Saturday, March 15, 2008

marchi 15, 2008 Baba mama na watoto

Nilikuwa nimebanwa na kazi kidogo:- Haya sasa wasomaji hapa duniani watu tumeumbwa tofauti kwa kila kitu. kwani mimi nilikuwa nadhani watu wote tuna mawazo sawa hasa katika jamii. Kama nilivyosema katika blogg ya vipi tunalea watoto wetu. Sasa hii ya baba, mama na watoto inanisumbua sana akili yangu, ukizingatia vipi sisi waafrika tunavyolelewa. kwa kweli mimi inanipa shida sana, ni vigumu kuelewa kwa nini dunia nzima wasiishi kama sisi waafrika. yaani kuwatembelea wazazi,ndugu na marafiki mara nyingi. Yaani huku watu wanasamini zaidi pesa kuliko jamii. Utakuta mtu anamwacha mama yake baba yake mzazi kwenye nyumba ya wazee ili atunzwe na watu wengine kwa sababu yeye ana shughuli nyingi. NImewauliza mara nyingi je wangeacha hao wazazi wako leo ungekuwa wapi? Lakini wao wanasema kila mtu na maisha yake. Na nimejiuliza je hii ni haki au vipi? Kwani najua sisi Afrika tunaweza tukaishi pamoja ukoo mzima na tunatunzana. Ndugu wasomaji mnasemaje mnaonaje upi ni utaratibu mzuri.

Na; Yasinta Ngonyani

Toa maoni

1 comment:

MARKUS MPANGALA said...

Mmh dada Yasinta ama kweli unatoa fikra ambazo ni muhimu katika ujenzi wa jamii za kiafika.Hata mimi inanipa shida aina ya maisha unasimulia hapa kwani nadhani kuna mambo ambayo jamii za ulaya zinashi katika njia potofu labda tokana na namna walivyoikuta na wanavyoishi na hali hiyo lakini naamini njia zao za maisha kama hivyo mimi nashindwa kukubaliana nao na niweke tu kwamba sikubaliani na mfumo huo kwani duniani tupo kwa ajili ya wengine hivyo kumwacha mzazi alelewe na wengine huku mwenyewe ukiwa na uwezo huo ni naamini kwa waafrika tuendeleza mila zetu kama hii ni nzuri sana