Sunday, November 29, 2015

MIMI "KAPULYA" NA DADA YANGU ANNA TWAPENDA KUWATAKIENI MWANZI MWEMA WA MAJILIO

Ndani ya migolole ntu na dada yako. Tumependeza eeehh-:) Wote kama tunavyojua majilio:- ni majuma manne ambayo ni kama kifananisho cha miaka elfu nne ambayo Wakristo hujiandaa kukumbuka siku aliyozaliwa Yesu  Kristo. Amina.

Friday, November 27, 2015

Monday, November 23, 2015

TUANZE JUMATATU YA LEO NA PICHA HII NA IWE PICHA YA MWEZI.....

Ni wasomi ambao ni Taifa la kesho, wakiwa wamevalia "kisomi zaidi" Najaribu kuwaza kama hapo mchakamchaka utaenda salama kweli? Au wenzangu unasemaje? Tuliangalie hili jambo kwa pamoja!!

Saturday, November 21, 2015

UJUMBE WA LEO TOKA KWA KAPULYA WENU......

Napenda kwatakieni wote Jumamosi njema. Panapo majaliwa tutaonana katika pitapia zetu au sivyo wandugu-:).

Wednesday, November 18, 2015

KATIKA DUNIA MAJI NI MUHIMU SANA KWA UHAI WA BINADAMU KAMA TUONEVYO KATIKA PICHA HII...

Akina baba hawa:- WanataFuta maji kwenye chanzo- Ni mradi wa maji ya mtiririko Kijiji cha Liganga. Picha nimeipata katika KALENDA 2015

Monday, November 16, 2015

POMBE SI MAJI....NA WALA SI RAFIKI ILA POMBE NI HATARI KATIKA MAISHA YETU.....


Karibu wiki  mbili  zilizopita nilishuhudia kisa hiki cha kusikitisha ambacho sitakisahau katika maisha yangu. Na kimekuwa fundisho katika maisha yangu. Ilikuwa siku ya  jumatano ya tarehe 5/11/2015, majira ya saa mbili asubuhi. Kulikuwa na mkusanyiko wa wafanyakazi ambao walitakiwa kuwa kwenye mafunzo (kozi). Sasa kwa bahati naweza nikasema bahati  mbaya dada mmoja jina nalihifadhi ila tumwite Maria. Alitoweka ghafla pamoja na bosi bila "wengine" kujua nini kimemkumba  dada Maria.

Lakini baada ya muda habari zikaja ya kwamba kuna wafanyakazi wenzake walipokuwa wakiongea na  Maria , wao waligundua harufu ya kinywa cha Maria ilikuwa inanuka pombe. Nao hawakuishia hapo, wakapeleka ripoti kwa bosi. Na hicho ndicho kilikuwa kisa cha Maria kutoweka ghafla. Kilichoendelea, Maria alipelekwa sehemu ili kuhakikisha kama kweli alikuwa na pombe katika mwili/damu yake. Majibu yalionyesha ni kweli Maria alikuwa na pombe mwilini. Siku ya Maria ilikuwa ni kitendawili alirudishwa nyumbani hakuweza/hakuruhusiwa kuhudhuria ile kozi  siku ile. Na mbaya zaidi ile siku ilipotea bila kulipwa alikatwa mshahara wake.

Niliwaza sana na kumfikiria dada Maria na nikaishia kusema ama kweli sheria kama hizi zingekuwepo dunia nzima :- Basi maendeleo yangekuwepo. Nikawaza  nchi nyingi zingekuwa na maendeleo sana kama zingefuata sheria zilizowekwa. Nikaanza kukumbuka nilipokuwa msichana mdogo nilivyokuwa nikiwaona baadhi ya walimu walikuwa wakienda kupata kupata "chai ulanzi" badala ya chai ile saa nne.  Je? hao vinywa vyao vilikuwa vikitoa harufu kiasi gani? Lakini hakuna sheria yoyote ilichukuliwa  na kama ingekuwa ikichukuliwa sheria je? Wangapi wangepoteza kazi zao?

NENO LA LEO:- NDUGU ZANGUNI POMBE SI MAJI NA WALA HAZITATUI MATATIZO. ISIPOKUWA ZINAHARIBU AFYA NA MWISHO ZINAUA.

