Showing posts with label songea. Show all posts
Showing posts with label songea. Show all posts
Saturday, July 6, 2019
Wednesday, October 17, 2018
LEO TUTEMBELEE KWETU SONGEA KIJIOGRAFIA
Huu ni mlima MATOGORO uliopo kkaribu na kijiji cha MAHILU kilichopo Songea
Hapa ni magharibi ya kijiji cha Mhukuru twakutana na mlima kipululu
Mlima Litimbanjuhi uliopo karibi na kijiji cha Namatuhi
Hapa pia ni mlima Manolo uliopo kijiji cha Namatuhi pia
Kama watoka Wino kuelekea Iringa utaona mandhari hii nzuri ya milima
Saturday, April 14, 2018
KUMBUKUMBU:- USISAHAU ULIKOTOKA KWANI NDIYO MSINGI WA MAISHA
Hapa ni kwetu MAHENGE SONGEA MAMA, MIMI NA BABA
NA ha pa ni kaka yangu mdogo XVERY ilikuwa mwaka jana mwezi wa kumi na mbili kwa kweli ilikuwa ni furaha sana kuweza kuonana
Wednesday, February 7, 2018
SAFARI HII NILIPOFIKA SONGEA/RUHUWIKO NILIKUTANA NA KITU HIKI
RUHUWIKO HUNT CLUB
Ndugu zanguni ufikapo/ukitembelea Songea usikosa kupitia hii sehemu ni sehemu nzuri kupumzika na kupata chakula kid
CHIPS NA SAMAKI
Tuesday, May 31, 2016
HUU NDI UTAMADUNI WETU NA UASILI WETU WANA SONGEA/RUVUMA
NGOMA ZIKIPIGWA TAYARI KWA KUCHEZA ´LIZOMBE
Na hapa ni kikundi cha mchezo wa lizombe tayari wakiwa wamevalia sare zao kwa umaridadi kabisa...tusisahau uasili wetu. Tuwasimulie watoto wetu kama tutakuwa hatuna picha au sauti iimbayo ni muhimu sana nao wajue wapi kiini kilipotoka.
Thursday, May 26, 2016
NGOJA TUTOKE MOROGORO NA KUELEKEA SONGEA KWETU AMBAKO NI NYUMBANI - KIJIJI CHA LUGAGARA
SHULE YA MSINGI LUGAGARA
Lugagara , ipo katika Kata ya Kilagano , Songea Vijijini , Mkoa wa Ruvuma Lugagara ni kijiji ambacho kipo nje ya Songea karibu na Peramiho katika Kata ya Kilagano . Kijiji hiki kina Wakazi wasiozidi 3,700. Thursday, May 12, 2016
UPELEKAJI MIHOGOCHINA WAZUA BALAA BUNGENI
Mbunge huyo alisema jana kuwa, kauli hiyo inapingana na hotuba ya waziri huyo iliyosheheni mipango ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo mwaka 2025.
Mbali na mbunge huyo, wabunge wengi waliochangia hotuba hiyo bungeni walionyesha wasiwasi wa Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa vile Serikali haielezi itajenga viwanda vya aina gani.
Gama alimtaka waziri huyo kufuta kauli yake ya kupatikana kwa soko la mihogo China kwani inapingana na mipango aliyoianisha na pia ni kuhamishia ajira nchini humo.
“Mheshimiwa Mwijage aone namna ya kufuta ile kauli. Kuna kauli moja alitoa Aprili 19, alisema anawaomba wananchi wa Lindi wazalishe kwa wingi muhogo umepata soko China,” alisema mbunge huyo.
“Sasa kwa maelezo haya, tukipeleka muhogo China maana yake tunahamisha ajira China. Kama viwanda viko China vya kuchakata muhogo kwa nini visije Tanzania?” alihoji.
Mbunge huyo alisema ni vyema viwanda hivyo vikajengwa Lindi na Songea ili mchakato wa kusindika muhogo ufanyike Tanzania na siyo China na kuwa katika hilo hatamuunga mkono.
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Annatropia Loikila aliitaka Serikali itumie msemo kuwa “ipo siku moja Tanzania inaweza kuwa na uchumi wa viwanda” badala ya kutoa hakikisho.
“Nimeona ni namna gani tunataka kuwahadaa wananchi kwamba Tanzania itakuwa ya uchumi wa kati ifikapo 2025. Ni bora tuseme iko siku moja tunaweza kwenda kwenye uchumi wa kati,” alisema.
Mbunge wa Bagamoyo (CCM), Dk Shukuru Kawambwa alisema tangu 2008 Serikali ilipofanya tathmini ya fidia, wananchi hawajalipwa ili eneo hilo liwe huru kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.
Hata hivyo, Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alisema Serikali ni lazima iwe na mtazamo unaoeleweka kwamba inataka kujenga viwanda vya aina gani badala ya kutoa kauli ya jumla.
“Waziri ni lazima utuambie unataka kujenga viwanda vya nini. Focus (mkazo) yetu ni nini? Tungeanza na viwanda vya sukari, mafuta ya kula na ngozi ili wakulima wetu wafaidike,”alisema.
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Hawa Mwaifuga aliitaka Serikali kulinda kwanza viwanda vya ndani kabla ya kufikiria kujenga vipya akisema bidhaa kutoka nje ndizo zinaua viwanda.
CHANZO:- Daniel Mjema, Mwananchi- Tuesday, May 10, 2016.
