wanasema katika maandiko matakatifu kwamba "upendo huvumilia, hauhesabu mabaya na kadhalika..." basi kama tafsiri sahihi ya upendo ikiwepo miongoni mwa wana ndoa basi mchezo umeisha, du ni hivi jioni hii nilikuwa nasikiliza kipindi cha maridhiano kupitia redio Maria Tanzania du, niliyoyasikia huko yanatisha kisa kusaka mtoto sijui ujiko kwa mwanaume! na kisa kingine kilikuwa wiki iliyopita ambapo mwanaume alienda kuazima dume ili limzalishie watoto, huko kote mwanamke alikuwa anashinikizwa lazima afanye mapenzi na hilo beberu!!

SIMON KITURURU said...
Bomba la somo hili Dada Yasinta!

Lakini sijui kwanini huu msemo wa kuwa Vikombe hugongana kabatini huwa na wasiwasi nao kwa kuwa nashindwa kuwa na uhakika kuwa kihalihalisi labda VIKOMBE hugonganishwa na HAVIGONGANI tu kienyeji ndani ya KABATI.


Anonymous said...
My sista unanikuna jamani hilo ni kweli my sista kwani kila mtu kalelea kivyake na malezi yake just meet with her /him ukubwani ni lazima kuwe na migongano ya hapa na pale nduguyo tu mwajibizana sembuse mtu baki ooh please Kaka Simon Kitururu kwani utakuta wewe ukisusa wenzio wanakula food yote lkn familia nyingine ukisusa watu hawali mpaka ujongee mezani,Kuna wengine hata hajui kumheshimu dadaake or kakaake yote ni malezi hp umeelewa brother from anaother mother meanz ya vikombe kugongana ni misemo ya mafumbo ya mababu zetu soo Open ya Eyes oky!!!!

chib said...
Big up Kitururu, huwa naupinga msemo huo wa vikombe kabatini kugongangana, ukweli kama kabati imetulia, vitagongana vipi, ni wale wenye mafujo tu ndio huvigonganisha, au kama unakaa Sumatra ambako matetemeko ya ardhi hayaishi, hapo ndio vitagonganishwa na tetemeko. Ypte kwa yote, somo hilo ni zuri kabisa kwa watu wote wenye ndoa na watarajiwa.

SIMON KITURURU said...
@Anony: nankunukuuu ``ooh please Kaka Simon Kitururu kwani utakuta wewe ukisusa wenzio wanakula food yote......''

Hapo si kunauwezekano kiwagonganishacho ni FUDI?:-)

Nimekuelewa lakini MKUU na pointi yako nimeipata.

@MKUU CHIB: Hapo kwa mtazamo wangu umemaliza NUKTA


Markus Mpangala said...
Ni MSARAGAMBO hapo

Yasinta Ngonyani said...
Nachukua nafasi hii kuwashukuruni wote kwa maoni yenu kwani huku ndio kujifunza. Maana kila mtu anajifunza toka kwa mwingine. Ila sifungi mjadala karibuni kujadili zaidi

Tuesday, October 5, 2010

Tusisahau! Misemo na metheli toka Tanzania kwa lugha mbalimbali!!

1. Kibena:- Atembea na moto mgongoni.
Maana ya methali hii ni kwamba kama wewe si mkarimu, basi ujitegemee mwenyewe kwa kila kitu popote utakapokwenda. Methali hii hutumika kwa fundisho kwamba hakuna myu anayeweza kutenda jambo bila msaada wa wenzake. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

2. Kisukuma:- Fahamu kazi, usifahamu ngoma.
Maana ya methali hii ni kwamba ni vizuri kufahamu mambo ya maana kuliko kufahamu mambo yasiyo na maana. Hatumika katika kumwasa mtu ambaye anaanza kuzurura ovyo badala ya kyfanya kazi kama kulima, kusoma n.k.

3. Kiiraqw;. Haraka na pupa huzaa chongo.
Methali hii inaonya juu ya kukosa uvumilivu. Mambo mengi yafanywayo kwa pupa hayatimiziki na pia huleta matokeo mabaya. Methali hii ni kama ile ya kiswahili "Haraka haraka haina baraka"

4. Kisambaa:- Iliyonona huanzia miguuni.
Maana yake ni kwamba mtu mwema hujulikana haraka. Hutumika hasa katika mashauri ya kuchagua watu kwa shughuli fulani au kijana ayeleta posa, adabu zake na anavyofanya siku za kwanza.