Friday, November 13, 2015

MAJINA YA WANAUME NA SIFA ZAO KATIKA MAPENZI......JE? ULIJUA HILI? KARIBU......

1. Andrew-mapenzi ya tamthiliya
2. Nicolas-muongo
3. Albert-domo zege ila mjanja mjanja
4. Mathias-anapenda mwanamke kwa muda mrefu
5. Joseph/Josephat/yusuph-kicheche
6. Jeryson-anapenda mademu ila wanawake wanamkataa
7. Shadrack-anapenda sifa kwa mademu
8. Richard-ana wapenzi wengi ila msiri
9. Mathew-anapendwa na wanawake ila domo zege
10. Thomas-anapendwa na mademu ila hajatulia
11. Prosper-hajui habari za mapenzi
12. Fidelis-mtaalam wa kutongozea mademu wenzie (kuwadi)
13. Aaron-maneno mengi ila vitendo sifuri
14. Costantine-wanapenda kutongoza hovyo ingawaje wana mpenzi mwaminifu
15. Elvis-handsome ila hapendwi na mademu
16. Edward-serious sana kwenye mapenzi
17. Moses/Mussa-mwepesi kutongoza na mwepesi kuwacha
18. Ally/Elly-wasiri sana kwenye mapenzi
19. Mohammedy-anapenda watu waliomzidi umri
20. Nickson-wakiingia kwenye mapenzi wanatendwa vibaya
21. Alpha-wanapenda sifa kwa wanawake ili wapendwe
22. Jimmy-wana mapenzi ya kejeli
23. Elias-wanapenda mademu ila wanaogopa kuwaambia
24. Frank-huyu mpole wanawake wanajitongozesha wenyewe
25. Joachim-hana habari na mademu,anaamini ipo ataoa tu
26. Omary-anapenda achape tu atembee
27. Steven-hana habari kabisa na wanawake ila ana bahati ya kupendwa
28. Gerald-mpole na antulia na mpenzi mmoja kwa mda mrefu
29. Elisha-anapenda wanawake wanaochukiwa katika jamii
30. Benard-akipenda kapenda
31. Juma-hawa kazi yao ni kuchafua wanawake wa mtaani na jamii inayozungukwa

32. Kassimu- anapend utukufu na kusifiwa hata na mkewe
33. Khalid -msumbufu na anapenda kupedwa kuliko kupenda wanawake
34. Daniel-anawivu sana mjanja na anapenda kujua mambo yaliyojuu ya uwezo wake.
35. Said-hajui kupenda na huwa anatamaa hasa kwa bint weupe.
36. Rajabu-mgumu kumuamin mwenza wake.
37. David-Kupenda kujionesha mbele ya wanawake kwamba anauwezo mkubwa hata kama hana.
38. Farid-Mpenda wanawake warefu wenye mwanya na shepu.
39. Rama-hupenda kusikilizwa yeye tuu na anapenda wanawake wenye makalio makubwa hasa wanene.
40. Seleman-anapenda ngono.
41. Issa -huwa na msimamo hasa katika maamuzi yake hat kwa mwenza wake
42. Fadhili- vitu vyake ni vya siri saana na hata mwenza wake ni ngumu kujua
43. Charles -Hapend kudumu katika mahusiano na hupenda kuwa pek yake
44. Karimu- hupenda kuwa na wanawake weupe
45. Laurence-hunyanyasika kwenye mahusiano hata huweza kulia hovyo
46. Masoud- anajua kujali na kuheshimu ndoa yake ila mkali sana.
47.Hamad-mpole pia hapend kutoa siri zake kwa mwenza wake pia hupend kunyenyekew na mpenz wake
48. Hasani -hupenda kupewa kuliko kutoa hata kwa wenza Wap
49. Alen-hupenda kulaumu hata kwa jambo dogo na hupend wanawak weupe
50. Luka- wanapenda kwa mda ukijichanganya utaumia ukiwa nae.
51. Jafari- Hupenda wake za watu

Thursday, November 12, 2015

NDUGU ZANGU ULE MSIMU WA KUANZA KUANDAA MASHAMBA UMEFIKA KWA HIYO JEMBE BEGANI....

