Sunday, October 22, 2017

JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE PAMOJA NANYI....

Walio wengi hudhani Baraka za Mungu ni kufanikiwa kimaisha pekee, kumbe hata kuiona siku ya LEO ukiwa mzima ni Baraka na Neema yake.
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA BARAKA, FURAHA NA AMANI VITAWALE NDANI YA MIOYO YENU .

2 comments:

NN Mhango said...

Maisha ni zawadi si haki
Hata uwe maridadimwenzio usidhihaki
Wote kule tutarudi kwa furaha hata dhiki
Maisha ukifaidi umshukuru Maliki
Kwani siku ya kurudi wote ni kindakindaki

Ukiona wapumua jua wapo wenye haki
Hawakuliona jua tofauti na waso haki
Hakuna anayejua vipimo vyake el Shaddai
muhimu ni kutambua kuwa hakuna unachodai
Kwa kila unapumua ni sababu ya al Muta'aali

Pumzi unayovuta ni yake Hamiydu
Na mali unayopata ni yake al Muyidu
Maringo unayonata ni yake al Maajidu
Mateso unayopata anayajua Assamadu

Yasinta Ngonyani said...

Duh! kaka Mhango umeyapatia madhaifu yangu ahsante. Na kweli ulichosema ni kweli yabidi tukumbushane....