Wednesday, August 29, 2018

PENDEZA KWA UBUNIFU WA KITANZANIA

Umuhimu wa kupendeza uko wazi kwa kila mtu,mara nyingi mavazi yamekuwa kama kipimo cha utanashati,basi ili kuongeza mvuto yafaa kuongezea vitu vya pekee vilivyotengenezwa kwa ujuzi wa kimasai ili tu kuonyesha utofauti kimitindo na utanashati..

Kazi za mikono ya wapendwa wetu ambao wanadumisha utamaduni  inapendeza sana

Monday, August 27, 2018

MIMI NDIO NILIMUA BATA MZINGA KWA BAHATI MBAYA


KATIKA PITAPITA ZANGU NIMEKUTANA NA HILI FUNZO NIKAONA NIWEKA HAPA ILI NA WENZANGU MUWEZE KUSOMA NA KUJIFUNZA KARIBUNI:-

Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lakini ghafla nilimwona dada yangu nyuma yangu akinitazama. Na akaniambia nimpe elfu moja ili asimwambie mama, nikamwambia sina ila tafadhali usimwambie mama. Siku iliyofuata mama alimwambia dada aoshe vyombo na kusafisha mazingira. Lakini dada akamwambia mama msafiri amesema atafanya, dada akaja na kuniambia nifanye zile kazi la sivyo atamwambia mama nilimuua bata mzinga. Pasipo kulaumu nikazifanya.

Siku iliyofuata mama akamwita tena dada na kumwambia akachote maji na kujaza pipa. Dada akamwambia tena mama nimesema nitafanya, akaja kwangu akaniuliza unakumbuka ulimuua bata mzinga? Sasa jaza maji kwenye pipa kama hutaki nimwambie mama. Ikanipasa nikachote maji nijaze pipa. Siku hyo hyo jioni mama akamtuma sokoni kununua nafaka na azisage. Akamamwambia tena msafiri amesema ataenda, akaja kwangu akasema "kumbuka kwamba bata mzinga bado amekufa" nenda sokoni ukanunue mfuko wa nafaka kisha ukasage, kama hutaki basi nitamwambia mama.

Nilisimama nikaenda kwa mama huku nikitiririka machozi machoni na nilimkuta amekaa ndani, nikapiga magoti na kumwambia huku nikilia..
"Mama nisamehe tafadhali nisamehe mno. Mimi ndio nilimuua bata mzinga kwa bahati mbaya, tafadhali mama nisamehe.
Mama akajibu- "Mwanangu siku ile ulipomuua bata mzinga nilikuwa dirishani na nilitazama kila kitu kilichotokea. Dada yako amekufanya mtumwa kwasababu hukutaka kuja kwangu kukiri na kuomba msamaha. Sasa umefanya hv uko huru na dada yako hawezi kukutumia tena.

FUNZO,
Kila mara tukiwa tunatenda dhambi Mungu anatuona, na dhambi hakika hutufanya kuwa watumwa siku zote. Hivyo tukienda mbele zake tukikiri na kuomba msamaha yeye ni mwingi wa rehema na atatusamehe.
*MUNGU ATUSAMEHE DHAMBI ZETU NA ATUWEKE HURU...*

Sunday, August 26, 2018

JUMAPILI YA LEO TUWE PAMOJA KWA MAOMBI NA HII NI SALA YANGU

Ee Mungu wajua sababu ya mimi kuendelea kuwepo kwenye uwepo wako, naomba uendelee kunijalia hekima na busara katika kukabiliana  na majaribu mbalimbali maana wewe ndiye wajua leo yangu na kesho yangu itakavyokuwa.
AMINA

Friday, August 24, 2018

NIMEVITAMANI SANA VYAKULA HIVI LEO

 KUMBIKUMBI
NA LIKUNGU...Mmmmmm  utamu mpaka mate yanadondoka

Wednesday, August 22, 2018

TUFANYE HII IWE PICHA YA SIKU

Leo ni Jumatano iliyochaguliwa nami Kapulya  kuweka picha hii iwe picha ya siku. NAWATAKIA SIKU NJEMA WOTE MTAKAOPITA HAPA.

Sunday, August 19, 2018

KUMBUKUMBU....NIMETAMANI SANA EMBE LEO....

Nawatakieni  mwisho wa juma uwe mwema amani na furaha vitawale moyoni mwenu.....Kapulya wenu!

Monday, August 13, 2018

NAWATAKIENI JIONI NJEMA YA JUMATATU HII KWA KUANGALIA NGOMA YA ASILI YA KINGONI

UJUMBE WA LEO:- Tusisahau utamaduni wetu ndugu zanguni, binafsi napenda sana uasili.JIONI NJEMA WANDUGU. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA.

Tuesday, August 7, 2018

NI WIKI NYINGINE TENA NDANI YA MWEZI HUU WA NANE... NA HII NI PICHA YA WIKI

Napenda kuwatakieni mwanzo mwema wa hili juma na furaha itawale mioyoni mwenu. Tutaonana tena panapo majaliwa.

Wednesday, August 1, 2018

TUANZE WIKI HII MPYA YA MWEZI HUU MPYA WA NANE KWA KUANZA NA KUSHIRIKIANA KULA CHAKULA HIKI

Karibu ugali wa muhogo, nyama ya kuku na dagaa. KARIBUNI SANA na muwa na wakati mzuri kwa kuanza mwezi huu wa nane.