CHANZO:- Daniel Mjema, Mwananchi- Tuesday, May 10, 2016.
Monday, April 18, 2016
TUANZE HII WIKI KWA KUUTEMBELEA MJI WETU SONGEA: TATIZO LA MAJI LAPELEKEA WANANCHI KUHARA DAMU ....
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkenda Songea Vijijini, Mkoani Ruvuma, mpakani mwa Tanzania na Msumbiji wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji na kulazimika kunywa maji yanayopatikana kwenye vidimbwi na maji ya Mto Ruvuma na hivyo kukumbwa na magonjwa ya kuharisha.
Thursday, February 11, 2016
SONGEA: MPUNGA WATUMIKA KUTENGENEZEA POMBE!
Pombe inayotokana na mpunga ikiandaliwa kwa kuchemshwa
Ubovu wa Barabara katika kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Wilaya ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma, unasababisha mpunga kutengeneza pombe ya kienyeji.
Pombe hiyo ijulikana kama pombe ya mpunga, inachangwanya kwa mapumba laini ya mpunga, kwa kuyaloweka kwa siku tatu, pia wanachanganya na uji wa ulezi uliolowe kwa kwa siku tatu.
Baada ya kuchanganya inalowekwa kwa siku mbili, siku ya tatu wanaweka unga wa mchele na kuipika katika pipa kubwa kwa masaa matatu, inakuwa imeiva tayari kwa kunywa. Lita moja Tsh. 400, ubovu wa barabara na kukosa soko la zao la mchele unaolima kwa wingi ndio unasababisha mchele huo tutengeneze pombe ya mpunga kwa kujipatia kipato
“Mazao mengi tunalima lakini hakuna barabara ya uhakika kusafirisha mazao mpaka soko kuu la mazao SODECO Songea, unaweka mpunga ndani mpaka unaliwa na wadudu na kuharibika, ukiwa na mpunga inakubidi utengeneze pombe ya mpunga ili usiharibike,” Alisema Emanuel Komba.
Wanakijiji wa Ifinga wanalima mazao ya chakula na biashara lakini wanakwama kufikisha katika soko la mazao SODECO kwa ubovu wa barabara, mazao hayo kama mtama, ufuta, tangawizi, ndizi, ulezi, uwele, mpunga, maharage na miwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Beatrice Msomisi, alikili kuwepo kwa ubovu wa barabara katika kijiji hicho, alisema sio Ifinga tu Vijiji vingi vya Wilaya ya Songea barabara zake ni bovu sana.
Kipindi cha Masika barabara mbalimbali za vijijini hazipitiki kiurahisi kwa sababu ya ubovu, sio mazao tu kuletwa sokoni, hata mgonjwa na kufikisha madawa kwenye Zahanati mbalimbali ni tatizo kubwa.
“Bajeti ninayopewa katika barabara ni ndogo sana napewa Tsh. Milioni 600 kwa mwaka, za kukarabati barabara mbalimbali za vijijini na mjini, pesa ni ndogo sana ukilinganisha na hali halisi ya ubovu wa barabara hizo na ukubwa wake,” alisema Msomisi.
Milioni 600 tunayopewa kwa ajili ya kukarabati barabara ni ndogo sana ukilinganisha na ubovu wa barabara zenyewe, pesa hiyo ukikarabati barabara kwa kiwango kizuri ikiwa inapitika kipindi cha masika na jua kali unakarabati barabara moja tu. Umbali wakutoka kijijini kwa kutumia gari ni masaa 2 na nusu kwa pikipiki ni masaa 3 hadi 4.
Aidha aliiomba Wizara husika kuwaongezea pesa katika ukarabati wa barabara mbalimbali za Wilaya hiyo, kwa sababu ziko katika hali mbaya sana na kipindi kama cha masika hazipitiki kabisa na kunakuwa hakuna mawasiliano kati ya Vijiji na Wilaya.
Kutoka Ifinga mpaka kufika makao makuu ya Wilaya ya Songea ni kilometa 219, na kilometa 48 ni barabara ya vumbi, Wilaya ya Songea ina ukubwa wa kilometa za mraba 16,000 idadi ya watu kwa sensa ya mwaka huu ni 170,000.
Imeandikwa na Mariam Mkumbaru January 3rd, 2013.
Ahsante kwa makala hii labda niingezee kidogo hapa ni kwamba kijiji hicho pia ni hulima machungwa au walikuwa wanalima machungwa na wwalikuwa wakibadilishana machungwa kwa chumvi kama mtu alikwenda huko na chumvi yake. Nasema hivi kwa vile kuna mtu ambaye yupo karibu sana nami alishafanya hivyo. Walifurahi sana kupata chumvi na yote inatokana na kutokuwa na usafiri/barabara nzuri.
Wednesday, January 27, 2016
Wednesday, October 7, 2015
SHUJAA WETU HAKUSALITI JAMAA ZAKE NA UTAWALA WAKE.....!!!!!
Nduna Songea Mbano, muda mfupi kabla ya kuuawa
Nduna Songea: Shujaa wa Wangoni aliyewapeleka puta wajerumani..SHUJAA WETU HAKUSALITI JAMAA ZAKE NA UTAWALAWAKE..!!. HUWEZI kuielezea na kuikamilisha historia ya vita ya Majimaji na ukombozi wa nchi yetu
bila kumtaja shujaa wa kabila la Wangoni, Nduna Songea Mbano ambaye jina lake lilipewa hadhi ya kuuita mji wa Songea kutoka kwenye jina la Ndonde mwaka 1906.
