Showing posts with label Furaha. Show all posts
Showing posts with label Furaha. Show all posts

Friday, September 21, 2018

NAWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA...HAYA TUFURAHI PAMOJA NA KIPANDE HIKI CHA NGOMA...



Tuwukeee tuwukeee kamwimbo katamu sana. Natamani kuungana  nao na kucheza ila nabaki kucheza peke yaangu....NAWATAKIENI MWISHO WA WIKI HII UWE WENYE FURAHA NA AMANI! KAPULYA WENU

Monday, March 26, 2018

USITAFUTE PESA TAFUTA FURAHA

Katika maisha kitu kigumu kuliko vyote kukitafuta sio pesa bali ni furaha. Pesa ni ngumu kuitafuta kwasababu kila siku tunaipoteza katika kuitafuta furaha. Pesa humaliza matatizo na matatizo humaliza pesa. Inawezekana hata aliyezigundua  alikufa na madeni, sioni sababu ya kufa kwa sababu ya kutafuta maisha, bora uzima.  Pesa sio kila kitu. Inaweza kununua nyumba lakini haiwezi kununua familia, inaweza kununua  kitanda lakini haiwezi kununua usingizi, inaweza kunuua saa lakini haiwezi kununua muda. Pesa inaweza kununua vitabu lakini haiwezi kununua akili. Na maskini sio yule tu ambaye hana bali hata yule aliyenazo lakini anazitaka zaidi. Tafuta furaha kila siku usisubiri mpaka muda maalumu ndio uwe na furaha. Kila siku hapa duniani ni siku  maalumu. Na kwa taarifa yako sio mwenye pesa tu anayeweza kuhamisha milima hata fukara kapuku kama wewe na mimi. Pesa sio kila kitu bora furaha, inaweza kununua madaraka lakini haiwezi kununua heshima. Inaweza kununua damu lakini haiwezi kununua uhai, inaweza kununua dawa lakini haiwezi kununua afya. Pesa  haiwezi kununua mapezi.
CHANZO.- NILITUMIA NA RAFIKI KMA VIDEO/SIMULIZI NAMI NIMEUGEUZA KAMA MADA..

Monday, September 4, 2017

TUANZE WIKI HII NA NENO FURAHA: HIVI KWANINI KUN SIKU MTU HUKOSA FURAHA?


Ndiyo...Furaha inatokana na ridhiko la ndani la mtu bila kuhusisha vitu vya nje. Mtu akishajua namna sahihi ya kuipata furaha basi hataipoteza kamwe. Yoyote anaeipoteza furaha huyo anakuwa anaitafuta nje yake kwenye mazingira ya nje.....
Lazima atakuja kuikosa siku moja kwasababu mazingura ya nje sio rafiki sana na binadamu kwasababu hubadilika badilika....

Mfano kuna wakati wa jua, masika na kiangazi za kawaida...
Kama umepanga kwenda kulipwa mapato yako fulani na umewekeza furaha yako kwenye hela halafu mvua ikanyesha lazima tu furaha yako itapotea....
Kuridhika kwa ndani kuna maana ya kujikubali jinsi ulivyo bila kutegemea hali ya nje iko namna gani...
Utakapo jikubali namna ulivyo kamwe hutajutia wala kukosa furaha hata siku moja

Sunday, January 15, 2017

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE...AMANI NA FURAHA ZITAWALA KATIKA NYUMBA ZETU!

Zipo furaha nyingi duniani, watu wanafurahia kufaulu mitihani, kupata ajira, mtoto, kuoa na kuolewa, kuwa na mali nyingi na mambo mengi kadha wa kadha. Lakini hebu tuone furaha iliyo kuu kuliko zote, "Ndipo wale sabini  waliporudi kwa furaha wakisema hata pepo wanatutii, YESU akawambia msifurahi kwa vile pepo wanawatii BALI FURAHINI KWA SABABU MAJINA YENU YAMEANDIKWA MBINGUNI. Kumbe furaha kuu ni jina lako kuwa limeandikwa katika kitabu cha uzima. Luka 10:17-20".  JUMAPILI NJEMA.

Monday, February 29, 2016

WIKI ILIYOPITA SIKU YA JUMANNE YA TAREHE 23/2 NILIFIKIWA NA MGENI DADA MERABY...

