Wednesday, October 31, 2012

TUTEREMKE KIDOGO MPAKA SONGEA MJINI SASA:- TATIZO LA MAJI NA PIA MAFUTA KUADIMIKA!!!

Tatizo la maji Songea mjini, ndoa moja ya maji shilingi 500....
 
Na hapa ni madereva wa pikipiki katika foleni ya mafuta hapa ni kituo cha mafuta cha Kisumapai. Ni kwamba sasa imefikia mafuta yanatolewa kwa mgao Songea yetu....Natumaini matatizo haya yataisha karibuni kwani vitu hivi vyote ni muhimu sana katika maisha ya binadamu.

Tuesday, October 30, 2012

SIKU YA MAHAFALI KATIKA SEKONDARI YA WILIMA/MADABA/MATETEREKA=SONGEA!!!!

Kutoka kushoto ni Meneja wa shule ya sekondari Wilima mzee Lucas Mayemba, katikari ni Mwl.Paul Mgaya wakati sisi tunaishi hapa alikuwa  mkuu msaidizi.  Hapa wapo katika jengo la utawala katika shule hiyo na mwisho hapo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Songea Bw. Rajabu Mtiula
 
 Mmoja wa Wahitimu akipokea Cheti cha kuhitimu kidato cha nne....Ni furaha ilioje kuweza kufika hapa tena ingwa kipicha. Nimefurahiiiiii sanaaaaa hasa kuwaona mzee Mayemba na  Mgaya PHD......Hapa ndipo nilipoanzia MAISHA YANGU. Picha http://mwambije.blogspot.se/ nakushukuru sana uliyepiga picha.

MIKUMI NATIONAL PARK/MBUGA YA HIFADHI YA WANYAMA MIKUMI 2011 MWEZI WA SITA!!!

 Jamani subirini kwanza sisi tupite...Nyani/tumbili hao walivyojua kuziba njia
 Hakuna mnyama mzuri kama twiga...habari jamani!!!
Tulipata bahati ya kumwona Nyati  pia mnyama asemekanaye mwenye hasira kuliko wote..Kwa mbele ni hawa Funo hawa hukosi kuwaona ukifika /pita Mikumi

Monday, October 29, 2012

HUYU NDIYE YASINTA NGONYANI!!!

Nimeamka leo na mawazo mengi sana kichwani mwangu kuhusu huyu mdogo wangu wa hiari Koero Mkundi. Sijawasiliana naye kwa muda sasa nafikiri yupo salama. Baada ya kufikiri sana nikakumbuka mada hii nikaona ngoja niiweka hapa ni kumbukumbu kubwa sana kwangu.

Yasinta Ngonyani, Picha kwa hisani ya Maisha Blog
Ni binti halisi wa kitanzania, ingawa anaishi ughaibuni lakini hujivunia asili yake na utaifa wake, ni binti pekee aliyejitolea muda wake kuwaelemisha watu wa rika zote bila kujali rangi, kabila, itikadi, taifa wala jinsia.

Binti huyu si mjivuni na hupenda kubadilishana mawazo na watu mbali mbali, na pia hupenda kufuatilia habari za nyumbani kwao alikotoka na haoni tahayari kuongea lugha ya kwao. Daima hujitambulisha kwa jina la asili ya kwao na huona fahari kutumia jina hilo.

Binti huyu hakuona ajizi kuwajuza wanae asili ya kwao japo wamezaliwa ughaibuni, amekuwa msitari wa mbele katika malezi ya wanae ili kuhakikisha wanae hao hawajitengi na asili ya aliotoka yeye.

Si mchoyo wa ushauri na kupitia makala zake aziwekazo kibarazani kwake amekuwa ni msaada kwa wengi, amekuwa mstari wa mbele katika kuilemisha jamii bila kujali rika. Amejitolea kufundisha kile akijuacho juu ya malezi na matatizo mbali mbali yanayowakabili wanandoa na malezi ya watoto.

Kibaraza chake kimekuwa ni kitovu chenye kukutanisha wadau mbali mbali wenye fikra pevu, na kuibua mijadala yenye kuelimisha, kufundisha, kuburudisha na kuhuzunisha pia.

Binafsi napenda kumuita dada na kwangu mimi ni zaidi ya dada, kwani amekuwa ni mwalimu mzuri kwangu nikijifunza mambo mengi kupitia kibaraza chake nimekuwa nikijifunza mengi, na sisiti kukiri kwamba chimbuko la kibaraza cha VUKANI ni kutokana na kile nilichojifuza kwake.

Ni mkweli na muwazi, na hasiti kusema wazi hisia zake, lakini huwa makini sana ili kuepuka kumuumiza mtu mwingine kihisia, na kama kwa kusema huko kutamkera mtu mwingine, ni mwepesi kuweka sawa maelezo yake ili kuondoa msigishano wa mawazo.

Nakumbuka wakati fulani nlipopata msongo wa mawazo kutokana na tofauti zangu na wazazi wangu, alikuwa ni mtu wa kwanza kunitumia email binafsi akijaribu kuniliwaza na kunitaka nisichukue hatua yoyote kujidhuru, naomba nikiri kwamba email ile ilinisaidia sana kurudi katika hali yangu ya kawaida na nilijisikia fahari kuona kwamba kuna mtu ananipenda na kunijali japo sijawahi kuonana naye uso kwa uso.

Huu kwangu ulikuwa kama muujiza, inakuwaje, mtu kusoma mawazo yangu kupitia blog tu halafu awe karibu nami kiasi hiki, ni kitu gani kimemvuta? Kusema kweli tangu siku hiyo niliamni kuwa maandishi yana nguvu sana na kupitia maandishi yawezekana mtu mwingine kukufahamu vizuri sana.

Nimekuwa karibu sana na binti huyu, na amekuwa ni mwema sana kwangu na mshauri wangu pia, na kupitia vibaraza vyetu, tumekuwa tukibadilishana mawazo na kupeana ushauri mbali mbali ili kuboresha ustawi wetu na wa familia zetu.
--------------------------------------------------------------------------
KOERO HUKO ULIKO MUNGU AKULINDE NAKUKUMBUKA SANA KILA SIKU UWE SALAMA.


NI JUMATATU YA MWISHO YA MWEZI HUU NAMI NIMEONA TUIANZE HIVI!!!NIMEUPENDA WIMBO/UJUMBE HUU KUHUSU KUPENDA UNAWEZA KUSIKILIZA UKIPATA WASAA!!!


JUMATATU NJEMA KWA WOTE!!

