Friday, October 20, 2017

BLOG YA MAISHA YA MAFANIKIO IMEONA HII PICHA IWE PICHA YA WIKI..KWA VILE...

Imenkumbusha Kapulya mimi  mengi sana wakati nikiwa shule ya msingi...hakuna kuongea kilugha shuleni. Kulikuwa na tabia wanafunzi kuongea sana kilugha mashuleni enzi zangu. Basi walimu wakabuni ya kwamba watengeneza aina ya kakibao kadogo kalikoandikwa hakuna kuongea  kilugha kwa mfano kingoni...basi ukijisahau unaongea unavalishwa kile kibao na mwisho wa siku mwalimu wa zamu anatangaza wote waliovaa/valishwa kile kibao wajitokeze na hapo wote ni bakola tu...Lakini unafikiri kesho yake wale waliochapwa waliacha kuongea kilugha aaahh wapi....Hiki kibao nimekumbuka  jinsi wanafunzi walivyokuwa wanapata mateso... Je nawe una kumbukumbu yoyote ile inayofanana na hii?...KAPULYA wenu....

2 comments:

NN Mhango said...

Haya ni matokeo ya elimu mfu na yenye sumu (toxic education) tuliyojazwa na wakoloni kiasi cha kujidharau wenyewe na mila zetu. Leo tunaitana makafiri, wenye dhambi kwa sababu ya kulewa mila na dini nyemelezi za kikoloni. Kwani kimakonde chiyo lugha kama nyingine? Afrika inahitaji kuanza kufikiri kuwa na aina mpya ya elimu yenye kulenga kuweka huru vichwa vyetu (detoxified education). Bila hii tutaendelea kuwa masanamu meusi yenye roho za kizungu kwa maafa yetu na vizazi vyetu hapo baadaye. Hii dhana nimeiongelea kwenye kitabu changu kijacho cha Decolonising Education to Achieve World Peace: Doing Away with Relics of Colonial Education Embedded in the Racist Dominant Grand Narrative .

Yasinta Ngonyani said...

Halafu unajua kuna wakati nilikuwa najuuliza hivi kama shule zote nchini zingekuwa zikifundishwa kilugha sijui watoto wangapi wangekuwa na uelewa zaidi kuliko sasa...ila pia najiuliza je na ofisi nazo tungesema kilugha? na basi ingebidi tuwe ndani ya nchi ...hapo nabaki bila jibu. Ila pia nasikitika kwa mtindo huu wa kuvalishana vibao na kuadhibiwa unapelekea lugha za asili kupotea...