Tuesday, May 29, 2018

NAWATAKIENI SIKU NJEMA YENYE AMANI NA FURAHA

Ni siku nyingine tena na jumanne ya mwisho ya mwezi huu nami nimeona niwatakieni kihivi. AMANI NA FURAHA VITAWALA MIOYONI MWENU. PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA KARIBUNI

Monday, May 28, 2018

JUMATATU HII YA MWISHO YA MWEZI HUU WA TANO TUANGALIE BAADHI YA METHALI ZETU

1. Aisifuye mvua imenyeshea
2. Baniani mbaya kiatu chake dawa
3. Bendera hufuata upepo
4. Fuata nyuki ule asali
5. Haraka haraka haina baraka
6. Mtoto wa nyoka ni nyoka
7. Sikio la kufa halisikii dawa
8. Ulimi hauna mfupa
9. Tamaa mbele mauti nyuma
NAWATAKIENI JUMATATU HII YA MWISHO WA MWEZI HUU IWE NJEMA SANA NA TUTAONANA TENA KARIBUNI.

Tuesday, May 22, 2018

HUU NI UJUMBE WETU WA LEO:- ETI NI MIPANGO YA MUNGU!?

                                 Hivi ni mipango ya Mungu au ni kujitakia?

Friday, May 18, 2018

NACHUKUA NAFASI HII KUWATAKIENI WOTE MTAKAOPITA HAPA MWISHO WA JUMA UWE WENYE MAPUMZIKO YA AMANI NA FURAHA....

 Chagu lako kupumzika kwa kunywa pombe ya kienyeji  komoni na  ulanzi  au
Pombe ya kisasa kwa jina la bia
IJUMAA NA MWISHO MWEMA WA JUMA

Monday, May 14, 2018

ZILE NDIZI/ULE MKUNGU SASA ZIMEIVA


Ni raha ilioje kula kazi ya mikono yako/yangu....kaka yangu  kanitumia  hii kunitamanisha ...-:)

Wednesday, May 9, 2018

KUMBUKUMBU:- SHULE NA KENGELE...

Je? unakumnuka hii kengele shule uliyosoma? AU kanisa ulilosali? mimi nakumbuka:-)

Friday, May 4, 2018

KUMBUKUMBU YA MAISHA...NILINUSURIKA KUFA KWA KUSOMA KWA MWANGA WA KOROBOI/KIBATALI

Sijui ni kumbukumbu nzuri au mbaya? Ila nimekumbuka mbali sana...ama kweli watu tumetoka mbali. NIWATAENI IJUMAA HII YA KWANZA YA MWEZI HUU WA TANO IWE NJEMA NA  YENYE KUMBUKUMBU NJEMA ZA FURAHA.

Wednesday, May 2, 2018

HAPA NI KWETU MBINGA..ANGALIA MANDHARI YAKE INAVOVUTIA.....!

Kama tuonavyo ni mandhari nzuri ya migomba,  na vinginevyo pia mwaona kuku wakidonoadonoa na bila kusahau banda ya nguruwe....
Mkungu wa ndizo(kaporota) kutoka katika hiyo migomba hapo juu kazi ya mikono ya kaka yangu amenitumia ili kunitamanisha na amenitamanisha  haswaaa
Bado ni bustani ya migomba na vingine kama vile mahindi na vinginenyo na kwa juu ndio nyumba yetu mpya ya huko Mbinga....karibuni
Nguruwe....pia wapo