Showing posts with label lundo. Show all posts
Showing posts with label lundo. Show all posts

Tuesday, March 26, 2019

LEO NIMETUMIWA ZAWADI HII NA RAFIKI YANGU

Baada ya kushukuru nimemlaumu sana kwa kunitamanisha.....ahsanten  kwa zawadi rafiki yangu umenikumbusha kwetu Lundo/nyasa

Monday, February 15, 2016

WIKI HII TUANZE NA KUTEMBELEA ALIKOZALIWA KAPULYA WENU KIJIJI CHA LUNDO/ WILAYA YA NYASA


 Hapa ni kilimo cha maksai katika kijiji cha Lundo Wilaya ya Nyasa
Na hapa ni Beach ya BioCamp-Kijiji cha Ndengere Wilaya hiyo hiyo ya Nyasa...  yaani nimefurahi, furahi mno kupata tena taaswira ya vijiji hivi  Ndengere, Lundo, nk...ni sehemu zangu nilizokulia yaani  nimekumbuka  mengi sana hasa mlo wa samaki na ugali wa mhugo:-)  hapa ndipo nilikotoka...

Monday, March 11, 2013

LUNDO SEKONDARI INA HALI MBAYA SANA KIELIMU

Tuanza na historia fupi ya shule ya Lundo: Shule ya Lundo ilianza kama shule ya msingi ya wakimbizi ..na ilikuwa inaitwa shule ya msingi wa wakimbizi Lundo. Na kama nakumbuka vizuri ilianza miaka ile ya sabini(1970) na baba yangu alikuwa moja wa walimu waanzilishi. Nami nilipofikia umri wa kuanza shule nilianzia shule hii, ila sikumalizia Lundo baba alipata uhamisho. Kwa hiyo ikaenda weee mpaka ....miaka ya tisini tisini (1990 ikawa Sekondari...sasa niliposoma makala hii hapa chini nimeguswa sana ...haya karibuni msome nanyi wenzangu.
..................................................................................................................................................................

Tangu kutanagazwa matokeo ya kidato cha nne shule mbalimbali zimekuwa na matokeo mabaya sana. Miongoni mwa shule hizo ni Lundo sekondari ambayo ilikuwa ikisifika kwa ubora wa wahitimu na matokeo mazuri.
Lundo sekondari iliwahi kuweka rekodi ya kufaulu wanafunzi wa kidato cha pili, hivyo hakuna aliyefeli kwa mwaka 1999. Sifa nyingi za shule hii ilikuwa nidhamu na wanafunzi kupenda masomo huku wakikabiliana na hali ya maisha na kuyazoea.
Wengi waliohitimu hapo wamefanikiwa kuwa watumishi imara na kuzalisha wanamapinduzi wazuri kifikra ambao wanaendelea kusukumu gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Nyasa, na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pamoja taifaletu la Tanzania.
Lakini kwa sasa hali ni tofauti. Licha ya kusifika wakati wa uongozi wa mkuu wa shule Bwan Ndunguru, sasa hali imekuwa mbaya sana. Maskini Lundo Sekondari.......masikini wilaya yetu Nyasa....
Inasikitisha kuona shule ile tuliyosoma, shule ile iliyokuwa kinara kwa ufaulu wa kidato cha nne tangu miaka ile ya 90's hadi mwanzoni mwa 2003.... Leo hii shule ni ya division 4 na 0 tuu.... Kwa mtazamo Wangu kutokana na vile nilivyokuwa nikifuatilia matokeo ya shule hii kwa miaka kadhaa,nimegundua shule imekosa Uongozi....
Samahani kwani huenda nitakuwa nimewagusa wengine moja kwa moja,lakini kwa nini wakati ule wa mzee Ndunguru mambo hayakuwa hivi.... Imeniuma kwa ujumla wa matokeo Kitaifa,lakini nimeumizwa zaidi na matokeo ya shule zetu wilayani Nyasa.... Sitaki kuamini kama Sisi ni Vilaza; Hapana
Na Richard Mwanja, Dar es Salaam

Tuesday, May 8, 2012

TUMEPUMZIKA SONGEA KIDOGO INATOSHA! SASA NAONA TUENDELEE NA SAFARI YETU !TUNAELEKEA KULE ALIKOZALIWA KAPULYA!!!