Twendeni kuandaa mashamba/ sisi wangoni tunasema (KUSANGILA) yaani maandalizi. Ila nawaombeni hakuna kuchoma moto... kwani ni kuharibu ardhi. Atakaye chelewa anarukiwa matuta:-)

Tuesday, November 10, 2015

TUNAPOISHI MAISHA YA WENGINE NA KUSAHAU YETU!!!

Maisha ya binadamu hapa duniani yanaanzia pale ambapo natoka kwenye tumbo la mama yake, japokuwa inawezekana kabisa binadamu alianza kabla ya hapo lakini kwa hapa duniani tunaanza kumhesabu kuwepo pale ambapo anatoka kwenye tumbo la mama yake na ndio maana umri wake unaanza kuhesabika kuanzia siku hiyo.

Binadamu huyu anapokuja hapa duniani kwa njia ya kuzaliwa wenyeji wake wa kwanza kabisa ni wazazi wake na ndugu zake wa familia hiyo kwa maana ya kaka na dada zake kama watakuwepo, hawa wenyeji wake wa kwanza ndio ambao wanaanza kumuelekeza na kumuonesha namna ya kuishi hapa duniani, kwa bahati mbaya sana ni kwamba hawa wenyeji kama wana mitazamo mibaya kuhusu maisha na dunia kwa ujumla ndivyo ambavyo mgeni huyu nae atayachukulia maisha ya hapa duniani kwa namna hiyo hiyo kwasababu wenyeji wake wamemuelekeza hivyo na kwasababu yeye ni mgeni basi hatakuwa na namna ya kupingana nao kwakuwa hajui lolote kuhusu maisha haya na dunia kwa ujumla.

Kimsingi makala yangu hii itaegemea sana hapo ili kuweza kuelezea kile ambacho ninataka kukielezea leo, wenyeji wetu hawa mara nyingi kama sio zote wametuaminisha na kutufundiosha mambo mengi sana ambayo yanakuja au yamekuja kutuumiza kwenye maisha yetu, kwanza kabisa kuna mambo ya aina mbili katika maisha yetu hapa duniani, nitajitahidi kuelezea kwa lugha rahisi kabisa ili niweze kueleweka zaidi.
1: Mabaya
2: Mema
Japokuwa kimsingi mambo yote haya yanategemea namna mtu mwenyewe anavyoyachukulia au kutafsiri baya na jema lakini bado haiondoi ukweli kuwa yote hayo yapo, kwa bahati mbaya au nzuri karibia binadamu wote tunayafasiri mambo haya kwa namna inayofanana hivyo tunajikuta kama ni matatizo basi tunakuwa na yale ya kufanana.

Wataalam wa masuala ya malezi wanasema kuwa binadamu anapokuwa na umri wa kuanzia mwaka 0 hadi 6 pale ndipo anapokuwa anaanza kujifunza na kuelewa mambo kwa kiwango cha juu sana kwenye mawazo yake ya kina, binadamu tuna mawazo ya aina mbili, kuna yale ya kawaida na yale ya kina ambapo ndipo "uhalisia" wa maisha yetu unajengwa, hili nitalielezea siku nyingine kwa kina, sasa basi wakati mtoto huyu anaandika mambo haya kwenye ubongo wake ambao unakuwa ni "mweupe" au kwa lugha nyingine tunasema uko mtupu kabisa mtoto huyu au binadamu huyu mpya anakuwa anaanza kujenga kitu kinachoitwa tabia.

Wataalam wanasema kuwa atakaeweza kuja kufuta kile ambacho mtoto amejifunza kwenye umri huo ni yeye mwenyewe tena kwa juhudu hasa maana sio kazi ndogo, katika kipindi hiki ndipo wengi wetu tunaharibikiwa au kuharibiwa na ndio kiini cha karibu kila tatizo katika maisha yetu, hata namna unavyoiona dunia na kuichukulia na namna unavyoyachukulia mambo chanzo chake ni huku, lakini pia kuna kipindi kingine ambacho binadamu huyu anaweza kujifunza ambacho ni cha miaka 7-18, inadaiwa kipindi hiki hakina nguvu sana kama kile cha utotoni japokuwa hata hiki nachoi kinaweza kumfanya mtu kuwa na tabia fulani lakini mara nyingi wanasema wataalam hawa kuwa msingi wa haya yote ni kipindi kile cha umri wa mwaka 0 hadi 6.