 Baada ya kupata chai/kahawa  kidogo tukawa tunaongea kuhusu makabila yetu kwa vile mimi nilikuwa nafanya utafiti wa neno MAMA kwa makabila yetu mbalimbali na kwa vile yeye ni MHAYA basi akanisaidia...:-) Ebu niona basi  kama umeandika ipasavyo....
 ...na hapa amechukua karatasi niliyoandika kuangalia kama nimeandika inavyotakiwa......
Hapa kwa pamoja dada Meraby na mimi Mama Maisha na Mafanikio kwa pamoja tunapia  orodha ya neno mama kwa makabila mbalimbali:-
Ilikuwa ni siku ya furaha sana katika Kaya yetu. Tuliongea mambo mengi sana hasa kuhusu vyakula na hasa ndizi/matoke....

Sunday, February 28, 2016

NI JUMAPILI YA TATU YA KWARESMA:- UJUMBE... MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO....

Mungu akikuacha katika hali fulani:-
Basi mshukuru wala usilalamike. Kwani yeye ndiye akujuaye zaidi. Pia usidhani kama maisha yamekamilika kwa mtu yeyote.
Kuna mwenye nyumba lakini hana gari, kuna mwenye gari lakini hana watoto, kuna mwenye watoto lakini hana pesa, kuna mwenye pesa lakini hana afya, kuna mwenye afya lakini hana kazi na kuna mwenye vyote lakini hana AMANI wala FURAHA. MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO.  Nami naanza kwa kusema AHSANTE MUNGU KWA KILA JAMBO.

Friday, December 25, 2015

NAWATAKIENI WOTE KRISMASI YENYE UPENDO, AMANI, FURAHA NA BARAKA TELE!!

Kamera ya Maisha ya Mafanikio ilikuwa mitaani lao na imepata picha hii ya mtoto Yesu..Hapa Papa Franciskus akimkabidhi mtoto Yesu  ili aende akalale holini ....Mwokozi amezaliwa. Na sasa hebu tusikilize mwimbo huu ambao ni zilipendwa wale wote wenye umri kama mimi na zaidi nadhani watakuwa wanaukumbuka..KARIBUNI.

YESU NDIYO SABABU YA KUWA NA HII SHEREHE YA KRISMASI...KWA HIYO BASI TUWE NA KRISMASI YENYE UPENDO, AMANI, FURAHA NA BARAKA....KRISMASI/NOEL NJEMA.

Thursday, May 7, 2015

CHAGUO LA MAISHA NA MAFANIKIO KWA WIKI HII NI HILI HAPA......

Nimependa usemi huu MAISHA POPOTE, MUHIMU FURAHA. Kuna siku moja mtu mmoja aliniuliza hivi ninyi watu mtokao AFRIKA kwanini kila wakati mnaonekana watu wa furaha tu? Na pia ni wakarimu hata ukiwa na kidogo au unaishi hali ya chini lakini mnaonekana ni wacheshi tu Je? kuna siku huwa mnanuna? Nakumbuka,  nilimjibu hata kama nikinuna, Je ndiyo nitafanikiwa? Akanijibu ni kweli...sasa ninyi wenzangu katika hilo swali mngejibu vipi? KARIBUNI TUJADILI.......

Friday, July 18, 2014

UJUMBE WA LEO !!!

Ni kwamba katika maisha ipo hivi: Pale unapowafurahisha  wengine, ndipo furaha yako inazidi kuongezeka. Kwa hiyo pale upatapo nafasi jaribu kumfurahisha labda rafiki, au wale walio karibu nawe.
PAMOJA DAIMA!!!

Monday, November 25, 2013

TUANZA JUMATATU HII NA SWALI HILI KUTOKA KWA KAKA BWAYA ...KUHUSU MAISHA NA FURAHA!!!

Kama mnakumbuka mwezi uliopita niliweka picha hii hapa kibarazani na baadaye kulitokea na maoni. Na baadhi ya maoni aliyotoa msomaji mmoja ambaye ni kaka Bwaya ambaye alikuwa ameadimika kwa muda mrefu na sasa yupo nasi tena. Nachukua nafasi hii kumkaribisha Kaka Bwaya......Haya na maoni yenyewe yalisomeka hivi;-
Bwayasaid...
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waishio katika maisha yanayoonekana kuwa duni, ndio wenye furaha zaidi. Mfano ni hawa. Swali: kwa nini? Naomba tusaidiane kujadili swali hili kwa pamoja....JUMATATU NJEMA!!!