 Sio kwingine tena ni hapa:- katika  pichani ni moja ya fukwe bora katika ziwa Nyasa eneo la Lundo. Na ndio alikozaliwa mdada huyu. Ni sehemu nzuri sana kwa kutalii ukitembelea maeneo haya siku moja usikose kutembelea na hapa.
Pomonda jiwe la ajabu lililopo ziwa nyasa.
Hili ni jiwe la Pomonda, moja ya vivutio adimu vya utalii ziwa Nyasa ..Kuna mambo mengi katika nchi yetu ambaye ni mazuri na ya kuvutia ebuliangalia jiwe hili  halafu angalia huo ufukwe hapo juu. Mweee mpaka raha kweli. 

Tuesday, September 7, 2010

HONGERA BLOG YA LUNDUNYASA KWA KUTIMIZA MIAKA MINNE!!!

Markus Mpangala wa lundunyasa


Miaka yaenda kasi mno tarehe 31/8/2007 blog hii ya LUNDUNYASA ilitimiza miaka 4. Blog ya MAISHA NA MAFANIKIO yakutakia yote utakayotenda yawe na mafanikio mema. Hongera sana na uwepo wako unathaminiwa sana. Ingia hapa utakuta mengi

Monday, August 11, 2008

AGOSTI 11,2008 LUNDO, KUMBUKUMBU

Leo nimekumbuka sana Lundo, eeh jamani ilikuwa kazi kweli. Wale wote waliofika Kijiji cha Lundo Tanzania. Yaani pale Lundo shule ya msingi ya wakimbizi kwa sasa inaitwa Lundo Secondary School.

Mnajua pale shuleni kulikuwa na matunda ya aina mbalimbali kama vile mapapai, machungwa, malimao, ndizi n.k. Na mimi ilikuwa kazi yangu kila baada ya shule nilirudi tena shuleni, nilikuwa mwizi wa malimao nilikuwa nakula sana malimao kwa siku nilikuwa nakula 10. Mama alikuwa analalamika sana. Kwani nilikuwa nakula na chumvi iliyochanganywa na pilipili. Nilikuwa siibi malimao tu chumvi pia.

Halafu magauni yangu na sketi zilikuwa na matobo sana, sababu nilikuwa nabebea malimao. Mmh! jamani Lundo sitasahau, yaani kujificha kwa kweli nilikuwa mwizi maalufu kwani sikushikwa. Ila sasa siwezi kula malimao zaidi ya nusu limao nimekinai kabisa.

LUNDO BAADA YA MIAKA ISHIRINI
Mmhh furaha, hisia pia raha vilinijia siku hii yaani mwaka jana 2007. Fikiria mwenyewe sehemu uliyozaliwa, sehemu ulianza darasa la kwanza halafu umeondoka na baada ya miaka 20 unarudi/tembelea tena.
Ila nilisikitika kidogo kwani sikuweza kujua ni nyumba gani nilizaliwa/ishi kulikuwa na mabadiliko mno. Ila cha kufurahisha zaidi ni kwamba nilionana na mjomba wangu ambaye sikumwona tangu 1985. Siku hii nilikuwa kama mtoto mdogo nilikimbia na kumrukia mjomba kwa jinsi nilivyokuwa na furaha. Mpaka machozi yalinitoka. Kwa vile mjomba anajua mimi napenda nini aliniandalia samaki What a joy. pia nilifurahi zaidi kujua alikumbuka jina langu la utani ambalo hata mwenyewe nilisahau. Mnataka kujua au? Okey ni (KANYANJA) kilugha kiswahili kanyasa. Sasa mnajua .