Friday, December 30, 2016

FAMILIA YA AKINA NGONYANI IMEPATWA NA MSIBA ....BINTI PHILOMENA HATUNAYE TENA

Majira ya saa nne leo binti yetu Philomena Ngonyani katuacha baada ya kuumwa kwa  kipindi kirefu. Tunamwomba eeehh Mwenyezi Mungu atutie nguvu katika kipindi hiki chote kigumu.
Nitakukumbuka daima Shangazi yangu,

HII IWE PICHA YA MWISHO YA WIKI HII NA LABDA MWAKA HUU 2016

Mara nyingi inasemekana ni wanawake tu huweza kufanya vitu zaidi ya viwili lakini hapa katika picha twaona kinyume....
UJUMBE WA LEO:- Nachukua fursa hii kuwashukuruni wasomaji wote wa MAISHA NA MAFANIKIO kwa kuungana nami kila siku. Maana bila ninyi nisingeweza kuendelea kublog maana hizi zote ni juhudi zenu. AHSANTENI SANA NA TUZIDI KUPEANA MOYO. KAPULYA

Wednesday, December 28, 2016

MANISPAA YA SONGEA:- MAZINGIRA NA WATU WAKE

 Sehemu ya eneo la Msitu wa Matogoro ambalo ni chanzo kikubwa cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Songea


 Wananchi wa Kijiji cha Chikunja Kata ya Matimila Tarafa ya Muhukulu
Wananchi wa Kata ya Kilagano waliokuwa wanafanya shughuli za Kilimo katika eneo la Hifadhi ya misitu
CHANZO CHA PICHA:- HAPA

Tuesday, December 27, 2016

BARABARANI SEHEMU FULANI MKOANI RUVUMA ...JE? UNAJUA WAPI?

Mazingira ...barabarani sehemu fulani mkoani Ruvuma ...unajua ni wapi?....zawadi nono imeandaliwa kwa wa watano wa kwanza kujibu:-)

Monday, December 26, 2016

UJUMBE KUTOKA KWANGU KUJA KWENU KWA KUFUNGA MWAKA HUU 2016.

Kuna wakati unaweza kuwa na furaha hadi unasahau na kujiuliza kama kuna shida hapa dunuani....
Na kuna wakati unaweza kuwa na huzuni/matatizo hadi unasahau  na kujiuliza kama kuna kitu
kinaitwa furaha hapa duniani.....
Yote ni mzunguko wa maisha tunapita milima na mabonde, kwenye miiba na kwenye asali kitu cha muhimu ni kumuomba Mungu na kumshukuru kwa chochote kinachokuja mbele yako

Sunday, December 25, 2016

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE KRISMASI NJEMA..PICHA MKESHA WA KRISMAS

 mtoto Yesu kalazwa holoni
Baraka na amani zitawale katika nyumba zet pia upendo . Leo ni sikukuu ya kuzaliwa/kumbukumbu ya Mkombozi wetu Yesu Kristo. UJUMBE TUPENDANE, NA MUHIMU ZAIDI TUKUMBUKANE.  KRISMAS NJEMA KWA WOTE MTAOPITA HAPA....

Wednesday, December 21, 2016

MAPISHI YA LEO:- PAI YA SPINACHI NA SALADI YA NYANYA

Ni pai spinachi:- unahitaji unga wa ngano vikombe 3 vya chai/3dl tatu, samli 125g, maji vijiko 3 vya mezani. Kisha maziwa vikombe 2/dl 2, na mayai mawili  koroga pamoja  na chumvi pia pilipili manga. Baada ya hapo katakata kitunguu  maji kimoja na kipande kimoja cha kitunguu saumu kaanga ila usiunguze kisha changanya spinachi geuza geuza kidogo.  weka kinyunga kwenye chombo na weka kwa oven dakika kumi. Halafu  weka spinachi na vitunguu halafu chizi/jibini vikombe viwili na mwisho yale maziwa na mayai uliyokoroga pamoja. weka kwa oven uliyoiandaa  kwa joto la 225 kwa dakika 30...Tayari kwa mlo:-)
Usisahau na kasaladi kidogo...mimi nilichagua nyanya tu ila saladi yoyote ni safi tu ....TUKUTANE TENA SIKU NYINGINE.....KAPULYA

Tuesday, December 20, 2016

SALAMU KUTOKA KWETU RUHUWIKO...KAZI YA MIKONO YANGU...

 Nakumbuka siku niliyopanda hili nanasi na mengine nilichekwa sana nikaambiwa nadhani watu wanapanda kama mihogo. Ila sikukata tamaa leo matunda ni haya:-) KAZI YA MIKONO YANGU
Na hapa ni ndizi...  kwa hiyo ndugu zanguni karibuni sana Ruhuwiko ...

Monday, December 19, 2016

SEHEMU FULANI TANZANIA NA ZIWE PICHA ZA WIKI HII

 NDIZI,  NDIZI, NDIZI
Nyumba za kitamaduni ...inapendeza kwa kweli. Je unajua hapa ni wapi?

Sunday, December 18, 2016

NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA-VAZI LA LEO CHUI CHUI:-)

 Leo ni shati la chui chui na sketi nyeusi
Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa juma hili linaloisha siku ya leo. Namwomba azidi kutupa afya wote ili tuweze kuifikia NOELI...JUMAPILI NJEMA KWA WOTE MTAKAOPITA HAPA:-) kapulya

Friday, December 16, 2016

Wednesday, December 14, 2016

HILI NENO, "MWANAUME NI KICHWA CHA NYUMBA," HUWAPA KIBRI SANA HAWA VIUMBE



Kuna jambo moja ambalo hufundishwa na viongozi wa dini mbalimbali, ambalo pia waumini hulihubiri vizuri kila mahali wapatapo nafasi ya kufanya hivyo. Nalo si jingine ni lile la ‘mwanaume ni kichwa cha nyumba,’ ikiwa na maana kuwa mwanaume ndiye mkuu wa nyumba au familia. Suala hili linazungumzwa kama kwamba, mwanaume kuwa mkuu wa familia ni jambo la kimaumbile, lakini pia huzungumzwa kama vile, ukuu huo ni tiketi ya mwanaume kuikandamiza familia au mke. 


Nijuavyo mimi, wanaume wengi kuwa wakuu wa nyumba au familia ni suala la mazoea zaidi kuliko maumbile. Kwa miaka milioni kadhaa, mwanaume amejikuta akiwa ndiye mkuu wa familia. Kutokana na mazoea haya, jambo hili limekuwa kama vile ni la kimaumbile, yaani haliwezi kubadilika au kubadilishwa.



Lakini mbona kuna wanawake ambao ndiyo wakuu wa familia na familia hizo zinakwenda vizuri tu. Lakini vilevile kuna wanawake ambao hawana waume na wanaongoza vyema familia zao. Kwa bahati mbaya kwenye jambo hili, ni kwamba, kumekuwa na msisitizo kuwataka wanawake wawaheshimu waume na siyo wanandoa kuheshimiana. ‘mwanaume ni kichwa cha nyumba, ndiye msemaji wa mwisho. Inabidi aheshimiwe.’ Kuna watu ambao bila aibu huzungumza lugha hii.



Ni kweli wanaume wanahitaji au wanapaswa kuheshimiwa. Lakini siyo wanaume peke yao, bali binadamu wote wanapaswa kuheshimiwa bila kujali wanafanya nini au wakoje. Kwa hiyo siyo kwa sababu ni wasemaji wa mwisho, basi wao ndiyo wanaopaswa kuheshimiwa. Kwa kuamini hivyo wanaume wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kuwakandamiza wake zao na hata watoto. ‘Mimi ndiyo msemaji humu ndani, nimesema sitaki, basi.’ Mara nyingi matumizi ya mabavu kwa namna hiyo hutumika.



Kuna haja kwa wanaume kujua kwamba, kuwa kwao viongozi wa familia hakuwapi ubora wa ziada. Wanawake nao wanapaswa kujua kwamba, kutokuwa kwao wasemaji wa mwisho wa familia, hakupunguzi hata chembe ya thamani ya ubinadamu wao, kwani binadamu na wanandoa wanapaswa kuheshimiana. 
HABARI HII NIMEITOA  KWA MDOGO WANGU KOERO HAPA

Tuesday, December 13, 2016

KUMBUKUMBU...KARIBUNI TUJUMUIKE NDUGU ZANGUNI....

Nimekumbuka mbali  sana enzi hizoooo mwaka 1947. Je nawe kuna  kitu umekumbuka?

Monday, December 12, 2016

SIKU NA WIKI NYINGINE TENA ....AMBAYO TUNAANZIA KATIKA ZIWA NYASA KWETU

Wavuvi wa dagaa wanatua nanga ufukweni tayari kusubiri wateja. Na mimi niliuwa mteja wa kwanza......wahi nawe upate kitoweo:-)

Sunday, December 11, 2016

NAWATAKIENI JUMAPILI HII YA TATU YA KIPINDI HIKI CHA MAJILIO IWE NJEMA...!