Thursday, February 14, 2013

Happy Valentines Day/Upendo Daima kwa siku ya wapendanao /Alla Hjärtans Dag

VALENTINES DAY.!!!!
Leo ni Valentineday/siku ya wapendanao/alla hjärtans dag. Sio kama siku zote watu hawapendani HAPANA bali ni kuhamasisha watu wazidi kupendana . Kwangu mimi ina maana kubwa kwani nimekuwa mwanaharakati bora wa Upendo kwa jamii haijalishi nimefika kiwango gani . Nashukuru hata kama sijafika robo. Nakuomba nawe shiriki kutangaza Upendo Duniani. Upendo ulimwenguni kote! na Heri ya siku ya wapendanao kwa wanablog wooooooooooooote! HAPPY VALENTINES DAY.!!!!

Monday, January 14, 2013

SIKU HIZI SITAZISAHAU ..HATIMAYE TUMEKUTANA USO KWA USO..

Yasinta na Kaka Albano Midelo Ruhuwiko/Songea Ilikuwa ni mwaka mpya huu 2013 kwa mara ya kwanza kaka Albano Midelo alikuja kututembelea kwetu Ruhuwiko yeye ni mmiliki wa blog ya Maendeleo ni vita
Yasinta na kaka Shaban Kaluse wakiwa Jangwani beach Dar es Salaam Haikuishia kukutana na kaka Midelo tu, pia kwa mara ya kwanza nikakutana na kaka yangu wa hiari kaka Shaban Kaluse Mzee wa utambuzi. Ilikuwa ni furaha ya ajabu sana kukutana na kaka huyu ...kwa kumfahamu zaidi unaweza kumsona hapa
Yasinta na Dada Ester Ulaya wakiwa wametulia ndani ya Savanah Lodge Sikuishia kukutana na hao akina kaka tu ..Nilipata bahati ya kukutana na Dada Ester Ulaya pia nadhani safari yangu safari hii ilikuwa yenye baraka sana kuweza kukutana na ndugu hawa..hapo tupo sehemu tuliyofikia Savanah Lodge ambayo ipo maeneo ya Banana..kuweza kumfahamu dada huyu ingia kwenye blog yake Rular and Urban
Na hapa ni picha ya pamoja hicho kiti kisicho na mtu ni cha mpiga picha ambaye ni mr. wangu, anayefuatia ni mmiliki wa hotel ya Savanh Lodge, halafu anafuatia kaka Kinunda, na halfu anafuatia ni mume wake dada Ester Cathbert Angelo Kajuna na ni mmiliki wa blog HABARI NA MATUKIO na pembeni yake ni mwenyewe dada Ester na halfu mimi nipo ila sijaonekana hapo na bila kusahau kaka Chacha naye tulikuwa naye ila alifika baadaye na katika kunogewa na hadithi tukasahau kupiga naye picha.Na halafu nisisahau tulikuwa na dada mkuu msaidizi katika maongezi yetu yaani kwa simu..si mwingine tena ni mwenyewe mwanamke wa shoka Dada Mija. Yeye anapatikana zaidi hapa. Tuulikuwa na wakati mzuri sana kwa ujumla.

Saturday, November 24, 2012

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWEPO/ISHIA IJUMAA YA JANA TULIPATA WAGENI TOKA NYUMBANI TANZANIA!!!

Hakika siku ya jana ilikuwa siku ya furaha sana kwetu. Kama mzaa vile baba wa nyumba akanipigia simu na kusema nina wageni hapa andaa msosi twaja. Nikafanya hivyo muda si mrefu wakatua nyumbani. Wageni kutoka nyumbani tena NYUMBANI kabisa. Kutoka kushoto ni kaka Ludovick Chahally, katikati ni dada Elizabeth Mahinya wao ni mke na mume..na halafu mwisho ni mimi mwenyewe kapulya:-) Nimesisitiza kuwa wanatoka NYUMBANI kwa vile dada Elizabeth anatoka SONGEA pia MNGONI..tuliongea kingoni we acha tu:-) Ni furaha sana kuonana na watu wa nyumbani na kubwa zaidi mnaotoka mkoa mmoja.

Nawatakieni wote JUMAMOSI NJEMA SANA. NDUGU SI LAZIMA AWE BABA NA MAMA MMOJA. HILO MIE NAAMINI KABISA. TUPO PAMOJA DAIMA.

