Sunday, January 29, 2012

WIMBO HUU NIMEUIMBA TANGU NILIPOKUWA MDOGO ILA ULINIPOTEA LEO NIMEUPATA:-SISI WANA WA DUNIA...


Yaani najisikia raha, roho yangu imekuwa kama vile ni mpya kwa jinsi utamu wa wimbo huu unavyopendeza. Kaka Baraka upo maana wewe najua unaupenda sana wimbo huu:-)MNAPENDWA WOTE..KWA MARA NYINGINE TENA JUMAPILI NJEMA!!!

6 comments:

Baraka Chibiriti said...

Yaani Dada Yasinta, umenipa zawadi kubwa sana....asante sana tena sana. Napenda sana hata mimi nikiwa mdogo na wenzangu tuliuimba sana wimbo huu, umenikumbusha mbali sana. Na jinsi ninavyompenda Mama mpendwa Maria, nimejisikia faraja sana.

Asante sana Dada Yasinta, kwa video hii, kama Yasinta wajina wako wa kwenye wimbo huu....ubarikiwe sana.

Baraka Chibiriti said...

Hapa nilipo nauimba wimbo huu kwa furaha sana.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Baraka yaaani hujui tu ni kiasi gani nilivyofurahi yaani hapa naimba utadhani ndo niliutunga. Raha yake siwezi kuielezea....Ahsante aliyeurekodi wimbo huu

Baraka Chibiriti said...

Ni wimbo mzuri sana, na wenye maana kubwa sana (hasa kwa wote wanao mpenda Mama Maria)....katika ujumbe wake. Kuna dada mmoja nilisoma nae shule ya msingi tukiwa darasa la saba wiki 2 kabla ya kufanya mtihani wa mwisho, alifariki ghafla....tulilia sana tena sana, na siku ya mazishi yake tuliimba sana wimbo huu, maana alikuwa anaupenda mno. Kila wakati darasani aliuimba, mwalimu wa dini alipofika darasani, ilikuwa lazima aanzishe wimbo huu....kwa wanafunzi wengine ikawa mpaka kero, lakini wengi tuliupenda sana. Yaani leo nimemkumbuka sana huyo dada, na Mwenyezi Mungu aendelee kumpumzisha mahali pema peponi.

Mimi binafsi huu wimbo sikuchoka hata kidogo kuuimba, wengine walilalamika, lakini kwasababu nilikuwa Monita wa darasa, pia Kilanja Mkuu wa Shule, nilimwambia aindelee tu....yeye huyo dada alikuwa mwimbaji mzuri sana wa shule yetu, na kwenye bendi ya shule alikuwa mwongoza bendi.
Kwakweli nimekumbuka mbali sana na kufurahi sana....asante sana dada Yasinta.

Swahili na Waswahili said...

Walisema tusali tusali rozari..........Ohh dadake kweli leo umetuamulia,Wimbo huu sasa kila duka la Mchaga,Mchana na Usiku kwenye vipindi vya Dini duuh.Ubarikiwe sana na Uwe na wakati mwema wewe na Familia,bila kukusahau kaka Chibiriti na Woooooote!!Mungu ni Pendo.

ray njau said...

Salamu za wikiendi kutoka kwa babu wa jukwaa la maisha ni mikikimikiki kwenda mama maisha na mafanikio pamoja na wadau wote wa kibaraza chake maridhawa.
Asalaam aleykum!!