NUKUU  "Mpendwa mwana wa Mungu, tukiendelea kwa furaha katika Majilio, leo tunaendelea kulitazama Neno la Mungu kwa furaha ili tujifunze na kuonja upendo wa Mungu kwa njia ya Neno wake. Ni Dominika ya III ya Kipindi cha Majilio, Mwaka C wa Kanisa, tukialikwa kufurahi kwa uchangamfu kwa maana Bwana yu karibu. Kama kawaida Dominika ya III ni Dominika ya furaha, kumbe, furahini katika Bwana. Katika Dominika hii tunatafakari Neno la Mungu pia tukimtazama Mtakatifu Yosefu, Baba mlishi wa Bwana."
JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGU. UJUMBE TUPENDANE!

Thursday, December 8, 2016

LEO JIKONI:- MAPISHI YA MAANDAZI

 
Leo nimepata orodha toka kwa watoto wangu baadhi ya vyakula walivyotamani ...namba moja ilikuwa maandazi...basi nikawa sina ujanja:-) kwa hiyo karibuni .

Wednesday, December 7, 2016

PICHA YA WIKI: VAZI LA KITENGE..SARESARE MAUA

Kwa kweli inapendeza kuona watu wengi wanaenzi vazi hili...ila binafsi ningependa hili gauni liwe ndefu kidogo:-)

Tuesday, December 6, 2016

MANGATUNGU (VELVET BEANS AU COWITCH BEANS) NI CHAKULA KWETU UNGONINI

KWETU UNGONINI TUNAITA MANGATUNGU. Chakula hiki inabidi upike kwa makini sana. Kwanza unachemsha kisha unamenya. Na hapo kazi inaanza unachemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi. Sababu ni kwamba inasemekana kuna sumu ndio maana maji ya mwanzo huwa meusi sana . Kwa lugha ya kiingereza huitwa "velvet beans au cowitch beans"...pia inasemekana:- Mangatungu ni dawa kama viagra, ni kahawa, na ni dawa ya kutibu magonjwa ya nerves kama vile Parkinson disease. Kwa habari zaidi soma http://en.wikipedia.org/wiki/Mucuna_pruriens#Uses
N a baada ya kuchemsha na kumwaga maji zaidi ya mara kumi na mwisho wake matokeo yake huwa hivi  tayari kwa kula...ni chakula kizuri cha asili...

Monday, December 5, 2016

KARIBUNI SONGEA: FAHAMU BAADHI YA MAMBO HALISI YA MJI WA SONGEA

Karibuni Songea Mji wa kitalii:

1. Kuna matuta makubwa ya barabarani Tanzania nzima (bumps) yapo Bombambili ambapo kabla ya
kufika Songea mjini lazima ukutane nayo.

2. Kuna pikipiki nyingi kuliko watu.

3. Kuna matunda mengi ya kipekee kama madonga, masuku, mfudu, mbula, mamvubula na mengine mengi.

4. Kuna mboga nyingi za kipekee kama Mangaukau, linamfusulela, chikandi, likungu, kipele,pitiku(mboga ya maboga), 
mangatungu n.k.

5. Majina mengi ya watu wake ni ya wanyama mfano Komba, Mapunda, Mbawala, Tembo,
simba (Kahimba), Nungu, Nyoka, Matembo, Ngonyani, Nyati, Kobe n.k.

6. Pia kuna ngoma nyingi mf. lizombe/kitoto, madogoli, beta, zilanga, ligambusa, kihoda, mganda, lindeku, 
Mandilo, Chomanga, Tumba, Puyanga.

7. Bila kusahau Dagaa watamu sana (Nyasa) na viazi vitamu kuliko vyote vinavyojulikana kwa jina 
la makaba.

Hiyo ndiyo SONGEA yetu, Mji uliobarikiwa, Chezea Songea yetu weye. KARIBUNI SANA HAPA NI BAADHI TU YA UHALISIA WA MJI HUU.

Friday, December 2, 2016

KANGAZIII:- IJUMAA NJEMA NDUGU ZANGU!

Haya jamani niseme kama mwalimu wa hesabu wa shule ya msingi alivyoitwa MWALIMU MWEZI MPYA ...nilikuwa namaanisha ni mwezi mpya na ni Ijumaa ya kwanza ya mwezi huu mpya na ni mwisho wa juma...nami nawatakieni IJUMAA NJEMA SANA!

Thursday, December 1, 2016

TUANZE MWEZI WA KUMI NA MBILI HUU KIHIVI..PALE UPATAPO UGENI......

 Ilikuwa siku ya furaha sana hii siku ...kama picha inavyojionyesha. Huwa napenda sana kufikiwa na wageni ni raha ilioje...Hawa wageni walitoka Bukoba.


