Saturday, December 30, 2017

Monday, December 25, 2017

SALAMU ZA NOELI KUTOKA RUHUWI/SONGEA. KHERI SANA KWA KRISMASI

Napenda kuwatakieni  wote mtakaopita hapa KHERI YA KRISMASI.
Mziki kidogo

Friday, December 22, 2017

PERAMIHO KIZIZINI LEO 22/12/2017 IJUMAA NJENA WANDUGU Mdada anafurshia kuwa nyumbani  -:)
Leo nilikuwa Peramiho  na hapa ni kizizini kwa wale  wenyeji wa peramiho wanajua. Na wasiojua ni sehemu ufugaji bora......

Wednesday, December 20, 2017

KARIBUNI TUJUMUIKE KWETU RUHUWIKO

 Matunda matunda  kwa wingi ni kutoka tu nje na kuchuma
Pia dagaa nyasa pia wanapatikana KARIBUNI

Tuesday, December 12, 2017

MKIONA KIMYA BASI JUENI NIMEKWENDA KULA LIKOLO LA NANYUNGU-:) NYUMBANI NI NYUMBANI


Napenda kuwatakieni wote afya njema kwa kipindi hiki kijacho cha NOELI. Binafsi nitakuwa katika mapumziko kula likolo la nanyungu. KARIBUNI SANA.
PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA NA KUSEMA. NI MIMI KAPULYA WENU.

Wednesday, December 6, 2017

JE? WEWE UNAPENDA MATUNDA GANI? MIMI NAPENDA MACHENZA NA MAPAPAI

Kwanza MACHENZA Haya ni mepesi kumenya,hayana ukakasi wala uchungu kwa kifupi ni matamu. 
Pili ni mapapai haya ni matamu sana pia ni safi sana kulainishia nyama kama vile nyama ya ngòmbe utapenda nakuambia....

Tuesday, December 5, 2017

VISODA NA MATUMIZI YAKE......UBUNIFU

 Wakati wengine wakitumia kama mapambo........urembo
wengine wanatumia kama vihesabio. Je? wewe  umewahi kutumia kifaa hiki kwa mtindo wowote mwingine?

Thursday, November 30, 2017

TUUMALIZE MWEZI HUU NA KIPANDE HIKI CHA URAFIKI MWISHO WA MWEZI...


NAWATAKIENI MWISHO MWEMA WA MWEZI NA AFYA NJEMA KUUPOKEA MWEZI MPYA...

Tuesday, November 28, 2017

KUMBUKUMBU. ...BISI

Nimekumbuka sana chakula hiki. Ukiweka na chumvi...kuteremshia ni kikombe kikubwa cha maji.....

Monday, November 27, 2017

TUMALIZE JUMATATU YA MWEZI HUU WA KUMI NA MOJA KWA MTINDO HUU....UREMBO WA ASILI

 Heleni ....ambazo ni kazi za mikono ya watu kwa ubunifu safi  kabisa
Na hapa ni pia ubunifu mzuri kabisa wa viatu/sandosi. 
NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII NA KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA JUMATATU NJEMA SANA NA OMBI LANGU NI KWAMBA TUDUMISHE UTAMADNI WETU....Kapulya wenu...!

Thursday, November 23, 2017

NDUGU ZANGU:- TUTAFARI KWA PAMOJA MALEZI YA WATOTO WETU

 

Ukimkosoa sana mtoto na kumkaripia mara nyingi unampunguzia ujasiri na uwezo wa kujitegemea awapo mtu mzima.
Msaidie kwa upole, muelekeze, mtie moyo, akikosea mweleze jinsi Mungu anavyoumia kwa kosa alilolitenda.
Usimwambie kuwa hana jema hata moja hasa akiwa binti, maana siku moja kuna vijana wataona jema lake na watamwambia kisha ataweka USIKIVU Wake kwao.
Muombee mwanao/wanao, Mfundishe/wafundishe kuomba mwenyewe/wenyewe  Bwana atamsaidia/wasaidia.
Hii ni pamoja kumchapa mtoto viboko, ni kumwongezea usugu tu 

Wednesday, November 22, 2017

MSIMU WA BARIDI ....THERUJI YA KWANZA KUANGUKA KUONA NYASI TENA MPAKA MWEZI WA NNE:-(

Leo huku nje ni kimbembe thuriji imeanza kuanguka juzi, lakini leo ndo kwanza inazidi na upepo juu....Ni taarifa tu kwa ufupi. Nawatakieni siku njema.

