Thursday, October 28, 2010

TANZANIA NAIPENDA SANA NA NADUMISHA AMANI NA MSHIKAMANO!

Tanzania; Utulivu na Amani ni siraha yetu, tudumishe Amani yetu tunu yetu njema. Tunu hii tumepewa kwa upendeleo...hatukuinunua kwa fedha tunu hii, bali Amani imetawala...Amani ni namba moja Tanzania.
Madaraka yasituchanganye, utajili usituchanganye, bali amani ni mhimu na ni namba moja kwa Tanzania. Tunapo kosoana wapendwa, tunapo elezana ukweli...Amani itawale daima! kwenye shida na kwenye furaha, kwenye njaa na kwenye huzuni...Amani itawale daima!
Tukumbuke ametupa bure, tukimwuzi ataiondoa Amani hii...tuitunze kama yai tunu hii njema ya Amani, tuilee na tuipambe vizuri tunu hii njema, tuitunze ili nayo itutunze, tuilishe na tuinyweshe daima kwa Utulivu na Amani sisi Watanzania hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
IDUMU DAIMA AMANI TANZANIA.

-Mimi kila ninapopata wakati mgumu wa kutafakari, wanapotupeleka viongozi wetu, huwa natafuta solitude kwenye Amani waliotuachia Wazee wetu wa enzi za Mwalimu, Baba wa Taifa letu. Unajua Amani ni kila kitu, hata kama umezingirwa na mafisadi...lakini walau unapata wasaa wa kuburudisha roho yako ukiwa kwenye Amani yako.
Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa letu, alicheza sana aliposema; Ukabila uishie utani, dini iwe ni mapenzi ya mtu na nafsi yake. Maneno haya yametuweka hapa tulipo leo. Nasikitika tu generation ya watoto wetu, maana sisi Baba zao tunadhani Amani hii tuliyo nayo Mungu anaona aibu kutuondolea na kuwapa wenye akili na mapenzi nae.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE!

Makala hii nimeipenda na nimeona si mbaya nikiibadika hapa. Ni kutoka kwa kaka Baraka CHibiriti. Duh! naa sasa ni siku tatu tu zimebaki kwa kweli naiombea nchi yetu Tanzania uchaguzi uwe wa amani. Mwenyezi Mungu atutangulie.

10 comments:

Faith S Hilary said...

Yaani asante dada Yasinta kwa kuiweka hii makala hapa japo washabiki wa Chadema, CUF na vyama vingine watanuna kidogo japo umeitoa article kutoka kwa mtu mwingine hehe (si unajua?). Ila hata mimi naiombea nchi yangu hususan kwa wakati huu wa uchaguzi, nina matumaini kwamba kila kitu kitakwenda salama ikiwa tu, watu wakitumia busara siku hii ya Jumapili. Mungu ibariki Tanzania

malkiory said...

Mtoa mada akumbuke kuwa amani haipo ndani ya CCM. Heri kuwa muwazi kuliko kuwa mnafiki,hapa ameongelea kuhusu amani wakati lengo lake likiwa ni kuifanyia kampeni CCM. Inajulikana wazi kuwa kura ni siri ya mtu, kwa hiyo kama yeye anayo nia ya kuipigia kura CCM hakuna haja ya kutueleza sisi.

Simon Kitururu said...

Nawasiwasi na swala zima la kuwa ``Amani ni namba moja Tanzania´´.


Natafakari!

John Mwaipopo said...

yasinta unatakiwa uwe makinini kidogo. sina haja ya kuyaingilia matakwa na utashi wako lakini katika hili you have been carried away unknowingly. yangekuwa mawazo yako 100% wala nisingalichangia hapa kwani huo ndio ungekuwa mtazamo wako.

kama amani ipo tanzania ipo kwa kuwa ipo tanzania lakini si kwa kuwa imeletwa na chama fulani. ipo kwa kuwa ipo. kama ni upendeleo wa mungu iwepo amani tanzania itaendelea kuwepo kwa kuwa mungu huyohuyo ataendelea kuipendelea tanzania. kama mungu ameipenda tanzania basi itaendelea kuwepo tu. mungua hajaipa amani tanzania kwa kuwa inatawaliwa na ccm. kama lengo la mungu ni kuipa amani tanzania basi hata chama kingine kikitawala haka kiitwe KOROKORO PARTY OF PEOPLE mungu huyo huyo ataendeleza amani tanzania.

sijamsikia mgombea yeyote asiye wa ccm anasema atamwaga damu akiwa madarakani. maana yake hiyo ndio tafsiri inayokuja kuwa kikichaguliwa chama kingine (ambacho si ccm) basi kitaanza kumimina risasi kwa watanzania kikiwa madarakani. unaposema dumisha amani kwa kuchagua ccm unamaanisha ccm wakiwa madarakani hawamiminii risasi wananchi. ila kikiingia madarakani chama kingine wananchi watakoma maana chama kingine kitaanza kunyuka watu hovyo.