Tunapokuwa tunalelewa katika kipindi hicho tunafundishwa kuyapenda zaidi mambo hasi au mabaya kuliko yale chanya au mazuri, unaweza kushangaa au kuanza kukataa, lakini usijali maana nitakueleza kwa mifano pia.
Mfano:-
Hebu chukulia umerudi nyumbani jioni halafu ukafika nyumbani kwako ukakuta taarifa kwamba jirani yako, yaani mliepanga nae nyumba amepita kwenye uchochoro huko njiani alipokuwa anakwenda kwenye shughuli zake na kuokota fuko la hela limejaa kweli kweli....

Baada ya kupata taarifa hii, kwanza utauliza ni kiasi gani na baada ya kupewa jumla ya fedha utapata wivu na baada ya kuona tu huna la kufanya utaishia kumpongeza alieokota na kusema "una bahati sana wewe", hautafikiria kama na wewe unaweza kuja kuokota fuko lile la hela na hata mtu akikuambia kuwa na wewe uwe unapita vichochoroni unaweza kukutana na fuko la hela unaweza kumchika sana mana hauamini kama inaweza kukutokea maana unajua na unaamini ni vigumu.

Lakini wewe huyo huyo siku nyingine ukirudi na ukakutana na taarifa kuwa kuna mpangaji mwenzako mwimngine ambae alipita kwenye barabara fulani kisha akakutana na vibaka na kumkaba kisha wakampora kila kitu, utaingiwa na huruma na utampa pole, baada ya hayo utaingiwa na hofu sana...

Hofu hiyo haitasababishwa na kitu kingine chochote isipokuwa utaamini kabisa na wewe kuna uwezekano mkubwa sana wa kuja kukutana na tukio kama alilokutana nalo mpamgaji mwenzako huyo, kama kuna mtu akikuambia usipite barabara ile aliyopita jirani yako maana kuna uwezekano wa kukutana na vibaka na kuporwa utaona ni ushauri wa maana sana na utaamini kabisa hili linawezekana kukutokea wewe.

Ndivyo ilivyo,wakati tunakua tuliaminishwa hivyo kuwa yale mabaya ndio yanaweza kututokea sisi lakini mazuri hayawezi kututokea sisi hao hao, aina hii ya imani au fikra imejengeka kwentu tangu tukiwa watoto wadogo na tumerithishwa kutoka kwa wazazi wentu na jamii yetu hivyoi kuikwepa ni kama haiwezekani mpaka utakapokuja kujifunza utambuzi na kujua matatizo haya.

Tatizo hili la kimalezi linakuja kuzaa tatizo lingine kubwa sana ambalo ndio msingi wa makala hii na tatizo hilo ni la kuja kuishi maisha ya wengine huku sisi tukiyaacha maisha yetu.

Je ni kwa namna gani hili linatokea? Hebu soma kisa hiki cha kweli kabisa halafu utanuelewa tu......

Niliwahi kupanga nyumba moja kipindi fulani huko nyuma na dada mmoja hivi ambae alikuwa na rafiki yake mmoja ambae alikuwa ameolewa, hebu tuchukulie kuwa huyu dada niliekuwa nimepanga nae nyumba moja alikuwa anaitwa Anna na huyu aliekuwa ameolewa alikuwa anaitwa Rebeca....

Anna alikuwa ni rafiki mkubwa sana wa Rebeca na walikuwa wanashaurina mengi sana, Anna alikuwa hajaolewa kama rafiki yake, huyu rafiki wa Anna alikuwa anaishi kwenye ndoa ya mateso sana maana mumewe alikuwa ni mfujaji wa hela na mlevi lakini pia alikuwa ni mtu wa kubadilisha wanawake sana,Rebeca alikuwa akipata kipigo karibu kila siku kutoka kwa mumewe na kila kitu alikuwa anamsimulia rafiki yake Anna

Anna alikuwa ni kama mfariji wa Rebeca kwenye mateso ya ndoa yake ile,baada ya muda Rebeca alianza kuugua maradhi ya moyo na pia alianza kupata matatizo ya miguu na baadae alianza kulazwa mara kwa mara,rafiki yake alijitahidi sana kwenda kumsalimia kila alipopata muda na baada ya mwaka mmoja wa kuugua Rebeca alifariki dunia akimuacha mumewe na mtoto mmoja wa miaka 6