Monday, November 20, 2017

NI WIKI NYINGINE NA JUMATATU NYINGINE...TUANZE WIKI NA PICHA HII YA KITAMADUNI KABISA

Wanawake  wakitwanga  nimekumbuka mbali sana  nilikuwa nikipata shida sana kutwanga watatu au wanne....:-)

Sunday, November 19, 2017

Wednesday, November 15, 2017

Tuesday, November 14, 2017

NIMEKUMBUKA MKAO HUU NA PIA KUJUMUIKA NA KULA KWA PAMOJA

Nimekumbuka miaka hile ya mwaka -47 wakati watu tulikuwa tunakaa kwa pamoja na kula tena sahani moja. Siku hizi  ni marachache sana kuona hii. Kwa kweli inanisikitisha

Friday, November 10, 2017

NAWATAKIENI MWISHO WA JUMA UWE MWEMA

Binafsi nafurahia taswira hii ya Moshi...ebu angalia Mlima wetu Kilimanjaro unavyoonekana....MWISHO MWEMA WA WIKI.

Wednesday, November 8, 2017

KOCHI LA LILILOTENGENEZWA KWA MITI NA KAMBA ZA KATANI.....!

Tudumishe utamaduni wetu na kuyaenzi na mambo yetu ya utamaduni wetu. Nimependa hii kochi.

Tuesday, November 7, 2017

LEO NIMEKUMBUKA ZILIPENDWA


Hakika nisikilizipo miziki aina hii nakuwa na furaha ya pekee maana mtu waweza kusikiliza na kujifunza kitu ...JUMANNE NJEMA WAPENDWA WA ZILIPENDWA.

Monday, November 6, 2017

JUMATATU HII YA KWANZA YA MWEZI HUU TUANZE NA UASILI...MAVAZI YA ASILI

Tubadilike sasa,  tuthamini utamaduni wetu, tuachane na hisia za kimwili, turudi katika utamaduni wetu wa asili ya mwafrika, tukumbuke mavazi yetu ya asili kama ilivyo pichani ili tudumishe mila na desturi zetu

Wednesday, November 1, 2017

NASHANGAA MARA HII TUNAANZE MWEZI MPYA NAMI NIMEONA TUANZE MWEZI HUU KIHIVI...

Mdada anashanga utadhani anatoka usingizini ...lakini hapo ni kwamba anashanga kumbe leo ni mwezi mpya....natumaini wenzangu hajashangaa kama mimi Kapulya....
PANAPO MAJALIWA...

Tuesday, October 31, 2017

MWANAMKE MWENYE MIAKA 120 ANAASA WANANCHI KUTOSHABIKIA VITA .

Mwanamke Mwenyeumri wa miaka zaidi ya  120  mkazi wa Peramiho B wilayani Songea mkoani Ruvuma ambaye huenda  akawa mmoja wa wa watu wenye umri mkubwa duniani Bi. Sophia Haule ambaye alishuhudia vita  ya kwanza ya dunia ,ya pili na vita vya maji maji anaiasa jamii kutoshabikia vita.
Ni simulizi ya kusisimua ya bibi. Sophia haule mwenye umri wa miaka  120  ambaye alishuhudia vita ya kwanza ya dunia mwaka 1914-1918, vita ya pili ya dunia mwaka 1939 hadi mwaka 1945 na vita vya maji  maji na kuona machungu ya vita na  anasema vita si vya kuvikimbilia.
Varelia ngonyani ni mwenye miaka 77 ni mtoto wa bibi  sophia haule pamoja na kueleza changamoto za kumtunza mzee huyo menye  umri mkubwa zaidi lakini anaeleza mambo aliyosimuliwa na mama yake yaliyokuwa yakifanywa na machifu likiwemo la kuzikwa na binadamu akiwa hai pindi chifu anapozikwa.
Jimbo la Peramiho limebarikiwa kuwa na watu walioishi umri mkubwa wa miaka 90 hadi 100 ambapo mwenyekiti wa kijiji cha peramiho b anasema anajivunia jambo hilo.
CHANZO: ITV


 