Sunday, October 28, 2012

NAPENDA KUWAYTAKIENI WOTE JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI HUU IWE NJEMA SANA!!

Leo ni Jumapili ya mwisho wa mwezi huu wa kumi nami nawatakieni wote Jumapili njema sana binasi itaishi kubeba mabox...JUMAPILI NJEMA KWA YOYOTE ATAKYEPITA HAPA NA KUSOMA UJUMBE HUU.

Thursday, October 25, 2012

UNATAKA KUNYWA SODA/VINYWAJI BARIDI? BASI JARIBU NA HII HAPA/AKILI NI NYWELE KILA MTU ANA ZAKE-UBUNIFU!!!

JIPATIE VINYWAJI BARIDI

Kuna namna nyingi ambazo sisi wanadamu tunaweza kujipatia huduma zetu tofauti na vile tulivyozoea. Ili kinywaji kiwa baridi tumezoea kukiweka kwenye jokofu/fridge ili kipate baridi, na hii hutumika zaisi maeneo yenye hali joto kama vile Dar Es salaam nakadhalika. Kwenye sehemu za baridi kwa Tanzania kama vile Njombe, Mufindi, Makambako n.k mara nyingi hawatumii majokofu, kwa kuwa vinywaji hivyo vinakuwa vya baridi tayari.
Sasa basi iwapo huna jokofu haimaanishi huwezi kujipatia kinywaji cha baridi. Ni hivi chukua soda na uziweka ndani ya maji yaliyomo ndani ya mtungi kwa usiku mzima, na asubuhi zinakuwa baridi  safi kabisa kwa kukata kiu yako.
Vyungu hivi hutengenezwa na sisi wenyewe waTanzania, na hutumika kwa matumizi ya kupikia, kuhifadhia na leo hii tunajifunza pia twaweza kufanya zoezi hili. Pia kuna aina nyingine ya ubunifu katka kutaka kinywaji kiwe baridi ni hivi:- Chukua soksi na uiweke chupa ndani ya soksi na halafu weka maji kwenye chombo chochote kile kama ndoo vile utaona matokeo yake itakuwa baridiiiiii..UJANJA eehh:-)

SI MWINGINE TENA BALI NI NURU WETU AMEFANYA TENA KILE ANACHOKIWEZA...HAYA EBU MSIKILIZE HAPA HUU WIMBO MPYA CHAPA LAPA!!

Nachukua nafasi hii na kumpongeza dada Nuru kwa kazi nzuri aliyoifanya.Ni ujumbe mzuri kama una muda sikiliza ...chapa lapa kaka sitaki tena mapenzi kila siku unachanganya danganya  danganya toto ..aahhh sikiliza mwenyewe...

Kila la kheri !!!

Wednesday, October 24, 2012

HIVI LINI UMECHEKA AU KUTABASAMU BASI UNGANA LEO NAMI KUHUSU HILI: Maongezi ya Mtoto na Baba'ke

Baba: We mtoto hebu niletee soda...
Mtoto: Cola au Pepsi?
Baba: Pepsi.
Mtoto: Kopo au Chupa?
Baba: Kopo.
Mtoto: Baridi au moto?
Baba: Baridi.
Mtoto: Ndogo au Bonge?
Baba: Aaa! Basi niletee tu maji.
Mtoto: Ya bombani au dukani?
Baba: We mtoto nitakupiga?
Mtoto: Na mti au chelewa?
Baba: N'takuua nakwambia!
Mtoto: Kwa kudu au bunduki?
Baba: Bunduki.
Mtoto: Kichwani au kifuani?
Baba: Mbaff, toka nje!
Mtoto: Sasa hivi au baadaye?
Baba: Sasa hivi.
Mtoto: Kwa hiyo maji hutaki tena?
Baba: (kimoyomoyo) "nilimwambia mke wangu tukilewa tusifanye, yeye anang'ang'ania, haya ndiyo matokeo yake..."
Source: http://www.wavuti.com

Tuesday, October 23, 2012

NIMEIPENDA PICHA HII NA NIMEONA IWE PICHA YA WIKI/WAREMBO WA WIKI!!!

 
Kwa kweli nimeipenda hii picha hebu iangalie wewe unaona nini katika picha hii? ukitaka kumsoma zaidi mdada huyu basi bonyezaga hapa...

WIKI HII NAONA ITAKUWA YA RUVUMA---TURUDI SONGEA TENA..


Wote tunajua MAJI ni muhimu kwa uhai wa binadamu ...kuwa na maji safi na salama kila mtu ana haki lakini si wote wanapata huduma hii...KILA LA KHERI

Monday, October 22, 2012

TUSIISHIE SONGEA NGOJA TUENDELEE MPAKA KWETU NYASA:- HIZI NI TASWIRA ZA NYASA

 
MAWINGU HAYO SIJUI NDIO MWANZO WA KUCHAFUKA ZIWA?
 
NA HAPA HAKUNA  HAKUNA TAABU YA KUSUBIRI SANA SAMAKI NI KUINUKA TU..PIA MAJI KARIBU ...naimekumbuka sana nyasa....

TUANZE JUMATATU HII KWA KUTEMBELEA KIJIJI FULANI SONGEA!!!

Kwa wale wanaotoka Songea au wale waliofika Songea hivi hapa ni wapi? Ni kijiji gani hiki? Jumatatu njema kwa wote

Sunday, October 21, 2012

NAPENDA KUWATAKIA WOTE JUMAPILI NJEMA NA MAPUMZIKO MEMA!!!

Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako kwa uchungu utazaa watoto na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. Mwanzo 3:16
JUMAPILI/DOMINIKA IWE YENYE UPENDO.

Saturday, October 20, 2012

Neno La Leo: Hakuna Ugumu Wa Kurudi Misri...

Habari hii nimetumiwa na kaka Mjegwa.....
-------------------------------------------------------------------------------------
Ndugu zangu,
Yanayotokea katika nchi yetu kwa sasa yanatutaka tufikiri kwa bidii. Kama nchi kuna safari tumeifunga. Na tulivyo Waafrika, tu mahodari wa kufunga safari, lakini si mahodari wa kupanga safari. Kufunga na kupanga safari ni vitu viwili tofauti.

Ndugu zangu,

Ni vigumu leo kwa Wana wa Israel kuamua kurudi tena Misri, hata kama, pamoja na chawa na kunguni walioaacha Misri, bado, kuna wanaokumbuka samaki na masufuria ya pilau waliyoayaacha Misri. Lakini, kijamii, na kwa kuingalia jamii yetu hii ilikotoka, ilipo sasa na inakoelekea, na tuone sasa, kuwa hakuna ugumu wa kurudi tena Misri. Na hapa nitazungumzia umuhimu wa sisi WaTanzania kujitambua.

