Friday, January 13, 2012

JE? KUNA TOFOUTI KATIKA PICHA HIZI MBILI?

Akina dada wamekaa mduara na nadhani wapo katika shindano fulani...maana inaonyesha katika mavazi yao..


........................na hapa ni kundi la watoto wamekaa kwa macho yangu mimi ni kama vile wamekaa na wanasikiliza hadithi?....wewe je unaonaje? IJUMAA NJEMA KWA WOTE!!!

6 comments:

sam mbogo said...

Hawa juu kweli ni mkao wa ki miss,hawa vijana picha ya pili, wako jandoni niwatoto wa kiume wakimsinkiliza ngariba wao. tofauti nikuwa hawa mamiss wako ufukweni mwa bahari na hawa vijana/watoto wako kwenye nyasi/porini kamasikosei wakisikiliza mawaidha kutoka kwa kiongozi wao.kaka s.

Swahili na Waswahili said...

Mimi naona kama hawa wa ju wana Amani/furaha.lakini hawa wa Chini kama hawana raha/Mawazoni au hawakohuru...........Mbarikiwe wooote duuuhh kaka wa Mimi Sama mwana wa Mbogo, Ngariba wale wakizamani hivi bado wapo au ndiyo mambo Hospitali?

Yasinta Ngonyani said...

Mimi naona tofouti ni kwamba hiyo picha ya juu mpiga picha alisimama tu bila kupima vizuri maana unaona miguu/mviringo ulivyo.
Na hii picha ya chini ya watoto mpiga picha alisimama upando huo huo ila alisimama kwenye kitu na ndio maana unaona watoto wengine vichwa vimekatwa ila mviringo wao ni mzuri zaidi. Na nadhani ndio nia kubwa ilikuwa.

sam mbogo said...

yasinta,VICHWA VIMEKATWA,umeviona wapi lugha yakao tata dada yangu.kaka s.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Sam! angalia vizuri katika hao watoto unaona vichwa vyao au sura zao wote? Lugha tata kaaaazi kwelikweli:-)

Sara Chitunda said...

kwa mimi ninavyoona ile picha ya kwanza wadada wamenyoosha miguu na mikono wameirudisha nyuma wote inawezekana wako kwenye shindano fulani lakini picha ya pili watoto wametengeneza mduara wakiwa wamenyoosha miguu na wengine wamekuja kidogo na mikono kila mtu na staili yake ni kama wanasikiza kwa makini kitu fulani wanachoambiwa. kwa kujaribu.