Tuesday, January 31, 2012

ULIKUWA UNAJUA MATUNDA HAYA YANAITWA MABUNGO?.....

......na yanapatikana ZANZIBAR. Je? kuna anayejua kama yanapatikana sehmu nyingine? kuna dada mmoja alikuwa huko na alionja na akayapenda. Binafsi sijawahi kuonja. Natumaini nitapata jibu kwani nimeulizwa swali hilo na nimeshindwa kujibu na nikaona hapa nitapata tu jibu..Natanguliza shukrani....

13 comments:

Swahili na Waswahili said...

Mimi nayajua Mabungo sasa sijui kama ni hayo au ni jina tuu,dar tunakula sana hasa watoto wa shule weweee, dadake tunakata juu na kuweka chumvi au pilipili ya unga,Pia unaweaza kutengeneza Jisi,Duuuhhh Mate yananitoka hapa da'Yasinta naona nawe umeanza Ugomvi,ngoja nikimbieeeee

Swahili na Waswahili said...

nilikuwa namaanisha Juisi wapendwa.

Anonymous said...

Hata mie nayajua! tumeyala sana wakati tukiwa primary school makurumla wee hivyo hivyo twakat juu twaweka pilipili na chumvi yummy yummy! Pia yanapatikana Tanga nadhani yapo kipwani zaidi,juice yake ni tamu sana.

EDNA said...

Aaah hayo nayajua ,nimekula sana dar ila sijui yanatoka wapi.Mate yananitoka.. naungana na Da Rachael naona umeanza ugomvi wako teh teh teh.Siku njema mdada.

ray njau said...

Zanzibar ni njema na atakaye aende.
Juisi ya mabungo iliyotengenezwa kwa uliotukuka na kuhanikizwa na marashi ya karafuu ndiyo maisha na mafanikio ya Zanzibar.
@Rachael hujakosea ila huyaamini madokezo yako.
@Edna maneno yamekuwa mengi hadi unasahau uliyoyasema.
@Mficha jina naye kasema yake na kuondoka bila kuagana na wenyeji.

ray njau said...

Kunradhi:
Juisi iliyotengenezwa kwa ufundi uliotukuka.

Anonymous said...

amabungo hata huko bukoba yapo matamu sana na ule ugwadu wake

chib said...

Kumbeee.....

Yasinta Ngonyani said...

Kumbe, halafu naona karibu wote mmekula/onja kasoro mimi tu:-) Swali hivi embe ngóngó ndizo hizo? Rachael mie wala sio mgovi si umeona Edna kasema ww ndio nr.1...LOL

Anonymous said...

embe ngongo sio hizo zipo tafauti kabisa,zenyewe kama zina makambakamba ndani

Anonymous said...

Labda pale Ubungo, pameitwa hivyo labda ni kwa ajili ya haya, labda palikua yanauzwa mengi mabungo na ubungo inamanisha ubongo mmoja, hmmm hata sijui, nimejaribu kufikiria tu kwa mtazamo wangu, wala sina uhakika.

Anonymous said...

Labda pale Ubungo, pameitwa hivyo labda ni kwa ajili ya haya, labda palikua yanauzwa mengi mabungo na ubungo inamanisha ubongo mmoja, hmmm hata sijui, nimejaribu kufikiria tu kwa mtazamo wangu, wala sina uhakika.

Ausal said...

Mi Yasinta nayajua mabungo ni
hayo hayo uliyoyatoa katika picha yanaliwa sana na watoto hata watu wazma pia yana ukakasi fulani ndio maana upenda kuweka na chumvi, wengine huwa wanatengenezea juice, yanapatikana hata Morogoro sehemu za milima ya Uluguru.