Nahofia, kuwa moja ya kiini ya haya yanayotukuta sasa ni dhambi ya Ubaguzi iliyoanza kututafuna pole pole. Taratibu tunapoteza uwezo wetu wa kujitambua. Ni ukweli sasa, kuwa Watanzania hatujitambui, na kibaya zaidi, baadhi ya viongozi wetu wa kisiasa na kidini wanapoonyesha wazi wazi kuwa hawajitambui.

Maana, tumeanza sasa kuzungumza lugha za ' Wao Wakristo' na ' Sisi Waislamu'. Tunasahau, kuwa sisi ni ndugu wa damu. Kuwa SISI ni Watanzania Kwanza. Na lililo la kwanza kwetu ni ' Nchi Yetu' na maslahi yake.

Hii ni Nchi Yetu Sote. Kila Mtanzania kwa nafasi yake ana lazima ya kupigania Usalama wa Taifa letu. Usalama wa Nchi Yetu tuliyozaliwa. Hatuwezi kuilinda na kuijenga Nchi Yetu kwenye mazingira ya kubaguana. Kwenye mazingira ya kugawanyika kwa misingi ya udini, ukabila na rangi. Na hapa nitamrejea tena Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na dhana ya Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa.

Ni Mwalimu Nyerere aliyeuanzisha na kuusimamia mradi mkubwa wa Ujenzi wa Umoja wa Kitaifa, hata hivyo, tunaona sasa unavyoporomoka na kuliacha taifa letu mashakani. Ndio, Mwalimu alijenga misingi imara ya Ujenzi wa Umoja Wa Kitaifa ( Nation Building).

Kuijenga jamii ya Watanzania yenye kuamini kwenye ukweli kuwa sisi sote ni ndugu. Kwamba Nchi yetu haina dini. Yenye kupiga vita ubaguzi wa aina zote, iwe wa rangi, kabila au dini. Ilimchukua Mwalimu na taifa letu miaka mingi sana kuijenga misingi hiyo iliyowawezesha pia Watanzania kuwa na mioyo ya uzalendo kwa Taifa lao.

Tunaona sasa, kazi hiyo iliyochukua miaka mingi, kutokana na ubinafsi na uroho wa madaraka ya baadhi ya wanasiasa wetu, wanapelekea kubomoka kwa misingi hiyo na kuliacha taifa letu kwenye hatari ya kuangamia.

Ndio, msingi wake ni ubaguzi wa kisiasa unaotokana na ubinafsi na tamaa ya mali kwa baadhi ya tuliowapa dhamana za kufanya maamuzi makubwa kwa niaba yetu. Ni hali ya baadhi ya tuliowapa dhamana za uongozi kuishiwa chembe chembe za uzalendo; mapenzi kwa nchi yao.Ni watu wenye kulinda maslahi yao na ya wanaowazunguka. Wako tayari hata kutumia mbinu za Umafia kutimiza malengo yao. Kuna Watanzania wengi sasa wanaopoteza mioyo ya uzalendo kwa nchi yao.

Kuna hata wenye kufikia kutamka; 'Nchi hii ina wenyewe'. Kuna anayetamka hilo kwa lengo la kumtishia mwenzake au kulazimisha kitu fulani kifanyike. Lakini, kuna wenye kutamka hivyo kuashiria kukata tamaa. Kuwa hata wafanye nini, hakuna anayewasikiliza ama kuwajali. Hizi si dalili njema kwa taifa. Kuna wanaoiba mali ya umma mchana wa jua kali. Hakuna anayewagusa.

Ukiuliza utajibiwa; “Ah! Nchi ina wenyewe!”. Kwamba kuna baadhi yetu hawajisikii kuguswa na nchi hii, hawajisikii kuwa na nguvu ya kupiga vita maovu yanayotusumbua. Baadhi yetu wameanza kupungukiwa na mapenzi na nchi yao.

Juni 16, 2004 nilipata kuandika hili kwenye gazeti la Majira; kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili.

Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndio, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbali mbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.

Ndugu zangu, Hakuna ugumu wa kurudi Misri. Tuna lazima ya kupanga safari ya kurudi tena Misri. Inawezekana.

Na hilo ni Neno la Leo.

Maggid Mjengwa,

Iringa,

0788 111 765, 0754 678 252
http://mjengwablog.com

Friday, October 19, 2012

DAR ES SALAAM /KARIAKOO HAKUNA AMANI LEO HII

Mwenyezi Mungu nakuomba uzidi kuiongezee Tanzania yetu ili kusizidi zaidi ya hapa. Watu wawe na upendo na amani kama mwanzo..MUNGU IBARIKI TANZANIA YETU PIA WATU WAKE....

BINTI ACHUMWA KISU NA MAMA KWA TUHUMA ZA "KUTEMBEA " NA BABA!!

Mfanyakazi wa ndani, Angel Lema (22) amechomwa kisu kwa tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba mwenye nyumba anakofanya kazi.

Angel anayefanya kazi za ndani katika kijiji cha Leganga wilayani Arumeru mkoani Arusha, inadaiwa alifanyiwa unyama huo na mama mwenye nyumba baada ya kumhisi ‘kutembea’ na mumewe.

Akizungumzia tukio hilo jana, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Dkt. Aziz Msuya, alithibitisha kumpokea msichana huyo akiwa na hali mbaya, kutokana na jeraha tumboni Oktoba 8. Dkt. Msuya alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi, ilibainika alichomwa kisu tumboni na mwajiri wake.

“Lakini binti huyu tulipomhoji, kwanza alikataa na kudai kujichoma mwenyewe, ila baadaye ilibainika alichomwa na mama mwenye nyumba kwa hisia za kufanya mapenzi na mumewe na kumeonya asimtaje kuwa ndiye amemchoma kisu,” alidai.

Dkt. Msuya alisema kutokana na jeraha kuwa kubwa, walihofia usalama wa utumbo wake na kulazimika kumfanyia upasuaji wa tumbo ili kuangalia usalama zaidi ndani, “Tulipomfanyia upasuaji tuligundua hajaathirika utumbo na ulikuwa salama, tukamshona,” alisema Dkt. Msuya na kuongeza: “Lakini cha ajabu kidonda kikiwa kibichi, msichana huyo alitoroshwa usiku Oktoba 14, kitendo kilichotushangaza,” alisema Dkt. Msuya.