Monday, October 30, 2017

TUANZE JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU NA UJUMBE HUU....PUNGUZA MZIGO, PUNGUZA MARAFIKI WANAFIKI,PUNGUZA KABISA TENA WAPUNGUZE SANA TU, WAPUNGUZE ILI UWE MWEPESI*Punguza marafiki ambao ukiwaambia unataka kufanya kitu wanakujibu "utawezaaa?" Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao kutwa wanataka mchafue meza bar. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao umeongea nao kitu mkiwa wawili mwisho wa siku unakikuta kimeenea sehemu nyingine. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao wako sahihi kila siku wenyewe hawataki kuambiwa wamekosea. Punguzaaaa!* 

*Punguza marafiki ambao wakija kwako wao urafiki unahamia kwa mumeo au mkeo aliyekaa sebuleni wakati wewe kakuacha nje. Punguzaaaa!* 

*Punguza marafiki ambao wanakuwa na urafiki na maadui zako kwa ukaribu zaidi. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki wa kwenye raha tu ukiwa na shida unajikuta peke yako. Punguzaaaa!* 

*Punguza marafiki wanaokusifu huku wakijua umekosea. Punguzaaaa!*

*Punguza marafiki ambao kila ukiwapigia simu na wao utawasikia yaani nilitaka kukupigia sasa hivi. Punguzaaaa!*

*PUNGUZA MIZIGO ISIYOKUWA NA UMUHIMU*
JUMATATU NJEMA  MAANA WIKI IJAYO ITAKUWA JUMATATU YA MWEZI MPYA WA KUMI NA MOJA:-)

Saturday, October 28, 2017

JUMAMOSI YAMWISHO YA MWEZI HUU WA KUMI NAWAKARIBISHENI MILO AIPENDAYO KAPULYA WENU:-) KARIBUNI TUJUMUIKE


Asubuhi:- Mihogo ya kuchemsha.........
..
.....kwa chai ya rangi bila sukari

Mchana ugali kwa maharage, dagaa nyasa, kachumbali kidogo na mbogo majani aina ya
chainizi...kutemshia ni maji...
Jioni ni ndizi mshale kwa nyama... hapa pia kitelemshio ni maji
NAWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA!

Friday, October 27, 2017

IJUMAA YA LEO TUANGALIE/TUCHEZE NGOMA YA MGANDA AMBAYO NI NGOMA MAARUFU ZIWA NYASA


Ngoma ya mganda ni miongoni mwa ngoma maarufu Tanzania ambayo inapatikana mwambao mwa ziwa Nyasa Mkoa wa Ruvuma. Ngoma hii pia maarufu katika nchi ya Malawi. Natumaini utaifurahia basi nikutakieni mwisho mwema wa juma hili. IJUMAA NJEMA!

Wednesday, October 25, 2017

MAISHA YA KIJIJINI YANA UZURI WAKE.....

....ebu angalia mandhari, hewa, vyakula bei nzuri na ndo kwanza vyatoka mashambani. Bila kusahau  ucheshi wa watu. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA...NI Kapulya wenu..

Tuesday, October 24, 2017

HAPA SIJUI MWALIMU YUPI NI BORA:-)

Anayeingia na bia/Kilimanjaro darasani au....
....anayeingia darasani  na silaha ?

Monday, October 23, 2017

JUMATATU HII TUANZE NA UJUMBE HUU....

NI VIZURI KUSAHAU JAMBO LILILO UMIZA MOYO WAKO.  LAKINI NI VIZURI KUKUMBUKA ULICHOJIFUNZA KATIKA JAMBO HILO.
NAWATAKIENI JUMA JEMA

Sunday, October 22, 2017

JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE PAMOJA NANYI....

Walio wengi hudhani Baraka za Mungu ni kufanikiwa kimaisha pekee, kumbe hata kuiona siku ya LEO ukiwa mzima ni Baraka na Neema yake.
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA BARAKA, FURAHA NA AMANI VITAWALE NDANI YA MIOYO YENU .

Friday, October 20, 2017

BLOG YA MAISHA YA MAFANIKIO IMEONA HII PICHA IWE PICHA YA WIKI..KWA VILE...