Kiongozi huyo alikuwa ni miongoni mwa wasaidizi ( Nduna) 12 wa Chifu wa kabila la wangoni (Nkosi) chifu Mputa bin Gwezerapasi Gama. Wasaidizi wake wengine walikuwa ni Mgendera Mawaso Gama, Kohongo Magagura, Mputa Mkuzo Gama, Magodi Mbamba Mbano, Mtekateka Muyamuya Tawete, Fratela Fusi Gama. Manduna wengine ni Maji ya Kuhanga Komba, Zimanimoto Gama, Mpambalyoto Soko Msalawani, Mtepa Hawaya Gama na Nduna Mkomanile ambaye alikuwa ni mwanamke pekee kuwa nduna.
Nduna Songea Mbano alikuwa maarufu kuliko manduna wenzake na hata chifu Mputa Gama alikuwa anamtegemea sana katika kuwaongoza manduna na wapiganaji wa vita ya Majimaji kiujumla. Mhifadhi kiongozi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea, Philipo Maligissu
akizungumzia maisha ya Nduna Songea Mbano katika viwanja vya Makumbusho hayo, anasema kuwa Nduna Songea Mbano weledi ndio uliompa umaarufu sana.
Kutokana na weledi na ushadi wake, aliwazidi wenzake 11 katika mbinu za kuandaa mikakati ya kivita, kutoa uamuzi mzito pasi na kutetereka na kusimamia utekelezaji wake kikamilifu.
Kwa umakini mkubwa, Nduna Songea Mbano aliweza kufanya kile alichokuwa akikiamini na uthibitisho wa jambo hilo ulianza kujitokeza Julai 12, 1897 katika viwanja vya Bomani kwa mkuu wa Wilaya wa Wajerumani, Luteni Engelhardt.
Maligissu anasema rekodi zilizopo zinaonesha kuwa tarehe hiyo Nduna Songea Mbano, alionekana kuwa ni mtu wa kipekee katika idadi ya manduna 11 ambao walikuwa wasaidizi
wa Chifu Mputa Gama kwa kitendo chake cha kubisha wazi wazi tamko la utawala mpya wa Wajerumani la kutaka Wangoni wakomeshe biashara ya utumwa.
Siku hiyo ilikuwa ni rasmi ambayo utawala wa kikoloni ulikuwa unaanzishwa katika mji wa Songea, wakati huo ukiitwa Ndonde na Mkoa wa Ruvuma kiujumla ukiwa chini ya Luteni
Engelhardt aliyekuwa Mkuu wa Jeshi Kanda ya Kusini.
Wajerumani walipofika kuanzisha makoloni yao katika maeneo ya ukanda wa kusini walikutana na msuguano mkubwa kutoka kwa tawala za Kiafrika, hasa tawala za Wangoni.
Maligissu anasema kuwa Wangoni walikuwa na tabia ya kwenda mikoa ya Lindi na Mtwara
kuvamia, kuchukua mateka na kuwapeleka Songea kuwafanyisha shughuli mbalimbali katika maeneo yao ya utawala wao.
Tabia hiyo ya Wangoni iliwachukiza sana Wajerumani, kwani walikuwa wanaheshimu sana makubaliano yaliyofikiwa kutoka kwenye mkutano wa Berlin wa 1884 /85.
Katika mkutano huo moja ya makubaliano ni na kila nchi yenye koloni barani Afrika ikomeshe biashara ya utumwa, hasa ikizingatiwa kwamba Wajerumani walikuwa wamejiimarisha sana.
Hivyo walipofika Ruvuma wakatoa tamko kwa Wangoni kuwa hairuhusiwi na haitaruhusiwa tena kwenda Lindi, Mtwara au kokote kuchukua mateka na kwamba mateka wote waliochukuliwa na Wangoni waachiwe huru.
Baada ya Wajerumani kutoa tamko hilo, ndipo Nduna Songea Mbano alipojitokeza waziwazi
na kusimama kujibu hoja iliyotolewa na Wajerumani kuhusu tamko hilo.
Nduna Songea Mbano alisema kuwa utawala wa kabila la Wangoni hauwezi kutekeleza tamko hilo na kwamba msimamo wao ni kutoutambua utawala mpya wa Kijerumani na tamko lao.
Kwamba ujio wa Wajerumani na tamko lao kwa Wangoni vililenga kudhoofisha utawala wa machifu na manduna katika maeneo yao kwa kufuata kanuni zao za kimila na kitamaduni.
Kuanzia hapo Wajerumani walimwona Nduna Songea Mbano kuwa ni mtu hatari sana katika utawala wao mpya, hivyo kumweka alama maalumu na kuanza kumfuatilia nyendo zake.
Alionekana kuwa kiongozi shupavu mwenye misimamo mikali na anayezingatia heshima na utu wa kabila lake bila kuyumbishwa. Alionekana kuwa pekee mwenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi katika mazingira yoyote kwa kushirikiana na wananchi wake ambao walikuwa
wanamheshimu sana na kumsikiliza.
Maligissu anaeleza kuwa Nduna Songea Mbano alikuwa na uwezo mkubwa wa kuwaunganisha
wananchi wake na kuwa na umoja, upendo na mshikamano na kwamba alikuwa akiwaelekeza jambo wanalifanya kwa umakini na kwa ukamilifu.
