Sunday, March 30, 2008

Machi 30,2008 HALI YA HEWA/PASAKA

Naam! wasomaji nafikiri mmesoma blug yangu kuhusu pasaka. kama hujasoma basi chukua fulsa na usome. Kwa kweli nakuambieni ama kweli watu wana mila na desturi. nimeshuhudia sio kula mayai tu kama nilivyosema isipokuwa kuyapaka rangi tofauti baada ya kuchemshwa. Haya sasa najua sehemu nyingine kama Afrika (TZ) pasaka imesheherekewa na jua/joto. Sio hapa kuna baridi na pia theruji ilianguka. Samahani kidogo nimeingia kwenye hali ya hewa hii yote ni kwa sababu sikutegemea kutakuwa na baridi kali hivi. Nafikiri ni kwa sababu hali ya hewa imebadilika kwani hii theruji ilibidi iwe krismas sio sasa. Lakini sasa inaonekana kuna mabadiliko. Ngoja nirudi kwenye Pasaka tena, kama nilivyosema. jumamosi kuu ndio sikukuu kubwa hapa sio Jumapili (pasaka kwa sisi ) nina maana watu wengi pamoja namimi tunajua kuwa jumapili dio PASAKA.
Katika blogu ya mdogo wangu KARIBU NYASA amenikumbusha mbali sana. Yaani ameniacha hai kabisa. Maana inaonekana huko Pasaka ilikuwa nzuri sana wamatengo na ngoma zao, wangoni/wamanda na zao pia vinywaji nk. mpaka natamani.

Na; Yasinta Ngonyani

Monday, March 17, 2008

machi 17,2008 pasaka

Haya wasomaji naona sasa pasaka inakaribia.Nimekaa na nimeamua niwaeleze kidogo mila na desturi wakati/kipindi hiki cha pasaka huku ninakoishi ni tofauti sana na huko nyumbani.ngoja nianze kuwaeleza kuliko kuanza kuwachosha. Ni hivi alhamisi kuu ni kama kawaida au nimesahau sijui yaani watu wanakwenda kazini kama kawaida. Ijumaa kuu baadhi ya watu hawafanyi kazi na JUMAMOSI KUU hapa ndio sikuuu kubwa sio kama huko nyumbani sikukuu ni jumapili. Haya sikiliza sasa siku ile ya jumamosi watu wote ni lazima kula mayai kadiri unavyopenda bila mayai basi si pasaka tena. Halafu kitu kingine siku hii ya JUMAMOSI KUU watoto wadogo wanavaa kama wazee wa zamani. Na pia wanakuwa na barua kwenye vikapu na wanapita kila nyumba na kubadilishana na pipi. Ni mila yaani ni kama jambo la kutakiana pasaka njema. Kwa hiyo kipindi kama hiki kila mwananchi inabidi awe na pipi au matunda kama huna huna hivyo viwili basi uwe na hela. mwanzoni nilishangaa lakini sasa nimezoea.

Na; yasinta Ngonyani

Saturday, March 15, 2008

marchi 15, 2008 Baba mama na watoto

Nilikuwa nimebanwa na kazi kidogo:- Haya sasa wasomaji hapa duniani watu tumeumbwa tofauti kwa kila kitu. kwani mimi nilikuwa nadhani watu wote tuna mawazo sawa hasa katika jamii. Kama nilivyosema katika blogg ya vipi tunalea watoto wetu. Sasa hii ya baba, mama na watoto inanisumbua sana akili yangu, ukizingatia vipi sisi waafrika tunavyolelewa. kwa kweli mimi inanipa shida sana, ni vigumu kuelewa kwa nini dunia nzima wasiishi kama sisi waafrika. yaani kuwatembelea wazazi,ndugu na marafiki mara nyingi. Yaani huku watu wanasamini zaidi pesa kuliko jamii. Utakuta mtu anamwacha mama yake baba yake mzazi kwenye nyumba ya wazee ili atunzwe na watu wengine kwa sababu yeye ana shughuli nyingi. NImewauliza mara nyingi je wangeacha hao wazazi wako leo ungekuwa wapi? Lakini wao wanasema kila mtu na maisha yake. Na nimejiuliza je hii ni haki au vipi? Kwani najua sisi Afrika tunaweza tukaishi pamoja ukoo mzima na tunatunzana. Ndugu wasomaji mnasemaje mnaonaje upi ni utaratibu mzuri.

Na; Yasinta Ngonyani

Toa maoni

Saturday, March 8, 2008

8/3 jumamosi Hali ya hewa

Hali ya hewa hapa sweden kwa kweli mara nyingine unaweza kushinda ndani tangia asubuhi mpaka jioni bila kutoka nje kwani ni baridi mmno. Ni mabadiliko makubwa sana kwa mtu atokaye kwetu afrika. Ukiangalia kwetu afrika tunavaa nguo nyepesi yaani sio nzito na sio viatu vikubwa. Mtu unaweza kuvaa ndala na unaendelea na safari. Lakini huku ndugu zangu ni ngumu sana kuvaa hivyo:, unahitaji nguo, koti kubwa, suruali pia viatu nk. Joto/jua tunaliona kuanzia mwezi huu wa tatu, mwezi huu tunaliona jua kwa muda wa masaa tu, tutaendelea hivi mpaka mwezi wa tano sita hapo ndo tutaliona jua. Na pia kutakuwa na joto kidogo kama umewahi kufika Makambako au Njombe ni sawa kabisa miezi hii mitatu. Kwa hiyo mara nyingine unaweza ukakaa na kutamani nyumbani. Nikikumbuka kuvaa gauni na kuvaa viatu au ndala bila soksi natamani sana nyumbani. Nyumbani ni nyumbani hata kukiwa porini au mnasemaje?

Na;Yasinta Ngonyani at 16.42

Toa maoni yako