Imenkumbusha Kapulya mimi  mengi sana wakati nikiwa shule ya msingi...hakuna kuongea kilugha shuleni. Kulikuwa na tabia wanafunzi kuongea sana kilugha mashuleni enzi zangu. Basi walimu wakabuni ya kwamba watengeneza aina ya kakibao kadogo kalikoandikwa hakuna kuongea  kilugha kwa mfano kingoni...basi ukijisahau unaongea unavalishwa kile kibao na mwisho wa siku mwalimu wa zamu anatangaza wote waliovaa/valishwa kile kibao wajitokeze na hapo wote ni bakola tu...Lakini unafikiri kesho yake wale waliochapwa waliacha kuongea kilugha aaahh wapi....Hiki kibao nimekumbuka  jinsi wanafunzi walivyokuwa wanapata mateso... Je nawe una kumbukumbu yoyote ile inayofanana na hii?...KAPULYA wenu....

Thursday, October 19, 2017

KUMBUKUMBU:- STADI/MFUMO WA MAISHA YA JAMII ZETU

Mabinti wakitoka kutafuta kuni mwituni...nimekumbuka mbali sana, siku hizi sijui kama kizazi cha sasa wanajua kuni ni nini?
na hapa ni usafiri wetu.

Wednesday, October 18, 2017

MSIMU WA JOTO WAELEKEA KIKOMO NA PIA KILIMO KWA HIYO IMENIBIDI NIZICHUME NYANYA ZANGU NA KUZIHIFADHI NDANI....

HAPA HIZI ZAONYESHA MAFANIKIO KIDOGO
 Na hapa sijui zitaiva au zitaoza? mwenye MBINU nyingine TAFADHALI nisaidieni...natumaini nitapata msaada toka kwenu...natanguliza shukrani

Kwa pilipili sina mashaka 

Sunday, October 15, 2017

DOMINIKA YA ISHIRINI NA NANE YA MWAKA A

NIMETUMIWA HII NA RAFIKI NIMEONA NI VEMA NIIWEKA HAPA KIBARAZANI ILI WENGI TUPATE KUJUA ...

MASOMO.
Isa.25 :6-10.
Flp.4:12-14,19-20.
Injili Mt 22: 1-14.

WAZO KUU: HAITOSHI TU KUBATIZWA NI LAZIMA PIA KUUISHI  UBATIZO.
UTANGULIZI.
Ndugu zangu leo ni Dominika ya Ishirini na nane ya mwaka A wa kanisa.Tumefika tena siku ya Bwana ili kumsikiliza na kumwabudu.Leo Masomo yetu yanatufakarisha juu ya mwaliko wa Mungu kwa wanadamu wote.Bwana Mungu anawaliaka watu wote kushiriki furaha ya heri ya milele.Mwaliko huo ni wa bure,kuuitikia ni heri,na kuukataa ni hasara kubwa kwa kukosa vinono kwenye karamu ya Mbinguni.Tumuombe Mungu atujalie neema zake ili kukubali mwaliko wake na kubaki katika kanuni za mwaliko huo daima.Tutafakari masomo yetu tukiongozwa na wazo hili,Haitoshi tu kubatizwa ni Lazima pia kuuishi Ubatizo.

UFAFANUZI.
Ndugu zangu,katika somo la kwanza nabii Isaya anaeleza uzuri wa karamu ya Bwana aliyowaanadalia watu wake.Bwana Mungu anawaalika watu wote kwenye sherehe yenye vitu vingi vizuri.Kwanza Mwaliko ni kwa watu wa Mataifa yote.Kutakuwa na vyakula vingi vinono, vilivyandaliwa juu ya mlima wake Mtakatifu.Pili kutakuwa na  uchangamfu mwingi, maana utaji uliotandwa nyusoni mwa watu kwasababu ya huzuni utaondolewa.Tatu Kutakuwa na furaha tele maana hakutakuwa na mauti tena kwa sababu Bwana ataangamiza mauti, kuyafuta machozi ya watu wake,na kuwaondolea aibu yao.