Nduna Songea Mbano aliendelea kujizolea umaarufu mkubwa na baada ya kutamka kuwa yupo tayari kwa lolote lile na hawezi kukubali kuona tawala za Kiafrika zinadharauliwa na wakoloni kwa namna yeyote ile.
Wajerumani wakaamua kuwaalika machifu na manduna wote Julai 13, 1897 Bomani kwa mkuu wa wilaya na kuwaambia kuwa mtu yeyote katika eneo lake atakayekaidi amri yoyote kutoka kwa uongozi mpya wa Wajerumani atapigwa risasi, kunyongwa hadi kufa au kufungwa maisha. Siku hiyo hiyo machifu na manduna walichukuliwa hadi juu ya mlima wa shabaha wa Chandamari, katikati ya mji wa Songea na kuoneshwa nguvu ya risasi inavyoweza kufanya kazi katika mwili wa binadamu na kwamba silaha za kijadi na kimila za Wangoni hazingeweza kufua dafu mbele ya silaha hizo.
Licha ya Wajerumani kutoa vitisho vingi, Nduna Songea aliendelea na msimamo wake wa awali wa kuchukia na kuupinga utawala wa Wajerumani na kuutetea utawala wa Kiafrika mpaka ilipokuja kutokea Vita ya Majimaji. Nduna Songea alitoa ushindani mkubwa sana katika vita hivyo na kuonesha ustadi mkubwa kwenye mapigano na katika sehemu zote ambazo Wajerumani walipigana, wameandika kuwa hawakupata ushindi mkubwa kama waliopata katika mkoa wa Ruvuma, zamani nchi ya Ungoni.
Viongozi wao hawakuwa wanafiki, kwani walijitoa kikwelikweli kusaka ukombozi na hadhi ya tamaduni zao mpaka dakika ya mwisho. Ndio maana idadi kubwa ya watu walionyongwa katika historia ya Tanzania walitoka katika himaya ya Nduna Songea Mbano na ushahidi upo wazi kuwa watu 67 walihukumiwa kunyongwa hadi kufa, akiwamo Nduna Songea Mbano.
Katika kuonesha kuwa Nduna Songea alikuwa na uwezo wa kufanya mambo kwa weledi mkubwa bila kusaliti dhamira yake kuanzia mwaka 1897 aliandaa jeshi lake la kupambana na utawala wa Wajerumani.
Akaanza kuchukua watu wake na kuwapeleka juu ya mlima wa Chandamari kufanya nao mkutano, kutoa mafunzo ya kivita na kuwaelekeza kwa nini Wajerumani wachukiwe.
Katika mlima huo ndipo alipoeleza kwa kina madhara ya kuukubali utawala wa Wajerumani
na kutoa ahadi kwa wananchi wake ya kuwaondoa Wajerumani kwa lazima na kuwa eneo hilo ni la Wangoni, wamekuwa wakiishi siku zote chini ya utawala wao, hivyo haiwezekani wapelekewe utawala mpya wakati hawauhitaji.
Chokochoko hizo zilizaa vita vya Majimaji na wakati mapigano yakiendelea Wajerumani walianza kumtafuta Nduna Songea ili wamkamate na kufanya naye mazungumzo ya maridhiano. Kumbe Songea Mbano alikuwa amejificha kwenye pango kubwa lililopo kwenye mlima wa Chandamari na usiku alikuwa akikutana na askari wake nje ya pango hilo na kuwapa mafunzo zaidi ya kivita. Maligissu anaeleza kuwa Nduna Songea alikuwa anaishi na ndugu zake katika eneo la Mateka, leo hii manispaa ya Songea na wakati wa vita ndipo Songea Mbano alikuwa anajificha katika pango hilo ili wasimkamate mpaka atakapotimiza malengo yake. Wajerumani walipoona wanaendelea kupata madhara makubwa kutokana na vita hivyo, waliamua kuwakamata ndugu na familia yake, Chifu Mputa Gama na manduna wengine na kuwafunga gerezani kwa lengo la kumdhoofisha Nduna Songea.
Baada ya Wajerumani kumdhoofisha Nduna Songea alipata taarifa zote na akaamua kutoka
kwenye pango hilo na kwenda kwa Wajerumani na kutaka watu wake waachiwe ili mapigano yaendelee. Ndipo naye alipokamatwa na kuswekwa gerezani na Wajerumani wakawahukumu wafungwa hao kunyogwa hadi kufa. Wafungwa hao waliamriwa kuchimba shimo kubwa bila kujua ndilo lingekuwa kaburi lao na ilipofika siku ya kifo chao, walinyongwa kwa zamu kwa muda wa siku mbili na maiti zao kuwekwa kwenye kaburi hilo hadi walipofikia 66 ndipo walizikwa kwa pamoja. Walimwacha Nduna Songea Mbano ili awasaidia kutimiza malengo yao kwa wananchi, kwani waliamini akiwa kiongozi jasiri na anayependwa na watu wake angesikilizwa vizuri. Tangu siku hiyo walipomwacha bila kumnyonga, Nduna Songea aliwasumbua Wajerumani na kutaka naye anyongwe kama ndugu zake, kwani hakuona sababu ya yeye kuishi wakati ndugu zake alishauawa; akasema wasipomnyonga angegoma kula na kunywa chochote mpaka afariki dunia. Ndipo Wajerumani walipoamua kumnyonga na kumzika katika kaburi la peke yake, wakiamini kuwa ni mtu wa pekee mwenye ushujaa, uamuzi mzito na msimamo usioyumba. Walimuenzi kwa kubadilisha jina la mji wa Ndonde na kuubatiza jina la Songea, ambapo mpaka sasa linatumika kuuita mji huo wenye hazina kubwa ya historia na utalii wa kitamaduni.

