Wednesday, October 3, 2012

Mwanamke maarufu kuliko wote duniani....

Kila mtu akiulizwa ni mwanamke gani maarufu au aliye ngangari zaidi, kama anatafakari vizuri, atasema kuwa ni mama yake, hasa kama alimlea kwa uadilifu. Pengine mwingine atasema ni mkewe, kutegemea na namna wanavyoishi kwenye uhusiano wao wa kindoa.
Lakini, linapokuja suala la mwanamke ambaye hakuhusu, ambaye unaamini au kudhani kwamba, ndiye ngangari zaidi hapa duniani, hasa katika siasa na uchumi, inaweza kuwa mtihani mgumu kwako kutoa jibu sahihi.
Ni kweli, unaweza kutoa jibu, lakini siyo lazima jibu lako liwe sahihi.
Kama ni sahihi, itakuwa ni kwa sababu tu, unamjua huyo uliyemtaja, na wengine huwajui.
Hivi ndivyo ambavyo imetokea kwenye kura iliyofanyika ya kuwataja wanawake wanaodhaniwa kuwa maarufu hapa chini ya jua kwenye nyanja ya siasa na uchumi.
Karibu kila Mtanzania angetarajia kuwa wakitajwa wanawake 100 duninai ambao ni maarufu kwa sasa, huenda Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro angetajwa. Matarajio hayo yangetokana na sababu mbalimbali.
Kwanza, unaibu wa Katibu Mkuu wa UN, siyo nafasi ndogo hapa duniani. Pili, kwa mwanamke kutoka Afrika tena kwa nchi ambayo ni miongoni mwa zile maskini kabisa, kushika nafasi hiyo, ni jambo la kinasibu zaidi kwa mitazamo ya mgawanyo wa dunia. Tatu, ingetarajiwa naibu atoke angalau bara Amerika, kwani Katibu Mkuu anatoka Asia, bara maskini karibu sawa na Afrika kwa uwiano.
Kwa bahati mbaya, jarida maarufu duniani kwa kufanya tathmini za viwango mbalimbali kuanzia utajiri, uzuri na umaarufu wa binadamu, la Forbes linaonesha katika taarifa zake za wiki mbili zilizopita kwamba, Migiro hayumo kwenye orodha ya wanawake 100 maarufu duniani katika nyanja za uchumi na siasa.
Kutoka Afrika ni wanawake wawili tu walio kwenye orodha hiyo. Kwanza ni , Waziri Mkuu wa Msumbiji, ambaye anashikilia nafasi ya 89 diuniani kwa umaarufu. Halafu anafuatiwa na Rais wa Liberia, , ambaye anashikilia nafasi ya 100.
Hii ina maana kwamba, Waziri Mkuu wa Msumbiji ni maarufu zaidi duniani, ukilinganisha na Rais wa Liberia, , nchi iliyoweka historia duniani kwa vurugu kubwa za kisiasa, zilizopelekea marais wawili kuuawa kinyama na mmoja kupamba vyombo vha habari dunia kuhusiana na mashtaka ya mauaji ya kimbari.
Rais Ellen Johnson ndiye Rais wa kwanza mwanamke barani Afrika, lakini anakuwa Rais baada ya uchaguizi huru na wa haki uliofuatia umwagikaji wa damu nyingi ya kutosha. Bado huyu anashikilia nafasi ya 100, wakati Waziri Mkuu wa Msumbiji anashikilia nafasi ya 89!
Hapa ndipo ambapo matokeo haya ya jarida la Fobes yanatia mashaka. Ni kweli kwamba, uchaguzi huo umefuatia kura kutoka kwa watu duniani kote.
Bahati mbaya ni kwamba, kura hizo kwa sehemu kubwa zimehusisha matumizi ya vyombo vya kisasa ambavyo havipo kwa wingi Afrika, hasa mtandano wa intaneti.
Katika orodha hiyo kuna majina ya wanawake ambayo huenda kwa umaarufu, akili ya kawaida inaweza kukuonesha kwamba, hawawezi kumzidi Asha Rose Migiro. Hebu kwa mfano, tuchukulie mwanamke kama , ambaye ni mtendaji kuuu wa Benki ya Leumi ya Israeli. Je, huyu mama uliwahi kumsikia au hata kumsoma kwenye chombo chochote cha nje? Huyu anashikilia nafasi ya 83 kwa umaarufu.
Huenda inabidi Afrika nayo sasa iwe na utaratibu wa kutafuta maoni ya dunia nzima ambapo waafrika nao watashiriki sawa kusema kuhusu nini wanaona, sawa na watu wengine duniani. Inaonekana wazi kwamba, hata viwango vya umaskini vinavyopangwa kutoka Ulaya na Marekani ni kwa vigezo ambavyo havifutu na kukidhi ukweli mkubwa zaidi unaowahusu Waafrika.
Kwenye orodha hiyo, inaonekana kuwa, Rais wa Ujerumani, , ndiye mwanamke maarufu zaidi duniani. Wu yi, ambaye ni makamu mwa Rais wa China anashikilia nafasi ya pili.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na ambaye ni mtendaji mkuu wa kampuni ya Temasek Holdings, ya Singapore.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, anashikilia nafasi ya nne.
Wengine ni , mwenyekiti wa kampuni ya PepsiCo ya Marekani. Namba sita ni , Rais wa India. Namba saba imeenda kwa, mtendaji Mkuu wa kampuni ya Anglo American ya Uingereza.
Nafasi ya nane anaishikilia ambaye ni mwenyekiti, kampuni ya Archer Daniels Midland ya marekani.
Namba tisa ni , mwenyekiti kampuni ya Kraft Foods ya Marekani, na namba kumi ni , Mtendaji Mkuu wa Alcatel-Lucent ya Marekani.
anashikilia nafasi ya 21, wakati Malkia Elizabeth anashikilia nafasi ya 23.
Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, , anashikilia nafasi ya 25.
Kama orodha hii ya Forbes inaonesha ukweli na uhalisia wa umaarufu unaotokana na michango ya wanawake katika jamii zao au jamii ya dunia, ina maana kwamba, kwa Afrika, wanawake hawajafanya lolote kwa jamii zao na jamii ya dunia.
Lakini, huo utakuwa pia ni uongo mkubwa, kwa sababu kuna idadi kubwa ya wanawke hapa Afrika ambao wamejitahidi kwa viwango vya kimataifa kubadili hali za watu wengine katika jamii.
Kama ni umaarufu kwa maana ya kujitangaza na kutangazwa sana na vyombo vya habari, ni wazi suala zima linakosa mantiki na linajaribu tu kuwavunja moyo wanawake wa Afrika. Orodha hiyo ni wanawake maarufu duniani katika nyanja za siasa na uchumi, ambapo ni uongo kudai kwamba, kati ya wanawake 100 duniani, Afrika inaambulia nafasi mbili, tena za mwisho.
Hii ina maana dunia inawatambua wanawake wawili tu Afrika katika nyanja hizo? Ndiyo maana naamini kwamba, Migiro angepaswa kuwemo kwenye orodha hiyo, kama kweli inakagua mambo kwa uhalali.
Lakini, mtu akikagua orodha hii tena na tena anaweza kupata picha kubwa zaidi na kuikubali, ingawa baadaye anaweza kuipinga. Ni matokeo ya kura yenye utata. Kwa mfano, Hilary Clinton anafahamika, kama ilivyo kwa Oprah Winfrey, lakini nao wametupwa hadi nafasi za 20, kama ilivyo kwa Malkia Elizabeth.
Lakini, hapohapo kuna majina kati ya namba 11 hadi 20, ambayo ni ya wanawake ambao hata watazamaji, wasomaji na wasikilizaji wazuri wa vyombo vya habari vya nje hawajawahi kuwasikia.
Kama ilivyo kwenye nyanja nyingine, hasa uchumi, vyombo vya habari vya Magharibi, bado vinaitendea Afrika kama vile ni bara wanamoishi wanyama, badala ya binadamu.
Vyombo vyetu vya habari, kwa bahati mbaya, navyo ni kama sauti za vyombo vya habari vya Magharibi.
Vikifanya tafiti zao, vinafanya kwa njia finyu na iliyofubaa, isiyoweza kuwahamasisha Waafrika.