maana ya makala hii imepotoshwa kuwa kikiingia chama kingine ole wenu. lakini kwa tafsiri ndogo tu ni kuwa haiingii akilini kuwa chama kinapokuwa madarakani kitachinja watu. kumbe tafsiri nyingine unapata kuwa watakaoondosha amani ni wale watakaokuwa wamanyang'anywa madaraka. mara zote mgomvi n i yule aliyekuwa madarakani na hataki kutoka. tazama kenya na zimbabwe

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Mwaipopo...mie mwanachama wa ccm lakini sikubaliani na huo upuuzi unaoelezwa hapo!

Hongera, ntakununulia ugimbi..oops, mvinyo tukionana!

Anonymous said...

Yasinta nilikuwa napenda sana kusoma blog yako lakini leo umedhihirisha wazi kuwa wewe unaona sahihi maisha wanayoishi ndugu zako kule ruhuwiko sijui wapi kwa vile wewe upo ulaya. Tuache kujidanganya maisha ya watanzania wengi leo vijijini ni maskini utafikiri tupo bado kwenye enzi za ujima wakati hii ni karne ya 21 karne ya sayansi na tekelinalokujia wewe Yasinta unasema amani, amani bila maisha bora inasaidia nini? Amani ilikuwepo itaendelea kuwepo hata ije Chadema,CUF,TLP,NCCR etc. ndivyo watanzania tulivyo acheni kukuza mambo wakati mnafahamu wazi watanzania wote hawaombei vita. Yasinta rudi kwenu kijijini wewe na familia yako halafu urudi utuletee huu mchango sio unaongea tu kwa vile upo dunia ya kwanza. Message sent.

Koero Mkundi said...

Dada kwa hili sitaungana na wewe, lakini sikulaumu, unaishi ughaibuni, utayajuaje madhila ya watanzania wenzio wanaoteseka na umasikini unaosababishwa na chama tawala cha CCM?
Ni mara nyingi umekuwa ukiandika shida tunazokabiliana nazo kuanzia maradhi, elimu huduma duni za kijamii, miundombinu na mengineyo, lakini cha kushangaza leo hii unashabikia wale wale wanaosababisha madhila tuliyo nayo?
leo umeniacha mdomo wazi dada!

John Mwaipopo said...

chacha O'wambura tena yangu ni yale maji taka ya ilala, haswa ile cas... ya bariiiidi.

inapokuja katika kuongelea mambo ya taifa ya ukweli na ya msingi huwa sina kigugumizi.

Yasinta Ngonyani said...

Ndugu zangu wapendendwa! Tanzania ni nchi ya kidemokrasi ambapo sisi sote tunawajibika kushiriki katika zoezi hili, na kwamba mawazo ya kila mmoja wetu ni muhimu katika kudumisha/kuimarisha amani, maendeleo na "uhuru wa maoni" na tukichukulia kwamba tupo ktk kampeni ya uchaguzi mkuu nimeona ni vyema tujadili kwa pamoja itikadi ya angalao vyama vitatu vinavyoshiriki katika zoezi hili, hivi nimeanza na CCM na baadaye tuweze kujadili kuhusu vyama vingine.(Na tusiangalie "opposition party" kama adui wa amani na maendeleo bali ni tofauti tu ya kufikiri kuhusu ratiba ya nchi yetu, kwani kwenye wengi hapakosi tofauti ya maoni).
Kwa hiyo dhumuni au nia kubwa ilikuwa sio kufanya kampeni ya chama kimoja au kingine bali kubadilishana mawazo mkichukulia kwamba ni wakati muhimu sana kwa maisha ya nchi yetu.

Baraka Chibiriti said...

Mimi ndie nilie andika mada hii, nawakumbusheni kuwa tupo nchi huru...hakuna mtu analazimishwa kuwa chama fulani au la! Kila mtu anahiari ya kuwa mwana chama fulani na wala si unafiki kabisa. Sasa kama CCM inawakwaza, basi mnisamehe si makosa yangu. Ila sioni kuwa kunamakosa ya jinai kuwa mwanachama wa CCM, kwahiyo acheni zenu hizo...sisi sote ni ndugu, CCM, CAF, CHADEMA n.k. Hakuna cha unafiki wala nini. Kama inakukera CCM, si kosa langu. Cha mhimu Amani itawale Tanzana.Pia Habari kama inakukera sana... si uiruke tu! Endelea na habari nyingine, tupo nchi huru kabisa....cha mhimu sijamtukana mtu yoyote wala kumdharau kabisa, wala kukidharau chama chochote Tanzani, na kama nimekutukana na kukudharau niambie...ili tongee na nikuombe msamaha.