KATIKA PITAPITA MTANDAONI NIMEKUTANA NA HII MADA YA KIHISTORIA YA WANGONI NIKAONA SI MBAYA KAMA NIKIWEKA HAPA MAISHA NA MAFANIKIO UKIZINGATIA ASILI YANGU NI MNGONI....PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA......NA CHILAWU MEWAWA/NA KESHO HIVYOHIVYO
Monday, June 22, 2015
HAYA JAMANI NI WIKI NA JUMATATU NYINGINE....TUTEMBELEE SONGEA KWETU ....
Ndo kwanza kunakucha .....na Jua hilo lachomoza...Basi niwatakieni wote jumatatu njema najua wengi mko mzigoni...Binafsi nitapotea kidogokidogo kuwa na famalia.Ila nipo:-)
Saturday, January 24, 2015
JUMAMOSI NJEMA...NIPO NA KAKA ZANGU KATIKA UPANDAJI WA MITI RUHUWIKO/SONGEA 2015 JANUARI
Nipo na kaka zangu tunapanda miti, huu mti niliosimama nao karibu niliupanda mwaka 2013 na sasa umenipita urefu kazi kwelikweli. Kata miti na pia panda miti kwani ndio uhai. Huu ndio ujumbe wangu wa leo!JUMAMOSI NA MWISHO WA JUMA MWEMA!! KAPULYA.
Sunday, November 30, 2014
JUMAPILI NJEMA NA KWAYA HII YA VIJANA KKKT SONGEA MJINI WIMBO WAITWA ZAWADI
Kama usemavyo wimbo huu basi nami napenda kumshukuru Mungu kwa kutupa afya njema mwezi huu. Maana nayo ni ZAWADI. Nimefurahi sana kuusikiliza huu wimbo nawe ukipata wasaa sikiliza. JUMAPILI HII YA MWISHO WA MWEZI IWE NJEMA KWA WOTE
Friday, July 4, 2014
NIMETAMANI NYUMBANI RUHUWIKO LEO
HAPA NDIPO KWETU RUHUWIKO ...NA LEO NIMEKUMBUKA MNO KUNYUMBA/NYUMBANI. NAWATAKIENI IJUMAA NJEMA PIA MWANZO MWEMA WA JUMA...KAPULYA WENU:-)
Thursday, April 3, 2014
UKIFIKA/PITA SONGEA USIKOSE KUPITIA HAPA ILI KUPATA CHAKULA CHA HARAKA NA KINYWAJI KIDOGO....SONGEA/LIZABONI!!!
Sehemu hii ipo Songea katika mtaa wa LIZABONI kwa wale wasio wenyeji wa Songea...Mara nyingi sana hapa huwa ni kituo chetu kupata nyama ya Nguruwe/kitimoto..mtanisamehe kwa wale waiotumia/kula mnyama huyu.
Kitu kingine kilichonifanya kuweka hii picha ni kwamba nimekumbuka enzi zileeee mtu unaweza kuwa safarini na usione sehemu ya kula kunywa ndo kabisa kama usipokuwa na chakula mwenyewe au kupita kwa ndugu na kupata chakula kidogo. Nakumbuka nilipokuwa nasafiri enzi hizo mama na baba walikuwa wananiandalia karanga zilizopondwa na chumvi(wangoni tunaita CHIMBONDI) Basi ukila hii inabidi uwe karibu na mto ili kupata maji ya kutelemshia. Leo vyakula vya haraka kila mji(Fasta food) Sijui ipi ni bora? Je nawe unakumbuka kitu kama hiki au tofauti?

Thursday, March 20, 2014
KWA KIFUPI:- HAPA NI HISTORIA YA MASHUJAA NA MAKUMBUSHA YA VITA YA MAJIMAJI SONGEA!!!
Siku ya leo nilikuwa najisomea kitabu changu kiitwacho THE HISTORY OF THE WANGONI KILICHOANDIKWA NA FR ELZEAR EBNER, OSB..Nitawaonyesha siku nyingine. Nachotaka kusema hapa ni kwamba mara nikakumbuka ziara yangu ya nyumbani Songea na hasa hapa katika makumbusho haya. Hakika kama hujafika Songea basi ukifika usikose kufika hapa Makumbushp ya mashujaa wetu. Basi fuatana nami kwa hizi picha chache na maelezo.......KARIBUNI SONGEA
Historia ya Makumbusho haya inahusu vita ya Maji Maji ilivyo tokea kati ya mwezi julai 1905 mpaka Agosti 1907. Vita hiii ilianza katika vilima vya Umatumbi kaskazini mwa mji wa Kilwa mnamo mwezi Julai mwaka 1905.