Hii iliandikwa kwenye gazeti la jitambue iliandikwa na Hayati Munga Tehenan.

3 comments:

Anonymous said...

Kwanini kila siku tusubiri Wazungu watufanyie eti tafiti zao halafu watuletee.Kwanini?

Yasinta Ngonyani said...

usiye na jina! swali nzuri sana nimejiuliza mara nyingi pia. inaonekana kama hatujiamini kwa yale tufanyao wakati ni mambo mazuri kabisa ..KUTUJIAMINI na KUAMINI YA WENGINE...Sijui mpaka lini?

sam mbogo said...

Da Yasinta, unabidi uwe mpole tu,kipengere hiki cha mwanamke maarufu,vigezo vyake wanavijuwa wenyewe,ila tu tatizo ni waandishi wetu nao hawa andiki sana mambo ya kiafrika na nivigumu sana kujuwa misimamo yao ya kiuandishi,kwamfano kama kuna machafuko sehemu fulani ya afrika, utakuta anacheongelea mwandishi/mwanahabari wa ulaya ndiyo hivyo hivyo itaripotiwa na mwandishi /mwanahabari wakiafrika,nikiwa namaana kutokea Afrika. kwa hiyo mambo mengine unaacha tu iposiku yatakaa sawa.mfano mwingine mrembo wa duni /miss world vigezo vyake unavijuwa wewe! mpaka leo Afrika hatujijuwi kama kwanini tunashiriki shindano hilo hasa Tanzania.kwa hiyo umaarufu unaanzia kwenu halafu ndo wengine sehemu mbalimbali watakujuwa..kaka s