5. Kipare:- Kabla hujamwua ndege usiwashe moto.
Maana ya methali hii ni sawa na ile isemayo:-
Usishone mbeleko kabla mtoto hajazaliwa. Asili ya maana ya methali hii hutokana na tabia za watoto za kuwinda ndege kwa pinde na mishale. Wakishamwua ndege humbanika na kumla. Jambo ambali linahitaji maandalio ya moto. Matumizi ya methali hii ni kuwaonya watu ambao wamezoea kupanga mipango juu ya mambo ambayo hayana uhakila asilimia kuwa yatatokea zaidi hutumika kwa mambo yanayohusu mali na ukwasi na mipango yako.

Monday, October 4, 2010

KITAMBI/UNENE: Ni dalili ya afya au ugonjwa?


Katika baadhi ya jamii zetu nyingi hasa kutoka bara la Afrika, kumejengeka dhana kuwa kitambi /unene huashiria utajiri. Mila, imani na desturi hii kwa kiasi fulani huchangia watu kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora, pengine hii inatokana na mwamko mdogo wa elimu ya afya jamii.

Wakati hali ikiwa hivyo miongoni mwa watu toka bara letu la Afrika, kwa upande wa nchi zilizoendelea, watu huamini kuwa unene/kitambi ni dalili tosha ya ugonjwa. Siyo hivyo tu bali pia historia ya magonjwa katika fani ya elimu afya jamii inatueleza hivyo.

Kuna unene wa aina kuu mbili, kwanza ni ule unaosababishwa na kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora / balance diet. Kwa mfano ulaji wa vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta na wanga, unywaji wa mara kwa mara wa pombe kama vile bia pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo. Aina ya pili ya unene ni ule unaotokana na urithi japo kwenye mada hii msisitizo zaidi ni kwenye aina ya kwanza ya unene.


Kuna matatizo mbali mbali yanayo ambatana na unene/kitambi. Mosi, madhara ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari aina ya pili /diabetes type II. Pili, madhara ya kisaikolojia, hasa pale mtu anapojishuku kupoteza mvuto/ aesthetic beauty. Hali imeshamiri sana hasa katika nchi zilizoendelea ambapo watu huchukulia unene/kitambi kama ulemavu fulani wa kimwili.

Pamoja na hayo, nadhani wakati mwingine tunafanya makosa kuwahukumu binadamu kulingana na mwonekano wa maumbile yao, kwani hakuna hata moja kati yetu anaweza kuingilia kazi ya uumbaji, ninasema hivi kwasababu hatuwezi kujua ni nini chanzo hasa ambacho kinapelekea mtu kuwa mnene au kuwa na kitambi. Kama nilivyosema awali, kuna aina ya unene/kitambi kinachotokana au kusababishwa na urithi.

Namna ya kukabiliana na matatizo yatokanayo na unene/kitambi, wakati watu katika mataifa yanayoendelea, hujikita zaidi kwenye matumizi ya magari hasa magari binafsi, kidogo hali ni tofauti katika nchi zilizoendelea ambapo msisizito kwao ni kwenaye matumizi ya usafiri wa umma, matumizi ya baiskeli na hata matembezi ya miguu kwa sehemu zinazofikika. Kwa hili wenzetu wa mataifa yaliyoendelea wamefanikiwa vya kutosha kwa kuwekeza na kutenganisha barabara za magari na zile za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu.

Mwisho, njia pekee ya kukabiliana na changamoto hii ya unene/kitambi, ni kwa kuzingitia kanuni za lishe bora kwa

Habari hii nimeipata hapa.

Friday, October 1, 2010

Ni Ijumaa mpja ya mwezi, kula kwanza halafu kunywa!!

Napenda kuwatakieni IJUMAA njema na mpya /ya kwanza ya mwezi huu wa kumi. Kila mtu leo atasema sasa nimemaliza kazi ngoja nipumzika na nipate moja baridi!ugimbi. Ni sawa lakini kumbuka kula kwanza ni MUHIMU sana. IJUMAA NJEMA!!!