Waanzilishi wa awali wa vita hii walikuwa ni Wamatumbi chini ya uhamasishaji wa Mganga wa jadi /Nabii aliyejulikana kwa jina la Kinjeketile Vita hii ilikuwa kama moto katika nyasi kavu na kusambaa katika makabila ya Wamwera, Wangindo, Wapogoro, Wangoni, Wabena, Wasangu na wengine. Watu hawa walipigana kupinga kukandamizwa na kulazimishwa na wakoloni wa Kijerumani namna ya kuishi, mazao ya kuzalisha na nani wa kumtumikia.
HAPA NI PICHA YA ASKARI WA KIJERUMANI
Jina la vita hii limetokana na imani ya matumizi ya dawa iliyochanganywa na Maji, punje za mahindi na mtama zilizosadikiwa kuwa zitampa mpiganaji kinga ya kutodhurika kwa shambulio la risasi za majeshi ya Wajerumani. Inakadiliwa watu 75,000 walipoteza maisha yao ukanda wa kusini mwa Tanzania baada ya vita. Katika eneo la Ruvuma inakadiliwa kuwa zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha yao.
Baada ya vita viongozi na askari walishiriki katika vita walikamatwa na kuhukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Tarehe 27 Februari 1907 ilikuwa siku ya masikitiko makubwa kwa watu wa Ruvuma ambapo kadri ya watu 60 walinyongwa kwa sababu ya kushiriki katika vita. Mashujuaa hawa walinyongwa nyuma ya eneo ambalo leo hii linajulikana kama "Songea Club". Baada ya kunyongwa miili yao ilizikwa katika kaburi la halaiki, lililoandaliwa na wafungwa kwa muda wa miezi miwili. Siku ya tatu baadaye Chifu alinyongwa na kuzikwa katika kaburi lilikoandaliwa na kaburi la halaiki.
Eneo walilozikwa mashujaa hawa limekuwa eneo muhimu sana. Tukio hili lilikuwa la kuhuzunisha sana kwa watu wetu hivyo watu hawakulizungumza kwa kitambo kirefu. Baada ya uhuru (1961). Baadhi ya wazee walianzisha harakati za kuwakumbuka mashujaa hawa. Walianza kufanya maombi yao na maadhimisho katika eneo lililo karibu na eneo walilonyongwa wapiganaji hao. Shughuli hizi zilifanyika katika nyumba ya Padre Chengula.
Wazo la kuwa na maadhimisho ya Kitaifa lilianzishwa na kamati wa wazee wa Kingoni. Walitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Bw. Martin Haule aliyekuwa ameteuliwa wakati huo. Baadhi ya wazee waliokuwa katika kamati hii ni pamoja na Xavery Zulu, Padre Chengula, Daudi Mbano, Ali Songea Mbano, Agatha Shawa, Alana Mbawa, Mwl. Duwe, Shaibu Mkeso na Daniel Gama.
Baada ya kuwasilishwa wazo hili kwa Mheshimiwa Martin Haule, alichukua hatua za dhati katika kulishughulikia jambo hili. hatua ya kwanza ilikuwa kutambua eneo ambalo Mashujaa hawa walizikwa. eneo hili walipozikwa Mashujaa lilitambuliwa na Bw. Jumbe Darajani ambaye alishuhudia tukio la kunyongwa kwa wahenga hawa (wakati wa utoto wake). Alama iliyotumika kufahamu eneo hili ilikuwa ni mti mmoja uliojulikana kwa jina la CHIKUNGUTI. Baada ya kutambuliwa eneo hilo mheshimiwa Haule alifanya uchimbuzi na kupata baadhi ya mifupa.
Kaburi la Songea Mbano ambaye alizikwa peke yake. Na la Mji wa Songea limetokana na jina lake.
Kabla ya Bwana haule kukamilisha kazi hii alihamishiwa Mkoa wa Ruvuma mwaka 1964. Wazo hili la kuwaenzi Wahenga hawa liliibuka tena mwaka 1979 wakati Bw Laurence Gama alipoteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma. Aliendelea na jitihada za kutekeleza wazo hili. Alianza kuhamasidha na kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa makumbusho kwa kushirikiana na wazee wa Ruvuma na wananchi wengine, ujenzi wa jengo la makumbusho ulianza na kukamilika mwaka 1980.
Pamoja na kukamilisha kwa ujenzi wa jengo hili pia zilijengwa Sanamu katika eneo la mbele ya jengo. Sanamu hizi zilijumuisha anamu ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mwl. J.K Nyerere na sanamu 12 zamachifu wa kingoni. Lakini kwa sasa sanamu wa hayati Mal. J.K Nyerere imetolewa baada ya kuona haina kiwango cha juu, hivyo inaandaliwa upya ili iweze kuwekwa upya . Kazi ya kutengeneza sanamu hizi ilifanywa na msanii mmoja huko Arusha.
Vifaa vya awali katika makumbusho haya vilitengenezwa na Mheshimiwa Laurence Gama, Padre Chengula na baadhi ya wazee. Vifaa vilivyokusanywa vilijumuisha ni silaha zilizotumika wakati wa vita ya Maji Maji kama vile:- Kwa lugha ya kingoni Chikopa (Ngao), Chibongo(Rungu), Chinjenje (Kishoka), pia baadhi ya viti vilivyotumiwa na Chifu Mputa,vifaa vya ndani na nguo za magome ya miti.