Saturday, July 28, 2012

NDIYO NIPO NANYI ...JUMAMOSI NJEMA WANDUGU,,,!!!


Likizo hii nimeona niwe hapa hapa si kwenda mbali sana kwa hiyo hizi siku nilizopotea nilikuwa hapa summer house ni mahali pazuri kwa kupumzika na kutafakari...wavuvi hao wanakwenda kutafuta kitoweo baba na kijana wake.....
...ila inakuja wakati lazima kurudi kuvuna mavuno hapa ni mboga za maboga, Bei rahisi fungu moja mia,,,:-)


 Hapa ni ni sehemu ambayo watu wengi wanapenda kwenda na watoto wao au wao tu kufurahi. Ni Skandinavian sehemu kubwa ya "water land" SKARA SOMMAR LAND.
..Bado tulikuwa kule ilikuwa ALHASMIS ..baba na kamanda wake wakiendesha magari kama kucheza----
NAWAKUMBUKENI SANA NA TUPO PAMOJA,,,,KILA LA KHERI!!!!

Saturday, April 21, 2012

JUMAMOSI NJEMA JAMANI!!! WANDUGU WANGU:)

Tazama  jinsi ilivyo veme, ndugu wakae pamoja kwa umoja Zab 133:1
Michezo huleta burudani na kujenga miili yetu. Itusaidie pia kuleta umoja na mshikamano kati yetu; badala ya sokomoko, chuki na fitina.

Thursday, March 29, 2012

POROJO YA LEO !!!

Bwana mmoja karudi nyumbani toka kazini amechoka ile mbaya, akaingia ndani na kujitupa kochini ili aangalie TV. Akamwambia mkewe:-
- Niletee bia, karibu inaanza .
-Mkewe akapumua na akampa bia.
- Baada ya dakika kumi na tano akasema :-
-Nipe bia nyingie maana karibu inaanza.
Mke wake akamwangalia kwa kuchoka choka lakini akampa bia nyingine:
Alipokuwa amemaliza ile bia baada ya dakika kadha akasema:-
- Nipe bia nyingie, kwani itaanza dakika yoyote ile.
-Mkewe akachukia na kumpigia kelele, akasema.
- Yaani huna kazi nyingine ya kufanya jioni hii, zaidi ya kukaa na kuangalia TV na kunywa bia?
Wewe huna lolote isipokuwa ni mvivu, mwanaharamu mkubwa.......
Yule bwana akapumua na kusema:-
-Sasa imeanza.......
Je wewe pia unajiuliza kama mimi ni nini kilichoanza?

Wednesday, February 22, 2012

NI NINI KINAFANYA MAISHA YAWE NA FURAHA?

NI JUMATANO NA NI KILE KIPENGELE CHA MARUDIO MBALIMBALI LEO NI MARUDIO YA November 25, 2008 NDANI YA MAISHA NA MAFANIKIO.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
Hakuna kitu kitakacho weza kufanya maisha ya yako/yangu kuwa na furaha kama hatutakubali kujipokea mwenyewe na kupanga mfumo mzima wa maisha yetu. Wengi tunajikuta katika mahangaiko na mafarakano katika uhusiano iwe wa ndoa, au marafiki wa kawaida. Je? ume/tumesha wahi kukaa chini na kujadili kwa nini hili litokee, na je ni kweli kwamba katika haya yote hakuna jibu kwa matatizo haya.

Mpenzi msomaji katika kuchunguza hilo nimegundua kwamba tulio wengi hatuipi nafasi mioyo yetu kuchagua kile kilicho halali kwa matakwa yetu. Bali tunafuata mwelekeo wa mapendeleo yetu na tunaacha nafasi muhimu ya moyo kuupa nafasi ya kuchagua kilicho cha thamani zaidi ya furaha ya siku moja, ambao tulio wengi tumekuwa tukililia au kujionea fahari. Hapa nina maana kwamba kama mwanamke ameahidiwa kuolewa basi atataka haja hiyo itekelezwe wakati hana uhakika wa kweli kama mpenzi wake anampenda kwa dhati.

Kuna misemo isemayo kwamba:- mwanamke anapotoa uamuzi wa kuolewa anafanya hivi akitegemea kwamba mwanamume anayeolewa naye atabadilika baada ya wao kuwa mke na mume; poleni sana wanawake tumepotea, badili mwelekeo olewa na mtu mwenye mapenzi ya dhati na ambaye yupo tayari kutoa dhamiri yake kwa ajili yako.