Katika Injili tumesikia Yesu akitoa mfanano wa Ufalme wa Mbinguni kwa Mfano wa Sherehe ya Harusi.Anasema Ufalme wa Mbinguni umefanana na mwaliko wa mfalme aliyewaalika watu kwenye karamu ya harusi ya mwanae.Walioalikwa  walikataa.Akatuma tena watumishi wake kuwaita walioalikwa wafike,vinono ni tayari.Hawa  hawakujali,wakatoa udhuru kuwa wamebanwa na shughuli zao wakaenda kwenye shughuli zao na waliosalia wakawakamata na kuwaua watumishi wa mfalme.Mfalme alikasirika na kuwaangamiza waalikwa wale walitenda mabaya hayo pamoja na mji wao.Kisha aliwatuma watumishi wake kuwaita hata waliokuwa wapitaji tu wa Barabarani ili harusi ijae watu.Harusi ikajaa wageni.Hivyo waalikwa wa kwanza si tu walikataa mwaliko bali pia waliwaua wajumbe waliotumwa kutoa ujumbe wa mwaliko.Nafasi yao ikachukuliwa na waalikwa wa awamu ya pili.Hawa nao waliofika  mmoja hakuwa na vazi la harusi.Alipohojiwa na Mfalme kuwa ameingiaje kwenye harusi bila vazi la harusi? Huyu hakuwa na la kujitetea.Basi Mfalme akaamuru huyu afungwe mikono na miguu na kutupwa nje.

Katika somo la pili mtume Paulo anasema anafaulu kufanya mambo mepesi na magumu kwa sababu ya nguvu ya Kristo anayopata toka kwa Kristo mwenyewe.Anasema anayaweza yote katika Kristo amtiaye nguvu.Anawashukuru wafilipi kwa ukarimu wao kwake kwa msaada waliompatia na anawaombea baraka ya Mungu.

MAISHANI.
Ndugu zangu,mwaliko wa Mungu ni mwaliko wa neema.Tumealikwa kushiriki heri na furaha ya milele bila mastahili yetu.Kama wale walioalikwa toka mwanzo au wale  walialikwa toka  barabarani hawakutarajia kupata mwaliko ule wala hawakufanya chochote ili waalikwe,vivyo hivyo tunaalikwa kushiriki heri ya Mbinguni kwa sababu ya upendo wa Mungu kwetu.Masomo haya yanatutafakarisha maisha yetu ya kikristo.Baada ya kukubali mwaliko wa imani  na kuupokea ubatizo tujue kwamba tunapaswa kuuishi Ukristo wenyewe.Masomo yanatukumbusha kwamba:

Mungu anawaalika watu wote kwenye heri ya Milele Mbinguni.Pamoja na kuwa mwaliko huo wa Mungu ni mwaliko wa furaha kati ya waalikwa hao,wapo wanaokubali na wapo wanaokataa kama ilivyo kwenye mfano wa Harusi.Ni bahati,heri na furaha kualikwa na Mungu.Wale wanaokataa mwaliko wa Mungu wanapata hasara kubwa sana.Ubaya mkubwa wa kuukataa mwaliko wa Mungu si adhabu au mateso atakayopata aliyekataa mwaliko bali ni Kukosa uzuri na vinono vya sherehe ile.Mimi nafikiri ni mateso makubwa sana kukosa kupata kilicho kizuri kuliko vyote na bila tumaini la kukipata tena.Hilo ni teso baya.Pamoja na kuadhibiwa kwa kupata mateso ni kibaya zaidi kukosa vinono.

Tukumbuke kwamba vyenye uzuri visichukue nafasi ya uzuri Mwenyewe.Maana vitu vizuri vimetoka kwa uzuru mwenyewe yaani Mungu.Tusifikiri kwamba mambo yanayoweza kusababisha tusiitikie mwaliko wa Mungu si lazima yawe mabaya.Tumesikia kuwa waalikwa wengine wa kwenye harusi hawakujali mwaliko wa Mfalme,wengine wakaenda shambani na wengine kwenye biashara zao.Si jambo baya kwenda shambani kufanya kazi wala kwenda kwenye biashara,maana hizo ni kazi za mtu kujipatia mkate wake wa kila siku.Ni mambo yaliyo mazuri.Lakini tusisahau kwamba haifai kujishughulisha na mambo mazuri na kumuacha Mungu aliye uzuri wenyewe.Mambo mazuri yanashirikishwa tu sehemu ya uzuri wa Mungu.Mungu ndiyo uzuri wenyewe.Haifai kujishughulisha na kazi za Bwana tukimuacha Bwana wa kazi.