Alisema baada ya kugundua hilo, walitoa taarifa Polisi, ili wachunguze tukio hilo ili kuokoa maisha ya msichana huyo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas baada ya kupigiwa simu na gazeti hili, kuuliziwa tukio hilo, alisema hana taarifa, “Mimi sina taarifa, lakini tukio hilo linaweza kuwapo… kwa kuwa niko mbali huku Moshi kwenye maziko ya Kamanda Barlow (Liberatus), bado sijapata muda wa kufuatilia taarifa za huko na kupata habari zaidi, lakini pia huku mawasiliano yanasumbua sana,” alisema.
Kamanda Sabas aliahidi kulifuatilia suala hilo mara atakapopata nafasi na kutoa taarifa.
---
Habari imeandikwa na John Mhala, HabariLeo, Arusha

LEO TUWATEMBELEE NDUGU ZETU WASUKUMA HUKO MWANZA NA UTAMADUNI WAO WA ASILI


NAWATAKIENI WOTE MWISHO WA JUMA UWE MWEMA SANA...

Thursday, October 18, 2012

YASINTA:-HIVI KWA NINI NINYI WAAFRIKA MPO HIVI?

Ni maswali nililoulizwa na wafanyakazi wenzangu pamoja bosi wangu..
Yasinta:Nikawauliza tupoje?
Wafanyakazi wenzake: Wakasema ninyi wakati wote mna furaha tu mkila, mkiwa na njaa. Mkiwa na nguo na msipokuwa na nguo ninyi/waafrika kwenye ni furaha tu. Inakuwaje?
Yasinta: Ndivyo tulivyo, hakuna sababu ya kumnunia jirani  itakuwa kazi bure.
Wafanyakazi: Au kwasababu kila wakati kunakuwa na jua ndo maana watu wanakuwa na furaha wakati wote?
Yasinta: Nikatabasamu..labda
Wafanyakazi: Yasinta, inasemekana kwamba ninyi/waafrika ni wepesi sana kucheza ngoma je? ni kweli?
Yasinta: Ni kweli.
Wafanyakazi: kwanini?
Yasinta: kwa sababu ni aina ya mila zetu.
Wafanyakazi: safi sana.
Na mwisho nikaa na kutafakari maswali yao nikagundua ni kweli tuna tabia hizo ila sina uhakika na majibu yangu na ndio nimeona nisaidiwe na ninyi ndugu zangu. Nitashukuru sana ....

Wednesday, October 17, 2012

KUMBUKUMBU:- KARIBU TUJUMUIKEJAMANI!!!

Picha hii imenikumbusha enzi zile miaka arobaini na saba familia nzima inajumuika pamoja na kushika chakula kiwe cha asubuhi, mchana au jioni. Hakika hii ilikuwa safi sana...kukaa hivi na familia yote kwenye mkeka/mpasa na kula chakula. Raha sana, halafu sasa muwe wengi hapo ndiyo chakula kita/kinanoga zaidi... Ila kuna baadhi ya watu wakiona watu wamekaa hivyo na kula chakula kwa mikono basi wanafikiri kuwa wana hali mbaya ..hapana hii ni moja ya tabia zetu yaani mila na desturi ambazo ni nzuri tu... ...je wewe nawe umekumbuka nini katika hili? JUMATANO NJEMA NA UKIPATA NAFASI KULA NA JIRANI YAKO AU RAFIKI.

Tuesday, October 16, 2012

KWANINI KUNA MAHINDI YA NJANO NA MAUPE?

 MAHINDI YA NJANO....
Na hapa ni mahindi MEUPE ambayo mimi binafsi nimeyazoea tangu nilipokuwa katoto kadogo. Ndiyo, nimewahi kuona mahindi mekundi meusi au mchanganyiko lakini hayo ya njano sijawahi kuona Tanzania yetu. Je? kwanini?

Monday, October 15, 2012

Sunday, October 14, 2012

JUMAPILI NJEMA KWA WOTE!!!

Haya wapendwa, leo ngoja tutembelee kanisa hili, ni kanisa la MATOGORO SONGEA..nimesali sana kanisa hili...MWENYEZI MUNGU NA AWABARIKI WOTE na tuzidi kudumisha upendo.

Saturday, October 13, 2012

Friday, October 12, 2012

KUMSHUKURU/KUSALI KABLA NA BAADA YA CHAKULA...!!!

JE? Wewe msomaji una tabia ya kufanya hivi kabla ya kula na baada ya kula? au unafikiri hawa wanafanya nini hapa?

IJUMAA YA LEO NGOJA TUWATEMBELEE NDUGU ZETU WACHAGGA NA NGOMA YAO HII YA JADI/ASILI!!!


Ni ngoma ya kabila la Wachagga kutoka katika Wilaya ya Arusha wakicheza ngoma ya Jadi/asili.....IJUMAA NJEMA NA MWISHO WA JUMA UWE MWEMA KWA WOTE!!!!!!

Thursday, October 11, 2012

TUNATHAMINI MCHANGO WA MWANAMKE??

Mama mjasiriamali tayari hapa kumekucha na kuwajibika ndiyo kama kawaida...na kama kawaida mara nyingi watoto wa kike hujifunza karibu kila kitu kupitia mama. Basi hapa tunaona binti huyu hayupo nyuma naye yupo mbele katika kujifunza maisha...hapa unadhani wanatoka kuuza au wanakwenda? 

Wednesday, October 10, 2012

KATARINA KWA NINI ULIKUFA?

Wapendwa wasomaji wa blog hii na wanablog wenzangu nimekuwa nikipokea email nyingi toka kwa wasomaji wa blog hii wa huko nyumbani Tanzania, wengi wakielezea uzoefu wao na wakitaka niziweke hapa ili tujadili kwa pamoja, na mimi sina kinyongo kwa kuwa blog hii inazungumzia Maisha, basi nitakuwa nikiziweka hapa ili wasomaji wengine wapate kujifunza
 Leo nimewaletea kisa cha kusikitisha cha binti aitwae Katarina, naomba muuangane na msimulizi wa kisa hiki.
 **********************************************************************
 Alikuwa ni mtumishi wa nyumbani na alikuwa na umri wa miaka 14 wakati huo, nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1993, ndio aliletwa kufanya kazi kwa shemeji yangu.
Nakumbuka nilikuwa naenda kwa shemeji yangu kila baada ya wiki kumjulia hali yeye na wanae.

Huyu Binti ambae alikuwa akijulikana kwa jina la Katarina mwenyeji wa kule Iringa alitokea kunipenda kweli na hakuficha hisia zake, kalikuwa ni kabinti kazuri na kadogo sana na kalikuwa na heshima kweli.