Na kwa upande mwingine, Mwanamume anamwoa mwanamke na kumleta ndani ya nyumba akitegemea kuwa hatabadilika; Mungu ndiye ajuaye kuwa mwanadamu ni kigeugeu, sasa atutendee nini ndipo tulidhike? Naamini wanawake wengi wanavumilia katika mahusiano ila wapo ambao nao ni wasumbufu, kwa sababu tu ya tamaa, na wengine hujikuta wanabadilika kwa kuwa maisha ni magumu ndani ya ndoa, na wengine umaskini, wanataka kupata chochote au kuiga ufahali wa wengine.

Swali linakuja je? unafikiri kukamatana ugoni na kuonyeshana kwenye vyombo vya habari kwamba nataka kumshikisha adabu ajifunze ni njia sahihi ya kutatua matatizo katika jamii kama watu hawatatumia njia ya kuiweka wazi mioyo yao kwa kile wanachokipenda na kukitamani?

Ni changamoto kwamba kweli tulichokiamua pamoja na kukubaliana basi kiheshimiwe na kuthaminiwa kama kweli humpendi mwenzako sema tangu mwanzo liwe wazi tusitake maisha ya mtelemko kwa kuwa unayemwoa ana nafasi nzuri na wewe unavimba kichwa kwa sifa ya kazi yake na sio mapenzi ya kweli. Wewe utakuwa msaliti.

Maisha ya ndoa ni kuwa tayari kwa ajili ya mwingine wakati wa raha na shida, kwa furaha na amani bila majuto.

Tuesday, February 21, 2012

HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA BINTI YETU CAMILLA!!!

Ni miaka kumi na nne iyopita siku ya jumamosi tarehe 21/2 saa sita kasoro dakika tatu alizaliwa binti Camilla. Kwa pamoja twapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumlinda binti Camilla. Pia tunamshukuru Mungu kwa kutupa nguvu sisi wazazi za kuweza kumpa Camilla malezi yaanayotakiwa.HONGERA KWA SIKU YA KUZALIWA BINTI YETU!!!!

Saturday, December 17, 2011

MANENO YA BUSARA AMBAYO NIMEAMBIWA ....

Moja ya furaha si lazima kwa yule ambaye ana kila kitu, lakini anaweza kuwa mmoja ambaye anajua jinsi ya kufanya kwa ubora kila kitu kilicho karibu yake.
.............JUMAMOSI NA JIONI NJEMA KWA WOTE...

Wednesday, November 9, 2011

TABASAMU!!!

Kama kawaida ni ile JUMATANO YA KIPENGELE CHA MARUDIO na leo Kapulya ameona tuangalia hili neno TABASAMU na nimeikuta hii mada hapa. KARIBUNI.

Tabasamu ni njia rahisi isiyo na gharama ya kubadilisha mwonekano wako.Tabasamu ni kitu gani? Tabasamu ni dirisha linaloonesha nini kilichopo ndani ya moyo wa mtu, ni kitu kinachonyoosha kila kitu kuwa katika mstari ulioonyoka. Ukiwa mtu wa kutabasamu unakuwa na marafiki wengi na ukiwa mtu wa ndita watu huanza kukukwepa.

Kila unapotabasamu kwa mtu yeyote ni ishara ya upendo, ni zawadi kwa yule mtu ni kitu kizuri. Tabasamu ni kusema karibu, tabasamu ni uwezo ambao unaweza kuifanya siku ya giza kuwa siku ya nuru, huweza kufanya pasipo na upendo kuwa na upendo. Inagharimu misuli 17 tu kutabasamu na inakugharimu misuli 43 kuwa na ndita kwa nini ujizeeshe mapema? Amani huanza kwa tabasamu!
Huwezi kuvaa ukapendeza bila kuvaa tabasamu, huwezi kuwa mrembo bila kuvaa tabasamu huwezi kuitwa beautiful one kama hujavaa tabasamu huwezi kuitwa handsome kama hujavaa tabasamu period! Tafiti zinaonesha mtu anayetabasamu huwezi kuongeza miaka mingi katika maisha yake. Hata hivyo watoto hujifunza kutabasamu kutoka kwa wazazi wao.
Umemaliza kusoma hapa, sasa zamu yako kutabasamu halafu kicheko!
AHSANTENI SANA NA TUONANE TENA PANAPO MAJALIWA JUMATANO IJAYO!!