Kwa Hiyo kuanzia mwaka 1980 baraza la wazee lilianza kuadhimisha maombolezo ya mashujaa walionyongwa kila ifikapo tarehe 27/2 ya kila mwaka. Makumbusho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 7/7/1980. Kuanzia hapo makumbusho haya yaliendelea kutoa huduma chini ya usimamizi wa Mkoa wa Ruvuma na wazee wanaendelea kufanya maadhimisho ya siku ya Mashujaa katika eneo la Makumbusho haya kila mwaka. Baadhi ya wazee ndio ambao wamekuwa wakitoa maelezo kwa wageni wanaotembelea makumbusho haya. Tarehe 1/9 2005 makumbusho haya yalikabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Miaka 100 ya vita ya Maji Maji iliadhimishwa Kitaifa katika Makumbusho haya tarehe 27/2/2006 na yalizinduliwa rasmi na Rais wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete.
TUWAKUMBUKE MASHUJAA WETU DAIMA WALIFANYA KAZI KUBWA SANA..
Thursday, November 21, 2013
NIMEONA TUBAKI MKOANI RUVUMA:-TATIZO LA UMEME SONGEA KITENDAWILI!!!
Katika pitapita nimekutana na habari hii ambayo imenikasirisha na kunikatisha tamaa sana maana nilikuwa katika harakati ya kuingiza umeme katika nyumba yangu. Ila najipa moyo na kuendelea ebu soma hapa habari hii iliyoandikwa Na Albano Midelo.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
“Mchawi ni ugonjwa wa majenereta ambayo vipuli vyake vimechoka na kuchakaa,tumechoka na kero hii kama sio ubovu wa vipuri utasikia mafuta ya kuendeshea mitambo yamekwisha,mara fundi wa kufunga vipuri anatoka nje ya nchi TANESCO tuambieni ukweli tumechoka’,anasisitiza.
Brighton Mwandata mmiliki wa studio ya kurekodi muziki Matarawe mjini Songea anasema umeme katika mji wa Songea haujapatiwa ufumbuzi wa kudumu anashindwa kurekodi kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara wakati mwingine inamgharimu kukodisha jenereta kwa gharama kubwa. Ingia hapa kwa kusoma zaidi habari hii.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Hapa ni baadhi ya vijana katika mji wa Songea wakifanya maandamano ya amani kudai umeme wa uhakika mjini Songea.
“TANESCO wanakata na kurudisha umeme bila taarifa na hata ratiba ya mgao haijulikani hali inasababisha hasara kubwa kwa wananchi ikiwemo kuungua vifaa vya umeme na vyakula vinavyohifadhiwa kwenye majokofu kuharibika’’,anasema diwani wa kata ya mjini manispaa ya Songea Joseph Fuime.
Fuime alidai kuwa tatizo la umeme Songea haliwezi kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuendelea kutumia mashine chakavu za kufua umeme ambazo vipuri vyake vinaharibika mara kwa mara badala yake alishauri serikali kuunganisha mkoa wa Ruvuma na umeme wa giridi ya Taifa.
“Serikali iliahidi mara baada ya kuanza kuchimbwa makaa ya mawe ya Ngaka wilayani Mbinga kutajengwa kinu cha kufua umeme katika mji wa Songea hata hivyo tangu mwekezaji ameanza kuchimba makaa ya mawe hadi sasa hakuna dalili za kufungwa kinu hicho pia mwekezaji ameshindwa hata kuwalipa fidia wananchi wanaoishi katika eneo la mgodi’’,alidai Fuime ambaye pia ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma.
Uchunguzi uliofanywa katika maeneo mengi ya mji wa Songea umebaini kuwa vibaka wakati wa usiku wameongezeka na kusababisha nyumba nyingi kukatwa nyanya za madirishani na wengine kuibiwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,mavazi,kompyuta za mkononi na samani mbalimbali.
Waandishi wanakwama kutuma habari zao kwa haraka na hata vituo vya matangazo vilivyopo mjini Songea vikiwemo Redio Maria,radio Jogoo,TBC Taifa, vinashindwa kurusha matangazo kwa wananchi kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara.
John Mapunda mfanyabiashara soko kuu la Songea anasema Kukatika kwa umeme na kuwaka bila taarifa katika mji wa Songea kunawasababishia hasara kubwa wafanya biashara wa vyakula hasa wanaouza samaki wabichi kutoka ziwa Viktoria, Tanganyika, Nyasa na bwawa la Mtera ,wao wanatunza samaki hao katika makojofu ambayo yanatumia umeme wa TANESCO hivyo samaki wengi wanaoza. "TANESCO katika manispaa ya Songea inaonyesha dhahiri kuwa mashine zao haziwezi kufua umeme wa kukidhi hata katika mji wa Songea,wananchi tunahoji kwanini umeme huo umesambazwa hadi mji mdogo wa Peramiho badala ya kusubiri umeme gridi ya Taifa’’,alihoji Mapunda. Frank Mbunda mkazi wa Mahenge mjini Songea anadai kuwa TANESCO wameshindwa kumaliza tatizo sugu la umeme ambalo linachangia umasikini kwa wakazi wa Songea ambao wanashindwa kufanyakazi zao za kiuchumi.
Mwanaharakati Mohamed Kudeka mkazi wa Songea anatoa wito kwa serikali kuachana na umeme wa majenereta ambao matatizo yake ya kuharibika kwa vipuri yamekuwa yanajirudiarudia na kusababisha kero kubwa kwa wakazi wa mji wa Songea ambao wanashindwa kufanya kazi za kiuchumi na kusababisha umaskini. Fuime alidai kuwa tatizo la umeme Songea haliwezi kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuendelea kutumia mashine chakavu za kufua umeme ambazo vipuri vyake vinaharibika mara kwa mara badala yake alishauri serikali kuunganisha mkoa wa Ruvuma na umeme wa giridi ya Taifa.