Siku moja shemeji yangu aliniambia kwa utani lakini, kuwa Katarina ananipenda na Kama nikitaka kuoa basi nisitafute mwanamke mwingine bali Katarina angenifaa zaidi.

Sikutilia maanani kauli ya shemeji yangu, na niliichukulia kama utani tu. Nilikuwa kila nikienda kwa huyo shemeji yangu Katarina atahakikisha ananipikia na kuniandalia maji ya moto ya kuoga tena kwa heshima kweli na nikishaoga kama nitalala pale alipenda sana kupiga soga na mimi na alikuwa akivutiwa sana na simulizi zangu za uongo na kweli.

Ilitokea nilipata kazi moja ya muda mfupi ambapo nililazimika kwenda Msolwa Morogoro ambapo nilikaa kwa miezi sita niliporudi nilikaa kama mwezi mmoja kabla sijaenda kwa shemeji yangu ambaye alikuwa akiishi Mbezi kwenye nyumba yake mwenyewe kumjulia hali.

Siku moja nilijikuta nikipata hamu sana ya kwenda kumuona shemeji yangu na nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1994 mwishoni. Nilipotoka kibaruani jioni nilikwenda kwa shemeji yangu, lakini nilipofika nilikuta kuna mtumishi mwingine pale nyumbani, nilikaribishwa na kwa bahati mbaya shemeji yangu hakuwepo nyumbani alitoka kidogo kwenda kwa shoga yake aishiye mtaa wa pili.

Kumbuka kwamba kipindi hicho kulikuwa hakuna simu za mkononi, ilibidi nikae pale sebuleni peke yangu kwani hata watoto wa shemeji walikwenda kwa marafiki zao kusoma tuisheni.

Nilikaa pale sebuleni peke yangu kama saa moja na nusu na ndipo shemeji akarudi na aliponiona alifurahi sana. Tulizungumza mambo mengi sana lakini sikumsikia akimzungumzia Katarina, mwishowe ikabidi nimuulize. “Shemeji, tangu nimefika hapa sijamuona Katarina, mchumba wangu, je yuko wapi?” niliuliza kwa utani.

Niliona uso wa shemeji yangu ukisawajika kwa huzuni na alinyamaza kimya kwa sekunde kadhaa, kabla hajasema kitu alimuomba yule binti aliyenipokea ambaye niliambiwa ni mtumishi wa pale nyumbani amletee maji ya kunywa.

Muda wote tukisubiri maji yaletwe tulikaa kimya na alionekana kuwaza sana, hali ile ilinitisha sana. Mara maji ya kunywa yakaletwa, alikunywa funda kadhaa za maji kisha akaweka ile glasi chini na kushusha pumzi ndefu, kisha akasema.

“Shemeji ni jambo la kusikitisha kukujulisha kuwa Katarina alifariki wiki iliyopita na taarifa hizo tumezipata juzi” Alisema shemeji yangu kwa upole, niliposikia taarifa ile kuna kitu kilinichoma moyoni kama msumari wa moto na nilijihisi kama natetemeka na kijasho chembamba kilinitoka.

“Amefia wapi, aliugua nini, na amezikwa wapi?” yalinitoka maswali mengi mfululizo.
Shemeji yangu alinisimulia kuwa, aliamua kumtafutia shamba boy wake wa zamani kibarua katika kiwanda fulani cha wahindi kwa kuwa alitarajia kuoa na kabla ya kuanza kazi alimtuma kwao Singida akamletee shamba boy mwingine ili amfundishe kazi awe ni mrithi wake kabla hajaanza kazi yake mpya.

Alikwenda Singida na akaja na huyo kijana na baada ya kumfundisha alikwenda kuanza kazi na kumuacha yule kijana mpya pale nyumbani.
Kumbe kuna siku yule kijana shamba boy mpya alimbaka Katarina, lakini alimtisha kuwa akisema atamuua na kukimbilia kwao Singida asionekane tena.

Katarina aliogopa kusema na akabaki kimya akiugulia maumivu baada ya kitendo kile. Haikupita muda , yule binti alianza kuumwa umwa na kutapika kusikoisha, ikawa kila anachokula anatapika. Utendaji wa kazi ukapungua na akawa anatumia muda mwingi sana kulala. Shemeji yangu akajenga wasiwasi ikabidi amdadisi kama ana mimba.

Awali Katarina alikataa katakata kuwa si mjamzito, lakini shemeji alimtishia kuwa atampleke Hospitali kesho yake akapime ili kujiridhisha Katarina alikiri kuwa ni mjamzito. Sasa Shughuli ikawa kwenye kumtaja mhusika, Katarina alikataa kabisa kumtaja mhusika shemeji ilibidi atumie mbinu ya kumtisha kuwa atampeleka Polisi na ndio akamtaja yule kijana lakini alisema kuwa alitishwa sana kuwa akimtaja atamuua ilibidi shemeji amfuate yule kijana chumbani kwake ili kumdadisi lakini kumbe yule kijana alikuwa akifuatilia ule mzozo kupitia dirishani na aliposikia jina lake likitajwa kuhusika na ile mimba alitoweka haraka sana asijulikane alipokwenda.

Ilibidi shemeji abaki na ule mzigo, kwanza alikuwa ni mjane pili hakuwa na mfanya kazi wa Ng’ombe maana yule kijana katoweka na pia mtumishi wake wa ndani yaani Katarina ndio huyo ni mjamzito, na yeye ni mtumishi serikalini, ilikuwa ni kaazi kweli kweli.
 Ilibidi afanye mawasiliano na marafiki zake na kwa kushirikiana na yule boy shamba wake wa zamani alifanikiwa kupata mfanyakazi wa ng’ombe mwingine, na baada ya wiki akapata House girl mwingine.

Baadae alimshauri Katarina arudi kwao Iringa na alimuahidi kumpa pesa ya kutosha ili imsaidie kujifungua na akijifungua alimtaka arudi kwake ili aendelee na kazi.
Ni kweli Katarina alikubali japo shingo upande na alikuwa na wasiwasi jinsi atakavyopokelewa nyumbani kwao na wazazi wake.
 Baada ya wiki moja Katarina alipakiwa ndani ya basi na kurudishwa Iringa na yule Shamba Boy wa zamani. Shemeji aliandika barua ndefu kueleza mkasa uliompata Katarina ili wazazi wake wasije kumuadhibu.