Baada ya msiba Anna aliendelea na maisha yake kama kawaida lakini alikuwa akisema hana hamu ya kuolewa kwasababu ya mateso aliyokuwa anayasikia na machache kuyashuhudia aliyokuwa anayapata rafiki yake ambae kwa wakati huo ni marehemu, lakini haikupita muda mrefu rafiki yake ya kiume Anna ambae pale nyumbani alikuwa mwenyeji na nilifahamiana nae pia maana alikuwa akija pale mara kwa mara aliamua kumuoa Anna. Anna alionesha kusita sana lakini baadae aliamua kukubali na ndoa ilifungwa na baadae Anna alihamia kwa mumewe.....

Maisha yalianza lakini baada ya miezi minne mumewe Anna aliachishwa kazi baada ya kampuni aliyokuwa anafanyia kazi kufilisika, alirudi nyumbani na kuanza harakati za kutafuta kazi nyingine, lakini huyu jamaa alianza kulalamika tabia ya mkewe kutomuamini haswa pale anapokuwa amechelewa kwenye harakati zake za kutafuta kazi maana kuna wakati alikuwa analazimika kwenda mbali kidogo na pale walipokuwa wanaishi kutafuta kazi.

Mumewe Anna alikuwa anasema mkewe alikuwa hampi hata hela ya nauli alipokuwa anataka kwenda kuhangaika kutafuta kazi na alikuwa anasema kuwa mkewe huyu alikuwa anasema kuwa akimpa hela atakwenda kuzinywea pombe na kuwahinga wanawake, huyu jamaa alishangaa sana maana hajawahi kunywa pombe na alikuwa anajiuliza sana kitu gani kinachomfabnya mkewe kufikiria hivyo,pia anasema hakuwa mtu wa wanawake pia na alikuwa akishangaa sana sababu ya mkewe kuhisi hivyo.

Aliendelea kumpuuza na kuhangaikia kutafuta kazi na wakati akiwa hajapata alikuwa akifanya vibarua vya hapa na pale ili kupata hela ya matumizi madogo madogo ambayo hakuwa akiipata kutoka kwa mkewe japokuwa alikuwa akifanya kazi iliyokuwa inamuingizia kipato kikubwa sana tu.

Kuna wakati ulikuwa unaibuka ugomvi miubwa sana kati ya Anna na mumewe kwasababu Anna alikuwa kimtuhumu jumewe kuchelew maksudi kwasababu alikuwa akitumia muda na vijihela vya vibarua kuhonga wanawake ma kunywa pombe.jamaa alikuwa anakasirika na ulikuwa ukiibuka ugimvi mkubwa sana mara kwa mara, taratibu ndoa yao ikaanza kupata ufa mkubwa sana na ikafikia wakati kukawa na mikwaruzano kila siku huku Anna akimlaumu mumewe kwa kuwa na wanawake wengi.

Mumewe huyu alikuwa anafahamiana na kijana mmoja ambae alikuwa mara nyinbgi wakienda wote kutafuta kazi maana kijana yule alikuwa amemaliza masomo yake ya elimu ya juu, kijana huyu alikuwa anashangaa sana sababu ya mkewe huyu jamaa kumtuhumu mumewe kuwa na wanawake kwasababu hajawahi kusikia huyu jamaa [mumewe Anna] kuzungumzia wanawake wengine achilia mbali kuwa nao.

Ndoa ya Anna ilifikia tamati baada ya miaka miwili tu ya ndoa hiyo na waligawana kila kitu huku Anna akiwa anaondoka kwenye ndoa hiyo akiwa na mtoto mdogo........


Ukitazama kwa juu juu huwezi kuona kiini cha tatizo la ndoa ya Anna, lakini hapo utaona kuwa Anna alikuja kuyaishi maisha ya marehemu rafiki yake, hapa badala ya kuyachukulia maisha ya rafiki yake kama shule yeye aliyachukulia kuwa yake.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya kuyachukulia matukio yanayotokea maishani mwetu kama shule na kuyachukulia yetu, mtu anaevuka barabara kwa mfano, huku akijiona kama mtu ambae atagongwa na gari, huyo ana uwezekano mkubwa sana kugongwa na gari kwasababu atababaika kila akivuka barabara na kupoteza umakini kitu kitakachomfanya agongwe kirahisi sana.