“Serikali iliahidi mara baada ya kuanza kuchimbwa makaa ya mawe ya Ngaka wilayani Mbinga kutajengwa kinu cha kufua umeme katika mji wa Songea hata hivyo tangu mwekezaji ameanza kuchimba makaa ya mawe hadi sasa hakuna dalili za kufungwa kinu hicho pia mwekezaji ameshindwa hata kuwalipa fidia wananchi wanaoishi katika eneo la mgodi’’,alidai Fuime ambaye pia ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma.
Uchunguzi uliofanywa katika maeneo mengi ya mji wa Songea umebaini kuwa vibaka wakati wa usiku wameongezeka na kusababisha nyumba nyingi kukatwa nyanya za madirishani na wengine kuibiwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,mavazi,kompyuta za mkononi na samani mbalimbali.
Waandishi wanakwama kutuma habari zao kwa haraka na hata vituo vya matangazo vilivyopo mjini Songea vikiwemo Redio Maria,radio Jogoo,TBC Taifa, vinashindwa kurusha matangazo kwa wananchi kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara.
John Mapunda mfanyabiashara soko kuu la Songea anasema Kukatika kwa umeme na kuwaka bila taarifa katika mji wa Songea kunawasababishia hasara kubwa wafanya biashara wa vyakula hasa wanaouza samaki wabichi kutoka ziwa Viktoria, Tanganyika, Nyasa na bwawa la Mtera ,wao wanatunza samaki hao katika makojofu ambayo yanatumia umeme wa TANESCO hivyo samaki wengi wanaoza. "TANESCO katika manispaa ya Songea inaonyesha dhahiri kuwa mashine zao haziwezi kufua umeme wa kukidhi hata katika mji wa Songea,wananchi tunahoji kwanini umeme huo umesambazwa hadi mji mdogo wa Peramiho badala ya kusubiri umeme gridi ya Taifa’’,alihoji Mapunda. Frank Mbunda mkazi wa Mahenge mjini Songea anadai kuwa TANESCO wameshindwa kumaliza tatizo sugu la umeme ambalo linachangia umasikini kwa wakazi wa Songea ambao wanashindwa kufanyakazi zao za kiuchumi.
“Mchawi ni ugonjwa wa majenereta ambayo vipuli vyake vimechoka na kuchakaa,tumechoka na kero hii kama sio ubovu wa vipuri utasikia mafuta ya kuendeshea mitambo yamekwisha,mara fundi wa kufunga vipuri anatoka nje ya nchi TANESCO tuambieni ukweli tumechoka’,anasisitiza.
Brighton Mwandata mmiliki wa studio ya kurekodi muziki Matarawe mjini Songea anasema umeme katika mji wa Songea haujapatiwa ufumbuzi wa kudumu anashindwa kurekodi kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara wakati mwingine inamgharimu kukodisha jenereta kwa gharama kubwa. Ingia hapa kwa kusoma zaidi habari hii.
Wednesday, October 9, 2013
KARIBUNI UTAANZA MSIMU WA MATUNDA HAYA YA PORI KWA JINA LA MASUKU/MAPOTOPOTO
Kama mnakumbuka kuna mada niliwahi kuiweka hapa kwa kuwakumbusha basi gongeni kapulya. Matunda haya ni maarufu sana katika Mkoa wa Ruvuma nasi huyaita masuku na wangoni wanasema Mapotopoto ni matamu sana. Na kwa kujipatia hela ni rahisi sana masuku kumi ni shilingi 100 kwa hiyo ukiwa nayo mia moja uongo mbaya...NAWATAKIENI JUMATANO NJEMA SANA WOTE NA PANAPO MAJALIWA TUTAGONGANA TU....
Wednesday, October 2, 2013
TUBAKI HAPA TANZANIA.......NA KWINGINE TENA BALI NI MKOANI RUVUMA KWETU!!!
MKOA WA RUVUMA -TANZANIA
MKOA WA RUVUMA:- Ni kati ya mikoa 26 ya nchi yetu Tanzania.Mkoa wa Ruvuma umepewa jina kutokana na mto RUVUMA ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Mkoa wa Ruvuma unapakana na Ziwa la Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa Mashariki. Kuna mikoa mitano ambayo ni (idadi ya wakazi katika mabano) Songea Mjini (131,336), Songea Vijijini (147924), Tunduru (247,976), Mbinga 404,799), na Namtumbo ni (185,131). Makao makuu ya mkoa ndipo Songea. Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,117,166 (sensa 2002).
Makabila makuu katika Mkoa huu wa Ruvuma ni Wangoni, Wanyao, Wamatengo, Wandendeule na Wandengereko.
Karibu na Songea iko monasteri/Seminari kubwa ya Peramiho ya watawa wa Wabenedikto kama wengi mjuavyo.
Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda Lindi ipo katika hali mbaya..
YATAKUJA MENGI KUHUSU MKOA HUU WA RUVUMA WENYE KUVUMA:-)
NA KAPULYA WENGU YUPO KINAMNA ....MCHANA/JIONI NJEMA KWA WOTE.
Subscribe to:
Posts (Atom)