Monday, March 11, 2013

LUNDO SEKONDARI INA HALI MBAYA SANA KIELIMU

Tuanza na historia fupi ya shule ya Lundo: Shule ya Lundo ilianza kama shule ya msingi ya wakimbizi ..na ilikuwa inaitwa shule ya msingi wa wakimbizi Lundo. Na kama nakumbuka vizuri ilianza miaka ile ya sabini(1970) na baba yangu alikuwa moja wa walimu waanzilishi. Nami nilipofikia umri wa kuanza shule nilianzia shule hii, ila sikumalizia Lundo baba alipata uhamisho. Kwa hiyo ikaenda weee mpaka ....miaka ya tisini tisini (1990 ikawa Sekondari...sasa niliposoma makala hii hapa chini nimeguswa sana ...haya karibuni msome nanyi wenzangu.
..................................................................................................................................................................

Tangu kutanagazwa matokeo ya kidato cha nne shule mbalimbali zimekuwa na matokeo mabaya sana. Miongoni mwa shule hizo ni Lundo sekondari ambayo ilikuwa ikisifika kwa ubora wa wahitimu na matokeo mazuri.
Lundo sekondari iliwahi kuweka rekodi ya kufaulu wanafunzi wa kidato cha pili, hivyo hakuna aliyefeli kwa mwaka 1999. Sifa nyingi za shule hii ilikuwa nidhamu na wanafunzi kupenda masomo huku wakikabiliana na hali ya maisha na kuyazoea.
Wengi waliohitimu hapo wamefanikiwa kuwa watumishi imara na kuzalisha wanamapinduzi wazuri kifikra ambao wanaendelea kusukumu gurudumu la maendeleo ya wilaya ya Nyasa, na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla pamoja taifaletu la Tanzania.
Lakini kwa sasa hali ni tofauti. Licha ya kusifika wakati wa uongozi wa mkuu wa shule Bwan Ndunguru, sasa hali imekuwa mbaya sana. Maskini Lundo Sekondari.......masikini wilaya yetu Nyasa....
Inasikitisha kuona shule ile tuliyosoma, shule ile iliyokuwa kinara kwa ufaulu wa kidato cha nne tangu miaka ile ya 90's hadi mwanzoni mwa 2003.... Leo hii shule ni ya division 4 na 0 tuu.... Kwa mtazamo Wangu kutokana na vile nilivyokuwa nikifuatilia matokeo ya shule hii kwa miaka kadhaa,nimegundua shule imekosa Uongozi....
Samahani kwani huenda nitakuwa nimewagusa wengine moja kwa moja,lakini kwa nini wakati ule wa mzee Ndunguru mambo hayakuwa hivi.... Imeniuma kwa ujumla wa matokeo Kitaifa,lakini nimeumizwa zaidi na matokeo ya shule zetu wilayani Nyasa.... Sitaki kuamini kama Sisi ni Vilaza; Hapana
Na Richard Mwanja, Dar es Salaam

5 comments:

ray njau said...

Kwa sasa hili ni suala la kitaifa na sasa tume ya mheshimiwa waziri mkuu inaendelea na uchunguzi kile kilichotokea kabla ya kurudisha majwabu kwa wadau.

Yasinta Ngonyani said...

Natumaini huo uchunguzi utakuwa wa manufaa maana sasa naona si Lundo tu kila sehemu utakayosoma ni kwamba matokeo si mazuri. Je ni walimu hawafundishi au wanafunzi hawasomi? SAMAHANI KWA KUWAZA KWA SAUTI..

Anonymous said...

Ni kwel kabisa lazima turudishe elemu yetu ya Tz kama zaman,hv tatzo ni kuanzishwa kwa shule za kata ndo kumechangia au?

Thomas Ndunguru said...

Watanzania kwakwel tuamke ili tuweze kupigania janga hili hatari,na viongoz wetu nao wawe makini.

ray njau said...

Mijadala mingi inayoendelea inawabebesha walimu na serikali lawama na kusahau kuwa mabadiliko ya tabia nchi kimaadili na wazazi kujiondoa katika wajibu wetu muhimu wa malezi mema na nidhamu kwa kuzingatia viwango na masharti kuwa ndiyo msingi mkuu wa anguko la elimu na taaluma hapa kwetu.