Wednesday, March 13, 2013

ZILIPENDWA KWELI NI NZURI HAPA ILIKUWA MWAKA 1993 WILIMA/MATETEREKA...MWANAMKE KANGA!!!

Macho ya huruma hufurahisha moyo, habari huburudisha mwili. Kuchukiana huendekeza fitina, kupendana husitiri makosa yote. Nilikuwa mgonjwa ukaja kuniona .Nilikuwa na njaa ukanilisha. Kumhudumia mgonjwa ni wito. JUMATANO NJEMA KWA WOTE . NA KUMBUKENI WOTE MNAPENDWA!!! NA PANAPO MAJALIWA BASI TUONANE TENA WAKATI MWINGINE.

10 comments:

emu-three said...

Oh mpendwa ndugu wangu, unanikosha, tupo pamoja

Ester Ulaya said...

Mwanamke Kanga...maneno Kuntu hayo

Yasinta Ngonyani said...

em-three! ni furaha kusikia nakukosha mupendwa ndugu wangu..pamoja sana.

Ester! kanga ilikuwa zamani nilipenda sana ila sasa napenda zaidi VITENGE:

Shalom said...

Naona miaka hiyo ukifunga kanga ww mjanja ila sasa mwanamke kitenge dada ulipendezaje wangu

sam mbogo said...

kanga avaee MZUNGU( Yasinta kumradhi)! wee acha tu zina anguka labda afunge nafundo la uhakika.wa dada na wamama wanapendeza sana na kanga,halafu watu hawajashitukia kanga inakaa vizuri sana kumwili wa mwanamke hasa akiwa na SHEPU!!. kaka s

Mija Shija Sayi said...

Kaka S, shepu gani unaongelea? could you please fafanua kidogo...LOL!!

Anonymous said...

Yasinta, kwa nini umehamia kwenye vitenge? siri gani ipo huko? Khanga zako nipatie mie basi!

ISSACK JIAH said...

SALAMU WALEKUM/BWANA ASIFIWE
WAPENDWA,Nilikuwa nimekwenda kulima shamba huko Tunduru,nimeacha mpunga unakuwa muda tuu utakuwa tayari napiga hodi kwenu kwani maada nyingi zimenipita,Ni kweli nyote mmesema ila dada mwenyewe hajasema yaani hajafunga mjadala na pia mjadala huu tuwaachie akina Rechel si wewe mbogo Kanga wanazijuwa kuchagua wamama kwani kanga ni mipasho mafumbo sasa wewe mbogo unajuwa mafumbo ya kanga utakuta umevaliwa kanga imeandikwa UKIPENDA BOGA UPENDE NA UA LAKE JE UNAJUA ANA MAAANA GANI?ASANTEN
CHE jIAH

Rachel siwa Isaac said...

Tehtehtehteh...Baba Isaack Mpunga huo wakati wa kuvuna nitakuja....

si kuna WANAUME Wengine huwa wanafunga KANGA wakienda Kuoga Au......
Umependeza na Kanga KADALA.......

ray njau said...

Mwanamke kitenge, khanga ni umbeya.