Aliporudi kutoka Iringa yule shamba boy aliyempeleka Katarina alisimulia kuwa walipokelewa lakini kwa wasiwasi kutokana na hali aliyokuwa nayo Katarina. Na kama si ile barua alioandika shemeji, basi yule shamba boy angelipishwa mahari na kuozeshwa yule binti, lakini ile barua iliposomwa ndio wakaamini japokuwa wapo walioitilia mashaka kuwa huenda imetengenezwa makusudi ili kumnasua yule kijana. Hata hivyo yule binti alikanusha kuwa yule kijana aliyefuatana naye hahusiki.
 Baada ya kupita mwezi mmoja shemeji yangu alipokea taarifa kuwa Katarina alifariki wiki moja iliyopita baada ya jaribio la kutoa mimba kushindikana.
Taarifa zaidi zilisema kuwa alipata manyanyaso pale nyumbani kwao kwa wazazi wake kutokana na kwamba walikuwa wanamtegemea na baada ya kurudi pale nyumbani wakawa wana hali ngumu na hivyo kumtupia Katarina lawama kuwa amekuwa mzembe kaharibu kazi kwa umalaya.

Katarina alikusudia kuitoa mimba ile ambayo ilishatimiza miezi sita na ndipo ikashindikana na akapoteza maisha yeye na kiumbe kilichokuwa ndani.
Nilishikwa na butwaa wakati wote shemeji yangu alipokuwa akinisimulia mkasa huo wa Katarina.
Ni miaka 15 sasa tangu binti huyu afariki Dunia, lakini leo katika hali ya kushangaza nimetokea kumkumbuka, sijui ni kwanini.

Dada Yasinta nakuomba uuweke mkasa wa binti huyu katika blog yako kama Dedicationa kwa binti huyu ambaye alifariki mwezi huu wa Oktoba japo tarehe siikumbuki.
Ni mimi msomaji wa blog yako Miki Malissa

Tuesday, October 9, 2012

HII ITAKUWA PICHA YA MWAKA KWA KWELI ..!!!!

Inasemekana maziwa ni lishe bora kwa watu/hasa watoto lakini ndiyo hivi kweli? Salama hapa?
Ngoja nisikilia hizi chuchu nyingine ili wengine wasije wakachukua....Nimewahi kusikia kuwa ni hatari kunywa maziwa bila kuchemsha  yaani moja kwa moja kama mtoto huyu. Je ni kwa binadamu tu au?Maana Ndama hadhuriki..Kaaaazi kwelikweli hapa..sijui mama alikuwa wapi?

Monday, October 8, 2012

HEBU FIKIRIA KIDOGO KUHUSU HILI!!!

Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba, ndoa sita katika kila kumi huvunjwa na wanaume au wanawake kutoka nje. Lakini inaonekana pia kwamba, wale wanaotoka nje ya ndoa zao, wengi ndiyo ambao huacha au kuachwa. Ni karibu ndoa nane katika kila kumi, ambazo hufikia ukomo kutokana na kutoka nje.
Wanawake ambao wako chini ya umri wa miaka 30, hutoka nje kwa kiwango karibu sawa na wanaume. Umri huo ndiyo hatari sana kwa wanawake kutoka nje.
Inaonyesha kwamba, bado dini haiogopwi sana linapokuja suala la kutoka nje. Waumini na viongozi wengi wa dini mbalimbali wanadaiwa kutoka nje kwa kiwango kikubwa kuliko inavyodhaniwa.
Karibu wanawake wawili katika kumi na wanaume watatu katika kumi, huwa wametoka nje ya ndoa zao katika maisha yao hapa duniani.
Uhusiano mwingi wa kiuzinzi hudumu kwa miaka mitatu tu na wapenzi huachana au kuachanishwa kwa kufumaniwa. Lakini mwingine hudumu maisha, ingawa na madhara yake nayo hudumu maisha.
Ni mwanamume mmoja kati ya kila kumi, ambao huwaacha wake zao na kuoa nyumba ndogo. Wengi hubaki na wake zao huku wakiwa na nyumba ndogo, au kuwaacha wake zao, lakini hawaoi nyumba ndogo.
Hata hivyo, wanane kati ya kumi miongoni mwa wale wanaowaacha wake zao na kuoa"nyumba ndogo," nao huja kuachana na nyumba ndogo hizo. Kwa hiyo, ni wawili tu kati ya kumi ambao hudumu na "nyumba ndogo" walizozioa baada ya kuachana na wake zao kwa sababu ya "nyumba ndogo" hizo.
Halafu wanane kati ya kumi ya kila aliyevunja au kuvuruga uhusiano wake na mume au mke kwa sababu ya hawara, huja kujuta baadaye. Ni wawili tu kati ya kumi, ambao uvurugaji wa uhusiano wake kwa sababu ya hawara, hawaji kujuta. Hawa ni wale ambao ndoa zao zilikuwa tayari na mashaka makubwa.
Huchukua mwaka mmoja hadi mitatu kwa ndoa ambayo imeingiliwa na fumanizi, wanandoa kuanza kuelewana tena kama awali. Hapo uhusiano huwa imara kuliko awali, au huingia mashaka ya sirisiri.
Chanzo:- kitabu Mapenzi kuchipia na kunyauka na Munga Tahenan.

Friday, October 5, 2012

NIMEONA TUBAKI SONGEA YETU NA NGOMA HII YA LIZOMBE KWANI NI SIKU NYINGI HATUJAISIKIA..UNGANA NAMI!!


HII HAPA NI KAZI YA MIKONO YANGU/NIMETENGENEZA MWENYEWE:-) Hakika ngoma za asili ni tamu...haya twende pamoja....

AU HALAFU TUENDELEE  KUSIKILIZA NA HAPA ....TUSELEBUKE..

Tuserebuke aaeeeX3  Maraha maraha kamla..ninapotaka mimi ni hapo tuX3 ninapochoka mimi ni hapo tu maraha maraha kamlaX3 duh naona nachelewa kucheza hapa endeleeni kuimba ....
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE IJUMAA NA PIA MUWA NA MWISHO WA JUMA NJEMA/MWEMA SANA..

Wednesday, October 3, 2012

NGOJA TURUDI MJINI SONGEA /NIMETAMANI NYUMBANI LEO!!

Waliofika mji wa Songea nadhani hawakosa kupita barabara hii . Je? ni sehemu gani hapa?
 
 

Mwanamke maarufu kuliko wote duniani....