Tuesday, November 29, 2016

JUMANNE HII YA MWISHO WA MWEZI HUU TUBAKI TU KIDOGO HAPA NYASA-MBAMBA BAY-LIULI

 MWONEKANO WA ZIWA NYASA
 WAVUVI KATIKA ZIWA NYSA
NA HAPA NI POMONNDA ROCK  KATIKA KIJIJI CHA LIULI HAPA HAPA NYASA. 

Monday, November 28, 2016

MLO KAMILI WA KWETU NYASA ...NA NDIYO MLO AUPENDAO KAPULYA WENU...!

Kwa vile Nyasa ni maalufu sana kwa kilimo cha MIHOGO:- Basi hapa ni ugali wa mhugo, maharage, samaki na dagaa.  NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA JUMA!

Friday, November 25, 2016

BADO TUPO MKOANI RUVUMA ...NGOMA YA ASILI YA NDUGU ZETU WAMATENGO


Ni ngoma ya uzinduzi wa harusi.... AU SI TUENDELEE TU KUCHEZA NA HII....


MUWE NA SIKU NJEMA. NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA.

Tuesday, November 22, 2016

LEO TUTEMBEE KWETU SONGEA:- TUSISAHAU YALIYOTOKEA WAKATI WA VITA YA MAJIMAJI


Hii hapa ni nyumba ya jiwe  ya SONGEA MBANO ambayo ipo Chandamali katika mlima wa Msamala Songea kwetu.

Monday, November 21, 2016


Leo nimetumiwa huu ujumbe na RAFIKI nami nikaona ni ujumbe mzuri nisiwe mchoyo nikaona niuweka hapa kibarazani kwetu...ukipata wasaa basi soma...

Bwana mmoja maskini sana aliishi na mkewe. Mkewe alikuwa na nywele ndefu za kuvutia. Siku moja mkewe akamwambia bwana huyu akamnununulie chanuo la nywele zake ili azichane zirefuke na kunawili vizuri. Bwana huyu alijibu hana pesa kabisa hata ya kutengenezea saa yake iliyokuwa imevunjika. Mwanamke huyu hakuendelea tena kusisitiza ombi lake. Kesho ilipofika bwana yule akiwa anarejea nyumbani alipitia dukani akaiuza ile saa yake na kununua chanuo kwa ajili ya mke wake. Alipofika nyumbani akiwa na lengo la kumshangaza mkewe  akastaajabu kumkuta mkewe kanyoa. Mke naye kumbe alizinyoa nywele zake na kuziuza kisha akamnunulia mumewe saa mpya. Wote walikuwa na furaha  ya kupendana na kujitoa kwa mwenzie wakajikuta wanalia kwa furaha.
UJUMBE:- KUMBUKA KUPENDA SIO KITU  ILA KITU NI KUPENDA . ILA KUPENDANA NI ZAIDI YA KITU. MPENDE AKUPENDAYE!

Friday, November 18, 2016

NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA JUMA HILI....PICHA YA WIKI!

Kwa wale wanaopenda ulabu ...hivi ndivyo pombe aina ya komoni inavyoanza kutengenezwa....msije mkasema tusubiri mpaka lini.......kuna
n
Hapa ni ulanzi...ni pombe ya kienyeji na ya asili...IJUMAA NJEMA KWA WOTE.

Wednesday, November 16, 2016

Tuesday, November 15, 2016

MAVAZI: VALI LILILOSHONWA KWA KITENGE...TWAPASA KUJIVUNA!

Waafrika/watania tuna haki ya kujivunia vazi la KITENGE NA KANGA ambalo linaweza kubuniwa kwa mitindo mingi sana ya mavazi ebu angalia hili vazi...NIMELIPENDA SANA ningejua wapi ameshona ningeagiza. Kama kunayejua TAFADHALI ANIJUZE.

Monday, November 14, 2016

TUANZE WIKI HII NA KUTEMBELEA HUKO IRINGA KUANGALIA MICHORO YA ASILI...KUMBUKUMBU

Kwenye hili jiwe tunaona michoro ambayo hapo kale ilichorwa kwa ustadi mkuu ni michoro kama ile ya Kondoa.
Hapa ni jiwe Igereka lambalo lipo katika mtaa wa Kihesa Kilolo katika Manispaa ya Iringa Nkoani Iringa. Ukiwa maeneo ya Iringa usikose kutembele...FAHARI YA TANZANIA... JUMATATU NJEMA!