Haitoshi tu kubatizwa ni lazima kuuishi Ubatizo.Tumesikia kuwa wale waliokubali mwaliko wa Harusi na kuingia harusini ,mmoja hakuwa na vazi la harusi.Kilichompata ni kutupwa nje ya ukumbi akiwa amefungwa mikono na miguu.Tulipobatizwa tuliitikia mwaliko wa Mungu.Ni lazima kuendelea kuvaa vazi la ukristo kwa kuuishi Ukristo wenyewe.Vazi la Harusi,yaani vazi la Ukristo wetu ni matendo mema,maisha ya fadhila.Haifai kabisa kuingia katika ukristo na  kuendelea kuvaa mavazi tuliyokuwa nayo kabla ya kubatizwa yaani kuendelea na maisha ya matendo mabaya,maisha ya vilema.Mfalme aliyetualika anataka kutuona na mavazi ya harusi.Tukiingia na mavazi yasiyo,basi tutatupwa nje hata kama tulikubali mwaliko.Tutatupwa nje hata kama ni wakristo.Haitoshi tu kubatizwa ni lazima kuuishi Ukristo.

HITIMISHO.
Hatimaye ndugu,tumalizie tafakari yetu tukijifunza ukarimu kwa watu wote hasa masikini na fukara.Injili inaeleza juu ya mwaliko wa Mfalme kwa watu ili washiriki harusi.Aliandaa vinono vingi kwaajili ya wageni wake.Tunajifunza ukarimu mkubwa wa Mfalme.Jambo hili litukumbushe kuwa mafiga matatu ya kutusaidia kuuishi vizuri ukristo wetu ni kujisomea na kutafakari  Neno la Mungu,Kupokea Sakramenti za kanisa  hasa Ekaristi na kitubio mara nyingi ,na kutenda matendo ya huruma ya mwili na ya roho.Mimi nafikiri haya mafiga matatu ni msaada mkubwa wa kujivalia vazi la harusi ili tusije tupwa nje maana haitoshi tu kukubali mwaliko wa harusi,ni lazima pia kuvaa mavazi ya harusi.

Tumsifu Yesu Kristo!
Na Padre Augustino Kamnyuka.
Parokia ya Kristo Mfalme Bologna-Italia.
Tarehe 15.10.2017.

Thursday, October 12, 2017

YA KALE NI DHAHABU...YAANI YA KITAMADUNI HASA

Ebu tuangalie kuanzia mavazi hadi mitindo ya nywele ...nimependa sana hii. Yabidi tuienzi ndugu zanguni...
...hapa pia ule mtindo wa kutwanga watatu watatu nimekumbuka mbali sana ...yaani mpaka raha..

Tuesday, October 10, 2017

HAYA MATUNDA NI MATAMU SANA....YANAITWA MAPERA

 Mapera yakiwa mtini na hapo unaweza kujua lipi lipo tayari kuliwa.... kuna wengi wanashindwa kula mapera kutokana na kuwa na .....
....mbegumbegu kama uonavyo hapa...basi ni bora kunywa juisi  yake ni tamu sana....Nimeyatamani sana mapera leo....Je kuna tunda wewe umelitamani kwa hivi karibuni?

Wednesday, October 4, 2017

TAFAKARI YA LEO...MWANAMKE ASIYE NA UPENDO KWA NDUGU WA MUME WAKE

Mwanamke asiyekuwa na upendo kwa ndugu wa mume wake tazama mumewe alichomfanyia................  

Siku moja wakiwa wamekaa pamoja mume pamoja na mke wake mume akamwambia mke wake

 "Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu dada zangu na hata baba na mama) tujumuike pamoja na kula pamoaj,,,,

Kesho nitawaalika ili tujumuike nao katika chakula cha mchana, itabidi uandae chakula kwa ajili yao."

Mke akasema kwa unyonge "Sawa mungu akipenda."

Asubuhi ya siku iliyofuata mume akatoka kwenda katika mishughuliko yake lakini baada ya masaa kadhaa akarejea nyumbani na kumuuliza mke wake.

"Mke wangu umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya kama muda wa saa moja watakuwa wameshafika."

Mke akajibu "hapana sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Mumewe akamwambia "Mwenyezi Mungu akusamehe mke wangu kwa nini unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya kuwa wazazi wangu wanakuja

Na kwa nini hukuniambia mapema kuwa hutopika ilihali baada ya muda wa  saa moja wazazi wangu watakuwa hapa nini unafanya mke wangu."

Mke akamjibu "waache waje nitawataka radhi kwani wao si wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Basi mume ikambidi aondoke pale nyumbani kwa kukwepa fedheha.

Baada ya dakika kadhaa mlango ukagongwa mke akaenda kuufungua.

Kwa mshangao mkubwa alipofungua mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake mamaake dada zake pamoja na kaka zake.