Kila mtu akiulizwa ni mwanamke gani maarufu au aliye ngangari zaidi, kama anatafakari vizuri, atasema kuwa ni mama yake, hasa kama alimlea kwa uadilifu. Pengine mwingine atasema ni mkewe, kutegemea na namna wanavyoishi kwenye uhusiano wao wa kindoa.
Lakini, linapokuja suala la mwanamke ambaye hakuhusu, ambaye unaamini au kudhani kwamba, ndiye ngangari zaidi hapa duniani, hasa katika siasa na uchumi, inaweza kuwa mtihani mgumu kwako kutoa jibu sahihi.
Ni kweli, unaweza kutoa jibu, lakini siyo lazima jibu lako liwe sahihi.
Kama ni sahihi, itakuwa ni kwa sababu tu, unamjua huyo uliyemtaja, na wengine huwajui.
Hivi ndivyo ambavyo imetokea kwenye kura iliyofanyika ya kuwataja wanawake wanaodhaniwa kuwa maarufu hapa chini ya jua kwenye nyanja ya siasa na uchumi.
Karibu kila Mtanzania angetarajia kuwa wakitajwa wanawake 100 duninai ambao ni maarufu kwa sasa, huenda Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro angetajwa. Matarajio hayo yangetokana na sababu mbalimbali.
Kwanza, unaibu wa Katibu Mkuu wa UN, siyo nafasi ndogo hapa duniani. Pili, kwa mwanamke kutoka Afrika tena kwa nchi ambayo ni miongoni mwa zile maskini kabisa, kushika nafasi hiyo, ni jambo la kinasibu zaidi kwa mitazamo ya mgawanyo wa dunia. Tatu, ingetarajiwa naibu atoke angalau bara Amerika, kwani Katibu Mkuu anatoka Asia, bara maskini karibu sawa na Afrika kwa uwiano.
Kwa bahati mbaya, jarida maarufu duniani kwa kufanya tathmini za viwango mbalimbali kuanzia utajiri, uzuri na umaarufu wa binadamu, la Forbes linaonesha katika taarifa zake za wiki mbili zilizopita kwamba, Migiro hayumo kwenye orodha ya wanawake 100 maarufu duniani katika nyanja za uchumi na siasa.
Kutoka Afrika ni wanawake wawili tu walio kwenye orodha hiyo. Kwanza ni , Waziri Mkuu wa Msumbiji, ambaye anashikilia nafasi ya 89 diuniani kwa umaarufu. Halafu anafuatiwa na Rais wa Liberia, , ambaye anashikilia nafasi ya 100.
Hii ina maana kwamba, Waziri Mkuu wa Msumbiji ni maarufu zaidi duniani, ukilinganisha na Rais wa Liberia, , nchi iliyoweka historia duniani kwa vurugu kubwa za kisiasa, zilizopelekea marais wawili kuuawa kinyama na mmoja kupamba vyombo vha habari dunia kuhusiana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Rais Ellen Johnson ndiye Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, lakini anakuwa Rais baada ya uchaguizi huru na wa haki uliofuatia umwagikaji wa damu nyingi ya kutosha. Bado huyu anashikilia nafasi ya 100, wakati Waziri Mkuu wa Msumbiji anashikilia nafasi ya 89!
Hapa ndipo ambapo matokeo haya ya jarida la Fobes yanatia mashaka. Ni kweli kwamba, uchaguzi huo umefuatia kura kutoka kwa watu duniani kote.
Bahati mbaya ni kwamba, kura hizo kwa sehemu kubwa zimehusisha matumizi ya vyombo vya kisasa ambavyo havipo kwa wingi Afrika, hasa mtandano wa intaneti.
Katika orodha hiyo kuna majina ya wanawake ambayo huenda kwa umaarufu, akili ya kawaida inaweza kukuonesha kwamba, hawawezi kumzidi Asha Rose Migiro. Hebu kwa mfano, tuchukulie mwanamke kama , ambaye ni mtendaji kuuu wa Benki ya Leumi ya Israeli. Je, huyu mama uliwahi kumsikia au hata kumsoma kwenye chombo chochote cha nje? Huyu anashikilia nafasi ya 83 kwa umaarufu.
Huenda inabidi Afrika nayo sasa iwe na utaratibu wa kutafuta maoni ya dunia nzima ambapo waafrika nao watashiriki sawa kusema kuhusu nini wanaona, sawa na watu wengine duniani. Inaonekana wazi kwamba, hata viwango vya umaskini vinavyopangwa kutoka Ulaya na Marekani ni kwa vigezo ambavyo havifutu na kukidhi ukweli mkubwa zaidi unaowahusu Waafrika.
Kwenye orodha hiyo, inaonekana kuwa, Rais wa Ujerumani, , ndiye mwanamke maarufu zaidi duniani. Wu yi, ambaye ni makamu mwa Rais wa China anashikilia nafasi ya pili.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya Temasek Holdings, ya Singapore.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anashikilia nafasi ya nne.
Wengine ni , mwenyekiti wa kampuni ya PepsiCo ya Marekani. Namba sita ni , Rais wa India. Namba saba imeenda kwa, mtendaji Mkuu wa kampuni ya Anglo American ya Uingereza.
Nafasi ya nane anaishikilia ambaye ni mwenyekiti, kampuni ya Archer Daniels Midland ya marekani.
Namba tisa ni , mwenyekiti kampuni ya Kraft Foods ya Marekani, na namba kumi ni , Mtendaji Mkuu wa Alcatel-Lucent ya Marekani.
anashikilia nafasi ya 21, wakati Malkia Elizabeth anashikilia nafasi ya 23.
Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, , anashikilia nafasi ya 25.
Kama orodha hii ya Forbes inaonesha ukweli na uhalisia wa umaarufu unaotokana na michango ya wanawake katika jamii zao au jamii ya dunia, ina maana kwamba, kwa Afrika, wanawake hawajafanya lolote kwa jamii zao na jamii ya dunia.
Lakini, huo utakuwa pia ni uongo mkubwa, kwa sababu kuna idadi kubwa ya wanawke hapa Afrika ambao wamejitahidi kwa viwango vya kimataifa kubadili hali za watu wengine katika jamii.
Kama ni umaarufu kwa maana ya kujitangaza na kutangazwa sana na vyombo vya habari, ni wazi suala zima linakosa mantiki na linajaribu tu kuwavunja moyo wanawake wa Afrika. Orodha hiyo ni wanawake maarufu duniani katika nyanja za siasa na uchumi, ambapo ni uongo kudai kwamba, kati ya wanawake 100 duniani, Afrika inaambulia nafasi mbili, tena za mwisho.
Hii ina maana dunia inawatambua wanawake wawili tu Afrika katika nyanja hizo? Ndiyo maana naamini kwamba, Migiro angepaswa kuwemo kwenye orodha hiyo, kama kweli inakagua mambo kwa uhalali.
Lakini, mtu akikagua orodha hii tena na tena anaweza kupata picha kubwa zaidi na kuikubali, ingawa baadaye anaweza kuipinga. Ni matokeo ya kura yenye utata. Kwa mfano, Hilary Clinton anafahamika, kama ilivyo kwa Oprah Winfrey, lakini nao wametupwa hadi nafasi za 20, kama ilivyo kwa Malkia Elizabeth.
Lakini, hapohapo kuna majina kati ya namba 11 hadi 20, ambayo ni ya wanawake ambao hata watazamaji, wasomaji na wasikilizaji wazuri wa vyombo vya habari vya nje hawajawahi kuwasikia.
Kama ilivyo kwenye nyanja nyingine, hasa uchumi, vyombo vya habari vya Magharibi, bado vinaitendea Afrika kama vile ni bara wanamoishi wanyama, badala ya binadamu.
Vyombo vyetu vya habari, kwa bahati mbaya, navyo ni kama sauti za vyombo vya habari vya Magharibi.
Vikifanya tafiti zao, vinafanya kwa njia finyu na iliyofubaa, isiyoweza kuwahamasisha Waafrika.

