Tuesday, January 10, 2012

LEO TUANGALIE VITENDAWILI VYA KISWAHILI:- KITENDAWILI…..

1. Haukamatika wala haushikiki.........
2. Anataga huku akitambaa...................
3. Ninapompiga mwanangu watu hucheza...................
4. Ubwabwa wa mwana mtamu........................
5. Kuku wangu katagia mayai mibani.................

12 comments:

ray njau said...

Vitendawili vigumu kuliko mawe!Hapa nimeshindwa nami nakupa mji nenda Songea.

Goodman Manyanya Phiri said...

Nimekipenda kitendawili: "Ninapompiga mwanangu watu hucheza..................."

Sijui maana ya kitendawili.

Nafurahia lakini ukweli ndani yake kwamba labda kila unapompiga mwanao maadui zako hufurahia ujinga wako.

Ukweli ni kwamba ziko namna nyingi za kumlea mwanao kwa nidhamu bila kumpiga.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

duh....nimepita kapa maana nikitoa majibu watu wanaweza kuvunjika mbavu...sasa sijui utawalipia gharama za kwenda huko India!!!

Swahili na Waswahili said...

Hahhahahahhaa kaka Manyanya umeniacha hoiiiiii,jibu NGOMAAAA, Nipe thawadi dada Yasinta!!!!!Mbarikiwe wooote!

sam mbogo said...

Majibu- 1 jibulake ni mwanga.
- 2 ushanga
- 3 ngoma
-4 matandu/ukoko
-5 nanasi
kaka s

Mija Shija Sayi said...

Nadhani kuna haja ya kukumbushana zaidi, Yasinta viongeze..

Kaka Manyanya kula tano kwa tafsiri...

Kaka Sam duh! Yaani umezipatia zote!!

Yasinta Ngonyani said...

Wapendwa ndugu zanguni kwa kweli inabidi tukumbushane daima maana naona watu wameanza kusahau ...ila Dada Rachel na kaka Sam mmepata hapo kwenye jawabu la Ngoma na kaka Sam hapo kwenye jawabu la Nanasi ...jaribuni tena mshindi zawadi nono imeandaliwa:-)

Yasinta Ngonyani said...

Naona ni afadhali nitoe majibu au je kuna mtu anataka kujaribu? Maana naona kama vitendewili vilikuwa vigumu kweli au?

Yasinta Ngonyani said...

Haya majibu yake ni haya:-
1. Moshi
2. Mboga
3. Ngoma
4. sungizi
5. Nanasi.
Nadhani siku nyingine mtaweza tu labda nifanye hii kila wiki kuchemsha bongo kiduchu:-)

king jr. said...

Weka vitendawili vingine naomba

Vansh Chavda said...

1. Moshi
2. Boga
3. Ngoma
4. Usingizi
5. Nanasi

obat vimax said...

vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg