Muda mrefu imekuwa inasemekana kutakuwa na mabadiliko ya usafiri nchini Tanzania. Lakini mpaka leo hakuna kinachoonekana. Nina maana kwa sasa hasa jijini Dar es salaam kuna tatizo kubwa la usafiri yaani daladala ni nyingi mno kiasi kwamba ni fujo tu. Afadhali kutembea au kutumia baiskeli kwa jinsi foleni za daladala zinavyosongamana. Naweza nikasema hakuna maana kuwa na gari Dar, kwenda kazini inabidi ujihimu mapema sana na ukichelewa basi itakuwa ule mtindo wa foleni. Na ukitaka kwenda sehemu ni afadhali ujue ni muda gani mzuri sio kuondoka tu.
Sijui mwenzangu mnasemaje? Kwani binafsi ningependa au pendekeza daladala zote zitolewe na kuwe na mabasi makubwa na pia train ya haraka. Nadhani kungekuwa na nafuu sana kwa wananchi. Kwa sasa naweza nikasema kwa kweli ni fujo, fujo, fujo sana. Maana magari mengi sana, pikipiki nyingi mno na daladala ndo uchafu tu.