Friday, October 15, 2010

NI MIAKA MITANO LEO TANGU BIBI NA BWANA KALUSE WAFUNGE PINGU ZA MAISHA!!

Kaka Shabani Kaluse,Mkewe na Mvulana wao Abraham
Katika ndoa inatakiwa uvumilivu, upendo, maelewano nk. Familia hii leo imefikisha miaka mitano ya ndoa yao na matunda pia tunayaona, si mengine tena bali ni mtoto Abraham. Binafsi napenda kutoa HONGERA nyingi sana kwa siku yenu hii ya ndoa na pia nawatakieni kila la kheri mzidi kupendana na kuishi mpaka vikongwe kabisa na muwe na wajukuu wengiiii. Hakika nafurahi sana kuwa KAPULYA maana unajua mangi mengi kuuliza si ujinga bali ni kujua mengiiiii. Picha nimetumiwa na familia yenyewe zaidi ingia hapa mzee wa utambuzi. HONGERENI SANA KWA KUTIMIZA MIAKA MITANO YA NDOA!!!!!!!!!!!!!!!!!!



4 comments:

Mija Shija Sayi said...

Wanasema ndoa ina matatizo, lakini hii inaonekana haina kabisa. Hongereni sana kwa kutimiza miaka mitano.

**Halafu kumbe Kaka anajua kuchagua...lol!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

halo halooooooh! leo twala ubwabwa...lol!


Da Mija, yawezekana si Kaluse alochagua bali mdada ndo alimchagua...lol!

Markus Mpangala. said...

Kaluse jabali la utambuzi,
Hima chukua hii pongezi,
Maishani daima kuienzi,
Ndoa yako imara anuai,
Mwana Abraham darajani,
Baba na Mama mahabubani,

Shaban bin Kaluse,
Pongezi kiduchu nikupe,
Ndoa isiwe kipupwe,
Asilani binti usimtupe,
Mtunze akutunze
Mahaba yajipambe,
utamu ukolee.
NB: sifa moja niliyoibaini kwa kaka Kaluse ni mtu mwenye msimamo mkali sana, napenda itikadi zake huyu jamaa.

Mzee wa Changamoto said...

Basi ambao hawajawahi kuwa kwenye ndoa watamshangaa Da Yasinta kwa kupongeza "miaka mitano tu".
Kwa kina sie ambao tumeyaona twajua miaka mitano ya ndoa ni zaidi ya kawaida. Ina-streeetch mpaka basi.
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hongereni saaana na kama ambavyo kila siku inaenda na kuweka "msingi" wa ile ijayo, miaka mitano hii na iweke msingi imara wa ile mitano ijayo ili hii na hiyo iungane na kuweka kumi na kumi ijayo ambayo itakuwa msingi wa ishirini ijayo.
Yaani kufupisha hizo blah blah zangu, ni kuwa nawatakia ndoa idumuyo
BARAKA KWENU