Lakini mtu anaevuka barabara hukua akijua kuna kugongwa na kulichukulia hilo kama suala la kumfanya ajue kuwa akiwa makini hawezi kugongwa na kuchukulia matukio ya watu kugongwa na magari kama shule kwake huyu atakuwa na utulivu wa hali ya juu na utulivu huo utamsababishia umakini mkubwa na kumfanya asibabaike na kufanya uwezekano wa kugongwa na gari kuwa mdogo sana au kutokuwepo kabisa.

Anna aliona maisha ya Rebeca ni maisha yake pia na akayachukua kama yalivyo kwenda kuyaishi kwa mumewe ambae masikini ya Mungu wala hakuwa na tabia kama za shemeji yake Anna [mume wa Rebeca] Anna alimuona mumewe kama ni mume wa Rebeca na akawa na hamaki na kuhisi mabaya kila wakati kumhusu.

Matatizo haya leo na sisi tunayo,chochote ambacho kinaweza kumtokea mtu fulani na kikawa ni kibaya basi tunakibeba na kukifanya chetu na matokeo yake tunaishi maisha ya wengine huku yetu tukiyaacha kabisa.

Tunapokuwa tunatafuta kazi tunakuwa tunatafuta huku tayari tukiwa tumekosa kazi hizo kwasababu fulani alishatafuta akakosa.

Tunapokuwa tunatafuta wachumba tunatafuta wachumba wa aina fulani au wenye sifa fulani kwasababu kuna hiki na kile kilishawatokea akina fulani, hatutafuti wachumba ambao sisi tunawataka isipokuwa tunatafuta wachumba wanaotofautiana na wachumba wa akina fulani maana tumeyabeba maisha yao na kuyafanya yetu.

Tunapokuwa tunasoma ni hivyo hivyo, yaani sisi hatupo kabisa, tumefundishwa kuyapenda mambo hasi na yakiwatokea mambo hasi wenzetu basi tunaamua kuyabeba na kuyafanya yetu, lakini yale mazuri hatuyachukui na tunaamini sio yetu kabisa.....

Malezi yetu yanatuumiza sana, tunaishi kwa matukio, hatumuamini Mungu tena na tunaona fulani kafilisika tunaona na sisi tuko njiani kufilisika, tunaona fulani kaachika kwenye ndoa kwasababu za mateso na sisi tunaona tuko njiani kuachwa na tunaanza kujilinbda na kuwa na tabia za ajabu ajabu.....

Ifikie wakati tujifiunze kuwa sisi ili tufanye maisha yetu kuwa mazuri na yenye furaha....

Habari hii nimetumiwa na Peter Shirima [King] 0786256380. Baada ya kuisoma kwa makini nikaona si vibaya  nikiiweka hapa Maisha na Mafanikio  ili wote tupate elimu hii. AHSANTE PETER!!.

Saturday, November 7, 2015

NAWATAKIENI KILA LA KHERI KWA KILA MTAKACHOKIFANYA....KWA UJUMBE/USEMIHUU!!!

Changamoto  kubwa katika maisha  ni kujigundua wewe ni nani/nini........
Na kikubwa zaidi pia cha pili ni kuwa na furaha kwa ulichokipata/gundua........

Wednesday, November 4, 2015

HAPA NI VITABU VYANGU NILIVYONUNUA HIVI KARIBUNI. ..BOOKSHOP YA PERAMIHO

Hakuna kitu kizuri kama kununua vitabu. Hivi ni vitabu vyangu kilivyonunua hivi karibuni....

Sunday, November 1, 2015

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE JUMAPILI HII YA KWANZA YA MWEZI WA KUMI NA MOJA....NA WIMBO HUU:- AMANI YA TANZANIA NI NGUZO IMARA......


Namshukuru Mungu tangu uchaguzi umeanza mpaka leo kumekuwa na AMANI na nazidi kumwomba Mwenyezi Mungu amani na utulivu vizidi kuendelea. Pia namshukuru Mungu kwa kutulinda na kutuepusha na magonjwa makubwa. Sisi sote ni ndugu na watoto wa baba mmoja kwa hiyo tupendane na tukumbukane.....Kapulya!