Friday, November 11, 2016

IJUMAA NA MWISHO MWEMA WA JUMA NA NDUGU ZETU WAGOGO...


MUWE NA MWISHO MWEMA WA JUMA .
UJUMBE: Afya sio kula vizuri tu. Afya pia ni kuhusu jinsi ya kufikiri na kusema.

Thursday, November 10, 2016

MICHEZO:NETIBOLI NI MCHEZO NILIOKUWA NIKIUPENDA SANA

Ukitaka mpira ni lazima uutafuta mie nafasi yangu ilikuwa kama huyo mwenye sketi nyeusi...kwa hiyo hapa mchezo mzima upo mikanoni mwako... 
 Kwa hiyo hapa mzuiaji inabidi afanya kazi sana ila kwa hapa naona itakuwa kazi rahisi kwa vile ni mrefu...Netiboli ni mchezo mzuri, kwana kwa afya na pia kwa mazoezi ....na mwisho inabidi uwe mwepesi kukimbikia:-)  Ila mmmhhhh siku hizi  kukimbia ....

Wednesday, November 9, 2016

KUMBUKUMBU:- UNAVIKUMBUKA VITU/VIFAA HIVI?

Kwangu sio vigeni kabisa ndivyo vilivyonipa maarifa yote na pia bado namiliki mpaka hivyi nisemavyo...Nimewahi  kusikia minongòno ya kwamba, hasa mwanaume akimiliki vifaa kama hivi siku hizi basi ajua mke atakimbia.....Swali kwani ni vifaa au mume ndiyo tuwapendao au wanatusingizia tu..Wanawake wenzangu mpo nami?...Eti binti/mwanamke akikuta vifaa hivi kwa manaume, penzi linakufa muda  huo huo....KWELI?

Tuesday, November 8, 2016

KARIBUNI TUJUMUIKE KATIKA MLO HUU WA UHAKIKA

UGALI WA ULEZI, MBOGA MAJANI NA SAMAKI
Hii picha imenikmbusha mbali sana huu ulaji kwa kushirikiana/kuchangia sahani moja na sio kila mtu na sahani yake...Hivi kwa nini hii tamaduni inakufa?

Sunday, November 6, 2016

JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGU KATIKA KRISTU.....


Kwaya Mt.Maria goreth chuo kikuu cha ushirika wimbo wa Dela dela. Wimbo huu kwa kawaida imeibwa na wangoni na kuchezwa katika ngoma ya lizombe lakini kumbe hata kwa maombi yawezekana nimeFURAHI SANA.

Friday, November 4, 2016

NAPENDA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA MWISHO MWEMA WA JUMA HII YA KWANZA YA MWEZI WA KUMI NA MOJA ...

:-) EMBE nimetumiwa hizi na rafiki nia yake kubwa ni kunitamanisha na kweli nimetamani  maana hapa nilipo mate yanachuruzika tu....MWISHO MWEMA WA JUMA!

Thursday, November 3, 2016

ILI MRADI VIIVE:- MCHAGUA JIKO SI MPISHI!!!!

 Hii nadhani wengi wetu tumepitia na bado tunaendelea kutumia hasa uwapo sehemu  kama vile mstuni kwa matembezi. Vyombo kama hivi ni muhimu sana kuwa navyo vipo vingi sana SIDO tena ni imara zaidi kuliko plastiki....
Hapa ni ubunifu wa kisasa ambao hata sijawahi kufikiria ...ila najiuliza kama yawezekana kupika mchele hapo au maji ya chai tu?
Au tu upo katika kuchimba labda shimo huku ukichoma taka labda na ghafla njaa inapiga hodi,,, je Ungejaribu?

Wednesday, November 2, 2016

JE WAKULIMA WA VIJININI WANATHAMINIWA?

Tanzania Iringa:- Ndugu zanguni! katika picha tunamwona bibi kikongwe akiwa na mzigo mkubwa wa kuni huku katika mkono wake wa kulia uliopata kufanya mamia ya shughuli ukiwa umeshika jembe, ni dhahiri kuwa bibi huyu ni mtu anayejali kazi zinazompatia riziki yake kwa kuwa dhana ya jembe ni kilimo na kuni ni chakula lakini serikali inawapa nguvu gani akina bibi kama hawa ili kuboresha kilimo chao mfano nyenzo za kilimo au mikopo.

wakulima wengi maeneo ya vijijini hulalamika kuwa serikali haiwapi msaada na matokeo yake wakulima hao hujikuta wakifanya kilimo duni, kila mwaka huwa hivyo tu. Je? mwaka mpya ujao (2017) inaweza kuwa ndo fursa ya serikali kuwainua wakulima.?