Friday, October 15, 2010

Mnyasa mimi kwa samaki hamnitoi kabisa....

Samaki jamini wana utamu wake
Wakati tunakula au labda kumwangalia tu huyu samaki ngoja tusikilize na wimbo huu hapa chini:-)
Nimeusikiliza wimbo huu na nimetafakari kwa nini pole samaki? Au ndo wanataka sisi wapenda samaki tuache kuwala samaki. Mmmmhhh! kwa mimi itakuwa kazi sana kuacha kula SAMAKI!! Haya jamani:- MWISHO WA JUMAMWEMA NA IJUMAA NJEMA NA KULENI SANA SAMAKI!!!

6 comments:

Faith S Hilary said...

Poleeeee samaki poleeee!!! Hahaha! Samaki kakaa vizuri kweli huyo yaani mmh....ngoja niache kumeza mate ila hapo kwenye ugali, kwangu ni mtihani mkubwa...hehe

Simon Kitururu said...

Samaki poa ila shombo la DUH!:-(

Katika huo wimbo lakini azungumzwaye WAFIKIRI ni samaki kama aliye pichani?

emu-three said...

Mhh, nyimbo nyingine zaweza kulenga samaki kumbe zalenga mtu...lakini huyo hapo ni samaki na dada yetu anatutamanisha...

ADELA KAVISHE said...

jamani umenitamanisha my dia napenda sana samaki

Baraka Chibiriti said...

Nyimbo za Taarabu achana nazo kabisa, huwa wana maanisha mambo mangine kabisa hao ndo zao. Usifikiri wanamwimba samaki hapo!

John Mwaipopo said...

wimbo na kitoweo havifanani/haviendani kabisaaa. hao wanamuziki wana lao jambo. mie simooo