Wednesday, October 4, 2017

TAFAKARI YA LEO...MWANAMKE ASIYE NA UPENDO KWA NDUGU WA MUME WAKE

Mwanamke asiyekuwa na upendo kwa ndugu wa mume wake tazama mumewe alichomfanyia................  

Siku moja wakiwa wamekaa pamoja mume pamoja na mke wake mume akamwambia mke wake

 "Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu dada zangu na hata baba na mama) tujumuike pamoja na kula pamoaj,,,,

Kesho nitawaalika ili tujumuike nao katika chakula cha mchana, itabidi uandae chakula kwa ajili yao."

Mke akasema kwa unyonge "Sawa mungu akipenda."

Asubuhi ya siku iliyofuata mume akatoka kwenda katika mishughuliko yake lakini baada ya masaa kadhaa akarejea nyumbani na kumuuliza mke wake.

"Mke wangu umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya kama muda wa saa moja watakuwa wameshafika."

Mke akajibu "hapana sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Mumewe akamwambia "Mwenyezi Mungu akusamehe mke wangu kwa nini unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya kuwa wazazi wangu wanakuja

Na kwa nini hukuniambia mapema kuwa hutopika ilihali baada ya muda wa  saa moja wazazi wangu watakuwa hapa nini unafanya mke wangu."

Mke akamjibu "waache waje nitawataka radhi kwani wao si wageni hapa watakula chochote watakachokikuta."

Basi mume ikambidi aondoke pale nyumbani kwa kukwepa fedheha.

Baada ya dakika kadhaa mlango ukagongwa mke akaenda kuufungua.

Kwa mshangao mkubwa alipofungua mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake mamaake dada zake pamoja na kaka zake.

Akashtuka kwa mshangao na kuwakaribisha ndani,

Baba akamuuliza kuwa mume wake yupo wapi?

Akajibu yule mwanamke, kuwa alikuwepo hapa ametoka dakika chache kabla hamjafika.

Baba akamwambia "mumeo jana alitupa taarifa kuwa, leo anatuarika hapa tuje kula pamoja chakula cha mchana sasa vipi yeye ametoka si busara."

Yule mwanamke akashtuka kwa taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya kuchanganyikiwa."

Ikambidi aingie ndani na kumpigia simu mume wake akamwambia "kwa nini hukuniambia kuwa wazazi wangu ndio wanaokuja?"

Mumewe akamjibu "Wazazi wangu na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti."

Mke akamwambia "Lete chakula huku chakula kilichokuwepo ni kichache hakitawatosheleza."

Mume akamjibu "Mimi nipo mbali na hao si wageni watakula chochote kilichopo kama wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu.

Hili liwe ni somo kwako juu ya kuwaheshimu wazazi wangu."

*Watendee watu kama vile unavyopenda kutendewa wewe* _Tafakari  na chukua hatua_

4 comments:

NN Mhango said...

Bonge ya somo kwa yale makabila yenye kusifika kwa mambo ya kipuuzi kama uchoyo. Japo si wote, wasichana wa siku hizi wamezidi roho mbaya. Wakati linachumbiwa linajifanya lina heshima na sifa zote. Baada ya kuingia ndani mengi yanatoa makucha na kuchukia wazazi na hata ndugu wa mume bila kujua kuwa bila wazazi lisingempta huyu linayetaka kummilki. Alichofanya huyu baba ni somo tosha ila kwa wenye akili. Asante sana da Yasinta kuleta kitu hii.

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Mhango naona hapa umekasirika sana...unajua kuna watu katika dunia hii hujijali sana wenyewe au niseme hujipendelea sana katika upande wake..Utakuta hata mke humkataza mume wake asiihudumie familia yake afadhali ya huyo alikataa kuwahudumia ndugu wa mume...huwa inachangaza sana...

Prince Emac said...

O.M.G!!!!!! Wanawake Mungu anawaona jaman duuuuh!!!!!

Yasinta Ngonyani said...

Prince ndugu yangu uzidi kuwaomnea wanawake.... Ahasnte kwa mchango wako.