Tuesday, July 31, 2018

LEO TUANGALIA /SIKILIZE NYIMBO/NGOMA ZETU ZA ASILI


Huwa napenda sana kuangalia au kusikiliza ngoma/nyimbi wa asili . Kwa hiyo nimeona niwashirikishe na wenzangu

Monday, July 23, 2018

JUMATATU YA LEO TUANGALIA BAADHI YA VYAKULA NILIMAVYO/KAZI YA MIKONO YANGU

Hapa ni kama itakuwa vizuri basi litakuwa tango....

.....na ni matembele ...kama huna ardhi kutosha basi hii ni njia nzuri kupata chakula

Thursday, July 19, 2018

EBU LEO TUANGALIE UTENGENEZAJI WA TOGWA....

 UTENGENEZAJI WA TONGWA
UNYWAJI WA TOGWA KUTUMIA KIKOMBE AU KATA. JE? WEWE UNAPENDA KUTUMIA KIKOMBE AU KATA?

Wednesday, July 18, 2018

KAZI YA MIKONO YANGU/ ALIMAYE ANAVUNA

Hapa ni vitunguu saumu 
na hapa ni nyanya
picha zaidi za bustani zaja

Tuesday, July 17, 2018

WIKI HII TUANZE NA KWETU NYASA ...KUMBUKUMBU

Kiukweli leo nimekumbuka sana NYASA/LUNDO kwetu  nilikozaliwa kwenda tu ziwani unapata samaki, dagaa na hata likungu. Naona fahari sana kuzaliwa Kando ya ziwa nyasa, Unajua samaki wanaotoka tu kuvuliwa wanavyokuwa watamu wewe acha tu... Niwatakieni JUMANNE NJEMA. WOTE MNAPENDWA. Kapulya!

Tuesday, July 10, 2018

LEO TUTEMBEE KANISA KONGWE LA MKOA WA RUVUMA-PERAMIHO

Hilo hapo juu ni kanisa lililo jengwa Peramiho na Wamisionari wa kikatolic miaka mia moja iliyo pita lakini mpaka leo halijanyiwa ukarabati wowote ,pamoja na kanisa hilo ipo saa ambayo nayo ina chukua miaka 100 bila kutengenzwa wala kurekebishwa

Monday, July 9, 2018

WIKI HII TUANZE NA KUANGALIA BUSTANI YA KAPULYA.... JUMATATU NJEMA WANDUGU TUPO PAMOJA

 mchicha 
 Mboga ya maboga
 Vitunguu, Mahindi na Viazi
Nyanya. Kutokana na uhaba wa sehemu basi nimetumia makopo

Wednesday, July 4, 2018

2/7 NI KUMBUKUMBU YA NDOA YETU IMETIMIZA MIAKA 25

2/7/ ilikuwa siku ya furaha kwetu ni miaka 25 ya ndoa yetu

Ni  chakula cha jioni ile nyama ya ngòmbe na viazi  pia kinywaji. Twamshukuru Mungu kwa safari hii ndefu.