Hii iliandikwa kwenye gazeti la jitambue iliandikwa na Hayati Munga Tehenan.

Tuesday, October 2, 2012

PICHA ZA WIKI:- ZILIPENDWA/UJANA!!!

 
unajua huyu ni nani?
 
...Na je unajua huyu pia ni nani ?..na je katika picha hizi ni kitu gani hawa watu wanafanana/ au hawafanani? JUMANNE NJEMA SANA!!!

Monday, October 1, 2012

NIMEUTAMANI KWELI MLO HUU UNGEKUWA MLO WANGU WA JIONI HII!!!

ila nitashindwa kwa vile kitu kikubwa zaidi ni kwamba sina unga ....mwisho nimebaki kumezea mate tu..hasa huyo samaki wewe acha tu...picha toka http://barakachibiriti.blogspot.se.
Nawatakieni kila la kheri au sijui jioni,mchana, asubuhi au usiku mwema.

KUMBE KUNA:- KIMWAGA MDADISI!!!

Jumatatu ya leo nimeona turudi nyuma kidogo ...kumbe kuna KIMWAGA MDADISI  pia sio KAPULYA MDADIDI TU....Hadithi hii kutoka kitabu cha JIFUNZENI LUGHA YETU KITABU 5...KARIBUNI
------------------------------------------------------------------------------------------------------------

 KIMWAGA NA BABU YAKE
HAPA NI KITABU CHENYWE KWA MBELE
Hapo zamani palikuwa na mtoto mmoja akiitwa Kimwaga. Mtoto huyo alimpenda sana babu yake Lukindo. Kimwaga na babu yake waliishi katika kijiji cha Kwemasafi, Wilayani Korogwe. Jioni, baada ya jua kuzama, Kimwaga alikuwa akikoka moto kwenye kibanda chao cha mazungumzo. Babu yake alikuwa akipenda sana kuota moto na kuzungumza na mjukuu wake.
Siku moja jioni, Mzee Lukindo na Kimwaga walikuwa wakiota moto. Kimwaga alikuwa mtoto MDADISI sana. Alimsimulia babu yake habari moja iliyomshangaza. Alisema, "Babu, leo tulikuwa tukilima katika shamba letu la shule. Mimi niliinua jembe kwa nguvu ili nichimbue magugu. Jembe likagonga jiwe, nikaona cheche za moto zinamulika. Hivi babu moto ulitoka wapi?
Babu yake akamwuuliza, "Hivi mjukuu wangu hujui hadithi ya moto?" Kimwaga akamjibu, "Sijui. "Babu yake akamwambia, "Basi nikueleze kidogo. Hapo zamani za kale binadamu hawakuwa na moto. Waliishi katika mapango yenye giza. Walikula matunda na nyama mbichi. Maisha yao yalikuwa ya taabu sana.
"Kwa bahati, siku moja mzee mmoja akachukua mawe, akayagongagonga ili yavunjike apate jiwe la kuchimbia viazi mwitu. Alipoyagonga aliona yakitoa cheche za moto. Alifikiri sana. Halafu akaweka manyasi makavu karibu na yale mawe, na akaendelea kuyagongagonga. Mara yale manyasi yakawaka moto. Kumbe alikuwa amegundua moto kama ulivyoona wewe leo wakati ulipolima huko shuleni."
Kimwaga akamwambia babu, "Kumbe hata mimi nimegundua moto." Kisha akaendelea, "Babu, juzi tulipokuwa tunatoka shule tulinyeshewa na mvua, tukalowa. Tulipofika kwenye shamba moja tulijificha chini ya kibanda kimoja kidogo. Mwenzetu Kimweri akapekechapekecha vijiti viwili vikavu. Mara tukapata moto, tukautumia kwa kukaushia nguo zetu. Je, babu moto ule ulitoka wapi?"
Mzee Lukindo akasema, "Aaa, wewe Kimwaga unadadisi sana. Basi sijakueleza hadithi nyingine. Hapo zamani sana, kabla mimi sijazaliwa, palikuwa na mtoto mmoja mtundu sana. Siku moja alitaka kutoboa kigogo kikavu ili atengeneze kidude cha kuchezea. Akachukua kijiti akaanza kupekecha. Kile kigogo kikatoa unga mweusi. Akaendelea kupekecha kwa nguvu sana. Akaona moshi. Mwisho ule unga mweusi ukashika moto. Akachukua nyasi kavu na kuziweka karibu na ule unga. Nyasi zikawaka moto. Kumbe naye alikuwa amegundua moto."
Siku nyingine tena, Kimwaga akamweleza babu yake namna alivyomtazama buibui. Akamwuliza babu yake , "Je babu, ule uzi ambao buibui hujengea nyumba unatoka wapi?" Mzee Lukindo akajibu, "Buibui ni mdudu wa ajabu. Anapotaka kujenga nyumba yake hutoa maji kutoka tumboni mwake. Maji haya yanapotoka nje tu huganda, na anapokwenda huonekana uzi."
Babu yake Kimwaga alipomaliza kusimulia habari za buibui, Kimwaga alikuwa anasinzia kwa sababu siku ile alichelewa sana kwenda kulala. Mzee Lukindo akamwambia, "Sasa mjukuu wangu, nenda ukalale. Nitakueleza hadithi nyingine kesho," Kimwaga akaenda zake kulala.
JUMATATU NJEMA KWA WOTE...