Akashtuka kwa mshangao na kuwakaribisha ndani,

Baba akamuuliza kuwa mume wake yupo wapi?

Akajibu yule mwanamke, kuwa alikuwepo hapa ametoka dakika chache kabla hamjafika.

Baba akamwambia "mumeo jana alitupa taarifa kuwa, leo anatuarika hapa tuje kula pamoja chakula cha mchana sasa vipi yeye ametoka si busara."

Yule mwanamke akashtuka kwa taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya kuchanganyikiwa."

Ikambidi aingie ndani na kumpigia simu mume wake akamwambia "kwa nini hukuniambia kuwa wazazi wangu ndio wanaokuja?"

Mumewe akamjibu "Wazazi wangu na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti."

Mke akamwambia "Lete chakula huku chakula kilichokuwepo ni kichache hakitawatosheleza."

Mume akamjibu "Mimi nipo mbali na hao si wageni watakula chochote kilichopo kama wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu.

Hili liwe ni somo kwako juu ya kuwaheshimu wazazi wangu."

*Watendee watu kama vile unavyopenda kutendewa wewe* _Tafakari  na chukua hatua_

Tuesday, October 3, 2017

KILIMO CHA KARANGA...KULE KWETU LITUMBANDYOSI KINALIMWA SANA

Karanga ni moja ya jamii ya kunde kwa wale wasiojua ila sidhani kuna mtu hajui karanga ni nini. Karanga hulimwa kwa lengo la chakula, kutengeneza mafuta  pia kwa ajili ya malisho ya mifugo.

Monday, October 2, 2017

NIMEKUMBUKA MBALI SANA....MAPISHI YA UGALI KWA MTINDO HUU

KUMBUKUMBU:- Mafiga matatu  ni mtindo uliozoeleka sana kwa jambo la mapishi  hasa sisi tuliokulia vijijini...HAYA KILA LA KHERI. JUMATATU NJEMA.

Friday, September 29, 2017

TEMBO ZAIDI YA LA KI MOJA WAMEUAWA KATIKA HIFADHI YA SELOUS MKOANI RUVUMA


Hayo yamebainishwa katika maadhimisho ya siku ya tembo kitaifa katika mji mdogo wa LUSEWA wilayani NAMTUMBO mkoani ruvuma katika pori la hifadhi ya wanyama pori SELOUS

Thursday, September 28, 2017

HII IWE PICHA YA WIKI....KATIKA WANYAMA NIWAPENDAO TWIGA NI NAMBA MOJA....

Wiki inakaribia kwisha sasa leo ni ALHAMIS nami nimeona hii iwe picha ya wiki hii sio mbaya kama ikiwezekana kufanya utalii wa ndani ili kupumzisha akili...
Chanzo cha picha ni kutoka kwa blog ya Mjegwa.  PANAPO MAJALIWA TUTAONANA. UJUMBE: TUKUMBUKANE SISI  SOTE NI WANANDUGU

Monday, September 25, 2017

WIKI HII TUANZE NA ZILIPENDWA KWA NJIA YA UJUMBE WA MZIKI


NAWATAKIENI WOTE MWANZO MWEMA WA SIKU AMBAYO KILA WIKI INAANZA NA JUMATATU:-) KAPULYA WENU.

Friday, September 22, 2017

BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO IMECHAGUA HII PICHA IWE PICHA YA WIKI

Napenda kuwatakieni wote mtakaopita hapa mwanzo mwema wa mwisho wa wiki tusisahau kutakiana hali, kwani salamu ni nusu ya kuonana...PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA AMANI NA FURAHA ITAWALE MIOYONI  MWENU. MNAPENDWA WOTE!

Thursday, September 21, 2017

MAZINGIRA NA BARABARA ZAKE MKOANI RUVUMA....TUTAFIKA KWELI?


Barabara ya Lituhi-Songea yafungwa  na wananchi wa Ruanda kwa sasabu ya vumbi za magari.....

Wednesday, September 20, 2017

TUKUMBUKE ZAMANI:- HISTORIA YA TAIFA LETU KATIKA PICHA.......

DAR ES SALAAM:- WANAWAKE WAFUNGWA WAKITENGENEZA BARABARA
ASKARI WAPO KATIKA GWARIDE  KATIKA HOSPITAL YA OCEAN ROAD